Tuache ushabiki wa kisiasa Prof Lipumba ni kichwa cha Uchumi Tanzania tunashindwa kumtumia. Umoja wa Mataifa wanamtumia Kuboresha Uchumi wa Nchi kubwa Duniani wakati Tanzania ni Maskini na Uchumi wetu ni Duni. Ipo haja ya kuweka mjadala wa Kitaifa kwa ajili ya kuwatumia Wataalamu wetu kwa manufaa ya ustawi wa Taifa letu. Prof Lipumba amelikosea nini Taifa hili mpaka linashindwa kumtumia? Tunaomba makosa yake yawekwe wazi.Ni aibu kubwa wataalamu wetu wanasaidia nchi nyingine wakati sisi ni maskini wa kutupwa. Kwa kipaji alichokuwa nacho Prof Lipuimba nadiriki kusema ni Rais Bora ambaye kura Hazitoshi kwa ajili ya kulisaidia Taifa hili,nawashauri Watanzania wenzangu tumtumie Prof Lipumba ainue uchumi wa Nchi yetu tuondokane na umaskini.