Waraka kwa Watanzania Wote: Amkeni

Landson Tz

JF-Expert Member
May 8, 2011
295
221
Tanganyika ilimilikiwa rasmi na Ujerumani tangu mwaka 1885 baada ya mkutano wa kugawana Afrika uliofanyika mjini Berlin nchini Ujerumani. Baada ya hapo Watanganyika walianza kutawaliwa rasmi na Mjerumu. Katika utawala wa Mjerumani, Mtanganyika aliondolewa kabisa majukumu ya uongozi na kazi hiyo kufanywa na Wajerumani. Vile vile mfumo uliotumiwa na Wajerumani kutawala, ulimnyima Matanganyika kuwa mtawaliwa anayejitambua na kumfanya awe mtumwa wa kufanya chochote alichoagizwa ikiwemo kufanyishwa kazi kwa shuruti bila malipo wala utashi wake.

Baada ya Ujerumani kushindwa vita ya pili ya dunia iliyopiganwa kati ya mwaka 1939 hadi 1945, Uingereza iliichukua rasmi Tanganyika na hivyo kumalizika kwa utawala wa Mjerumani uliochukuwa zaidi ya miaka 60 (yaani 1885 hadi 1945). Mwingereza aliendeleza utawala wa kinyonyaji kwa Watanganika kuanzia mwaka 1945 hadi mwaka 1961 ambapo Tanganyika ilikabidhiwa uhuru wake. Hivyo Mwingereza alitawala Watanganyika kwa jumla ya miaka 16 (yaani 1945 hadi 1961). Kwa hiyo ukiunganisha utawala wa Mjerumani na Mwingereza, Mtanganyika alitawaliwa zaidi ya miaka 76.

Kama ilivyokuwa kwa Tanganyika, baada ya muda mrefu wa ukoloni katika bara la Afrika, waafrika walilemaa katika kujiongoza, kuongozwa, kuongoza. Lengo la kueleza kwa ufupi historia ya ukoloni katika nchi yetu nilitaka tuelewe namna ambavyo Watanganyika walivyopata kilema cha kujiongoza, kuongoza na kuongozwa kwa muda mrefu.

Hivyo baada ya uhuru, Watanganyika walianza mazoezi ya kujiongoza, kuongozwa na kuongoza. Haya mambo makuu matatu hayakuwekwa bayana mara tu baada ya uhuru. Watanganyika waliendeleza mazoezi haya bila kujua wala kuweka muda wa ukomo wake. Baada ya miaka mitatu baada ya Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar ziliunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuzalisha Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania (1964) na kufikia ukomo wa Tanganyika hivyo katika maandishi yangu nitafuta neno Tanganyika na badala yake nitatumia Tanzania.

Kwa mtazamo wangu, muda wa mazoezi hayo ulishakwisha zamani sana japo kuwa naona Watanzania wakiendelea na mazoezi. Mazoezi hayawezi kudumu kwa muda wote huu bila Watanzania kuelewa namna ya kujiongoza, kuongozwa na kuongoza. Basi kwa kuwa imeshakuwa hivyo naomba tutangaze rasmi mwisho wa mazoezi haya kuwa mwaka huu, 2023. Na hivyo, kipindi cha mazoezi kimedumu kwa miaka 62 (1961 hadi 2023). Kipindi hiki ni kirefu kuliko kipindi alichotutawala Mjerumani na karibia mara nne (4) ya kipindi alichotutawala Mwingereza.

Hivyo tusipokubali kwa pamoja kuachana na kipindi hiki cha mazoezi, muda sio mrefu kitakuwa zaidi ya kipindi cha ukoloni. Hivi kuendelea na pindi hiki cha mazoezi tutakuwa tunamkomoa nani? Maana hata kidogo tulichovuna wakati wa mazoezi kinaweza kutokomea wakati raia wakidai uhuru kamili.

