MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,223
- 22,299
Binafsi nakubaliana 100% kwamba bunge ni muhimu kwenye kuisimamia serikali kwa mujibu wa katiba ila siridhishwi na jinsi lilivyo kwa sasa. Mimi maoni yangu kuhusu bunge ni kama ifuatavyo;
1. Viti maalum vibaki vile 10 vya Rais tu. Hivi vingine vifutwe.
2. Majimbo yapunguzwe. Majimbo 264 ni mzigo kwenye huu ulimwengu wa kidigitali. Kama ni uwalikilishi wanatosha hata wanne kwa mkoa mzima. Kimsingi kwa sasa kuna watu mitandaoni wanawakilisha matatizo mengi kuliko hata wawakilishi wanaolipwa kwa kodi zetu. Mtu kama Malisa anafaa kuitwa mwakilishi wa wananchi.
3. Wabunge wawe na elimu kuanzia degree. Bunge ni chombo cha kutunga sheria ambacho kwa sasa kimejaa wabunge wengi wasio na uwezo wowote hata wa kusoma miswada ya kisheria wakaielewa vya kutosha. Tuwaondoe bungeni wabunge wenye elimu duni. Hawa wanachangia kupitishwa kwa sheria kandamizi.
4. Spika wa bunge asiwe mbunge au mwanachama wa chama chochote. Agombee hiyo nafasi toka nje ya bunge.
5. Mishahara na stahili zingine zipunguzwe kwa 50%.
Wewe una maoni gani?