Watalii kutokuja tena Tanzania?

Wilderbeast2.jpg
 
Neno udini linatoka wapi mbona katika maandiko sikuone neno dini ama ni mawazo mfu tu kila mara wakitajwa waarabu means Uislam ? Mtoa habari kaongelea uhalisia wa eneo na matukio sasa mnatuondoa kwenye hoja za maana mnaanza udini ?
 
Na kwanini mtalii asiwe mwarabu, mwafrika, mchina? Hata sisi tusishabikia masuala ya dini tunaona wazi kuwa Streotype ndio iliyofanya kuwa mwanzo wa thread hii.

Nchi inayoongoza barani Afrika kwa utalii ni Egypty. Kama waMarekani wanaweza kwenda nchi ya KiArabu kutalii, kwanini asije Tanzania.

Infact watu wanaiangusha JF kwa kuleta mambo ya kidini directly and indirectly.

Kasome kitabu cha Dambisa Moyo Dead Aid au sikiliza mahojianao yake. Na anasema nchi zenye reserve za pesa ni nchi za kiArabu, India na China. Hivyo mentality kuwa mzungu ndio mwenye mshiko is completely wrong.
 
babukijana,
Mkuu haiwezekani hawa kuwa AL SHAABAB kutokana na mavazi yao.. Wewe huwezi kuona tofauti ila sisi tunaofahamu na itakuwa kazi nyingine kukufahamisha na nina hakika huwezi kuamini pia. Ila inanipa picha mbaya sana kuona hawa jamaa wakifanya uwindaji pasipo uangalizi wa vyombo vyetu.. Waswahili wanasema trust no one!

unajua shule muhimu sana katika maisha

hivi Mkandara ushawahi kwenda kuwinda maishani mwako?

Si zungumzii kuwinda ndezi au kuvua Sangara Victoria, nazungumzia uwindaji halali wa wanyama kama Nyati na kadhalika kwenye mbuga za wanyama Tanzania?

Man you need to get out into the real world sasa hivi umeishia kuingia kwenye kundi la speculators tuuu hujiulizi kwa nini lile kundi lingine la maswahiba wako halijakuunga mkono?

Aaah GT wewe acha tu Mkandara anaogopa ataambiwa mdini. Yaani niliposoma hiyo hoja ya bastora nimecheka sana!

Kweli JF ni home of Great Thinkers!

Mkandara yuko kama vile mtoto mwenye identity crisis lakini usipate tabu I am working on helping him aweze kuthink independently
 
Mbona mnazunguka mbuyu tu? semeni tatizo nini. wengine mnakereka na mavazi tu basi, wengine muonekano wao hao jamaa ni militaristic, wengine nchi imeuzwa.

Mnahangaika tu mnashindwa kusema ukweli wenu kuwa tatizo hao ni waislamu na waarabu hivyo hawatakiwi wanaotakiwa hapo ni wazungu tu kwa sababu hao ni wagalatia wenzenu.

Kama mpo objective mngetuletea na picha za wazungu wanaowinda huko, kwani wawindani ni waarabu tu? Na je kuwinda ni ujangiri? Kwani hawana vibali vya uwindaji hao? Na utakuta watia saini wa vibali ndio ninyi wagalatia.

Njoo na takwimu kuna makampuni mangapi ya uwindaji huko na wamiliki ni akina nani ndio mtaona mnavyoongozwa na chuki

Udini tu hamna lolote!

Of all people hata wewe Mkandara?

Haya tuwaone hao wenye haki ya uwindaji basi

Giraffe.jpg

http://i249.photobucket.com/albums/gg209/mbuyanzi
/Simba4.jpg

Lion.jpg

Hunting3.jpg

Cheetah.jpg

Wilderbeast.jpg

Gazelle.jpg

Hunting3.jpg
Body language ya wawindaji uliowaweka hapa inaonyesha habari nyingine kuliko zile za awali ambazo zinaleta hisia tofauti, hasa ukizingatia namna ya kuwepo kwao Loliondo.
 
Body language ya wawindaji uliowaweka hapa inaonyesha habari nyingine kuliko zile za awali ambazo zinaleta hisia tofauti, hasa ukizingatia namna ya kuwepo kwao Loliondo.

Its simple wale ni WAISLAM

hao wengine ni wazungu WAKRISTO

sasawhy hit around the bush?
 
saa zingine huwa siamini kama ni wewe unayeongea maneno kama hayo...sasa whats the difference kati yako wewe na wengine wenye upeo mfupi wa kuangalia mambo kwa mapana na marefu au basi tuu ndio katika mambo ya band wagoning?

