Waraka wa TAMSYA kwa vyombo vya habari

Naona madai yenu ni ya msingi japo sijajua ni ya msing kias gan maana inaonekana kila tukio lilifanyiwa uchunguz na hava stahik zikachukuliwa.walichukua hatua hiz kwa kuwa uchunguz umefanyika wako sahih.nashangaa vijana wa kiislam kila siku kulalamika juu ya hatua wanazochukuliwa kila waendapo kinyume.mbona vijana pia wa kikristo au iman zingine wanafukuzwa shule,vyuo au kusimamishwa masomo pindi waendapo kinyume na madai yao hayaandikwi kwenye vyombo vya habar?why muslims tuu?nadhan kila mtu akihitaj matakwa yake binafs yatekelezwe nchi haitatawalika.kwa nin kipind cha awamu ya tatu ya urais mambo haya hayakuwepo?au kwa kuwa rais aliyeko madarakan ni mwislamu?achen udin shenz zenu.kila siku tunaomba kuwa wamoja halafu ninyi mnaturudisha kwenye udin huku mmevaa vaz la kondoo mkidai hak kumbe ni wadini kama nin.andamanen had 2015 mkiona hak haijatendeka maana mnasema mtaendelea kuchukua hatua zaid.niny hamna tofaut na bokoharam,al-shabab au warabu wanaopenda kujitoa muhanga.tumewazoe kusikia mnajitoa mhanga fanyen hvyo ikibid .uwiano pia ktk masomo hautakaa utokee mpaka mwisho wa dunia maana waislam ni wachache waliosoma na wengine wanaoendeleo kusoma elimu haiwasaidii zaid ya kulalamika tuu.kuwen wastaarabu kama watu wa din zingne walivyo ambao niny huwaita makafir kumbe niny ndio makafir na wazandik wakubwa.
 
Nashauri Kanisa Katoliki lidai kurudishiwa shule zake zilizoporwa na Serikali-Ndanda. Umbwe, Weruweru girls, Pugu, Tabora boys and girls, na nyinginezo. Ndio dawa tu ya kurudisha heshima. BAKWATA wakajenge za kwao.
 
Naipenda dini ya kiislamu,lakini nawachukia waislamu,wengi ni makanjanja hawajui misingi ya dini yao,kazi yao ni kuchanganya dini na siasa,na ndio maana wanapata tabu sana na mfumo huu wa serikali,cha ajabu raisi ni muislamu,mawaziri wengi ni waislamu,wakuu wa vitengo vingi vya serikali wanaochaguliwa na raisi ni waislamu.Mna taka nini ninyi watu?
 
Nashauri Kanisa Katoliki lidai kurudishiwa shule zake zilizoporwa na Serikali-Ndanda. Umbwe, Weruweru girls, Pugu, Tabora boys and girls, na nyinginezo. Ndio dawa tu ya kurudisha heshima. BAKWATA wakajenge za kwao.
Kumbe Hayati Nyerere alifanya kosa kubwa kutaifisha shule za wakristo............
 
@ Barubaru. Mkuu na mimi nilipita JKT Ruvu,hakuna Kuruta alikuwa anaruhusiwa kwenda kusali ama kuswali mpaka tulipo pass out ndipo tukapata angalau muda wa kusali/kuswali lkn kama hauna majukumu muhimu kwa mfano hauko ulinzi ama kazi yoyote muhimu.
 
"...ACHENI KUTUDHALILISHA NA KUTUNYANYASA WANAFUNZI WA KIISLAM MASHULENI NA MAVYUONI SASA BASI INATOSHA TUNAOMBA WAISLAM WOTE NA WAPENDA AMANI WOTE MTUUNGE MKONO KATIKA MAANDAMANO HAYA YA AMANI...."

Shida ninayoipata mimi nisomapo au kuwasikiliza wenzangu waislamu wa SIKU HIZI ni wao ku-generalize issues! mwanafunzi mmoja wa kiislamu akawa na ugomvi na mwenzie, na ikatokea bahati mbaya akatolewa tusi, basi kama mwenzie ni mkristo basi inachukuliwa wakristo wote wamewatukana waislamu. MIMI Tangu zamani nimeishi na waislamu, tumekula tumekunywa na kucheza nao, tumegombana na hata kupigana kama watoto- hatukuona huo udini baina yetu. Na leo tunaendelea kuishi nao. Lakini leo hii akikukosea mwislamu inabidi uwe mwakini usije ukatoa tusi- mfano ukimtukana 'nguruwe' unaweza kutafisiriwa umetukana dini! Haya Mambo ni FITINA tu- Hamna MOU kama mnavyodai, ila kuna mashauriano jinsi ya kujilinda na wenye siasa kali, wenye kujilipua na bahati mbaya hawa wamekuwa na mwelekeo wa dini ya kiislamu- lakini hatusemi Islamu inawatuma vijana wafanye haya.

