Waraka wa pongezi kwa Miss Judith

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Dear Miss Judith,

Nimesukumwa na upendo mwingi wa dhati uliojaa furaha kukuandikia waraka huu mfupi kukupongeza na kukutakia heri ktk maisha yako mapya ya ndoa unayokaribia kuyaanza hivi karibuni, taarifa niliyoipata kupitia thread yako ya ”Mwaka Mpya na Maisha Mapya... Ooh, Glory to God!”

Maamuzi haya si madogo, ni maamuzi ya kuunganisha koo mbili zilizokuwa hazifahamiana na kujikuta zikijenga umoja wa kifamilia na undugu. Hapa ndipo Mawifi, Mashemeji, Wajomba, Mashangazi, Mama Mdogo, Wakwe na ndg wengine wapya huzaliwa.

Ndoa mara nyingi hufurahiwa na wengi, lakini pia wapo wachache ambao kamwe hawafurahii kusikia taarifa hizi. Wapo ambao wangependa kuona hufanikiwi, wanapenda kukuona ukiharibikiwa, mipango yako ikikwama na hufurahia kuona ukikosa furaha na amani ktk maisha yako. Watu hawa huanza kama marafiki na baadaye kukuletea umbea na maneno mabaya. Kataa maneno ya umbea, chuki, majivuno, kiburi, infedility na mengine yafananayo na hayo! Utapoteza ndoa!

Nakushauri, ili ndoa yako idumu, jitahidi sana kutimiza majukumu yako kama mama wa kiafrika. Mpende Mumeo, kumbuka kuwa Kazi ya mama ni kutunza familia, contrary na kazi ya baba ambayo ni kulinda familia! Maandiko yanasema “Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake … na mpumbavu huvunja nyumba yake …”, pia baba ni “kichwa cha nyumba …” Ubeijing usikutawale sana, ukizidi ni hatari, nimeshuhudia ukivunja ndoa nyingi. Pika, fua na shiriki kazi za ndani ukisaidiwa na msichana/mvulana wa kazi. Upendo huo, utamvuta baba pia akusaidie ktk majukumu ya ndani. Nakushauri ujifunze kuwa mnyenyekevu kwa mumeo, atakupenda, kukusaidia na kamwe hata kuacha.

Usijisahau ukasema mumeo mtarajiwa kaokoka hivyo hawezi kukamata nyumba ndogo, utakuja kulia! Tumeshuhudia watumishi wa Mungu wakinasa ktk kupata utamu usio halali! Kumbuka kumchunga kwa kumuombea na kumtunza vyema. Mfanye aone nyumbani ni sehemu ya kimbilia au tulizo la moyo wake, atakupenda daima.

Sababu za kuvunjika ndoa, ni nyingi na baadhi yake ni kutokuwa muaminifu ktk ndoa, kutokuwa na upendo wa dhati, tamaa za pesa & mali, kutokujisheshimu, kukosa mapenzi ya dhati, kulipiza kisasi, ndoa kuingiliwa na ndg, majirani & marafiki, kutokuridishana ktk mapenzi, mitazamo tofauti nk. Jiepushe na hayo ili udumu ktk ndoa yako.

Kuna yale mambo mema ambayo mlionyeshana wakati wa uchumba wenu.Yale mema na mazuri yaliyowasukuma mpaka mkaamua kufunga pingu za Maisha, hayo myadumishe, yatawadumisha pia. Usisahau mipango ya maendeleo. Kumbuka kuwapenda ndg wa pande zote, ila usiwape nafasi ya kutawala ndoa, ishi nao kwa hekima hasa mawifi!

Nakutakia mema yote ya ndoa yakukute. Ndoa yako izae matunda ya watoto wa kukutosha, wake kwa waume, na amani na upendo utawala familia yako Mpya.

Mungu awe nawe daima,
Wako,

HorsePower
 
dah...................... waraka mkali si mchezo!!.................. itabidi na mimi nikifikia hatua ya kupiga hizo pingu niwajuze wakuu huenda nikapata maushauri na mabaraka kama haya.................. hivi alisema ubwabwa wenyewe utaliwa tarehe ngapi??............. i cant miss this......... but hongera kigori wetu, hope this time lazima zile nyavu zichanike!!..................
 
Hongera sana Miss Judith!
Wengine tulisha kucheza siku nyingi sana juu ya maisha ya ndoa na vikwazo vyake, tokea siku zile za mambo ya Loliondo kwa babu, naamini ulisha'save kila ushauri kwenye pc yako!
Cha ziada kwa leo ni kidogo tu, ukumbuke kuwa MFUMO DUME UPO, NA UNAFANYA KAZI 24 HRS!
HONGERa sana.
 
hongera sana miss judy,si kazi ya kitoto uliyoifanya hadi jamaa akaona wewe ndio unafaa kuwa alpha na omega ukizingatia hasa vijana wa leo walivyo wabishi kuoa,wanajua kuchezea tu.HONGERA SANA BIBIE!
 
Hongera sana Miss Judith, Mungu ni mwema, akutangulie katika maisha yako haya mapya,yawe ya furaha na upendo.
 
Bila shaka Miss Judith (Keren Happuch) atazingatia sana huu ushauri kwa msaada wa hekima anazozipata kwa Mungu kwani ninavyomfahamu judith ni mcha Mungu sana.
Heee!:A S 465::A S 465::A S 465::A S 465:
Inawezekana hao watu wawili ni mtu mmoja?
Mbona itakuwa maajabu ya aina yake?
 
Back
Top Bottom