Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

Ritz, heshima mkuu..

Ningependa kuchangia thread yako NZURI, lakini kabla ya kufanya hivyo, ningependa kujua definition yako ya msomi/wasomi? Na je, wewe ni miongoni mwao(wasomi)?

Mkuu hippocratessocrates,

Tunapoengelea "usomi" wa utawala unaitaji elimu ya chuo kikuu ili kuweza kufahamu sheria za mikataba na mambo ya utawala, Mkuu wewe ni msomi kwenye fani yako ya udaktari huwezi kuwa mtaalamu wa tiba bila kuwa msomi wa fani hiyo.

Kuna usomi wa mazingira ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuyamiliki mazingira yanayomzunguka kwa ajili ya maendeleo yake na jamii yake kwa ujumla.

Mkuu ukiangalia mikataba inayoingiwa na wanasheria wetu ambayo ni wasomi inasikitisha sana mfano Chenge alivyokuwa mwanasheria wa serikali kapewa hiyo nafasi kutokana na usomi wake.
 
Last edited by a moderator:
ijulikane wazi kuwa wanasiasa wamekuwa na nguvu ya kisera kuliko wataalam na ndio maana unaona hata watendaji wakuu wa wizara na hata majaji wanakosa nafasi ya kuamua uamuzi huru hata katika mambo yaliyowazi mpaka wamuulize mwanasiasa ambaye huwa ni kilaza wa kutupwa ili aweke baraka zake hapo ndipo maamuzi hutoka ya kimihemuko zaidi kikada na output inakuwa ovyo sasa initiates za msomi hapo huwa tayari zimeharibika
 
Mkuu hippocratessocrates,

Tunapoengelea "usomi" wa utawala unaitaji elimu ya chuo kikuu ili kuweza kufahamu sheria za mikataba na mambo ya utawala, Mkuu wewe ni msomi kwenye fani yako ya udaktari huwezi kuwa mtaalamu wa tiba bila kuwa msomi wa fani hiyo.

Kuna usomi wa mazingira ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuyamiliki mazingira yanayomzunguka kwa ajili ya maendeleo yake na jamii yake kwa ujumla.

Mkuu ukiangalia mikataba inayoingiwa na wanasheria wetu ambayo ni wasomi inasikitisha sana mfano Chenge alivyokuwa mwanasheria wa serikali kapewa hiyo nafasi kutokana na usomi wake.

Okay, kumbe linaloongelewa hapa ni usomi wa utawala
"administration"!!

Nadhani mkuu, katika hili tungeweza kuangalia UWEZO wa Taifa, MAHITAJI ya Taifa na VIPAUMBELE vya Taifa.

1. UWEZO:
Sidhani kuna haja ya kuongelea katika hili, kwamba tuna uwezo mkubwa hasa kwa maana ya vyanzo asilia(Natural Resources) vilivyopo nchini kwetu, na kuna hili la wataalamu "wasomi" wa fani/kada husika ambao nao pia si haba.

2. MAHITAJI:
Kama Taifa tuna mahitaji mengi (kila sekta/wizara/n.k), haya yote ni muhimu kufanyika, kwamba yatekelezwe kulingana na hoja namba moja hapo juu(UWEZO).

3.VIPAUMBELE:
Nionavyo mimi, hapa ndiyo kwenye shida...mfano tinaweza kuwa na vitu D, E, F na G. Lakini kwa kuangalia uwezo ulionao/tulionao na kuona huwezi kufanya yote..Ndipo pale unaweza kuchagua kufanya jambo E, ili kwamba kwa lenyewe lifanikishe jambo F na G. ..yaani;

Badala ya kuepuka KUTIBU magonjwa(yanayotomana na kujikinga), kuepusha watu kuwa wategemezi na KUTOA MISAADA kila siku nk...unaamua kuwekeza katika ELIMU, ukitegemea wanafunzi wanapohitimu(na kukiwa na channel za ajira, au ukimwezesha kwa kiasi kidogo sana) ataweza ku-excel kwa kutumia elimu aliyopata kujikinga na magonjwa, kujiajiri.n.k

Sasa nadhani hata kama TAIFA ZIMA tukiwa ni "WASOMI" lakini hakuna kuweka vipaumbele vya msingi hatutafika popote..we seriously need to priotize our priorities.
 
Wasomi nao kama wanasiasa siku hizi, wamesahau wajibu wao, wameambukizwa na wanasiasa roho ya umimi, wamekalia kuandika madokezo tu!. Wewe tembelea tu taasisi za serikali utawakuta maafisa wakiulizana, "hivi lile dokezo limeshasainiwa tayari?, njaa kali!. Hawaulizani,hivi hili tatizo tulimalize vipi?
 
