Wakazi kaonyesha kipaji kwenye Muziki wa Taarab. Ana pesa zake nyingi kwenye Muziki wa Mwambao

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,230
22,308
Mimi kama mtu mwenye talanta ya kuweza kuona vipaji vya watu ambapo wakati mwingine wenyewe hawavioni ninapenda kuutaarifu umma kuhusu kipaji kipya nilichokiona. Ndugu yetu Wakazi Wasira ambaye anatajwa kama mwanafamilia ya muziki wa Hiphop amekuwa akipoteza muda kurap wakati kipaji chake halisi ni uimbaji wa muziki wa Taarab. Muziki wa mwambao unamhitaji.

Ninamshauri ndugu Wakazi asizidi kupoteza muda zaidi kwenye Hiphop na badala yake achukue hatua za haraka kujiunga na kundi lolote la taarabu litakalomsaidia kukuza kipaji chake.

Mzee Yusuf na Malkia Khadija Kopa wanaweza wakampa mwongozo utakaomsaidia zaidi. Taarab ina maokoto yake. Na kwasababu ni mjuzi wa lugha ya kiingereza anaweza achia wimbo mmoja wa Taarabu kwa lugha ya malkia.

Pia aache kushindana na wanahiphop halisi kama Roma Mkatoliki ili kutoendelea kupuuzwa.
 
Back
Top Bottom