Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake..

Hawa wasomi wamewasaidiaje hawa watanzania masikini ambao hawakwenda shule?

Mkuu ritz, msomi yeyote hawezi kumsaidia au kuinua kipato cha mtanzania maskini bila serikali kuwa na mipango mahsusi ya kuwezesha wasomi kutumia utaalamu wao kwa manufaa ya hao unaowaita watanzania masikini. labda kama unaongelea msomi kuchukua pesa zake mfukoni Na kumpa masikini kama 'mtoto wa mkulima' anavyofanya. Na hiyo si kumsaidia au kumwezesha masikini bali ni kumfanya awe omba omba milele!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu hippocratessocrates,

Tunapoengelea "usomi" wa utawala unaitaji elimu ya chuo kikuu ili kuweza kufahamu sheria za mikataba na mambo ya utawala, Mkuu wewe ni msomi kwenye fani yako ya udaktari huwezi kuwa mtaalamu wa tiba bila kuwa msomi wa fani hiyo.

Kuna usomi wa mazingira ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuyamiliki mazingira yanayomzunguka kwa ajili ya maendeleo yake na jamii yake kwa ujumla.

Mkuu ukiangalia mikataba inayoingiwa na wanasheria wetu ambayo ni wasomi inasikitisha sana mfano Chenge alivyokuwa mwanasheria wa serikali kapewa hiyo nafasi kutokana na usomi wake.

Mkuu ritz, nchi hii wasomi hawapewi mamlaka ya kitaalamu kwa kuzingatia upeo wao kitaaluma. Wanapewa kwa kuzingatia uwezo wao wa kuweza kutumika na wanasiasa. Chenge alitumika tu kama rubber stamp. kazi ameifanya vizuri na kajipatia vijisenti vyake. Ila kaonja asali, amenogewa na sasa yuko kwenye harakati za kuchonga mzinga!
 
Last edited by a moderator:
Acheni lawama kwa "wasomi." Kabla ya kumnyooshea kidole "msomi" hebu jiulize: "NIMEIFANYIA NINI NCHI YANGU kuikwamua ktk au kuikandamiza zaidi ktk lindi la umasikini?"

Kwani waliomrejesha Kikwete na CCM yake madarakani 2010 ni WASOMI pekee? Tanzania inavuna inachopanda: bangi huzaa bangi,sio maboga. Ukichagua kiongozi kwa vile kakuhonga t-shirt au pishi ya sembe,au kwa vile ni handsome,haya ndo matokeo yake.
 
Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake..

Hawa wasomi wamewasaidiaje hawa watanzania masikini ambao hawakwenda shule?

ritz swali lako nazani inabidi wakristo ndo wakujibu maana hao kilasiku hawaishi kujisifu wao ndo wasomi, jamani wakristo mjibuni ritz mi elimu yangu ya madrasa.
 
KIKWETE amewasaidia sana vijana!!! Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa ungewaona Bungeni vijana wakitukana serikali na viongozi wake? Thubutu....
Sikubaliani nawe moja kwa moja. Hawa wabunge vijana sio kwamba Kikwete kawachagua yeye ila wamechaguliwa na watu/wananchi na kingine ni kwamba wengi wametoka vyama vya upinzani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuchaguliwa na wananchi, na kusimikwa na rais ili mradi tu anatembea na dada yako ama kwa faida yake yeye mwenyewe (rais).

Hili suala la vijana wabunge kumtukana waziri fulani ama kiongozi fulani ni dhaifu si kitu ambacho Kikwete ameleta au kulegeza. Toka mwanzoni mwa miaka ya tisini wakati tumeleta mfumo wa vyama vingi pia tukakubali kuwa na kitu kiitwacho freedom of speech, maana kwamba mtu una ruhusa ya kuongea yako ya moyoni kwani ni maoni yako.

Hii kitu si Kikwete aliyeleta, yeye aliikuta hivyo hana mamlaka ya kukataza watu kuzungumza yanayowasibu, au mwenzetu ulilala? Kulala kwa wabunge bungeni si hoja, mbona Wasira mpaka leo bado analala tu na anajisahau kabisa mpaka anajamba na wabunge wenzake humkimbia kwani hawakai naye tena.
 