Kama Mkristo na mwalimu napata changamoto nyingi sana baada ya huu mlipuko wa kulaumiana. Kuna siku kidogo nipoteze sifa zangu kwa jambo ambalo sikulishtukia. Nilipelekwa kusimamia mitihani. Wanafunzi wote isipokuwa mmoja niliweza kuwatambua kwa vitambulisho- na wawili hawakuwa wanafunzi - walikuwa ni mabandia walioajiriwa kuja kuwafanyia wenzao mtihani. Huyu mmoja nilimwomba afungue uso wake ili niweze kumtambua- alikataa, nikamsihi akakataa! Mwanafunzi mmoja mwenye busara tena Mkristo alinisogelea na kunitafadhalisha nimruhusu tu- na kunihakikishia anamfahamu. Mimi nilidhani alikuwa ananikatalia nisimtambue kama ni mdanganyifu! Sasa kweli Hijabu lakini udanganyifu ni mwingi! Tufanye nini ili tuweze kuendelea na shule bila kuwa na wasiwasi wa kudanganywa. Ndugu zangu Waislamu mnapaswa mtufundishe jinsi ya kupambana na matatizo ya kileo katika dunia hii wakati mmeficha nyuso za kina dada! Ni nini wahenga wa uislamu walilenga kutaka vazi kama hilo? Je uislamu haubadiliki! Naam kweli enzi zile ukiacha matatizo ya uzinzi na matamanio, hapakuwepo na mambao ya kina dada kwenda shule. Je inawezekana leo - nakumbuka kile kitabu cha 'Is it Possible" hata Masai wameona sababu ya kuacha mikuki na sime ili wakumbatie kalamu( pengine huu mfano sio mzuri- nisameheni tu- kama napotosha- sio nia na haitakuwa hata siku moja kudharau imani ya mwenzangu!)

Dah, post yako nzuri(to some extent) kwani imejaa 'soft messege' inayoonyesha kuwa kuna mambo(ya kiislam) huyafahamu lakini hukusudii kuyakaidi kwa chuki bala ueleweshwe! Nadhan wachangiaji wengi wangelikuwa capability kama hii,walau ingesaidia ku-address kile kinacholalamikiwa. Oh, sory naona fajr imeingiya wacha niiwahi,then nitumikie 'chajio' then, jion-Inshllh tutaendelea kujuzana kwa kadri tutakavyowezeshwa!
 
Lakin swala za ijumaa na ijumaa pili zinakuwa kama kawaida.

Nakumbuka Ruvu tulivyokuwa tunaswali kule vibwende au kwa babu. na siku ya ijumaa Mlandizi town.

we ndo maana uliamua kurudi kwenu uarabuni!!mkoa wa pwani hakuna kitu kama hicho kwenye red..
 
Nashauri Kanisa Katoliki lidai kurudishiwa shule zake zilizoporwa na Serikali-Ndanda. Umbwe, Weruweru girls, Pugu, Tabora boys and girls, na nyinginezo. Ndio dawa tu ya kurudisha heshima. BAKWATA wakajenge za kwao.


Vipi na zile BILIONI 91 wanazokwapua kila mwaka kutoka Serikali ya Muungano kupitia MoU zitakuwaje?, je watazirejesha tokea MoU iliposainiwa 1992?
 
naomba nikueleze ndugu yangu kuhusu ratiba ya shule
siku ya ijumaa ratiba inaisha saa sita kwa wanafunzi wanaoingia asubuhi aidha kwa wale wanaoingia mchana ratiba itaanza saa nane ili watu waende kusoma katika uwo muda ambao ni free na vpindi vya dini vinatakiwa viwe muda wowote au siku yoyote tofauti muda wa sala elekezi nilioutaja juu tuache kuna haja ya hawa walimu kubadilisha ratiba yao ili watu wakaswali hebu fikiri kwa nini serikali kupitia raisi wa awmu ya tatu mh b w mkapa aliamua siku ya ijumaa vpindi viishe saa sita na nusu ili watu waende kuswali na wanfunzi wa kike waruhusiwe kuvaa hijabu na sio kwa waislamu tuu vipindi vinaisha kwa shule nzima bila ubaguzi na sio kwa ajili ya kipindi cha dini ..........tafakari


Nafikiri ndugu yangu kuna mambo mawili unayachanganya hapo.
Mosi, Muda wa kuswali
Pili, vipindi vya dini.