1) Kuna ubaya gani Sheikh Mohammed na contigency yake kwenda kuwinda Loliondo?

2) Huyo ni kiongozi wa nchi na anatembea na bodyguards wake ambao kisheria wanaruhusiwa kuwa na among other things ni hiyo bastola

3) Je angekuwa Obama ndiye aliyekwenda Loliondo kuwinda na walinzi wake ungequestion kwa nini mmoja kati ya watu wake ana bastola?

4) Je wangekuwa Prince Charles na timu yake ndio wameenda kuwinda kule ungelalamika?
Mkuu kuna tofauti kubwa baina yangu na wewe ktk kutazama na kufikiri swala kama hili..
Kwanza kinachoingia akilini mwako ni huo Usheikh! yaani unaingiza Uislaam kabla ya kuwatazama wahusika hawa kama Waarabu na Wasaudia..Hawa watu hu8ko kwao hata kama mtakuja na billioni dollar hawawezi kuwauzia kipande cha jangwa ambacho hakina hata mdudu wa kumtazama..Na huwezi pata Uraia hata kama umezaliwa na mababu kumi waliopita ndani ya Saudia.. Wee unawatukuza kwa nini kama sio hizo fikra finyu!

Nimezitazama picha na kuelewa kitu tofauti kabisa na nyie wenye kutazama rangi ama mavazi nacho ni Kwanza haya yote yanatokea kwa sababu tumeuza Loliondo na hawa sii Watalii wawindaji isipokuwa wanakuja ktk mali yao na kufanya wayatakayo kiasi kwamba hata Ulinzi ni wao wenyewe na hakuna Mdanganyika anayeruhusiwa kuwa karibu...

Huyo Obama au Prince Charles hawawezi kutua Loliondo pasipo idhini ya hawa jamaa na sidhani kama Obama wala Charles wanaweza kufanya hivyo kwani watapoteza kabisa hadhi zao kwa kuua wanyama kama sehemu ya mchezo (sports)..They prefers Jogging na huwezi kuwaona walinzi wao wamebeba bastola viunoni sehemu isiyohusiana hata kama....Kisha hata kama ingewezekana Obama au Prince kuja kuwinda, nina hakika JK angekuwa pembeni na walinzi, wataalam na kadhalika wakifuatia kwa karibu..

Mkuu Picha hizi zinadhihirisha tumeuza nchi na sijali kama wameuziwa WaSaudia, Wamarekani au Waingereza..
 
The issue hapa ni yale yale ya POLITICS OF HATE na NARROW MINDEDNESS ya baadhi ya wachangiaji humu

Je hizo picha zingekuwa za akina Prince William au royal family ya Britain isingekuwa tatizo lakini kosa la hawa jamaa ni asili yao sasa itatafutwa kila namna ya kuwafanya waonekane hawafai and so on

Nyie mshatangaza utaliii ili wageni waje wa kila namna na hawa wanaenda kuwinda hilo lishakuwa kosa?

Kama huko Loliondo hakuna huduma mnazotaka sasa hilo nalo kosa la Sheikh Mohammed?

acheni kuwa na mitazamo finyu...mnajua fika tatizo ni SERIKALI na si jukumu la hao waarabu kupeleka maji na huduma za afya huko hilo ni jukumu la serikali yenu na kama mnatafuta mchawi then huko ndiko kwenye mchawi wenu na si kuanza kutafuta uchawi kusipo

halafu so far sijaona hata tone moja la ushahidi kuwa yote ambayo yanasemwa kuhusu Loliondo ni kosa la waarabu au kwa sababu ni easy target?

If anything wabaya wenu ni hao mnaowatuma wanegotiate hiyo mikataba yenu na bila kusahau wanasheria wenu. Mimi at this moment nishaacha kulaumu external forces kwenye hii mikataba ambayo hamuishi kulalamikia

hebu mie niende nikasome episodes za Kafulila na Zitto.

Hapa unakosea. Hao unaowazungumzia, wakina Prince William wasingeweza kupigwa picha kama hizi. Kwani aristocrats wangapi wameishatembelea au kuwinda katika mbuga zetu? Kinachogomba kwa wengine si uarabu au uislamu wa hawa jamaa. Ni hiyo mikao ya Rambo. Kama ilivyoisha ulizwa bastola ya nini humo mbugani? Wewe unayejidai umeishwahi kwenda kuwinda, unataka kutuambia uliingia mbugani bastola kiunoni na rifle mkononi? Hapa hatupingi uwindaji. Tunachopinga ni namna uwindaji huo unavyoelekea kufanywa. Mimi mwanzo nilitilia shaka picha hizi hadi nilipoona namba za gari.

