Hilo mbona liko wazi kabisa Boss. Na nashangaa kwa nini watu wanabisha. Sijui wanataka watu tuanze kutoa darasa la Business administration 101.
Ngoja nikupe mfano. Evander Holyfield, yule former world heavyweight champion ana bonge la jumba. Hili jumba alilichukulia mkopo (mortgage) kipindi kile bado anapigana na wakati hela ilikuwa inaingia kwa wingi.
Sasa hivi jamaa kaishiwa. Hana tena hela kama ilivyokuwa zamani. Ana watoto 9 na 6 au 7 kati ya hao 9 anawalipia child support. Hilo jumba lake (na ni jumba kweli kweli - ni estate) gharama za matunzo kwa mwezi zinadzidi dola laki sita kwa mwezi.
Bila steady stream of good income hawezi kumudu matunzo ya hilo jumba, hawezi kumudu monthly mortgage note yake, na ukiongezea child support ndo kabisa inakuwa mbinde.
Jamaa ana miaka karibu 50 sasa hivi na bado eti anapigana. Anafanya hivyo kwa sababu hajui kitu kingine zaidi cha kufanya zaidi ya kupigana ngumi za kulipwa. Huyu jamaa alitengeneza hela nyingi sana enzi za ushababi wake. Unwise investments ndiyo zimemponza.
Hilo jumba kuna kipindi, miaka takribani 9 iliyopita lilikuwa appraised kuwa worth around 10-15 million US dollars. Sasa hivi kwa sababu housing market ni mbaya sana thamani yake haizidi hata dola milioni 7.
In the last 5 years mortgage lender wake kajaribu kuli-foreclose hilo jumba mara kadhaa. Kuna wakati waliliweka kabisa katika orodha ya nyumba za kupigwa mnada ambazo zimekuwa forclosed. Evander aka-maneuver akaweza kulipa hiyo outstanding balance yake akaliokoa jumba lake kutopigwa mnada.
Sasa kweli hilo lijumba mtu unaweza kuliita asset? Kwa sababu hata akiamua kuliuza sasa hivi hataliuza kwa ile bei aliyolinunulia enzi hizo miaka ya katikati ya 90. Ataliuza kwa bei ya chee mno. Hilo jumba siyo asset. Hilo jumba ni liability!
mkuu sijui unawaza kutumia nini.?
hahaha....kumbe huku JamiiForum nako kuna vilaza!!!!kasome kitabu cha koyosaki, RICH DAD, POOR DAD" GARI NI LIABILITY
..... watoto ni "liabilities" and not assets. .....
Tulizo...huku unaenda mbali zaidi.Hazole,
Duh! ...sijui watoto wakae upande gani wa balance sheet (Liabilities? Assets?) kwani mimi naamini watoto wako katika kundi la "Owner's Equity" yaani sehemu ya familia ambayo inabidi iongezeke kama Mungu alivyosema tuzae ..tuongeze mtaji wa dunia..
Haya nipe.."Owner's Equity iko upande gani wa balance sheet?