Kumbuka hivi vyote viwili ni muhimu kwa kila mwanafunzi kuweza kuhudhuria. Haiwezekani kabisa muda wa swala ukawa ni muda wa kipindi cha dini. Kwani swala ni kitu kingine na Kipindi cha dini ni kitu kingine. Lazima ratiba zenu zitenganishe hayo na kutoa fursa kwa wote kuhudhuria vipindi vyote vya swala na vipindi vya dini.
 
Tatizo la wanafunzu waislamu ni wengi wao kuwa wakorofi kwa kisingizio cha dini
1.mimi nikiwa shule serikali moshi hawa jamaa walipewa nyumba waliyotumia kama msikiti but wakawa hawaendi darasani,hawaendi paredi wanakaa tu msikitini kwa kujua kwa waalimu wakristo hawataweza kwenda kuwakurupusha huko.
2.Imagine wewe ni mwalimu unafundisha and then mtu anachomoka darasani saa sita anakwenda kuswali je tutakua tunafuata ratiba za masomo au ratiba za swala tano?
3.Shule zote zilizokua za kanisa zina miundombinu ya kikisto kwahiyo wasilazimishe misikiti kujengwa ndanda being one of them.
JENGENI SHULE ZENU NI MISIKITI MUWEKE NO ONE WILL ASK YOU

Naomba uniulizie kama pale Al-Haramain kuna kanisa.
Tafadhali usiulize kwa nini wanawalazimisha watahiniwa tena binafsi (private candidates) wa kike kuvaa hijabu/baibui ili kuruhusiwa kuingia shuleni. Ukiuliza we utakuwa umeathiriwa na mfumo kristo.
Bado sijawasikia Freemasonry tu, hii serikali mbona itakoma na matamko. Kah!!
 
Haya yote yanasababishwa na joka kuu linaloendekeza udini JK

Haya yalipandwa na JKN na wengine wamekuwa wanapalilia tu. Wakristo hususan Wakatoliki walizoea kudekezwa na kujiona ni first citizen kulinganisha na wengine. Na ndio maana wao wapo nje ya makanisa mengine ya kikristo na wanajipambanua kipekee zaidi. Ukitaka kulona hilo angalieni anapoapishwa rais wenu wa Muungano, utaona kuna mwakilishi wa makanisa ya kikristo, mwakilishi wa wakatoliki na wawakilishi wa waislam na mwakilishi wa wahindu.

Sasa ukweli unasimama, kila mtu anadai haki yake.

 
acheni uongo, mimi nimesoma lyamungo, hakuna kanisa wanafunzi wanasali kwenye vyumba vya madarasa, na wanafunzi wa kiislam pia wana sehem yao kwenye chumba cha darasa, hakuna kanisa wala msikiti, kuhusu hizo nyingine kama umbwe na pugu, mtambue hizi zilikuwa ni shule za kanisa, so makanisa yalijengwa tangu enzi za ukoloni, mngewaambia walioleta dini yenu, yaani waarabu nao wajenge misikiti wala kusingekuwa na tabu.
kweli ndugu zetu wanapotosha umma kwa kusema eti lyamungo kuna kanisa, si kweli mimi nimesoma umbwe jilani zetu lyamungo najua ile shule.umbwe ni kweli kuna kanisa tena zuri sana wakoloni waliumiza kichwa kulijenga:embarassed2::embarassed2:
 
Nafikiri ndugu yangu kuna mambo mawili unayachanganya hapo.
Mosi, Muda wa kuswali
Pili, vipindi vya dini.

Kumbuka hivi vyote viwili ni muhimu kwa kila mwanafunzi kuweza kuhudhuria. Haiwezekani kabisa muda wa swala ukawa ni muda wa kipindi cha dini. Kwani swala ni kitu kingine na Kipindi cha dini ni kitu kingine. Lazima ratiba zenu zitenganishe hayo na kutoa fursa kwa wote kuhudhuria vipindi vyote vya swala na vipindi vya dini.

