Elections 2010 Watanzania kwa nini tunakuwa wepesi kuamini uongo wa CCM?

Mkandara,

Kiranga anasema kuwa, kwa vile hatuna serikali, vyama na ideology kwa standard yake, basi tuachane kabisaaa na investment kwenye human resource. Kwa maoni yake, ni upotevu wa pesa za serikali kutoa elimu ya msingi kwa raia wa nchi yako.

ohhhh then... I give up

Unastretch maneno yangu, mimi nakwambia kwa nini unataka kuiamini sana serikali mbovu? Kwa nini usiweke misingi ya decentralization of resources watu walipe shuleni instead of shule kutegemea kodi ya serikali, au hata kama shule zikitegemea serikali kwa nini kusiwe na mifuko maalum inayojulikana kwamba haya ni mapato ya 20% ya Watanzania wanaojilipia elimu, watu waweze kujipima vizuri zaidi ?
 
I gotta mrs Kolimba,

Mirengo ya kulia katika nchi za kibepari imeishi na free education for all kwa miaka karibu 50 sasa. Na kwa jinsi nilivyomfuatilia PM Brown wa UK wakati wa debate na baada ya kukamata uongozi, torries hawaonekani kama wataachana na free education (achilia mbali health system) in the near future.

Unachokiadvocate hapa, hakijatokea nchi yoyote iliyoendelea. Nchi zilizoendelea zimegundua umuhimu wa an educated population na wanafanya kila wanachoweza kuelimisha kila mtu.

Nchi zilizoendelea elimu bure ya umma haikuwepo mpaka 20th century, tena wala si early 20th century.

One has only to read Dickens and Churchill to know that the Oliver Twists of 19 century England did not have educational options at all, let alone free public ones. Ukitaka tufuate mfumo wa nchi zilizoendelea utasema nusu ya watoto wa shule waache shule waende kuwa wana Apollo katika migodi pamoja na kulima mashambani. Ndicho walichofanya walivpokuwa katika level yetu ya maendeleo.

Usitake kupotosha watu.

But then again who reads Dickens and Churchill anymore ?
 
Nchi zilizoendelea elimu bure ya umma haikuwepo mpaka 20th century, tena wala si early 20th century.

One has only to read Dickens and Churchill to know that the Oliver Twists of 19 century England did not have educational options at all, let alone free public ones. Ukitaka tufuate mfumo wa nchi zilizoendelea utasemanusu ya watoto wa shule waache shule waende kuwa wana Apollo katika migodi pamoja na kulima mashambani.

Usitake kupotosha watu.

But then again who reads Dickens and Churchill anymore ?

Imebidi hapa nirudi kukujibu...

nilichoandika ni hiki:

Mirengo ya kulia katika nchi za kibepari imeishi na free education for all kwa miaka karibu 50 sasa

Nadhani miaka 50 iliyopita inaanzia karne ya 20, au wewe unasema nini? Nani anataka kupotosha hapa?

Kiranga, take time mkuu, haya mambo ya winning at all cost muda mwingine yanaharibu umakini wako.
 
Unastretch maneno yangu, mimi nakwambia kwa nini unataka kuiamini sana serikali mbovu? Kwa nini usiweke misingi ya decentralization of resources watu walipe shuleni instead of shule kutegemea kodi ya serikali, au hata kama shule zikitegemea serikali kwa nini kusiwe na mifuko maalum inayojulikana kwamba haya ni mapato ya 20% ya Watanzania wanaojilipia elimu, watu waweze kujipima vizuri zaidi ?
Mkuu kwa sababu ndio kazi ya serikali laa sivyo huna sababu wala haja ya kuwa na serikali. Kisha kila siku nakwambia hivi mkuu wangu kwa kila mkakati wowote ni lazima utazame WATU na MAZINGIRA yao wewe unaanzisha mfuko wa elimu hali watu wenyewe hawana elimu na uwezo huo. nani machangie nani ikiwa leo tu watu wanachanga fedha za harusi na vifo kwa maelfu wakiacha watoto wao pasipo elimu.

Huo mfuko auanzishe nani wee tazama hapa JF tu watu tunakimbia mchango iwe kuelemisha mtoto wa Kiranga iwe jukumu langu! Utawala mbovu unaanza na maamuzi mabaya kama haya ya kuweka elimu kama ni privilege..Hizo nchi unazosema ziliweza vipi kusema education is compulsory ikiwa wananchi walitakiwa kulipia..Hii inakuingia akilini?