Ni zaidi ya miaka 50 tangu tupate uhuru mwaka 1961 ugumu wa maisha unazidi kuongezeka licha ya rasilimali lukuki tulizojaaliwa lkn wanaofaidi ni wachache na kupelekea utabaka miongoni mwa watz.je wasomi wetu wanaliona hili,upi mchango wao kujenga taifa?
 
Umasikini wa mtanzania unatokana kipato chake.....Hawa wasomi wamewasaidiaje hawa watanzania masikini ambao hawakwenda shule?

Katika mfumo ambao Mtaalamu ambaye pia ndiye Mtendaji akiwa chini ya Mtu ambaye qualification yake ni kuchaguliwa tu kisiasa unatarajia akusaidieje wakati maamuzi yake hata yawe mazuri na ya kitaalamu namna gani lazima yakubaliwe na aliye juu yake?

Mfano mdogo tu tunao Wakurugenzi wa Wilaya/Manispaa ambaye ni Wasomi wazuri. Kwa sheria zetu Wakurugenzi wako chini ya Madiwani. Madiwani wanaweza kuamua kumfukuza kazi mkurugenzi au kumuharasi wapendavyo kama halindi maslahi na kusikiliza matakwa yao.

Ukijifanya unasimamia Taalumu na Haki basi Ukurugenzi si saizi yako. Labda ualimu vyuoni na mashuleni. Kama Ritz wewe ndiyo msomi aliyepewa hii nafasi utafanyaje? Mbaya zaidi unaamrishwa na kuelekezwa na mto asiye na elimu yoyote.

Nimeshangaa kubaini ukweli kuwa hata Mabalaza ya Manispaa na Majiji yamejaa Madiwani wa Dalasa la Saba. Hili nilidhani ni tatizo la Wilaya za Pembezoni kama kwetu huku.

Ukiwa na mtu hajui hata kuandika jina lake vizuri lakini huyo huyo ndiye anamtawala Msomi na Mtendaji usitegemee Utaalamu ukupe tija!
 
Wasomi wa Watz wamefungwa kufuli na wanasiasa. Kwa hiyo wamepuuzwa na hawasikilizi na wanasiasa ndo maana nchi yetu inaendelea kutambaa badala ya kutembea. Wasomi wametoa ushauri mwingi sana wa kitaalamu lakini wanasiasa hawasikilizi. Kumbuka wenye kufanya maamuzi katika nchi hii ni wanasiasa tofauti na nchi kama Marekani na nchi nyingi za Ulaya ambapo decision makers ni think tanks za nchi na wala si wanasiasa. Kumbuka maamuzi mengi mengi ya wanasiasa hasa CCM yanalenga kushibisha matumbo yao za familia zao badala ya kuzingatia maslahi ya nchi. Ndo maana si jambo la kushangaza siku hizi kuona wabunge wa CCM wanapitisha muswada bila hata ya kuusoma kwa sababu wao bungeni ili kupata posho wala si kuwahudumia wananchi. Hilo ndo tatizo ndugu yangu Ritz
Serikalini ndio kumejaa wasomi na ndio watendaji wanapanga mipango ya uchumi baada ya kukusanya kodi zetu, labda wewe tuambie na mwingine mwenye jukumu la kuitoa Tanzania kwenye dimbwi la umasikini?
 
KIKWETE amewasaidia sana vijana!!! Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa ungewaona Bungeni vijana wakitukana serikali na viongozi wake? Thubutu...... Wangeishia kuwa vibarua tu. lakini leo vijana wamepewa madaraka makubwa sana hata humu JF utawasikia kiongozi wa nchi wakimwita "dhaifu" na majina mengi tu. Zamani Bungeni ukioneshwa kwenye picha (sio television kama ilivyo sasa) utaona ni vichwa vyeupeeeee na watu wanasinzia ovyo. Lakini sasa utaona vijana wamesimama wakirusha mikono kuponda tu wakisahau kuwa bila KIKWETE kulegeza misimamo kuhusu vijana wasingalikuwamo bungeni. Kumbukeni mlikotoka jamani. Kazi ya ubunge zamani ilikuwa inaonekana ni ya watu waliokwisha staafu lakini leo kazi ya ubunge inahitaji mtu mwenye nguvu ambaye ni kijana.