Ni ujinga wa namna hii ndio unaowafanya mnakuwa nyuma kitaaluma halafu mnasema mnasahihishiwa vibaya mitihani yenu. Mara zote, kwenye shule zote kumekuwa na tatizo la walimu kushindwa kumaliza syllabus achilia mbali kufanya revision ambayo pia ni muhimu. Sasa wewe mwenye akili sana, unashauri kuwe na muda wa msikitini na bado upatikane muda mwingine wa vipindi vya dini! Kwa mtindo huu hiyo syllabus inakwisha au shwari tu hata ikiishia katikati kama Masjid Kuba na Al Haramain?

Hebu kuweni na akili za kimaendeleo, academic discipline ni very serious issue na inadetermine matokeo ya mwanafunzi darasani. Hivi mmeshawahi kujiuliza kama ingekuwaje endapo kila mtu angekuwa na mawazo kama yenu?

Wakati wenye kupenda shule wapo tuition, nyie mpo madrassa au kwenye mihadhara lkn siku ya kusahihisha mitihani, inamlazimu msahihishaji abalansishe matokeo ili waislamu wafurahi, au? Safari yenu ndefu sana.

Unajua kisa cha viwanda vya waarabu kuendeshwa na wazungu? = akili kama hizi zako. Ndio maana BP anaongoza kwa uzalishaji wa mafuta, japo si yake ni ya Saudia.
 
kweli ndugu zetu wanapotosha umma kwa kusema eti lyamungo kuna kanisa, si kweli mimi nimesoma umbwe jilani zetu lyamungo najua ile shule.umbwe ni kweli kuna kanisa tena zuri sana wakoloni waliumiza kichwa kulijenga:embarassed2::embarassed2:

Tunapowalaumu hawa watu, tuzingatie pia ni nani aliwaletea hii dini yao. Wale waarabu, pamoja na utajiri wooote ule wa mafuta, ni BP ndio anaongoza uchumi wao. Shida ni akili za namna hii. Wakijengewa msikiti tu, hawana shida nyingine. Angalia Dubai inavyojengeka baada ya waarabu wa huko kugundua umuhimu wa shule. Wazungu wooote wanaelekea UAE.

Huyu barubaru yeye hajifunzi kitu huko oman, kazi zake ni kuosha vyombo huku akituma tusent kwa wapemba wenzake wafanyie mihadhara badala ya kuwalipia ada wakasome.
 
Heko vijana wa Kiislam kumbukeni mnatakiwa kuiondoa dhulma hiyo kwa mikono yenu na sio kuchukia moyoni. Kwani hiyo ni imani dhwaifu kwenu.

Mola yu pamoja nanyi na sisi sote tupo pamoja kwa hilo kwani hiyo ni haki yake sio tu kisheria bali hata kibin'Adam.

Kudai haki ni wajibu kwa sote. Haki haiombwi bali unadai.
Nina wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo kisomi, umekuwa unajinasibu kama msomi wa PhD, lakini huonyeshi kabisa uwezo wa mwenye elimu hiyo katika kuchambua mambo. Hao vijana unaowashabikia ni waleta fujo na vurugu mashuleni kwa kisingizio cha uisilam. Wanafunzi waislamu wa Ndanda waliofukuzwa kwa kuhatarisha amani shuleni hapo walipewa nafasi kisheria kukata rufaa dhidi ya hukumu waliyopewa, wao badala yake wanashindwa kufanya hivyo nakukimbilia kwenye vyombo vya habari. Barubaru, uislamu sio kufanya fujo na kuchochea chuki dhidi ya watu wengine kama unavyofanya wewe na shetani mwenzako Mohamedi said. Mungu wenu hawezi kuwa dhaifu kiasi cha kusubiri utetezi wenu dhaifu usio na maana. Amani ni tunu adimu lakini ninyi kwa ubinafsi wenu mnataka kuiharibu washenzi wakubwa!
 