Hello guys,Hivi karibuni viongozi kadhaa wa serikali wamesikika wakiongelea kuhusu ajira kwa vijana,baadhi yao ni Lowasa,sita na Membe.Kweli hawa watu wanania ya kweli ya kuwaendeleza vijana au wanakamilisha ule msemo kwamba SHETANI AKIZEEKA HUJIFANYA MALAIKA?

Think grey not Green

Hao wote uliowataja wana ndoto za u-rais, wameona waanze kubwabwaja mapema ili waonekane wanawajali vijana.
 
Mimi ni mmoja wao. Yes, nina masters (MSCIS) in Information Technology. Niliporudi Tanzania miaka kama 10 iliyopita nilijaribu kuomba kazi wizara ya mawasiliano na nikapata ila bahati nzuri nilipata offer nyingine ya NGO ambayo inalipia almost two times and half kwa hiyo nikaenda kwa NGO. Nilihamua hivyo kwa sababu serikali yetu hii is a joke haizingatii usomi wa mtu.

Utakuta wewe umesoma shinda bosi wako lakini yeye ndo ana mamlaka zaidi shinda wewe uliyesoma na kujua zaidi yake. Mfano ulio hai; si unaona wewe Ridhiwani Kikwete, huna chochote cha maana kwani hata waliosoma nawe wanakucheka, ila Sitashangaa kama wewe una mamlaka zaidi ya wakili mkuu wa serikali.

Kwa hiyo inakuwa vigumu kwa wasomi kuja nchini kuchangia maendeleo kutokana na ujinga kama huu. Hakuna nchi inayoendeshwa kihuni kimakusudi ikawa na maendeleo, uongo?
 
Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake..

Hawa wasomi wamewasaidiaje hawa watanzania masikini ambao hawakwenda shule?

Kwani huko shule huwa wanafundishwa kuondoa umaskini? Wanafundishwa jinsi ya kupata pesa? Au huwa wanafundishwa jinsi ya kujiajiri??? Jibu ni hapana...... Huwa wanafundishwa si namna ya kupata pesa bali kuzitunza pesa (hawaambiwi zimepatikana vipi) na pia huwa wanaandaliwa kuwa waajiriwa bora!! Sasa jiulize ukiajiriwa Tanzania utalipwa mshahara wa shilingi ngapi? Si ni vijihela vya kulipia bili za mwezi na kununua chakula tu?? Sasa huo umaskini utauondoaje maana UTAJIRI NI MABAKI YA MATUMIZI KATIKA ZIADA. Na wewe unalipwa kiasi kidogo ambacho hakitoshi kutoa ziada......Tafakari. Kwa hiyo kusoma Tanzania hakuondoi umaskini bali huondoa ujinga tu.
 
Waulize Magamba wenzio wanaogawana rasimali za taifa na kuuza hadi wanyama hai,. taifa litaendeleaje? Tanzania hata kama una taaluma kubwa na ya kipekee kama hupo kwenye mfumo wa kifisadi na magamba nani atakusikiliza? nenda botswana, namibia, south africa wamejaa wataalamu wa kitanzania nyumbani hawapewi! umuhimu! linganisha mshahara wa daktari, mwalimu au mhandisi ambao ni wataalamu na wabunge, mawaziri ambao hawana utaalamu wowote zaidi ya bla blaa za kisiasa utapata jibu la swali lako!
 
Hao wote uliowataja wana ndoto za u-rais, wameona waanze kubwabwaja mapema ili waonekane wanawajali vijana.

Propaganda hii ya kujifanya wanawajali vijana alianzisha Kikwete mnano 2005 alipojifanya yeye ni mvaa kata kun.du (alisikika akihutubia) kuwa vijana ni taifa la kesho na kuwafagilia bongo fleva artists. Nao wakamuona kuwa ni mtu poa na kumfagilia kwenye campaign zake mbele ya umma. Jamaa akapita na ile ahadi yake ya kusaidia vijana iko wapi? Mbona hali ni ile ile na vijana wengi wamekata tamaa na kujikita kwenye ubwiaji unga bcs there's nothing for them. Kwa kweli katiba mpya inabidi iwe na kipengele cha kuwashitaki maraisi wezi na mawaziri wake pia. Yule atakayebainika aliiba mali ya umma lazima anyongwe.
 
