Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake..
Hawa wasomi wamewasaidiaje hawa watanzania masikini ambao hawakwenda shule?
Mkuu ritz, msomi yeyote hawezi kumsaidia au kuinua kipato cha mtanzania maskini bila serikali kuwa na mipango mahsusi ya kuwezesha wasomi kutumia utaalamu wao kwa manufaa ya hao unaowaita watanzania masikini. labda kama unaongelea msomi kuchukua pesa zake mfukoni Na kumpa masikini kama 'mtoto wa mkulima' anavyofanya. Na hiyo si kumsaidia au kumwezesha masikini bali ni kumfanya awe omba omba milele!