Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 228
- 550
Nakumbuka zamani miaka ya mwishoni mwa 90's na hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000's jamii ya watanzania walikuwa wanaheshimu sana wimbo wa Taifa hasa hasa panapokuwa na tukio la kitaifa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa watu wote walisimama wima huku mikono yao ikiwa imekunjwa ngumi ya "kike" na kushushwa chini na wote (wengi) waliimba kwa sauti ya juu na kutamka maneno ya wimbo huo barabara kabisa na hata waliopita mita chache ya eneo ambalo wimbo ulikuwa unaimbwa walilazimika kusimama wima.
Kadiri siku zinavyoenda, siku hizi kwenye matukukio ya kitaifa ambayo na viongozi waliopaswa kuhimiza heshima ya wimbo wa Taifa ma DJs ndio wenye jukumu la kuplay wimbo na hakuna sauti za wananchi zinazosikika. Wanasimama huku midomo ikiwa imefumba kana kwamba hawaujui wimbo huo.
Sambamba na hilo, usimamaji wa wima sio lazima wala muhimu, hakuna utulivu na wanaopita karibu na eneo panapoimbwa wimbo wa Taifa hakuna anayejali. Watu wanaendelea na safari zao.
Tabia hii inazidi kujengeka na kuzoeleka kiasi kwamba kuna wasiwasi kama juhudi hazitachukuliwa wimbo wa Taifa utabaki kuonekana kama nyimbo za wasanii wengine na umuhimu wake utapotea.
Naamini wananchi wengi wanaufahamu wimbo wa Taifa vizuri kabisa hivyo sioni sababu ya ku play wimbo badala yake waachwe watu waimbe wenyewe ili kutopoteza umuhimu na kuendelea kuwafanya wananchi wathamini na kuheshimu wimbo wa Taifa.
Kama issue ni kuongeza ladha na kuboresha, ni vizuri DJ a play biti ya blass band tu kwa sauti ya chini ili kuruhusu sauti za wananchi kusikika vizuri na kwa ufasaha kwasababu katika Taifa lililohai wimbo wa Taifa ni nembo ya msingi wa Taifa husika. Kuendelea kuwazoesha wananchi kutoona umuhimu wa wimbo wa Taifa ni kuua Taifa.