Waraka maalum kwa wana Mtwara na kusini kwa ujumla

Hata kama sio mwanakusini anahitaji kujibiwa kwa hoja! mleta mada kaleta hoja sio unajibu majibu mepesi na yenye kebehi! hii ni JF mpya ya zamani watu walikuwa wanaficha "upumbavu" wanajibu hoja kwa hoja, siku hizi watu wanaonyesha "upumbavu" wanasahau kujibu hoja!:shock:

Hoja yake haina uzito wowote zaidi ya kuwakebehi wana mtwara
 
gesi kwanza,wanantwara hatujaambiwa kinaganaga pato halisi la gesi litakuwa kiasi gani kwa kila ujazo cm3 1 bei gani,pia product nyingine zitokanazo na gesi zitachakatwa wapi, pia cylinder package za kupikia,kuchomelea nk zitafanyikiwa wapi hatujasikia upembuzi yakinifu kama ulofanywa wa kutandika bomba kwa miezi18, je? package kwenye cylinder itafanyikia wapi maana ndo inaweza kutoa ajira nyingi zaidi,tunataka kujua mipango ya serikali sio Dangote mnigeria
 
HAPO UMENENA NDG,MAANA TUNAKIMBIZANA PASIPO SABABU,TUACHANE NA HAO WANASIASA AMBAO WANATURUDISHA NYUMA KILA SIKU.KAMA MPK HUDUMA MUHIMU ZINASITISHWA WADHANI MAENDELEO YATAKUJA KWA MTINDO HUO?:smash:
 
Wana jf habari zenu. Hoja hujibiwa kwa hoja na sio kumkejeli mtu, mimi namuunga mkono mleta mada. Na zile kauli zinazosema muwataje hao wanaotumiwa ikiwa hawajui jee ndio aseme hakuna wanaotumiwa. Mfano wewe MKOROSHO KIGOLI unatumiwa ili hoja za maendeleo uzipinge bila ya kuleta utetezi wa kuzipinga hoja hizo. Penye maendeleo siku zote hutokeza watu wavivu wasiopenda maendeleo na ukiwaletea maendeleo wao wanataka uwaweke ofisini tu. Kwenye utendaji hawataki. Tuwalaani wavivu na tuwapongeze wanaotuamsha kihabari na kutupa mbinu za kuweza kujipatia kipato, japo kutoa huduma kwa waajiriwa.
 
:yell:WANA MTWARA TUTAFAKARI MBONA SERIKALI IMETULETEA MWEKEZAJI ANAJENGA KIWANDA CHA SARUJI NA VIJANA TUTAPATA AJIRA! MBONA YETU INAJENGWA NA RELI KWENDA KIWANDA CHA SARUJI VYOTE VINALETA AJIRA KWETU! SERIKALI INASEMA GESI GESI KWETU KWANZA NA ITAKAYO BAKI NDIYO ITASAFIRISHWA ILI KUPATA SOKO NA MAPATO ZAIDI. HAYA YOTE NI MAENDELEO KWETU TUSIKUBALI KUTUMIWA NA WATUILI WAPATE MASLAHI YAO. KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI ILI NASI TUPATE AJIRA MAISHA YETU YAWE JUU. WATU WASIOTUTAKIA MEMA WANATUSHAWISHI ILI TUGOMEE MAENDELEO ILI WAENDELEE KUKUTUMIA KWA FAIDA ZAO, MTWARA TUAMKE TUKATAE MAANDAMANO, TUWEKEZE NGUVU ZETU KUTENGENEZA MAENDELEO YA MTWARA, TUSIWAKUBALI WANAOTAKA KUTUTUMIA VIBAYA, TUAMKE SASA! :nod:

Wewe si mwana Mtwara.Wewe ni Bwana Mtwara.
 
Hoja yako ni ya msingi. Fursa zinawafaa waliondaliwa. Wanamtwara mmeandaliwa kielimu? Ajira zitawanufaisha wenye ujuzi wao. Wanamtwara wasiosoma watafanya kazi ngumu za vibarua tu! Kazi za ujuzi kwenye viwanda vya Saruji zitafanywa na wageni! Piganieni Elimu. Raslimali ya nchi ni kwa wazawa. Wazawa hawajaandaliwa! Maccm na watoto wao yatavuna raslimali ya Mtwara na kuwekeza Uswiss! Amkeni! Itafuteni Elimu kwanza. Kaeni na ndoto za gas. Wahenga wetu waliporwa nchi kwa kukosa Elimu na siraha bora tukatawaliwa na wakoloni! Geukeni Nguvu na mamlaka ya umma ndio suluhisho. Kaeni na ujamaa na kujitegemea ulimshinda Mwalimu! Mtwara oyeee.. M4C suluhisho lenu 2015
 
Mnaandama kwa ajili ya gas mnashindwa kuandamana kwa ajili ya matokeo mabaya ya ufaulu drs 4,7,kidato cha pili na cha 4. Hahaha! Watoto wenu hawana madawati na vitabu! Tushikamane kuleta mabadiliko ya kweli ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Tanzania Oyeee.,
 
1. We bwana mleta mada hujui hoja za wanaMtwara wala kilio chao. Hivyo mada yako haina na inakosa mashiko.

2. Karibia viongozi wote wenye uthubutu wameshasema wazi kuwa wanaMtwara wana hoja za msingi hivyo wanapaswa kusikilizwa. Na wale waliobaki kimya ni wale ambao kazi yao haina tofauti na uifanyayo wewe hapa jamvini.. Kuchumia tumbo kwa maslahi ya Magogoni na Lumumba.

3. Wewe sio mfuatiliaji wa historia ya sakata hili na hujishughulishi kuutafuta ukweli bali unasubiri kusikia Mtwara kuna jambo ndipo unarukia kuandika chochote kufurahisha kundi unalolijua wewe.

4. Hali ya mambo hapa Mtwara si kama wengi mnavyodhani na kujifariji kuwa suala hili lina mkono wa wanasiasa. Suala hili ni matunda ya sera mbovu za Serikali yetu tangu uhuru kuhusu mgawanyo wa raslimali. Ni suala la wakati.

5. Nakushauri jaribu kufuatilia suala hili ktk media tofauti na hizo unazotumia hadi kusababisha niamini umelishwa uozo unaosambazwa na watawala wetu kuhusu Mtwara na sakata zima la gesi asilia.

HAITOKI GESI MPAKA KIELEWEKE.....
GESI KWANZA UHAI BAADAE... Habari ndio hiyoo!
 
Nyie mnaotumwa na mafisadi ccm ingekuw vema sn hayo maneno muje kuyazungumza hadharani huku Mtwara ili mubaini ukweli kuw wanakusini wametumwa au ni uma wenyewe umeerevuka n kujua haki yao! Then kuna vilaza wengine wanajaribu kutetea wizi wa mafisadi eti kwa kudai maslahi ya uma....kuchimba bandari Bagamoyo na kuiacha ya Mtwara ambayo ni kubwa na natural huo ndo utaifa?? Kuua mradi wa Mtwara Coridor na kuhamishia Bagamoyo huo ndo utaifa?Mtwara, Lindi na Ruvuma hakuna hospitali ya rufaa je mbona hayo hamuhoji?? EBWANA CCM NA SERIKALI YENU MUSHATUDHARAU SN TANGIA UHURU NA SS BAAAASI, GAS HAITOKI KAMWE P.MB.FU.
 
Back
Top Bottom