Mkuu hippocratessocrates,

Tunapoengelea "usomi" wa utawala unaitaji elimu ya chuo kikuu ili kuweza kufahamu sheria za mikataba na mambo ya utawala, Mkuu wewe ni msomi kwenye fani yako ya udaktari huwezi kuwa mtaalamu wa tiba bila kuwa msomi wa fani hiyo.

Kuna usomi wa mazingira ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuyamiliki mazingira yanayomzunguka kwa ajili ya maendeleo yake na jamii yake kwa ujumla.

Mkuu ukiangalia mikataba inayoingiwa na wanasheria wetu ambayo ni wasomi inasikitisha sana mfano Chenge alivyokuwa mwanasheria wa serikali kapewa hiyo nafasi kutokana na usomi wake.
wewe unafikiri mikataba wanayoingia hawajui? wanajua sana wanachosaini ila kwa ufisadi na rushwa wanapofushwa macho na kusaini liwalo na liwe, Chenge amesoma Harvard University miongoni mwa vyuo vikuu vinavoheshimika sana duniani anachofanya au alichofanya ni kuwa aliongozwa na rushwa na ufisadi ndio maana walimuwekea pesa huko kwenye visiwa vya Jersey!
 
WASOMI TUNAO WENGI ILA HAWATUMII AKILI ZAO NA TAALUMA ZAO KWA MAENDELEO YA TAIFA ILA WAPO KWA MASLAHI YA CCM, MFANO MUKANDARA, KIKULA, MLACHA NA WENGINE WENGI, NA WACHACHE WAZALENDO WANAISHIA KUUWAWA AU KUKANDAMIZWA NA SERIKALI MFANO Dr Kitila Mkumbo, Prof Shivji, Sungusia, na wengine wengi, ila CCMna mapupet wao wote their days are numbered.

Mkuu usikimbilie kuwalaumu wasomi wa Tanzania. Hebu sikia hii:
Kuna msomi mmoja alimaliza mwaka 2006 digrii ya pili ya Uchumi kutoka chuo cha Oxford Uingereza (ambako alikuwa akijisomesha kwa gharama zake). Akarudi Tanzania ili kuisaidia nchi yake kuleta maendeleo. Akaomba kazi serikalini akapata lakini mshahara akaambiwa atalipwa shilingi laki sita (kabla ya kodi) na cheo chake atakuwa sawa na mwenye digrii ya kwanza. Jiulize, alitumia shilingi milioni 40 ili kupata eliimu bora kabisa sasa kwa mshahara wa laki sita (hata kama baada ya kodi) hela yake aliyotumia kujisomesha atairudisha baada ya kulipwa mshahara wa miezi mingapi?
 
wewe unafikiri mikataba wanayoingia hawajui? wanajua sana wanachosaini ila kwa ufisadi na rushwa wanapofushwa macho na kusaini liwalo na liwe, Chenge amesoma Harvard University miongoni mwa vyuo vikuu vinavoheshimika sana duniani anachofanya au alichofanya ni kuwa aliongozwa na rushwa na ufisadi ndio maana walimuwekea pesa huko kwenye visiwa vya Jersey!

Hapa tunajadili mustakabali wa nchi yetu wasomi wetu wamelisaidiaje taifa letu...jenga hoja tufanyaje.
 
Zifuatazo ni baadhi ya sababu:

-Hakuna utashi wa kisiasa kuruhusu wasomi kuwa washauri wa namna ya kuendesha nchi. Wanasiasa wamekuwa waamuzi wa kila kitu hata kama hawana utaalamu.

-Elimu ya Tanzania imepotoshwa; kwa wengi elimu inamaanisha mshahara na hili ndilo limekuwa lengo kuu la watu kusoma. Kwa maana nyingine, mtu anasoma kwa ajili yake si kwa ajili ya Taifa, akishapata kazi hafikirii chochote kuhusu Taifa.

-Nafasi za kitaalamu hupewa watu wasio na utaalamu, kigezo ni kufahamiana na 'wakubwa'!!
 
Kwani huko shule huwa wanafundishwa kuondoa umaskini? Wanafundishwa jinsi ya kupata pesa? Au huwa wanafundishwa jinsi ya kujiajiri??? Jibu ni hapana...... Huwa wanafundishwa si namna ya kupata pesa bali kuzitunza pesa (hawaambiwi zimepatikana vipi) na pia huwa wanaandaliwa kuwa waajiriwa bora!! Sasa jiulize ukiajiriwa Tanzania utalipwa mshahara wa shilingi ngapi? Si ni vijihela vya kulipia bili za mwezi na kununua chakula tu?? Sasa huo umaskini utauondoaje maana UTAJIRI NI MABAKI YA MATUMIZI KATIKA ZIADA. Na wewe unalipwa kiasi kidogo ambacho hakitoshi kutoa ziada......Tafakari. Kwa hiyo kusoma Tanzania hakuondoi umaskini bali huondoa ujinga tu.