Acha hizo stori za kusimuliwa vijweni,hakuna utawala umetoa madaraka makubwa kwa vijana wasomi kama wa Mwl. Nyerere. haya, majina karibu yote makubwa unayosikia wamepewa uongozi wa kisiasa,serikalini,mashirika ya umma na taasisi za serikali wakiwa vijana wadogo baada ya kuhitimu vyuo.
 
Sikubaliani nawe moja kwa moja. Hawa wabunge vijana sio kwamba Kikwete kawachagua yeye ila wamechaguliwa na watu/wananchi na kingine ni kwamba wengi wametoka vyama vya upinzani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuchaguliwa na wananchi, na kusimikwa na rais ili mradi tu anatembea na dada yako ama kwa faida yake yeye mwenyewe (rais).

Hili suala la vijana wabunge kumtukana waziri fulani ama kiongozi fulani ni dhaifu si kitu ambacho Kikwete ameleta au kulegeza. Toka mwanzoni mwa miaka ya tisini wakati tumeleta mfumo wa vyama vingi pia tukakubali kuwa na kitu kiitwacho freedom of speech, maana kwamba mtu una ruhusa ya kuongea yako ya moyoni kwani ni maoni yako.

Hii kitu si Kikwete aliyeleta, yeye aliikuta hivyo hana mamlaka ya kukataza watu kuzungumza yanayowasibu, au mwenzetu ulilala? Kulala kwa wabunge bungeni si hoja, mbona Wasira mpaka leo bado analala tu na anajisahau kabisa mpaka anajamba na wabunge wenzake humkimbia kwani hawakai naye tena.

teh teh, anajamba? Duh
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu sasa jinsi upeo wa wa Tanzania unavyo badilika, nilicho gundua ni kwamba safari hii Wa TZ wamebadilika sana kiuelewa wamekuwa wepesi wa kupokea mambo na kuchambua na kujua ni lipi liko sahihi katika muda sahihi, Kwa maana hiyo ni kwamba nimegundua kwamba wa TZ wa sasa wamekua wenye maono halisi wameacha kutegemea nguvu zisizoonekana (magic Power) kutatua matatizo yao, na sasa wameanza kutumia Akili zao wenyewe kuchambua mambo na kuchukua hatua stahiki bila kumuogopa mtu Yeyote iwe ni kwa Ubabe wake au Pesa Zake,

Kwa kuliona hiolo sasa nadhani ni muda sahihi kwa wasomi wetu "WASIO WABINAFSI" kutumia mda huu ambao uelewa wa waTZ upo juu ukilinganisha na kipindi cha nyuma Kusambaza elimu ya uraia zaidi ili watu wengi zaidi wanaoonekana kuwa tayari kuipokea elimu waipate na kutusaidia kulikombqa taifa hili ambalo tunashuhudia "ASALI NA MAZIWA YAKE" vikisafirishwa kwenda ng'ambo na sisi tukibakiwa na masega na ng'ombe waliokondeana....CHONDE CHONDE wasomi wetu tusaidieni sasa maana wakati ndio sasa. Nawasilisha.
 
nimefanya utafiti kwa muda nikagundua kuwa wasomi wa tanzania ni waoga kuliko.nadhani kuna kitu magamba wanawafanyia kusababisha hali hii.wasomi fungukeni jamaniiiiiiii.nchi inaangamia.matukio muhimu yanatokea nchini lakini wasomi wetu wametulia tulii. !!!!!!!
 
Wasomi wa tz si wote wanauelewa, tena kwa kipindi hiki ambacho elimu yetu imepoteza uelekeo. kunaweza kukawepo hao unaowaita wasomi wakawa wanaelewa lkn wakaupotosha ukweli.kwa kuwa kila kitu kinachofanyika ni deal, mtu akipata bingo anajinyenyekeza kwa serikali anakuwa mnafiki anaficha ukweli, watu kama akina lukuvi mfano, Tambwe Hiza, Mwigulu, werema,manyanya. huwezi kupata ukweli hapo.sasa utajiuliza hawa ndo wasomi wa tz? ukombozi wa nchi hii utafanywa na si tu na wasomi wazalendo, bali wenye hekima, uzalendo na wenye kupenda haki.
 