Katika kipindi cha ukoloni, wakoloni walikuwa na malengo mahususi kwa ajili ya kunufaisha mataifa yao. Malengo hayo pamoja na unyonyaji wa kiuchumi, kufanya biashara (masoko), kujipatia utajiri kirahisi na faida kubwa, kujitutumua kwa kumiliki makoloni, kuleta ukristu na ustaarabu wa kimaghalibi, kujipatia nguvu kazi kwa kuwalazimisha watawaliwa kufanya kazi bila malipo (pamoja na watumwa), kusambaza tamaduni zao pamoja na kutawala.

Katika kipindi cha mazoezi malengo hayakuwekwa wazi. Maana baada ya uhuru, kuna watu walikabidhiwa serikali na mamlaka ya wakoloni. Ikumbukwe kuwa kabla ya ukoloni hapakuwepo na kitu kilichoitwa Tanganyika wala Tanzania. Hakukuwepo na sehemu yoyote duniani iliyojulikana kama Tanganyika, hivyo kupokea Tanganyika na kuendelea nayo bila kufanya maridhiano yoyote na watu waliokokuwa wanaishi katika eneo hilo kwa kutawaliwa kwa nguvu na wakoloni haikuwa sawa. Ilikuwa ni sawa na muendelezo wa ukoloni ila kwa kutumia wakoloni weusi. Mfumo huu uliwafanya watawala weusi kuwa vibaraka wa wakoloni bila kujua.

Kutokana na manung’uniko ya chini kwa chini dhidi ya dhana hii, watawala weusi walijenga serikali yenye mfumo wa kudhibiti raia badala ya raia kudhibiti serikali. Nisiende mbali bali nikubali kuwa yote yalifanyika kwenye kipindi cha mazoezi, na Kama ilikuwa ni mazoezi ya kujiandaa kuridhiana basi tunaweza kuelewana lakini sasa mbona muda umekuwa mrefu sana?

Hivyo, ninapenda kuwajulisha kuwa tukubaliane kwa pamoja kuwa muda wa mazoezi umeishakwisha tuingie kazini. Na kazi hii si nyingine bali kujenga ustawi wa maisha yetu kama watanzania na Tanzania yetu kama taifa. Kazi hii tunapaswa kuianza kwa kufanya maridhiano ya kukubaliana namna ya kuishi katika kipande chetu cha ardhi, ardhi ya Tanzania. Maridhiano si mengine bali katiba. Kwa bahati nzuri kabla sijaandika andiko hili tayari watanzania wameishaonyesha nia ya kuandika haya maridhiano. Nia yao iko katika sheria ya katiba mpya ya mwaka 2014. Pamoja na mambo mengine, kuna hatua ambazo zilikuwa zimefikiwa ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni, kuandika rasimu ya katiba pamoja na kuandika katiba pendekezwa japo yemeye kasoro nyingi.

Chakushangaza naona tena homa ya mazoezi imerudi tena, nakuturudisha kwenye kipindi cha mazoezi tena. Kwakuwa wanamazoezi wameishazoea mazoezi basi inaonekana kama hakuna shida. Lakini shida ni kubwa sana maana Mazoezi yana angamiza taifa, na tayari watu wengi wameanza kuumia na kuchoka na haya mazoezi. Je? Tunatoakaje tena kwenye kipindi hiki cha hatari? Hapa nikili kutolaumu mtu yeyote juu ya kuendelea kuwa kwenye hiki kipindi kibaya sana cha mazoezi, bali jamii nzima yaani wanamazoezi ya kujiongoza, kuongoza na kuongozwa. Ila sasa, kuanzia sasa nimekuja kuwakumbusha kuwa pakitokea mabaya kutokana na kulazimishana kuendelea na hiki kipindi cha mazoezi nisilaumiwe kwakuwa nimewakumbusha tena. Akili iliyotuingia tukawaza katiba mpya ndio mwangaza pekee uliokuwa unaliponya taifa kutoka kwenye kilema cha ukoloni na mazoezi. Hivyo, nawasihi amkeni kumekucha tuandike katiba yetu sasa.