Wenye slave mentality ni nyie ambao mnashindwa kumkosoa Master hata iweje. Wenye identity crisis ni nyie ambao mnachukua majina ya colonial masters wenu hata yasipoendana na imani yenu (Eddie na uislamu wapi na wapi).

Zakumi. Ni watalii wangapi kutoka bara Asia wanaotembelea mbuga zetu? Hawa kama tulivyo sisi hawana tamaduni ya kwenda porini kumpiga picha mnyama. Kwa hawa, kama ilivyo kwetu sisi, m-nyama ni kiumbe cha kuwindwa au kutumikishwa. Watalii kutoka Asia wanapendelea sana mambo ya heritage isiyo hai ndiyo maana utawakuta wa-japan na wachina kibao wamejazana Paris wakipiga picha majengo, waarabu na wahindi kibao wakiwa nchi za magharibi wakifanya shopping na kutembelea theme parks. Mbugani kwetu au hata Afrika ya Kusini? Wachache sana.

Msitake kututisha tusichangie kwa kuingiza suala la dini kila anapokoselewa yule mnayeamini ni mwenye dini yenu. Si kila mtu mwenye mtizamo wenu.

Amandla........
 
Hii hali ilivyo sasa mbugani waarabu kuweka makazi yao namna hii , Kweli Mmarekani ataweza kuja mbugani na hali ikiwa hivi jamani hii mbona kubwa kuliko ni kwanini tujipotezee mapesa ya wazungu wakati wazungu toka enzi na enzi ndio ambao wamekuwa wakitusaidia,
sisi hata kama hatwendi mbugani kuangalia maliasili zetu ni uwezo tu ila tunazipenda sana tena sana ningependa Mbuga ziheshimiwe waachwe wanyama pekeyao wasiletewe usumbufu.
Lakini kwanini nyinyi tu jamani mbona Kenya haya mambo hayapo? are we stupid? %%%%#####**** griiiiiiiiiiiiiii

i680_fazza3tanzanya16.jpeg

i683_fazza3tanzanya18.jpeg

i688_fazza3tanzanya36.jpeg

i695_fazza3tanzanya122.jpeg

Acheni hao jamaa wawinde tatizo haswa nin nini?, kwani waliwalazimisha kusaini mkataba? kwani mliwaambia wasije na nguo za kijeshi ama kuweka bastola viunoni? Kama wanawinda kinyemela hapo sawa tunahaki ya kupiga kelele lakini kwa hili sidhani kama tunawatendea haki.

Amani.
 
Na yule mzungu wa Gurumeti ambae kipindi fulani alitaka kujenga airstrip bila ya ruhusa jee yeye na nia gani na nchi hii? Na jee ni Mwinyi ndio alimpa hilo eneo ambalo ni sehemu ya mapito ya wanyama?

Angalieni pande zote zote wakati wa kuzungumzia haya mambo
 
Mzungu wa Grumeti ameishasemwa sana.Hususan kutokana na kitendo chake cha kuwazuia wa-Hadzabe kuwinda katika eneo alilomilikishwa. Lakini hata siku moja hajawahi kushtakiwa kwa uwindaji wa ki-Rambo usiongalia sustainability ya eneo lake.

Tunajitahidi kuangalia pande zote na kutomuonea haya yeyote bila kujali rangi, dini au nguo alizovaa! Tunapokosea tusahihisheni kwa kutoa mifano inayoendana na hoja. Kama kuna mahali mwingine anafanya uwindaji wa aina hii, mwanikeni hapa bila kujali dini, jinsia, rangi yake nae tutamchambua.

Amandla........
 
Mbona mnazunguka mbuyu tu? semeni tatizo nini. wengine mnakereka na mavazi tu basi, wengine muonekano wao hao jamaa ni militaristic, wengine nchi imeuzwa.

Mnahangaika tu mnashindwa kusema ukweli wenu kuwa tatizo hao ni waislamu na waarabu hivyo hawatakiwi wanaotakiwa hapo ni wazungu tu kwa sababu hao ni wagalatia wenzenu.

Kama mpo objective mngetuletea na picha za wazungu wanaowinda huko, kwani wawindani ni waarabu tu? Na je kuwinda ni ujangiri? Kwani hawana vibali vya uwindaji hao? Na utakuta watia saini wa vibali ndio ninyi wagalatia.

Njoo na takwimu kuna makampuni mangapi ya uwindaji huko na wamiliki ni akina nani ndio mtaona mnavyoongozwa na chuki

Udini tu hamna lolote!