Wasomi wa tz si wote wanauelewa, tena kwa kipindi hiki ambacho elimu yetu imepoteza uelekeo. kunaweza kukawepo hao unaowaita wasomi wakawa wanaelewa lkn wakaupotosha ukweli.kwa kuwa kila kitu kinachofanyika ni deal, mtu akipata bingo anajinyenyekeza kwa serikali anakuwa mnafiki anaficha ukweli, watu kama akina lukuvi mfano, Tambwe Hiza, Mwigulu, werema,manyanya. huwezi kupata ukweli hapo.sasa utajiuliza hawa ndo wasomi wa tz? ukombozi wa nchi hii utafanywa na si tu na wasomi wazalendo, bali wenye hekima, uzalendo na wenye kupenda haki.

umemsahau dr. bana!!!!
 
Naffikiri pia inatakiwa ifike mda mfumo wa rais kuteua wakuu wa vyou ubadilike kwasababu wanaoingia kuviongoza vyuo vyetu ambao ndio wapishi wakubwa wa hawa tunaowaita wasomi wanakua na interest za serikali na mwanafunzi yeyote anayeonekana kutetea uhuru wa kifikra basi atafanyiwa kila aina ya fitna na kufukuzwa chuo mapema kabia kwahiyo kwa kifupi mfumo naona ndio haswaa unaochangia uoga wa wasomi wetu.
 
Wasomi wamekua wana siasa..nao wanatoa majibu yale yale mepesi kwa maswali magumu!
 
Wasomi wapi hao ndugu ikiwa wote wapo kwenye siasa na ndiyo wanaoongoza kwa wizi wa rasilimali za nchi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ni kweli kiongozi inasikitisha sana kuona wasoma tunafumba macho kuhusiana na mambo kadha wa kadha yanayoendelea nchini ukiwepo mchakato wa MTWARA,nimekuwa nikijiuliza huenda hatuna wasomi Tanzania bali tuna wasomaji tu,nina kila sababu yakusema hivyo 1.Tumekuwa ni watu wa kupigania posho tu a.k.a Boom,2.Tumekuwa watu wa jamii ambayo haina mchango wowote kwa jamii,3.Tumekuwa ni watu tunaofumbia macho uovu wa serikali na mengine mengi yanayofanana na hayo,HEBU TUJIULIZE NINI MCHANGO WETU KWA JAMII?UMOJA WA VYUO VIKUU TANZANIA(TAHILISO) NINI WAJIBU WENU jamii inatuamini ,inatuhitaji na inatutegemea tuache unafiki na ushabiki wa kisiasa tujenge hoja ukweli uko wapi ndugu zangu wasomaji ambao tunajiita wasomi.
 
Wasomi wetu wanafanya kazi sana lkn huoni wakiandamana kutafuta haki zao na madai mengine wanafukuzwa huko vyuoni !! Na wakifukuzwa hawaungwi mkono hata na wazazi wao au wanachi wa kawaida kutaka kujua kwanini wanafunzi wa vyuoni wanafukuzwa bila sababu,watu wanakaaa kimya tu na kuanza kusema ohoo watu huko hawaendi kusoma wanaenda kuandamana tu,,watu wenyewe /watanzania hawataki mabadiliko ,,,wananchi wote wanatakiwa kuingia barabarani kujua kwanini madai mengi ambayo serikali iliahidi hatimizi kabisa?,,sasa unazungumzia wasomi watu wametolewa kucha,mtu kapigwa bomu barabarani ,hata hapo wanatakiwa wasomi hapa hakuna mtu wa kutolewa chambo cha msingi wote twende barabarani tu bila kujali kazi zetu na vyeo vyetu.nani aliemchukua mtaani mwanafunzi aliyefukuzwa kwa ajili ya kudai haki zake na kumlipia ada ya chuo akasome kwingine? Wabongo wanaongea sana akishakuwa kapata sehemu ya kupata laki tatu unaona kabisa kama mdomo umewekewa supa gruu ndio utanzania wenye elementi za uowoga ,ulio ambatana na umasikini,,,siku zote mtu masikini kudai haki zake peke yake hawezi hivyo.wasomi na wasio wasomi bongo ni masikni ni nani atakusikiliza ,,baba zetu waliofanya kazi eac walipigwa maji ya kuwasha,nani alilalamika baba yangu alivua nguo kwa ajili ya kupuliziwa maji ya kuwasha ni nani ambae hakujua kuwa haki za binadamu zilikiukwa,leo unataka kusema nini.poor tz
 
Back
Top Bottom