Haiwezeni taifa kuwa la ajabu kiasi hiki hadi watu wengine wanadhani raia wa nchi yetu hatuna akili timamu! Akili tunazo ila mazoezi yametukandamiza hadi kushindwa kujikwamua kwenye aibu nyingi. Dunia inakimbia mbio nyingi na inaendelea kutuacha, kisa tumenogewa na mazoezi. Labda niulize aliyesimamisha mchakato wa katiba mpya ni nani? Je ni kundi la mazoezi ya kuongoza au kundi la mazoezi ya kuongozwa? Hata kama hatutajua ni kundi lipi sawa tu, lakini muda umewadia wa kutoendelea kupuuza mambo ya muhimu kama haya ya kuweka maridhiano. Kukaa bila maridhiano ni sawa na kukaa bila kuwa na uhakika wa ustawi wa taifa letu na maisha yetu kwa siku za usoni.

Kuandika katiba ni hatua ya muhimu sana katika kuachana na kipindi cha mazoezi na kuanza maisha halisi ya taifa huru. Kwa sasa bado tuko kwenye kipindi cha mazoezi ya kuwa taifa huru na si taifa huru. Nina imani kuwa wengi mnakubaliana na mimi kuwa taifa letu haliko huru. Hayo mambo ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni siyo uhuru, ni mkoloni kuondoka. Kuondoka kwa mkoloni hauwezi kutafsiriwa kuwa ndio uhuru wakati tumebaki bila kuwa huru. Uhuru gani katika lindi la umaskini?
 
Tujitawale mpaka kwenye dini, tuutupe uislam, tuutupe Ukristo mbali, twende na dini zetu hizi ndizo fikra halisi.
 
..Nina imani kuwa wengi mnakubaliana na mimi kuwa taifa letu haliko huru. Hayo mambo ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni siyo uhuru, ni mkoloni kuondoka. Kuondoka kwa mkoloni hauwezi kutafsiriwa kuwa ndio uhuru wakati tumebaki bila kuwa huru. Uhuru gani katika lindi la umaskini?
Una hoja mujarab, usikilizwe
 
Naomba wakuu GT,mjikite kwenye kujadili hoja sio makosa ya uandishi.

"Akili kubwa hujadili hoja,akili ya wastani hujadili matukio na akili ya chini kabisa hujadili watu"Socreates

Wapigania uhuru wengi katika bara la Afrika hawakufaham vema wanacho pigania,ndio maana baada tu ya uhuru wengi walijikuta wakoloni weusi, tena walikuwa hatari kuliko hata wakoloni weupe.

Suala la katiba mpya Tanzania ni muhimu kwa ustawi wa taifa kwa kizazi Cha sasa na kijacho,shinda kubwa iko kwa wahafidhina ambao ni wanufaika wa katiba hii kwa kulinda vyeo vyao.

Ni muda wa kuwa na kauli mbiu "anaye kataa katiba mpya ni adui wa umma"
 
Tanganyika ilimilikiwa rasmi na Ujerumani tangu mwaka 1885 baada ya mkutano wa kugawana Afrika uliofanyika mjini Berlin nchini Ujerumani. Baada ya hapo Watanganyika walianza kutawaliwa rasmi na Mjerumu. Katika utawala wa Mjerumani, Mtanganyika aliondolewa kabisa majukumu ya uongozi na kazi hiyo kufanywa na Wajerumani. Vile vile mfumo uliotumiwa na Wajerumani kutawala, ulimnyima Matanganyika kuwa mtawaliwa anayejitambua na kumfanya awe mtumwa wa kufanya chochote alichoagizwa ikiwemo kufanyishwa kazi kwa shuruti bila malipo wala utashi wake.

Baada ya Ujerumani kushindwa vita ya pili ya dunia iliyopiganwa kati ya mwaka 1939 hadi 1945, Uingereza iliichukua rasmi Tanganyika na hivyo kumalizika kwa utawala wa Mjerumani uliochukuwa zaidi ya miaka 60 (yaani 1885 hadi 1945). Mwingereza aliendeleza utawala wa kinyonyaji kwa Watanganika kuanzia mwaka 1945 hadi mwaka 1961 ambapo Tanganyika ilikabidhiwa uhuru wake. Hivyo Mwingereza alitawala Watanganyika kwa jumla ya miaka 16 (yaani 1945 hadi 1961). Kwa hiyo ukiunganisha utawala wa Mjerumani na Mwingereza, Mtanganyika alitawaliwa zaidi ya miaka 76.