Of all people hata wewe Mkandara?

Haya tuwaone hao wenye haki ya uwindaji basi

Giraffe.jpg

http://i249.photobucket.com/albums/gg209/mbuyanzi
/Simba4.jpg

Lion.jpg

Hunting3.jpg

Cheetah.jpg

Wilderbeast.jpg

Gazelle.jpg

Hunting3.jpg
mkuu hapa tofauti utaiona,kama ukiangalia vizuri utaona hao watu weusi hapo,hao ni waangalizi na track kwa ajili yta kuangalia jamaa wasiwinde wanyama wadogo au wasiue mnyama ambaye hawajamlipia leseni,pia hawa wawindaji wanawinda kwa kipindi maalum tu,nafikiri mwezi wa sita mpaka december,baada ya hapo hatakiwi kuonekana tena mbugani mpaka baada ya miezi sita,na pia kipindi cha uwindishaji hao wote unawaona hapo,kila mmoja kalipa kodi na kukata leseni ya mnyama aliekuja kumwinda licha ya yule mkodishaji wa block kulipia,katika mtiririko huo unaona ni kiasi gani taifa linaingiza pesa,sasa tofauti wanachofanya hawa waarabu ni uwindaji holela na bila kufuata sheria yoyote ya uwindaji,kwani madai yao block wameinunua,at the end ndio maana wanawakimbiza wale wamasai kwasababu ukatili wanaoufanya huko porini wanyama wanakimbia na kuhama na wao wanataka waongezewe eneo zaidi la kuwindisha hata iwavyo vyote,na sidhani kama kuna mwangalizi yeyote unayemuona katika hilo kundi lao.
 
Hii hali ilivyo sasa mbugani waarabu kuweka makazi yao namna hii , Kweli Mmarekani ataweza kuja mbugani na hali ikiwa hivi jamani hii mbona kubwa kuliko ni kwanini tujipotezee mapesa ya wazungu wakati wazungu toka enzi na enzi ndio ambao wamekuwa wakitusaidia,
sisi hata kama hatwendi mbugani kuangalia maliasili zetu ni uwezo tu ila tunazipenda sana tena sana ningependa Mbuga ziheshimiwe waachwe wanyama pekeyao wasiletewe usumbufu.
Lakini kwanini nyinyi tu jamani mbona Kenya haya mambo hayapo? are we stupid? %%%%#####**** griiiiiiiiiiiiiii

Ni roliondo hukoooo nini maaana nasikia hawa jamaaaa huwa wanakuja na kufanya mambo yao usipime kule ni kama kanchi fulani na wana Run way yao madege hushuka kule, muulizeni mwinyi na kina ndolanga walipewa nini mpaka waka gawa hiyo Aridhi??

Mzungu wa Grumeti ameishasemwa sana.Hususan kutokana na kitendo chake cha kuwazuia wa-Hadzabe kuwinda katika eneo alilomilikishwa. Lakini hata siku moja hajawahi kushtakiwa kwa uwindaji wa ki-Rambo usiongalia sustainability ya eneo lake.

Tunajitahidi kuangalia pande zote na kutomuonea haya yeyote bila kujali rangi, dini au nguo alizovaa! Tunapokosea tusahihisheni kwa kutoa mifano inayoendana na hoja. Kama kuna mahali mwingine anafanya uwindaji wa aina hii, mwanikeni hapa bila kujali dini, jinsia, rangi yake nae tutamchambua.

Amandla........

Fundi,

Unajichanganya vibaya sana. Unawa hukumu hao waarabu kuwa wanawinda "kirambo" Sasa kutembea na bastola ishakuwa uharamia!. Wangapi Tanzana wanatembea na bastola as long as taratibu za kumiliki silaha zimefuatwa tatizo lipo wapi?

Kama ni mavazi ndio uwindaji wa kirambo unataka kuwapangia hata cha kuvaa?

Tatizo lako wewe ni mdini SANA na michango yako humu inathibitisha hivyo. Ndio maana unauliza eti Eddie na uislamu wapi na wapi, nani kakwambia kama mimi muislamu? Kwanini ukejeli jina na kuli nasibisha na dini.

Tuambie sheria gani imevunjwa kwa hao jamaa kubeba bastola? Sheria gani imevunjwa kwa hao jamaa kuwinda kirambo rambo? yaani kubeba silaha nzito kama riffle iwe sawa kosa liwe kubeba bastola!

Acha kuzungusha sema kinacho kukera.
 
Back
Top Bottom