John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
- Thread starter
- #41
Bigup sana mh. Mnyika na pole kwa majukumu mengi najua unachoka sana kibinadamu ila mungu akutie nguvu na faraja. Naomba kuuliza juu ya daraja la ubungo msewe sijui kama kuna mpango gani labda kwa sasa au baadae.
Asante. Daraja muhimu zaidi la Msewe tulilipigia debe mwaka jana na huu kama sehemu ya kupunguza foleni na hatimaye TANROADS wamelijenga na limeanza kutumika. Tatizo ni maafuriko ya tarehe 20 Disemba yamevunja daraja lingine la mwanzo (sio hili jipya), hili tayari nimeshatembelea na kuona hali halisi wakati tunashughulikia kifo cha Mzee Ibrahim pale darajani. Kazi hii itagharimu kati ya milioni 200 mpaka 300; tayari kupitia kwa Manispaa ya Kinondoni ofisi ya Waziri Mkuu imejulishwa kuingiza kwenye mahitaji ya dharura. Nitaendelea kufuatilia ili serikali iweze kuchukua hatua za mapema. Hata hivyo kwa sasa nawaomba mtumie njia mbadala ya Kimara Bahama mama na kupitia daraja la Msewe jipya mpaka Chuo Kikuu au mnaweza pia kupitia njia ya Golani.
JJ