Taifa lolote lenye wasomi wanaojitambua siku zote wasomi wake huwa wanaacha athari kutokana na usomi wao kwa wale ambao hawakusoma.
 
Hapa tunajadili mustakabali wa nchi yetu wasomi wetu wamelisaidiaje taifa letu...jenga hoja tufanyaje.

ok shida yako ni hiyo? fine let politics remains as politics and professinalism remains as professionalism, never allows one to influence or guide the other! that is possible ONLY if we get rid of CCM!
 
Wanabodi.

Kila siku najiuliza sipati jibu sahaihi kuhusu wasomi wetu wa Tanzania..

Kwa mujibu wa data za World Bank na IMF Tanzania ipo kwenye kundi la nchi 20 maskini wa kutupwa duniani.

Baadhi ya nchi zimekuwa masikini kutokana kuwa na vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe kama vile Rwanda, DRC, Burundi, Somalia..

Hawa wasomi wetu kila kukicha wanajitapa na kijisifia na wengine wapo humu JF kuwa ni wasomi..

Ni kipi cha maana hawa wasomi wetu wa Tanzania wamelisadia taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini?

Kama kuna wasomi tunaomba mnijibu ni kipi mlichoifanyia taifa letu la Tanzania..
Nawakilisha...

Thread yako inaonesha ni ya tarehe 29 October 2012 saa nane na dakika 13 mchana, lakini leo ni tarehe 28 October 2012, wewe utakuwa umeiandika hii thread ukiwa AUSTRALIA???
 
Propaganda hii ya kujifanya wanawajali vijana alianzisha Kikwete mnano 2005 alipojifanya yeye ni mvaa kata kun.du (alisikika akihutubia) kuwa vijana ni taifa la kesho na kuwafagilia bongo fleva artists. Nao wakamuona kuwa ni mtu poa na kumfagilia kwenye campaign zake mbele ya umma. Jamaa akapita na ile ahadi yake ya kusaidia vijana iko wapi? Mbona hali ni ile ile na vijana wengi wamekata tamaa na kujikita kwenye ubwiaji unga bcs there's nothing for them. Kwa kweli katiba mpya inabidi iwe na kipengele cha kuwashitaki maraisi wezi na mawaziri wake pia. Yule atakayebainika aliiba mali ya umma lazima anyongwe.

KIKWETE amewasaidia sana vijana!!! Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa ungewaona Bungeni vijana wakitukana serikali na viongozi wake? Thubutu...... Wangeishia kuwa vibarua tu. lakini leo vijana wamepewa madaraka makubwa sana hata humu JF utawasikia kiongozi wa nchi wakimwita "dhaifu" na majina mengi tu. Zamani Bungeni ukioneshwa kwenye picha (sio television kama ilivyo sasa) utaona ni vichwa vyeupeeeee na watu wanasinzia ovyo. Lakini sasa utaona vijana wamesimama wakirusha mikono kuponda tu wakisahau kuwa bila KIKWETE kulegeza misimamo kuhusu vijana wasingalikuwamo bungeni. Kumbukeni mlikotoka jamani. Kazi ya ubunge zamani ilikuwa inaonekana ni ya watu waliokwisha staafu lakini leo kazi ya ubunge inahitaji mtu mwenye nguvu ambaye ni kijana.
 
Hii ni thread NZURI inalinganishwa na thread yangu ambayo imefutwa bila sababu '' je wahandisi (mechanical engineers) wetu kutoka UDSM wanasaidiaje wiwanda vyetu?''

JIBU NI KWAMBA WASOMI WATAKUWA EFFECTIVE KUSAIDIA NCHI YAO ENDAPO WANASIASA WATAKUWA WAMEFANYA HOME WORK ZAO VIZURI. NA HII NI KWAMBA BADO HAWAJAMALIZA HOME WORK ZAO, KWA HIYO HATA MICHANGO YA WASOMI SI RAHISI KUONEKANA MPAKA HAPO BAADAE!

SWALA NI KWAMBA NI LINI HAWA WANASIASA WATAMALIZA HOME WORK ZAO!!!
 
