Elections 2010 Wasanii Nyota wa Bongo Flava wachangia CCM

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Binafsi sikulitegemea hili kufanywa na kijana yoyote mwenye umri chini ya miaka 40. Ni miaka zaidi ya 50 toka nchi yetu ipate uhuru lakini bado majority ya watanzania tumetopea kwenye lindi la umasikini uliovuka kipimo cha utu. Hii yote imesababishwa na serikali mbovu, dhaifu na isiyo na mipango madhubuti ya kuleta maendeleo katika taifa letu.

Binafsi, sikumbuki kama nilishawahi kuvaa ama kushika ama kusogea karibu na either bendera ama Tshirt ama khanga ama skafu ama chochote kile kinachohusiana na CCM hata kwa kupewa pesa, pombe na pilau za bure.

Je hawa vijana wanajua wanachokifanya?

Je nyimbo zao za kulaumu utendaji kazi wa serikali ya CCM hasa katika masuala ya Rushwa na ufisadi zina maana gani kama leo hii wanashiriki ku support serikali mbovu iendelee kutawala?

Au ni njaa inayowafanya washiriki kwenye hizi kampeni?

Au hawajui walifanyalo??

Cheki picha hizo hapo chini.........

Wasanii nyota wa bongo fleva wachangia CCM

ccm_changia_prof_jay_A5.jpg

Profesa J

ccm_changia_nature_A5.jpg

Juma Nature

ccm_changia_mwana_fa_A5.jpg

Mwana FA

ccm_changia_makini.jpg

Joe Makini

ccm_changia_dully_A5.jpg

Dully Sykes

ccm_changia_diamond_belle_A5.jpg

Belle 9 (shoto) na Diamond

ccm_changia_cp_A5.jpg

CPwaa

ccm_changia_chidi_mwansiti_A5.jpg

Mwasiti (shoto) na Chidi Benz

ccm_changia_amin_A5.jpg

wana THT


Source: Michuzi Blog​
 
Wasanii na waandishi ndio watu ambao hutumainiwa sana kuifundisha jamii kuhusu mwelekeo wa nchi; nawapongeza sana Mrisho Mpoto pamoja na Nakaaya Sumari kwa kujaribu kufanya hivyo.

Nikiangalia jinsi waandishi walivyopiga foleni kugombea vyeo vya CCM mwaka juzi, halafu na hawa wana bongofleva walivyojipanga kuipigia debe CCM, basi naona kuwa kada hii nayo imeamua kututosa kabisa. Haya ni matokeo ya vitu viwili tu; ufukara wa mali na umaskini wa mawazo.
 
Bongo kinacho tusumbua sana ni njaa, njaa kweli ni mbaya na ni adui wa haki.
 
mimi hii kitu imenikatisha tamaa!

njaa kweli mbaya, ukifikiri pengine pesa zenyewe walizopewa hazimalizi mahitaji yao ya mwezi! aggggr
 
Tatizo ni umaskini wa mawazo/maarifa na kipato kwa wasanii wetu na vijana kutokukaa katika nafasi zao ambazo wamekusudiwa. Bora kuwa maskini wa kipato kuliko na ukawa na utajiri wa mawazo/maarifa kwa wasanii wetu hawa.

Tazama IYohana 2:14 - Mungu anawatazama vijana kama watu wenye nguvu.

Hosea 4:6 "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...."

Tafadhali wana JF, tuwasaidie vijana wetu hawa wakae katika nafasi zao katika jamii, wafanye yale yaliyokusudiwa.

Kwa kukosa maarifa ndio maana hata nyimbo zao zote maudhui yake ni mapenzi tu hakuna kingine zaidi ya hilo ukiondoa wasanii wachache sana wenye mitizamo tofauti.
 
Nafikiri aliyeturoga watanzania alishakufa na kutuachia akili ya kuvuka barabara tu!!
 
Naona blogu ya Michuzi ni propaganda nzuri ya CCM!

Hawa celebrity wa Bongo ni scum bags,ni njaa tu. Sijui wamelipwa ngapi kuvaa nguo hizo za kijani.

Mimi nasikiliza Western Jazz Band,Tabora Jazz Band,Afro 70 ,Mlimani Park etc.

Ukipata nafasi nenda youtube,utaona mengi mazuri ya bedi za 60s,70s na 80s.
 
Hawa sio njaa hata kidogo, ila ni upeo mdogo wa kuelewa. Kifupi ni kuwa hata wenyewe hawajitambui ni nani na kwa nini wako hapo walipo.

Heko CCM kwa kupanda ujinga kwenye vichwa vya vijana hawa,ila ole wako siku wakiamka na kujitambua na kukufahamu CCM umewafanya nini wakiwa usingizini.
 
SWALI: Je hili ni tangazo, au vijana hawa wameichangia CCM? Je wanaridhika na serikali inavyoendeshwa?

Je in case ni Tangazo, Je wameridhika na hali halisi, au wenyewe wanaangalia fedha tu kutokana na tangazo.
 
usanii na uandishi wa habari ni taalumu mbovu ambayo wengi wanaoikimbilia ni wale wanaofeli std 7, form 4&6. Ni wachache sana waliofaulu wanaokwenda uandishi wa habari na kubongo flava.

IQ zao ni sifuri kabisa. hata muwaseme vipi hawataelewa zaidi mtabishana tu. Solution ni kuwasaka na kuwaadabisha kwa adhabu yo yote ile.
 
sio wasanii wa malaria no more hawa? naomba nielezwe kati ya hawa wangapi walishiriki tamasha hilo
 
Sijui kama wanajua walitendalo! Wanafurahi kushibisha matumbo yao kwa kukitoa kafara kizazi chao
 
In business, just like in politics, there are no permanent friends or enemies!

1.jpg
 
Sijui kama wanajua walitendalo! Wanafurahi kushibisha matumbo yao kwa kukitoa kafara kizazi chao

Kwa kweli hawajui walitendalo. Hao wamevaa ma-tshirts kuna wengine na singo za kampeni wametoa kabisa. Damn, inaudhi sana!!!
 
kimsingi nawasupport kwa kuhamasisha watu ili na wao wassanii wapate kula.infact PONGEZI ZANGU ZIENDE KWA NAKAYA SUMARI AMBAYE AMEKUWA MSTARI WA MBELE KUJITOKEZA NA KUSEMA WAZI WAZI KUWA YEYE CHADEMA.OK NUFURAHI SANA NA NAKUTAKIA KILA LA HERI,


nb; AACHENI KUWA LIMBUKENI STAND AND SHOW YOUR STAND
 
Back
Top Bottom