Ilboru kuna Kanisa. Na waisilam wamepewa darasa wanalituia kama msikiti.

historia ya Ilboru inajulikana wazi kuwa ile ilikua shule ya dini kabla ya kutaifishwa, ndo maana kuna kanisa na wala kanisa hilo haliko ktk eneo la shule, lipo just baada ya duka la shule then barabara ninapajua sana ilboru nahata hivyo wakuu ukisema wakristu unamaanisha nini?, mie ni mkatoliki wenye kanisa ni walokole, na waislamu wamepewa sehemu ya kuabudu sawa na wakatoliki wanaotumia semina room.

huyo mama mkwizu inatakiwa mumjue ni mtu mwenye silika gani (jinsi anavyokabiliana na changamoto zake) kikawaida kabla ya kumchukulia kuwa ni mdini.

nionavyo mimi wa2 waruhusiwe kuabudu mashuleni kwa muda maalumu e.g nusu saa au saa kwa kupewa maeneo ya kuabudu eg madarasa jioni kabla ya kuanza prepo ila wasiwe kikwazo kwa maendeleo ya kitaaluma ya wasio amini.

When we blindly adopt a religion, a political system, a literary dogma, we become automatons. We cease to grow
 
Ni ujinga wa namna hii ndio unaowafanya mnakuwa nyuma kitaaluma halafu mnasema mnasahihishiwa vibaya mitihani yenu. Mara zote, kwenye shule zote kumekuwa na tatizo la walimu kushindwa kumaliza syllabus achilia mbali kufanya revision ambayo pia ni muhimu. Sasa wewe mwenye akili sana, unashauri kuwe na muda wa msikitini na bado upatikane muda mwingine wa vipindi vya dini! Kwa mtindo huu hiyo syllabus inakwisha au shwari tu hata ikiishia katikati kama Masjid Kuba na Al Haramain?

Hebu kuweni na akili za kimaendeleo, academic discipline ni very serious issue na inadetermine matokeo ya mwanafunzi darasani. Hivi mmeshawahi kujiuliza kama ingekuwaje endapo kila mtu angekuwa na mawazo kama yenu?

Wakati wenye kupenda shule wapo tuition, nyie mpo madrassa au kwenye mihadhara lkn siku ya kusahihisha mitihani, inamlazimu msahihishaji abalansishe matokeo ili waislamu wafurahi, au? Safari yenu ndefu sana.

Unajua kisa cha viwanda vya waarabu kuendeshwa na wazungu? = akili kama hizi zako. Ndio maana BP anaongoza kwa uzalishaji wa mafuta, japo si yake ni ya Saudia.


Wewe ndie ulie mbaguzi.

Kama mtu anataka kumaliza sylabus basi asiwe na mapumziko. Kwanini watu wanapumzika siku za ijumaa pili na ijumaa mosi. Kwanini wasitumie muda huo.

Kumbuka kuwa unapoweka siku ya kipindi cha dini ni siku ya ijumaa wakti waislam wanakwenda kuswali wengine wanasoma dini hiyo ni dhulma. Kwani wakristo watapata muda wa ijumaa pili kwenda kusali wakti ni siku ya mapumziko na waislam watakosa kipindi cha dini.

Kumbuka kuwa Katiba yenu imejipambanua wazi kwa kuweka kipengele cha uhuru wa kuabudu. Na kumbuka kuwa katika mifumo yenu ya elimu kuna mitihani ya bible knowledge na Islamic knowledge na inatolewa na NECTA.

Ni vizuri muwape wote nafasi za kusoma na kusomeshwa masomo hayo bila kuathiri ibada za wanafunzi.
 
Kama kila kitu anachofanya muislamu wakati wowote, yaani saa 24 za siku ni ibada basi kuna tatizo kubwa katika kuitafsiri dini hii!

Tatizo kwako ni kutokujuwa maana ya neno ibada. Kumbuka hilo ni neno lilitokana na neno la Kiarabu kwa hiyo sikushangai kama huijui maana yake.

Ibada ni 24/7 kama humuabudu aliyekuumba kwa kufata mema na kuyaacha mabaya basi unaabudu shetani wakati unapofanya mabaya na kuwacha mema ya Muumba wako.

Neno ibada linatokana na neno "abd" (servant) sasa kama wewe sio "abd" wa aliyekuumba kwa kufata anavyotaka yeye (kumuabudu), basi wewe ni "abd" wa shetani anaekutaka ufanye kinyume na aliyekuumba.

Hata kwa kukuelezea huku nna mashaka kama umeipata maana halisi ya ibada.

NB> hata hiyo "servant" ni kwa ukaribu tu wa maana lakini si maana halisi.
 
Back
Top Bottom