Utawala mzuri ni ule unaokubali jukumu hilo kwani kumlea mtoto mmoja inatakiwa nguvu ya kijiji kizima na serikali ndio kijiji chetu..Na usidanganywe na mtu, malezi ya mtoto ni ELIMU..Chadema tutamlea mtoto huyo ili apate elimu ya kumwezesha yeye kuwa mwajiri kesho ndio malengo sio kuagizia Wakenya hata kuwa receptionist..Wageni waje hapa wakute kazi ya kulinda nyumba na kukata majani sio kuchukua kazi za wananchi kwa elimu ya lugha.

Mkuu wangu hata ufanye mipango gani yenye kila aina ya lugha na mapambo maadam wananchi wako hawana elimu huwezi kujenga kitu...Elimu ya ubaguzi ndio tool iliyotumiwa na mkoloni kuendelea kutawala nchi zote, ulichosoma huko nyuma kinahusiana zaidi na kutawaliwa na sio nchi huru. Kuendelea kufanya kama wao ni kuzalisha matabaka ambayo tayari yamekwisha anza jitokeza..
 
I gotta mrs Kolimba,

Mirengo ya kulia katika nchi za kibepari imeishi na free education for all kwa miaka karibu 50 sasa. Na kwa jinsi nilivyomfuatilia PM Brown wa UK wakati wa debate na baada ya kukamata uongozi, torries hawaonekani kama wataachana na free education (achilia mbali health system) in the near future.

Unachokiadvocate hapa, hakijatokea nchi yoyote iliyoendelea. Nchi zilizoendelea zimegundua umuhimu wa an educated population na wanafanya kila wanachoweza kuelimisha kila mtu.

Sahihisho,

Hapa nilitaka kumuongelea PM Cameroon wa Torries
 
Unastretch maneno yangu, mimi nakwambia kwa nini unataka kuiamini sana serikali mbovu? Kwa nini usiweke misingi ya decentralization of resources watu walipe shuleni instead of shule kutegemea kodi ya serikali, au hata kama shule zikitegemea serikali kwa nini kusiwe na mifuko maalum inayojulikana kwamba haya ni mapato ya 20% ya Watanzania wanaojilipia elimu, watu waweze kujipima vizuri zaidi ?

Kiranga,

Tofauti na wewe, mimi sisubiri kuwa na perfect government ili kupata au kutoa vitu vya msingi. Elimu ni kitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote ile. Serikali iwe ya kijeshi au kiraia, iwe ya wagonjwa na majambazi kama ya ccm au ya watendaji kama (....), bado inabidi serikali hiyo ifanye kila iwezalo kuelemisha raia wake (hata kama ni kwa elimu ya msingi na upili).

Hii ni sababu nyingine naiunga chadema katika uchaguzi huu - wanajali wananchi wao na wanaonesha hilo kwenye sera zao.
 
Imebidi hapa nirudi kukujibu...

nilichoandika ni hiki:

Nadhani miaka 50 iliyopita inaanzia karne ya 20, au wewe unasema nini? Nani anataka kupotosha hapa?

Kiranga, take time mkuu, haya mambo ya winning at all cost muda mwingine yanaharibu umakini wako.

Hahaha,

Nimecheka nilipoona "winning at all cost".

Kati yangu ninayetaka wenye uwezo washirikiane na serikali katika gharama za elimu, na wewe unayetaka serikali ichukue mzigo wote katika vita dhidi ya ujinga, nani anataka "winning at all cost" ?
 
Kiranga,

Tofauti na wewe, mimi sisubiri kuwa na perfect government ili kupata au kutoa vitu vya msingi. Elimu ni kitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote ile. Serikali iwe ya kijeshi au kiraia, iwe ya wagonjwa na majambazi kama ya ccm au ya watendaji kama (....), bado inabidi serikali hiyo ifanye kila iwezalo kuelemisha raia wake (hata kama ni kwa elimu ya msingi na upili).

Hii ni sababu nyingine naiunga chadema katika uchaguzi huu - wanajali wananchi wao na wanaonesha hilo kwenye sera zao.

Nani kasema anasubiri perfect government? Mimi nimesema siamini katika governmental paternalism, especially if the government is almost nonexistent.
 
