KERO Wanafunzi wa Rutabo High School (Kagera) hawapewi chakula cha kutosha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto ya mazingira ya chakula hasa katika hizi Shule za Serikali zinazowaweka Wanafunzi bwenini.

Mara kadhaa Wanafunzi wamekuwa wakilalamikia uhaba wa chakula lakini suala hili limekuwa halichukuliwi hatua yoyote wakati sisi wenyewe tumepita huko.

Binafsi nilipitia changamoto ya aina hiyo na ninajua wapo wengi waliopita huko, tunatakiwa kutambua kuwa kuna kizazi kinapitia changamoto ileile.

Nikitoa mfano wa Shule ya RUTABO HIGH SCHOOL, Wilaya ya Muleba iliyopo Mkoani Kagera ina changamoto ya kuwapikia Wanafunzi chakula kidogo mpaka inafikia Wanafunzi kugombania chakula kama wakimbizi na kupelekea kuomba hela mara nyingi kwa wazazi na walezi wao.

Tatizo hili tumekuwa tukuliona sisi kama Wananchi lakini pia shule kama shule wameendelea kulifumbia macho.

Tunaomba jamii itusaidie kumulika katika shule hii ili watoto waweze kusoma kwa amani na kupata ufaulu mzuri.

==== ======

AFISA ELIMU
Alipotafutwa na JamiiForums. com kwa ajili ya ufafanuzi, Afisa Elimu Sekondari Kagera, Michael Lugola amesema "Nimepokea hayo malalamiko na maoni nitafuatilia kwa kuwa ndio nayasikia na pia ndio kwanza nimekabidhiwa ofisi wiki iliyopita."

Pia soma - Madai ya Wanafunzi wa Rutabo kupewa chakula kidogo, Afisa Elimu asema 'tatizo ni siku ya Wali na Nyama'
 
Kumekuwa na changamoto ya mazingira ya chakula hasa katika hizi Shule za Serikali zinazowaweka Wanafunzi bwenini.

Mara kadhaa Wanafunzi wamekuwa wakilalamikia uhaba wa chakula lakini suala hili limekuwa halichukuliwi hatua yoyote wakati sisi wenyewe tumepita huko.

Binafsi nilipitia changamoto ya aina hiyo na ninajua wapo wengi waliopita huko, tunatakiwa kutambua kuwa kuna kizazi kinapitia changamoto ileile.

Nikitoa mfano wa Shule ya RUTABO HIGH SCHOOL, Wilaya ya Muleba iliyopo Mkoani Kagera ina changamoto ya kuwapikia Wanafunzi chakula kidogo mpaka inafikia Wanafunzi kugombania chakula kama wakimbizi na kupelekea kuomba hela mara nyingi kwa wazazi na walezi wao.

Tatizo hili tumekuwa tukuliona sisi kama Wananchi lakini pia shule kama shule wameendelea kulifumbia macho.

Tunaomba jamii itusaidie kumulika katika shule hii ili watoto waweze kusoma kwa amani na kupata ufaulu mzuri.
Inawezekana wanapewa wanapewa ratio ya kawaida ila wao hawashibi, kushiba ni relative term, inategemea na eneo. Hiyo kanda iko serious sana kwenye misosi ukilinganisha na mikoa mingine hasa pwani. Ipo haja ya kugawa misosi kwa kuangalia mikoa. Haiwezekani mtoto wa bagamoyo apewe msosi sawa na mtoto wa kasulu au geita. Mm nafkir hivyo.
 
Mwalimu wa menu, stookipa na hm wamejiongeza.

Lazima mwalimu wa menu hubeba begi Kila siku.
 
Back
Top Bottom