Kama ilivyokuwa kwa Tanganyika, baada ya muda mrefu wa ukoloni katika bara la Afrika, waafrika walilemaa katika kujiongoza, kuongozwa, kuongoza. Lengo la kueleza kwa ufupi historia ya ukoloni katika nchi yetu nilitaka tuelewe namna ambavyo Watanganyika walivyopata kilema cha kujiongoza, kuongoza na kuongozwa kwa muda mrefu.

Hivyo baada ya uhuru, Watanganyika walianza mazoezi ya kujiongoza, kuongozwa na kuongoza. Haya mambo makuu matatu hayakuwekwa bayana mara tu baada ya uhuru. Watanganyika waliendeleza mazoezi haya bila kujua wala kuweka muda wa ukomo wake. Baada ya miaka mitatu baada ya Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar ziliunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuzalisha Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania (1964) na kufikia ukomo wa Tanganyika hivyo katika maandishi yangu nitafuta neno Tanganyika na badala yake nitatumia Tanzania.

Kwa mtazamo wangu, muda wa mazoezi hayo ulishakwisha zamani sana japo kuwa naona Watanzania wakiendelea na mazoezi. Mazoezi hayawezi kudumu kwa muda wote huu bila Watanzania kuelewa namna ya kujiongoza, kuongozwa na kuongoza. Basi kwa kuwa imeshakuwa hivyo naomba tutangaze rasmi mwisho wa mazoezi haya kuwa mwaka huu, 2023. Na hivyo, kipindi cha mazoezi kimedumu kwa miaka 62 (1961 hadi 2023). Kipindi hiki ni kirefu kuliko kipindi alichotutawala Mjerumani na karibia mara nne (4) ya kipindi alichotutawala Mwingereza.

Hivyo tusipokubali kwa pamoja kuachana na kipindi hiki cha mazoezi, muda sio mrefu kitakuwa zaidi ya kipindi cha ukoloni. Hivi kuendelea na pindi hiki cha mazoezi tutakuwa tunamkomoa nani? Maana hata kidogo tulichovuna wakati wa mazoezi kinaweza kutokomea wakati raia wakidai uhuru kamili.

Katika kipindi cha ukoloni, wakoloni walikuwa na malengo mahususi kwa ajili ya kunufaisha mataifa yao. Malengo hayo pamoja na unyonyaji wa kiuchumi, kufanya biashara (masoko), kujipatia utajiri kirahisi na faida kubwa, kujitutumua kwa kumiliki makoloni, kuleta ukristu na ustaarabu wa kimaghalibi, kujipatia nguvu kazi kwa kuwalazimisha watawaliwa kufanya kazi bila malipo (pamoja na watumwa), kusambaza tamaduni zao pamoja na kutawala.

Katika kipindi cha mazoezi malengo hayakuwekwa wazi. Maana baada ya uhuru, kuna watu walikabidhiwa serikali na mamlaka ya wakoloni. Ikumbukwe kuwa kabla ya ukoloni hapakuwepo na kitu kilichoitwa Tanganyika wala Tanzania. Hakukuwepo na sehemu yoyote duniani iliyojulikana kama Tanganyika, hivyo kupokea Tanganyika na kuendelea nayo bila kufanya maridhiano yoyote na watu waliokokuwa wanaishi katika eneo hilo kwa kutawaliwa kwa nguvu na wakoloni haikuwa sawa. Ilikuwa ni sawa na muendelezo wa ukoloni ila kwa kutumia wakoloni weusi. Mfumo huu uliwafanya watawala weusi kuwa vibaraka wa wakoloni bila kujua.

Kutokana na manung’uniko ya chini kwa chini dhidi ya dhana hii, watawala weusi walijenga serikali yenye mfumo wa kudhibiti raia badala ya raia kudhibiti serikali. Nisiende mbali bali nikubali kuwa yote yalifanyika kwenye kipindi cha mazoezi, na Kama ilikuwa ni mazoezi ya kujiandaa kuridhiana basi tunaweza kuelewana lakini sasa mbona muda umekuwa mrefu sana?