Hahaha,

Nimecheka nilipoona "winning at all cost".

Kati yangu ninayetaka wenye uwezo washirikiane na serikali katika gharama za elimu, na wewe unayetaka serikali ichukue mzigo wote katika vita dhidi ya ujinga, nani anataka "winning at all cost" ?

Nimemaanisha kushinda debate...

Back kwenye issue, Unajua ungechukua muda kusoma unachoandika kwa makini ungejicheka sana. Unapoongea kuwashirikisha wenye uwezo (unamaanisha kuchangia/kutoa pesa). Kwa nini unadhani kuwa kuchangia moja kwa moja kwa kulipia na kuchangia kwa kutoa kodi ni dhana mbili tofauti?

Serikali bado itakuwa inawashirikisha wenye uwezo. Wewe mwenyewe hapo juu umesema kuwa wenye uwezo kina Mengi wanatoa kodi nyingi Tanzania. Kina Mengi wakiamua kuleta watoto wao kwenye free public school, watakuwa bado wamekuja kutumia "pesa zao" walizozitoa (changia) serikalini kwa njia ya kodi.

Swala la ushirikishi liko pale pale iwe kwa kodi au kwa ada
 
Ubaya wa kuwa na elimu bure ya msingi na upili ni upi?

NN, labda wewe utajibiwa. Nimeuliza swali hili na mengine mengi ila yeye atajibu anachopenda.
Mimi natoka kidogo maana Kiranga kama kawaida yake hajibu maswali mara nyingi. Naendesha kwenda somewhere kutulivu for a long quite weekend.Next paycheck ni zamu ya nani kuchoma nyama?
 
Ubaya wa kuwa na elimu bure ya msingi na upili ni upi?

Kuwa na elimu bure ya shule za msingi na upili, kwa wasioweza kumudu malipo, hakuna ubaya.

Tatizo kwangu ni pale tunaposema "elimu bure kwa wote" hatujali wewe Rostam Aziz wala Reginald Mengi, una uwezo wa kujilipia au huna.

Ukienda kushoto watakwambia "From each according to his ability, to each according to his need" ukienda kulia wewe mzee wa GOP unajua wanavyosema kuhusu welfare state.

Ukija kati kwa utilitarians kina Kiranga wanakwambia wasio na uwezo wasaidiwe, wenye uwezo walipie.

Huu mfumo utafanya watoto wa wachimba chumvi wasiojiweza Kibondo wakose nafasi kwa sababu wajanja waliopiga bingo ya EPA wamewahi nafasi.
 
NN, labda wewe utajibiwa. Nimeuliza swali hili na mengine mengi ila yeye atajibu anachopenda.
Mimi natoka kidogo maana Kiranga kama kawaida yake hajibu maswali mara nyingi. Naendesha kwenda somewhere kutulivu for a long quite weekend.Next paycheck ni zamu ya nani kuchoma nyama?

Mazee ana expose colors zake.

Unaniuliza swali halafu unalalamika najibu ninachopenda, wewe ulitaka nijibu unachopenda wewe kumbe ?
 
NN, labda wewe utajibiwa. Nimeuliza swali hili na mengine mengi ila yeye atajibu anachopenda.
Mimi natoka kidogo maana Kiranga kama kawaida yake hajibu maswali mara nyingi. Naendesha kwenda somewhere kutulivu for a long quite weekend.Next paycheck ni zamu ya nani kuchoma nyama?

Safari ijayo tunajumuika kwa Mwanakijiji....on the ones and twos atakuwepo Ab-Titchaz akispin Ikibinda nkoi, kwasakwasa, n.k.

Kwenye grill nitakuwepo mwenyewe wenu mtiifu nikifanya mavitu yangu.....mratibu wa ulabu atakuwa mazee Ogah....bila kumsahau FMES atakayekuwa atakayekuwa moderator wa mijadala....
 
Kuwa na elimu bure ya shule za msingi na upili, kwa wasioweza kumudu malipo, hakuna ubaya.

Kuna ubaya gani elimu hiyo ya bure kutolewa kwa wote bila kujali madaraja ya walionazo na wasionazo?

Tatizo kwangu ni pale tunaposema "elimu bure kwa wote" hatujali wewe Rostam Aziz wala Reginald Mengi, una uwezo wa kujilipia au huna.