Wanabodi.

Kila siku najiuliza sipati jibu sahaihi kuhusu wasomi wetu wa Tanzania..

Kwa mujibu wa data za World Bank na IMF Tanzania ipo kwenye kundi la nchi 20 maskini wa kutupwa duniani.

Baadhi ya nchi zimekuwa masikini kutokana kuwa na vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe kama vile Rwanda, DRC, Burundi, Somalia..

Hawa wasomi wetu kila kukicha wanajitapa na kijisifia na wengine wapo humu JF kuwa ni wasomi..

Ni kipi cha maana hawa wasomi wetu wa Tanzania wamelisadia taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini?

Kama kuna wasomi tunaomba mnijibu ni kipi mlichoifanyia taifa letu la Tanzania..
Nawakilisha...

Mkuu umeleta mada nzuri ambayo haina hata mjadala mrefu kwani jibu lake liko wazi.
Tatizo hapa ni serikali ambayo haithamini wataalamu wake na hivyo kutokuwa na mikakati ya kuwatumia kwa ajili ya Maendeleo ya nchi.

Hapa Tanzania wanasiasa wamegeuka ndio wataalamu. Wataalamu hawapewi kazi zao za kitaalamu.

Nchi yoyote ile ili wasomi wake wawe na mchango unaoonekana na jamii ni lazima serikali iliyopo madarakani iwe na sera za wazi zinazoshirikisha wasomi na wataalamu wake kwenye kutekeleza mipango mikubwa ya Maendeleo ya nchi.

Ni lazima serikali iwe na mikakati ya kuandaa na kutumia wasomi na wataalamu wake kwenye miradi mikubwa ya nchi badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje.

Tuchukue tu mfano mdogo na wa wazi. serikali tangu uhuru inajua nchi hii tuna dhahabu na madini mengine lukuki. lakini serikali haiandai wananchi wake wawe na uwezo wa kutafiti, kuchinba na ku-process hayo madini.

Matokeo yake wanaleta watu kutoka nje kana kwamba kilikuwa ni kitu cha dharura. Badala ya nchi na wananchi wake kufaidika, nchi inafaidiwa na washenzi. Nchi yetu na sisi wananchi wenyewe tunaendelea kuwa masikini. Halafu hawa washenzi wanatudharau na kutuona watanzania wote ni wajinga!

Kutothaminiwa na kudharauliwa kwa wasomi wa nchi hii kunajionyesha dhahiri. Wewe mwenyewe angalia hata mishahara wanayopata wataalamu wetu, utasikitika. Angalia madaktari wanavyonyanyaswa, angalia ma-injinia, angalia watumishi wengine wa serikali-pasipo na malalamiko ni pale ambapo watumishi wanashirikisna na wanasiasa kutuibia.

On the contrary, nenda TRA, Benki kuu nk; mshahara anaopata hata mtu anaepanga mafaili utadhani wao hawako Tanzania.

Wasomi hawathaminiwi wao na kazi zao, mfano pia angalia ukienda library, utakuta tafiti nyingi sana za hawa wasomi zimezikwa huko na Hakuna mpango wa kuzitumia kwa manufaa ya nchi.

Wataalamu na wasomi katika nchi hii Wamekata tamaa. Baadhi yao ndio unawashuhudia wameamua kutokomea nje ya nchi, wengine kuacha taaluma zao na kujiingiza kwenye biashara, na wengine ndio Kama hao maprofesa na madaktari walioamua kuacha taaluma zao na kujiunga na chama chako cha CCM ili wapate ulaji! Hata wewe Nadhani uko huko kwa sababu umehakikishiwa ulaji.

Halafu nikuambie Mkuu Ritz, hawa wataalamu si kwamba hawana uwezo, ni wataalamu wazuri na nchi wanazolowea wanakuwa asset kubwa sana. Mfano kwa mtu aliyewahi kufika Malaysia zile Barabara unaziziona pale miongoni mwa Architect wakuu wa nchi ile ni watanzania. Nenda kama Botswana utawakuta ma-injinia na madaktari wanafanya kazi ambazo hapa mnawapa wazungu.

Nenda na baadhi ya nchi zingine za ulaya na marekani, utakuta wataalamu wa kitanzania wanaoaminika na kutegemewa. Huko wanasiasa wanathamini wataalamu.

Ndugu yangu Ritz, mchango wa wasomi na wataalam wetu utaonekana pale tu nchi hii itakapopata serikali inayosimamia maslahi ya wananchi.
 
Back
Top Bottom