Tukubali tukatae ukweli ni kwamba kuna watu wana maslahi yao binafsi hapa, na hao watu wahatufai kwa sababu wabinafsi hawana uzalendo wala hawaweki maslahi ya taifa mbele, tusipokuwa makini tutaumia
Mbona mnasema tu kuna watu wanamaslahi binafsi bila kuwataja hao watu na hayo maslahi yao?
Sisi wana Ntwara tunaamini wenye maslahi binafsi ni mafisadi wa ccm wanaouza rasilimali za Nchi kwa kisingizio cha uwekezaji.
Wana Ntwara hatutaki kuwa kama watu wa Tarime mliowaachia mashine pale Buhemba baada ya dhahabu kuisha.
Tutapambana mpaka mwisho lakini gesi haitoki.