Elections 2010 Wasanii Nyota wa Bongo Flava wachangia CCM

Hawa wasanii ndio maana hawaendelei kila siku wanalalamika mauzo ya kazi zao yanaibiwa kutokana na mifumo mibovu iliyowekkwa na serikali ya CCM, leo wanalipwa vihela kiduchu wanavaa hizo tshirt kuipigia debe ishinde ili kazi zao ziendelee kuibiwa na kupotea kutokana na mifumo mibovu ya CCM ama kweli sijui ni ujinga au kutokuwa na shule
 
Siwaelewi labda waniambie watumia msemousemao ukishindwa kupigana nao ungana nao[wizi mtupu]
 
Wana JF hivi Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba ni wakereketwa wa CCM?

Kwa nini wasitangaze interest zao ili kila mtu ajue kama ilivyo radio Uhuru FM?
 
kichefuchefu...................
kizunguzungu..................
 
In business, just like in politics, there are no permanent friends or enemies!

1.jpg

You got that right! No permanent friends or enemies, just permanent interests.

On the flipside, I don't see anything wrong with them endorsing CCM. They have the right to endorse whomever and for whatever reason(s). So there is no need to fuss about it.
 
Hawa sio njaa hata kidogo, ila ni upeo mdogo wa kuelewa. Kifupi ni kuwa hata wenyewe hawajitambui ni nani na kwa nini wako hapo walipo. Heko CCM kwa kupanda ujinga kwenye vichwa vya vijana hawa,ila ole wako siku wakiamka na kujitambua na kukufahamu CCM umewafanya nini wakiwa usingizini.
nakubaliana na wewe mkuu, upeo ndio tatizo. Nafikiri hata elimu pia ni ndogo. Wenzao wa uganda wana pesa za kutosha kutokana na kazi yao, mikakati yao katika kazi ya sanaa sio sawa hata kidogo, hawa wanataka njia ya mkato. Lau wangekuwa kama SUGU wasingekuwa hapa, waliishia kuzushia majungu akawaachia soko lao kajiendea Ulaya. Ukiwauliza watakwambia tunaogopa kuitwa wapinzani na kufilisiwa (kwa lipi nyie vidampa?)

Siwaamini tena, mmeonyesha sura mbili na hamuhitaji kuitwa wasanii, elimu yenu ina upendeleo. Hongera Mkuchika na wenzako kuwamaliza kabisa wajasiriamali uchwara hawa
 
Jamani msisahau kuwa hawa vijana wana haki ya kuchagua vyama vya siasa watavyo [ninasikia Nakaaya ameingia chadema] Ingawa wengi wanaona kuwa ccm haifai kuongoza lakini wengi zaidi wana imani kubwa na chama hiki hivyo kuwalaumu itakuwa siyo haki kabisa.
 
Jamani msisahau kuwa hawa vijana wana haki ya kuchagua vyama vya siasa watavyo [ninasikia Nakaaya ameingia chadema] Ingawa wengi wanaona kuwa ccm haifai kuongoza lakini wengi zaidi wana imani kubwa na chama hiki hivyo kuwalaumu itakuwa siyo haki kabisa.

Nakuunga mkono pamoja na miguu yangu yote miwili. Kila mtu ana haki ya kumpigia debe yeyote yule apendaye.
 
Niliweka maoni yangu hapa: Vijana FM: Wamechangia, wewe je?, lakini sio mbaya nikiyaweka tena...

Binafsi, sipingi kile CCM wanachofanya, ila ningependa kusikia kutoka kwa wahusika nini hasa kilichowafanya kukubali kusaidia chama fulani kwenye kampeni. Kuna mtu amemtaja Nakaaya..lkn na yeye hakutuambia anakubaliana na sera zipi hasa za CHADEMA...

Swali ni hili, je, wanakubali "image" yao itumike kama chombo cha kuwahamasisha Vijana kufuatilia na kujishughulisha na Siasa za chama fulani? Bila shaka jibu ni ndio (kwasababu sasa hivi wako kwenye mabango)!

Lakini ukisikiliza nyimbo za baadhi ya wasanii waliotumiwa utasikia vilio kwa Serikali au viongozi "wanaofanya nao kazi" sasa hivi. Je, wamesahau vilio na kauli zao? Hawa viongozi walizisikia zile nyimbo?

Kuhusu hii 'tactic'..dah, lazima uwanyooshee mikono Sisiem..Wanatisha kusema ule ukweli. Sasa, kazi ipo kwa vyama vingine.

Na mwisho kabisa, vipi suala la Pinda kuwa kamanda wa VIJANA...akitawazwa na Kingunge (kamanda wa VIJANA CCM Kitaifa)???
 
