MAONI MBELE YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UTAWALA, SHERIA NA KATIBA
6 January 2024
Katibu Mkuu chama cha walimu (CWT) Mwl. Japhet Maganga ashauri ma- DED waendelee kusimamia Uchaguzi Mkuu mwaka 2025
Wadau mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Japhet Maganga ambaye ameshauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea kuwatumia Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025, huku uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ukiendelea kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na wadau wengine wakitoa maoni yao.
Wadau wanaopendekeza wasisitiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ma-DED kuendelea kusimamia uchaguzi, wasema ma-DED ndiyo wanaelewa hali halisi katika jiografia wilayani, tamaduni za wakazi wa maeneo pia wana rasilimali fedha na mamia ya waalimu ambao hutumika kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.
Wadau hawa wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Bunge linaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.
Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya utawala, sheria na katiba, mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama (Mbunge CCM) aliwapa miongozo ya jinsi ya wadau kuwasilisha maoni yao.
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya bunge amewaomba wadau hao 367 kuwa wavumilivu kusikiliza hoja za makundi mbalimbali hata kama vinakinzana kwani zoezi hilo la kusikiliza maoni ni kwa ajili ya kuboresha, kuweka mapya au kuondoa baadhi ya mambo yaliyowakilishwa ktk miswada muhimu.
Nia ni kupata kitu kitachosaidia kamati ya bunge na bunge kufanya maamuzi yamayozingatia umma mpana wa Tanzania unataka mabadiliko gani ktk miswada kadhaa ikiyowakilishwa bungeni.

Mwalimu Japhet Maganga na wadau wengine wa Usawa wa Kijisia, vyama vidogo vya siasa, asasi kadhaa za kiraia, makundi ya vijana n.k wanazungumza kutoka Bungeni Jijini Dodoma leo Jumamosi, Januari 6, 2024 wakati ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia masuala ya Utawala, Sheria na Katiba inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada ya sheria mbalimbali ikiwemo inayohusu uchaguzi.Wakurugenzi wa wilaya DED wapigiwa debe kuwa wana wanaishi huko wilayani na wana Ufahamu wa jiografia, utamaduni wa wakazi na rasilimali fedha pia watu