Hapa si tunazungumzia shule za serikali, au siyo? Kama ndiyo na wewe ni Rostam ubaya uko wapi kwa mwanao kusoma shule ya serikali? Kama hutaki mwanao asome shule hizo si unampeleka tu unakotaka wewe? Kigumu ni kipi hapo?

Ukienda kushoto watakwambia "From each according to his ability, to each according to his need" ukienda kulia wewe mzee wa GOP unajua wanavyosema kuhusu welfare state.

Tufanye mambo kivyetu vyetu ni si kuiga mirengo ya kisiasa ya watu wengine. Siyo kila right winger anapinga huduma zitolewazo na serikali.

Ukija kati kwa utilitarians kina Kiranga wanakwambia wasio na uwezo wasaidiwe, wenye uwezo walipie.

Sawa, lakini kwa elimi za msingi na upili, kama uwezo tunao, basi zitolewe kwa wote kwani watoto wetu wote ni wadau ktk mustakabali wa taifa. Hii ningependa zaidi iwe kwenye elimu ya juu na si msingi wala upili.

Huu mfumo utafanya watoto wa wachimba chumvi wasiojiweza Kibondo wakose nafasi kwa sababu wajanja waliopiga bingo ya EPA wamewahi nafasi.

Mfumo upi? wa elimu ya bure ya msingi na upili?

Bado hamjanishawishi kwa nini elimu ya msingi na upili isitolewe bure kama tunaweza.
 
Kuna tofauti kati ya political will na applied economics. Kama ni political will mbona ningetaka mpaka PhD watu waende bila kujilipia wenyewe. Lakini tatizo linakuja, tunaweza ku afford nini? Ni mfumo gani unatumia resources zetu vizuri zaidi ?

Kwa ngu mimi, mfumo unaotumia resources vizuri zaidi ni kuruhusu wasio na uwezo kusoma bure, na wale wenye uwezo wajilipie.Kwa maana tuna limited resources, na kuwaachia wenye uwezo wa kujilipia kuchukua nafasi hizi fixed maana yake ni kuwanyima wasio na uwezo, au kunyima nyanja nyingine za uchumi zinazohitaji fedha hizi.
 
Elimu ya bure kwa wote inawezekana leo na hata kesho, mambo ya oo wenye uwezo waio na uwezo hayana msingi. elimu bure inawezekana na bado ikawa elimu bora kabisa kwa rasilimali zilizopo. kama ccm hawawezi ndiyo wakati wao huu kuachia nchi kwa wenye uwezo huo ili tuje kuwahukumu baada ya miaka mitano.stop
 
Yaani sioni ugumu wowote kwa nini isiwezekane na sioni sababu yoyote ya msingi kwa nini isitolewe kwa wote hadi kiwango cha upili.
 
Tuseme tuna nafasi moja ili kutolea mkazo na kulielewa vizuri swala la "limited resources"

Mtoto wa mkulima hawezi kwenda Feza Academy, Kenya, Afrika ya Kusini, Uingereza wala Marekani kusoma.Kwa hiyo kimsingi akikosa nafasi hii anarudi kulima, anakosa elimu.

Mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, hata akikosa nafasi hii ya elimu ya bure ana nafasi ya kwenda kokote kutafuta elimu, na kukosa nafasi ya kusoma bure hakutamuathiri sana.

Ndiyo maana nasema nafasi hii ya bure apewe mtoto wa mkulima ambaye hana uwezo, na kama tunataka kumpa mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, Mr. X alipishwe ada ili ada hii ama itumike kumsomesha mtoto mwingine wa mkulima asiyejiweza, au itumike katika huduma nyingine za kijamii. Hata huyo Karl Marx aliyetetea mifumo ya serikali kuchukua majukumu ya huduma za jamii alisema "From each according to his ability, to each according to his need". Hata Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa ni bingwa wa kutetea elimu ya bure kwa wote mwishoni alikubali kwamba serikali maskini kutaka kumlipia kila mtu katika mtindo wa "mtego uwanasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa" halikuwa jambo la busara, kwa maana ya kwamba wenye uwezo wa kujilipia na wajilipie.

Tunapenda kuamini kwamba "elimu bora kwa wote" italeta huduma sawa kwa wote kwenye elimu, lakini mimi naona itawanyima maskini zaidi ya itakavyowanyima matajiri.
 
Back
Top Bottom