John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
- Thread starter
- #21
Nafahamu uzito wa shughuli zako ni Ubungo kwanza. Ubunge ni zaidi ya Ubungo. Ni nini msimamo wako juu ya haya:
-Posho. Kokote ziliko. Bado unazichukua?
-Udini. Huu unainyemelea NCHI yetu taratibu lakini kwa uhakika.
-Bunge. Bunge letu sasa ni kubwa sana. Dar peke yake ina majimbo 7 ya uchaguzi! Ya nini yote haya. Kudai maji toka DAWASCO?
-VITI MAALUM vya Ubunge. Hizi gharama zinazoambatana na viti hivi na uwingi wa viti vyenyewe na jinsi wanavyopatikana unalionaje?
-etc.,etc.
Wildcard,
Asante kwa maswali yako.
Kuhusu posho, nimeshasema: JOHN MNYIKA: Msimamo wangu juu ya suala zima la Posho!, kimsingi sichukui posho kwenye vikao vyote vya madiwani vya Manispaa, vikao vyote vya Jiji, Vikao vyote vya RCC, na bodi ya barabara. Kwa wanaohudhuria nami vikao hivyo wanajua kwamba sina kawaida ya kuchukua. Pia, posho za vikao vya kamati za kibunge ikiwemo kamati ya nishati na madini huwa wakileta mkononi nazikataa. Hata hivyo, hivyo naamini zaidi katika mabadiliko ya kimfumo zaidi ya kuwa suala la mtu mmoja au kada moja katika utumishi wa umma. Ukisoma waraka wangu wa pili kwa wananchi wa ubungo utapata pia nalichukuliaje suala la posho za vikao.
Kuhusu udini, naamini kwamba wapo viongozi ambao wanapandikiza mbegu hiyo kwa maslahi yao ya kisiasa ndio maana kwenye mchango wangu wa kwanza kabisa bungeni nilikemea hali hii na bado ni maoni yangu kwamba kadiri tunavyopigia upatu suala la udini ndio tunapandikiza mbegu hiyo. Tusiingizwe katika mitego ya kuondolewa kwenye mijadala muhimu ya kitaifa, unaweza kurejea hapa:JOHN MNYIKA: Hotuba yangu Bungeni katika Mkutano wa Pili
Kuhusu Bunge na Viti Maalum; nimekuwa nikipigia debe suala la kubadilishwa kwa mfumo wetu wa uchaguzi ili tuwe na mfumo mchanyato/mchanganyiko baina ya wabunge wa kuchaguliwa moja kwa moja na wabunge kutokana na uwakilishi wa uwiano. Nakubaliana na wote wenye maoni kwamba wilaya/halmashauri zetu ndio ziwe majimbo ya kiuchanguzi; kwa kufanya hivyo tutapunguza pia ukubwa wa bunge. Mathalani Dar es salaam nzima itakuwa na wabunge wa kuchaguliwa moja kwa moja watatu; wengine watatokana na uwakilishi wa uwiano. Hii itawezesha pia kuboresha mfumo wa uwakilishi wa wanawake ili uwe na tija zaidi. Unaweza kurejea uchambuzi wangu wa mwaka 209 kuhusu suala hili kupitia: JOHN MNYIKA: Tubadili mfumo wa uchaguzi tupate uongozi bora wenye uwiano wa kijinsia-2Kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba, nashauri uusome kwanza huu waraka kwa ukamilifu wake kwa kuwa maswali uliyouliza mengine waraka tayari umeshayajibu.
Tuendelee kujadiliana.
JJ