Mabulangati
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 796
- 164
Naona wanaochangia mada mmepotea kiuzakendo na kimantiki ya utanzania. wewe hata uende wapi utabaki kuwa mtanzania. Kimsingi ni Wimbo wa Taifa ni sala/dua au unaweza sema ni maombi kwa MUNGU/MOLA bila kujali dini rangi nk. sasa mtu anapofananishwa kutokusali na kupotoka kwa viongozi wetu, na wizi unaofanywa na malaghai hili haliingii akilini. kama mtu kashindwa kuimba wimbo wa Taifa maana yake ameshindwa hata kuliombea Taifa lake liondoke katika wimbi la matatizo linalolikabili. Wangapi wanaiba lakini ndiyo wanaoimba wimbo wa taifa vyema? wangapi ni majizi/wachawi/mafisadi lakini kwenye ibada wao ndiyo viongozi wa nyimbo na sala? Nafikiri Mtoa mada ana swali zuri sana kwetu kutafakari kwa kina na kutoa jibu lenye mwelekeo wa kujenga na siyo kila kitu politiki jamani.