Hivyo, ninapenda kuwajulisha kuwa tukubaliane kwa pamoja kuwa muda wa mazoezi umeishakwisha tuingie kazini. Na kazi hii si nyingine bali kujenga ustawi wa maisha yetu kama watanzania na Tanzania yetu kama taifa. Kazi hii tunapaswa kuianza kwa kufanya maridhiano ya kukubaliana namna ya kuishi katika kipande chetu cha ardhi, ardhi ya Tanzania. Maridhiano si mengine bali katiba. Kwa bahati nzuri kabla sijaandika andiko hili tayari watanzania wameishaonyesha nia ya kuandika haya maridhiano. Nia yao iko katika sheria ya katiba mpya ya mwaka 2014. Pamoja na mambo mengine, kuna hatua ambazo zilikuwa zimefikiwa ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni, kuandika rasimu ya katiba pamoja na kuandika katiba pendekezwa japo yemeye kasoro nyingi.

Chakushangaza naona tena homa ya mazoezi imerudi tena, nakuturudisha kwenye kipindi cha mazoezi tena. Kwakuwa wanamazoezi wameishazoea mazoezi basi inaonekana kama hakuna shida. Lakini shida ni kubwa sana maana Mazoezi yana angamiza taifa, na tayari watu wengi wameanza kuumia na kuchoka na haya mazoezi. Je? Tunatoakaje tena kwenye kipindi hiki cha hatari? Hapa nikili kutolaumu mtu yeyote juu ya kuendelea kuwa kwenye hiki kipindi kibaya sana cha mazoezi, bali jamii nzima yaani wanamazoezi ya kujiongoza, kuongoza na kuongozwa. Ila sasa, kuanzia sasa nimekuja kuwakumbusha kuwa pakitokea mabaya kutokana na kulazimishana kuendelea na hiki kipindi cha mazoezi nisilaumiwe kwakuwa nimewakumbusha tena. Akili iliyotuingia tukawaza katiba mpya ndio mwangaza pekee uliokuwa unaliponya taifa kutoka kwenye kilema cha ukoloni na mazoezi. Hivyo, nawasihi amkeni kumekucha tuandike katiba yetu sasa.

Haiwezeni taifa kuwa la ajabu kiasi hiki hadi watu wengine wanadhani raia wa nchi yetu hatuna akili timamu! Akili tunazo ila mazoezi yametukandamiza hadi kushindwa kujikwamua kwenye aibu nyingi. Dunia inakimbia mbio nyingi na inaendelea kutuacha, kisa tumenogewa na mazoezi. Labda niulize aliyesimamisha mchakato wa katiba mpya ni nani? Je ni kundi la mazoezi ya kuongoza au kundi la mazoezi ya kuongozwa? Hata kama hatutajua ni kundi lipi sawa tu, lakini muda umewadia wa kutoendelea kupuuza mambo ya muhimu kama haya ya kuweka maridhiano. Kukaa bila maridhiano ni sawa na kukaa bila kuwa na uhakika wa ustawi wa taifa letu na maisha yetu kwa siku za usoni.

Kuandika katiba ni hatua ya muhimu sana katika kuachana na kipindi cha mazoezi na kuanza maisha halisi ya taifa huru. Kwa sasa bado tuko kwenye kipindi cha mazoezi ya kuwa taifa huru na si taifa huru. Nina imani kuwa wengi mnakubaliana na mimi kuwa taifa letu haliko huru. Hayo mambo ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni siyo uhuru, ni mkoloni kuondoka. Kuondoka kwa mkoloni hauwezi kutafsiriwa kuwa ndio uhuru wakati tumebaki bila kuwa huru. Uhuru gani katika lindi la umaskini?
Tanzania haijawai kuwa colony la muingereza chukua hio
 
Ni WARAKA sio Walaka
Uingereza ilichukua mamlaka ya Tanganyika baada ya vita vikuu vya kwanza sio vya pili
Hoja hapa siyo kujua historia vizuri au kiswahili, hoja ni kwamba watanzania tunahitaji katiba ili tuanze rasmi maisha katika Tanzania huru
 
Back
Top Bottom