Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Ukira na wakubwa ukianza kura nyama unachapwa. Ukira na wakubwa ukabakia ugari kidogo ukanawa ukambakizia mkubwa utachapwa. Ukira na wenzako ukawakodolea macho wenzako utachapwa. Ukimega tonge kubwa kuzidi mkubwa utachapwa.
 
  • Thanks
Reactions: e2n
Ukira na wakubwa ukianza kura nyama unachapwa. Ukira na wakubwa ukabakia ugari kidogo ukanawa ukambakizia mkubwa utachapwa. Ukira na wenzako ukawakodolea macho wenzako utachapwa. Ukimega tonge kubwa kuzidi mkubwa utachapwa.
Dah... ukira ugari??
 
Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu unaweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo:

1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa ukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.

15 na 16 hahaaa
 
Ndio maana Waafrika wengi tunakosa uthubutu na kujiamini, tunakua kwa taabu na maonevu sana aisee.
 
Back
Top Bottom