Taifa Gas yafanya kampeni maalum ya kuelimisha matumizi ya gesi wakati huu wa mwezi wa Ramadhani

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
WhatsApp Image 2024-03-19 at 22.33.30_cecc6c8e.jpg

Katika kuhakikisha Jamii inakuwa na uelewa mkubwa kuhusu matumizi ya nishati ya gesi Pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwafikishia ujumbe Wananchi wake kutumia nishati hiyo, timu ya Taifa Gas imefanya kampeni maalum wakati huu wa mwezi wa Ramadhani tarehe 19 mwezi wa tatu mwaka huu 2024.
20240319_182325.jpg

Timu hiyo imetembelea Migahawa kadhaa Jijini Dar es Salaam ikiwemo African Food, Mkongwe Restaurant Kigamboni, Neeko Fast Food Kigamboni, Geza Fast Food Kigamboni Hot Fast Food Sinza ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kampeni hiyo itakayoendele hadi mwisho wa mfungo wa mfungo.
WhatsApp Image 2024-03-19 at 22.33.29_e3ca8ab9.jpg

Afisa Masoko wa Taifa Gas Wilaya ya Kinondoni na Bagamoyo, Arnold Wilfred Salewa amesema wamewapatia mitungi na zawadi mbalimbali wahusika wa sehemu walizotembelea.

“Dhumuni la kampeni hii ni kuweza kusogeza elimu ya nishati safi na salama kwa ajili ya kupikia, ili kuendeleza juhudi za Serikali na raia wote katika kutunza mazingira yetu kwa ajili yetu sote na vizazi vijavyo.
20240319_182442.jpg

“Pia dhumuni lingine ni kuweza kusogeza ufahamu wa bidhaa zetu na kuwaelezea Watanzania wenzetu kwanini Taifa Gas ndio chaguo lao pekee katika matumizi ya nishati Safi na salama. Kwanza bei zetu ni rahisi na huduma zetu ni Bora maradufu ukilinganisha na bei tunazouza,” amesema na kuongeza:

“Usalama wa mitungi yetu ni wa kiwango kinachokidhi Kimataifa kwani mitungi yetu ina valve ya usalama ambayo inapunguza pressure ndani ya mtungi pindi inapopanda na kuondoa athari za ajali au milipuko.
20240319_182434.jpg

“Vilevile tunakufikia Hadi nyumbani Bure pindi unapotuhitaji kukujazia pia mawakala wetu wanafurahia sana huduma zetu kwani tumesambaa nchi nzima na ndio kampuni pekee yenye vituo vya kujazia nishati kwa Kila mkoa nchini Tanzania.

“Malengo yetu kama Taifa gas ni kuweza kuwafikia watanzania wote nchini Kila nyumba bila kuacha Kijiji Wala mtaa Hadi tutakapotokomeza kabisa matumizi ya Kuni na mkaa kwa manufaa ya nchi yetu na kizazi kijacho.”
IMG-20240319-WA0041.jpg

Naye, Lulu Mringo ambaye ni Mmiliki wa Mama Land amesema “Nimefurahia kutembelewa na Taifa Gas, kwani tangu nimeanza kutumia gezi zao ni kuwa ina presha kubwa na haiishi haraka, wanahudumia wateja kwa haraka.
 
Safi, huyo Afisa masoko wilaya ya kinondoni nimefanya naye Kazi Mbinga Ruvuma , NI mtu poa Sana , mpe hai Sana
 
Back
Top Bottom