Wasanii wa Nchini Ghana 🇬🇭waja juu na kutaka Nchi yao ipige mziki ya Ghana pekee

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Katika kikao kilichofanyika huko Jijini Accra, Nchini Ghana, kilichoandaliwa na wasanii wa Afro beat kutokea Nchini gani, kimezua taharuki baada ya wasanii hao kuchachamaa na kutaka Sehemu zote za burudani na maeneo ya Starehe pomoja na vituo vya burudani vya TV na Radio vipige mziki wa Ghana tu, kwa sababu Mgeni leo akiingia Ghana hajui mziki hupi ni kutokea Ghana kwa sababu Maeneo mengi upiga mziki wa Kigeni.

Msanii mmoja katolea mfano, Ukienda nchini Kenya, mziki unaopigwa kwa wingi ni wa East Africa (hapa alijichanganya maana Kenya yenyewe inalalamika kuwa Tanzania na Nigeria ndio zimeshikilia soko la mziki wa Kenya), vilevile akasema sio kwa sababu ya Ushindani bali ni kwa uhai wa soko lao wenyewe la mziki, akasema kwamba hawaipingi NIGERIA,

Kwa sababu mziki wa Nigeria haukwepeki, ila ni vizuri tu kupiga mziki wa Ghana, hawakutaja Nchi yoyote ambayo muziki wake unapigwa sana Ghana, ila kitakwimu Muziki wa Nigeria ndio unaoshikilia Soko la mziki wa GHANA kwa zaidi ya asilimia 70.


View: https://www.instagram.com/reel/C06L9TIonf8/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==


Hata hivyo wanaijeria wengi wameonesha kukwazika na kitendo cha wasanii wa Ghana kutaka nchi yao ipige mziki wa Ghana tu, na si miziki inayotoka Nje ya Ghana. Wanaijeria wengine wametishia kususia miziki ya Ghana, wengine wameshutumu kuwa wasanii wengi wa GHANA wanapata Soko kubwa la usikilizaji kutoka Nigeria, kwa nini wasusie miziki ya Nigeria.
 
Hahaha kwa hio wanataka kuwapangia cha kusikiliza watu karne hii? Waache upuuzi, watengeneze hit songs tu,

Wanataka nyimbo za wageni zisipigwe nchini mwao, ila si ajabu kwenye hicho kikao walizungumzia jinsi wanavyoweza teka mziki wa Africa
 
Back
Top Bottom