Wasanii 13 wa taarab wafa ajalini

Mimi nina maoni tofauti kidogo. Hapa naona tatizo siyo Magufuli wala barabara mbovu au mabango. Barabara hiyo naifahamu sana na ina viwango vya hali ya juu kabisa. DANIDA wameipanua vizuri kwa kuiwekea mabega.

Tatizo ninaloliona mimi ni la dereva. Nimeona picha ya basi liliopata ajali. This guy wa flying in the night! Hata kama angekumbana na ng'ombe mmoja mambo yangekuwa mabaya tu. Fikiria kuwa dereva alikuwa anataka kulipita hilo lori lakini akaona gari lingine mbele yake kwa hiyo ikabidi arudi upande wake na kuua watu kikatili hivyo.
 
Ukweli kuhusu eneo la ajali ni kwamba ajali hiyo imetokeo maeneo ya doma,mbele ya mikumi kama unatoka mikumi kuja morogoro,watu waliofariki ni kumi na tano na miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa morogoro
Miili hiyo itasafirishwa kesho kwenda dar kwa mazishi
chanzo cha ajali ni mwendo kasi uliosababisha dereva kuvamia lori lililokuwa limeharibika na kupaki pembeni ya barabara
Kundi lilikuwa likitokea mkoani mbeya lilipoluwa limekwenda kwa ajili ya shoo
source:TBC1
 
May God in His abundant grace and mercy Rest them in eternal peace!
 
Ibara ya 9 (1-10) za Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 zilizopitishwa kwa Tangazo la Serikali Namba 21 la Tar 23 Januari 2009 zinaipa TANROAD mamlaka ya kuondoa magari yoyote yaliyoharibika na kukaa barabarani kwa zaidi ya masaa 6 mijini na masaa 24 vijijini. Lakini kwa kuwa kuwasimamia TANROAD kutekelza wajibu huu hakutoi mwanya wa kuwepo waanddishi wa habari na wananchi kujua leo Magufuli kafanya nini, waziri huyu hana habari na sheria hii ambayo laiti kama inetekelezwa ingepungua idadi ya ajali mabya za barabarani, vifo, majeruhi na mayatima,

Magufuri,

Simamia sheria hii kwanza ili kupunguza ajali za barabarani badala ya kukurupuka na bomoa bomoa.
 
Back
Top Bottom