Jamani mbona mnapoteza lengo ???? Darasa la michuzi halina hoja katika hili na vilevile kuwaita vijana hawa mbumbumbu ni sawa na kuwatusi kwani inawezakana tanzania wanayoitaka wao ni tofauti kabisa na ufikiriavyo [kama una wototo wa umri huo utaelewa nina maana gani]
Let them be this is their country too
 
JF, This is nothing but a marketing campaign....... Si kwamba hawa jamaa wanaipenda CCM kihivyo au ndio wameshaichangia... Actually they have been paid by CCM for these ads.....

And of course just like any other marketing campaign, the target market is youth....
 
Ni sawa kwa nakaya sumari kwa kuwa mwanachama wa chadema lakini siyo sawa kwa wasanii wengine kuonesha mapenzi yao kwenye chama cha ccm. WHAT A FARCE FOR THINKERS
 
Ni sawa kwa nakaya sumari kwa kuwa mwanachama wa chadema lakini siyo sawa kwa wasanii wengine kuonesha mapenzi yao kwenye chama cha ccm....

Shukrani kwa kudokeza kwenye hili suala. Mi' binafsi - kama nilivyosema hapo juu - ningependa kusikia malengo au sera zipi haswa za chama husika wanazozipigia debe (Nilimuuliza hili Nakaaya kwenye blog yake lakini sikufanikiwa kupata jibu lolote lile). Kwasababu kama wana uwezo wa kuhamasisha watu, hawana budi kutueleza sababu au sera zilizowavuta kwenye chama husika au siasa kwa ujumla.

Au tunyamaze tu kwa kuwa wana uhuru na haki ya kufanya wanachokitaka?
 
Kwani wewe walikuuliza sera za chama kipi unazipigia debe??? Mimi nadhani mambo haya yanaanzia kwenye individual level na hii inatokana haki ya msingi ambayo pia imeainishwa katika katiba ya tz
 
Mimi ni kijana wa kawaida tu kama wananchi wengine. Lakini wao wanaweza kutumiwa kama kioo au taswira fulani..Kwanini wamewatumia hawa wasanii (sijamsahau Nakaaya*)? Mimi na wewe tunajua sababu zao...

Baadhi yao watatumiwa kwenye majukwaa ya kampeni kama tulivyoona miaka iliyopita. Lakini kama unaniambia nichangie au nikipigie kura chama fulani tu kwasababu wewe ni Prof. Jay...Mimi binafsi nitahitaji sababu. Kama nitakubaliana nao sawa..kama nisipokubaliana nao sawa.

Kwa kifupi, mi' ninachoogopa ni Vijana kuanza kufuata mkumbo -- na hii ndio itakavyotokea -- bila kuuliza maswali ambayo mimi nadhani ni ya msingi.


*Jiulize kwanini Nakaaya alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa amejiunga CHADEMA. Au ni haki yake tu iliyoainishwa kwenye katiba ya TZ kuwa kila kijana akijiunga na chama atangaze kwenye vyombo vya habari?
 
Katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu sidhani kama sera ni issue, binafsi naamini CCM wamekuwa na sera nzuri sana katika chaguzi karibu zote ukiondoa mapungufu madogo madogo ambayo pengine yanatokana na utofauti wa mawazo.

Tatizo kubwa lipo kwenye kutekeleza hizo sera.......hapo ndo utumbo na takataka hutokea. Na cha kustaajabisha zaidi, wanarudi tena kwenye kampeni za 2010 na uongo kibao......huku wana wa nchi tukikenua menu kwa nderemo na vigeregere tukiwa tumevaa Tshirt na Khanga zimeandikwa "Chagua CCM, Chagua Kikwete" huku mkononi tumeshika bendera na vipepershi vikiwa vina maneno ya "Maisha Bora kwa kila Mtanzania"

By the way exchange rate leo ni Tsh. 1436/USD. Hayo ndo mafanikio ya Kikwete ambae alikabidhiwa nchi wakati USD 1 ilikuwa sawa na Tsh. 1153 (Tsh. 1153/USD) miaka 4 tu imepita.

What irresponsible government!!!
 
Ukweli utabakia kwamba CCM ina mbinu nyingi sana. Na hakika hili ni bao safi la kisigino ktk Kujitangaza... Muziki na BongoFlava ndio huchukua asilimia 80 ya vipindi vyote vya television Tanzania na hakika watu wataupokea Ujumbe huu..

Hawa vijana wana haki sawa na yenu kuchagua Chama wanachokipenda. Ndio Demokrasia tuloitaka sote pasipo kuzingatia kwamba demokrasia kwa watu wenye njaa (watu na Mazingira) haiwezi kuwa safi ama sawa na wenzetu waloshiba waanzilishi wa mfumo huo. Na haya ni matunda yake!
 
Back
Top Bottom