Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Baada ya kuchomewa nyumba na biashara zao, wale Watanganyika wenzetu bado wanaendelea kuteseka kwa kuishi maisha mabaya kuliko hata wakimbizi. Kwa sasa wamehifadhiwa katika vyumba viwili vidogo, kimoja wanalala wanaume, kingine wanawake. Ni zingira la kutisha ambapo wanalala zaidi ya watu 40 katika chumba ambamo hamna kitanda, wala godoro wala chandarua na mbu ni wengi.
Kina mama wanaishi na watoto katika chumba hicho kidogo, kwa kweli ni pabaya kuliko hata zizi. cha kusikitisha zaidi, eneo hilo hamna hata choo.
Binafsi naamini serikali haina sababu ya kukaa kimya ikiwaacha wananchi wake wakiteseka ugenini huko kwenye machozi. Lazima kitu kifanyike kuwakomboa hawa wenzetu.