Watanzania wengi hawawezi kuimba wimbo wa taifa

Naona wanaochangia mada mmepotea kiuzakendo na kimantiki ya utanzania. wewe hata uende wapi utabaki kuwa mtanzania. Kimsingi ni Wimbo wa Taifa ni sala/dua au unaweza sema ni maombi kwa MUNGU/MOLA bila kujali dini rangi nk. sasa mtu anapofananishwa kutokusali na kupotoka kwa viongozi wetu, na wizi unaofanywa na malaghai hili haliingii akilini. kama mtu kashindwa kuimba wimbo wa Taifa maana yake ameshindwa hata kuliombea Taifa lake liondoke katika wimbi la matatizo linalolikabili. Wangapi wanaiba lakini ndiyo wanaoimba wimbo wa taifa vyema? wangapi ni majizi/wachawi/mafisadi lakini kwenye ibada wao ndiyo viongozi wa nyimbo na sala? Nafikiri Mtoa mada ana swali zuri sana kwetu kutafakari kwa kina na kutoa jibu lenye mwelekeo wa kujenga na siyo kila kitu politiki jamani.
 
Uko sahihi mkuu, wimbo wa taifa ni SALA. Naungana na Nyunyu kuwa shule sasa hivi huwezi hata kujua wanafundisha nini! Mtoto wa darasa la tano hawezi kuimba wimbo wa taifa bila kukosea!
 
Wimbo ni national unit, ni sara ambayo haichagui dini, chama, kabila wala rangi ya mtu. Ili tuwe na umoja tunahitaji kitu cha kutuunganisha. I think something need to be done, not only for the national anthem but also to make us feel proud to be one Tanzanians
 
Niliacha kuimba wimbo wa Taifa nilipofikishwa mahakamani baada ya kuweka wimbo wa Taifa kama ringtone kwenye simu yangu.
Si ajabu kukuta watu hawaimbi wimbo wa Taifa. Mara kibao bendera ya Taifa hugeuzwa juu chini.
 
Tuwe wazi na kusema ukweli...kati ya vitu ambavyo Tanzania tumepoteza kwa kiasi kikubwa ni kupoteza UZALENDO....Nasema hizi kwasababu vijana na kizazi cha leo tunafahamu mengi kuhusu nchi za magharibi kuliko ya nchi yetu,nakumbuka nikiwa standard III miaka hiyo tulikuwa tunaimba ahadi za TANU darasani kabla ya jambo lolote,Tulikuwa tunaimba wimbo wa Tanzania Tanzania Nakupenda na wimbo wa Kusifia maliasili zetu na ZAIDI WIMBO WA TAIFA.Sijui kama mambo haya bado yapo huko mashuleni....sababu ni nini?

  1. Shule zetu hasa za msingi hakuna tena kufundishwa mambo hayo,na hii inasababishwa na motisha ndogo wa wawezeshaji yaani mwalimu.Ni aibu kwa mtu kushindwa kuimba wimbo wake wa Taifa narudia tena AIBU....
  2. Vijana wengi kuwa na mawazo ya kimagharibi zaidi na kusahau hata angalau baadhi ya mambo ya Taifa lao
  3. Yawezekana pia ni kizazi cha mafisadi na uzalendo unapotea kwa haraka....mtoto wa nyoka ni nyoka
 
hz shule ze2 za watakatifu wtt hawafundshw tn wmbo wa Taifa! Cjui ni kwa nn? Kn mtt nlwah kmulza km shlen huw wnaimba wmbo wa taifa! Akajb ndio. Nlpomwambia aimbe akaanza kuimba Tanzania, Tanzania. Nkabak nakodoa macho kama Fund saa.
 
Niliacha kuimba wimbo wa Taifa nilipofikishwa mahakamani baada ya kuweka wimbo wa Taifa kama ringtone kwenye simu yangu.
Si ajabu kukuta watu hawaimbi wimbo wa Taifa. Mara kibao bendera ya Taifa hugeuzwa juu chini.

Very sad my broda! these things can be discouraging, sorry 4 that.. so nini ilitokea kwa mahakama?
 
Freud angesema Watanzania subconsciously hawaamini katika taifa la Tanzania, na wanajionea karaha hata kuimba huo wimbo.
 
Hapo umeongea kweli mie watoto wangu hawajui kabisa nimewaambia waimbe hakuna anayejua hzi senti nini sijui ndo tumekwisha kabisa watoto wanafundishwa kizungu tu
 
Hapo umeongea kweli mie watoto wangu hawajui kabisa nimewaambia waimbe hakuna anayejua hzi senti nini sijui ndo tumekwisha kabisa watoto wanafundishwa kizungu tu

Sipati picha In 20yrs to come!?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom