Waraka: Alphonce Lusako alias Emekha Ikhe kwako prof. Rwekaza Mkandala

Mhimili wa uovu!
Hata kama haumo ktk mhimili huo lkn u mtetezi wa Mhimili huo mwovu. Anyway, matunda ya hao unaowatetea tumeanza kuyaonja; kwenye matokeo ya kidato cha nne na mauaji yanayohusishwa na dini.

matunda kivipi au hukuelewa topic
 
Pole Alfonce. It is a touching story japo sielewi kwa undani matatizo haya. Bottom line Mkandala ni SSM, ni mtua yuko kwenye mfumo. Ikumbuke REDET na kazi zake!!! Na yeye aliiongoza!!! Ila tu kwa uongozi wake Chuo kimedorora mno!!! Sifa ya The University of Dar es Salaam imepotea kabisa, iliondika na VC aliyepita!!! Ila nakuhakikishia kuwa Mungu amekupangia maisha mengine tena ya mafanikio sana!! Kuna watu wameishia form vi and are doing extremly better. Na hatimaye utaweza kujisomesha mwenyewe nchi za nje miaka ijayo. Do not worry kabisa. Wewe jisanganye tu na watu bila kujali na utanyanyuka kimaisha tu.
 
Pole sana kijana. Mungu atakufungulia njia nyingine. Siku zote AMINI KWAMBA njia A ikifungwa, basi njia B itafunguliwa. Na ni mara nyingi sana, NJIA B ni bora kuliko njia A. Hivyo, kamwe usikate tamaa, kwani hakuna ajuaye, na si wote waliofanikiwa wamepata elimu ya chuo kikuu.

Narudia tena, poleni sana, kwani maelezo yako yana uchungu sana.

NB: Nimeona sehemu, mmoja wa watu waliosoma habari hii hapa JF na kupeleka hii habari kwenye website ambayo Prof. Mukandala ana access nayo, akishauri ulinzi zaidi kwa VC na Manaibu wake hasa wanaposafiri na hata wanapokuwa kwenye mazoezi binafsi. Usishangae, kwani hawa ndiyo wasomi wetu wa siku hizi, wasiotaka kuchukua muda na kufikiria na kuleta au kupendekeza ufumbuzi wa matatizo mengi yanayoyotukabili, na badala yake wanafikiria kujipendekeza kwenye system ili baadaye waweze kupewa nafasi kwenye teuzi za kisiasa.
 
hakika kijana hata kama una msimamo huo ulionao lakini kumbuka ungeweza kujishusha chini na kukubali kuomba msamaha ili uweze kupata elimu amabayo unasema ni haki yako,ukiwa na msimamo huo utaendelea kulilia humu mitandaoni bila tija yoyote,wale uliowapigania sasa wengine wameshamaliza na wapo makazini we bado una hangaika tu.

.kwangu mimi hao hata kama ni hofu,shaka na woga ndio vilivyowafanya waombe msamaha kama unavyosema wewe:naona ni watu waliochukua maamuzi ya busara ili tu waweze kupata kile wanachokihitaji kwani kama ni mapambano wanaweza kuyafanya hata baada ya kupata kile wanachokihitaji.

ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE. ?

NB:pOLE KWA YALIYOKUKUTA ILA USHAURI WANGU NI KWAMBA BORA UFANYE YALE WANAYOYATAKA KWA MUDA HUU ILI UWEZE KUTIMILIZA NDOTO YAKO YA KUPATA ELIMU VINGINEVYO NDUGU YANGU MALALAMIKO YAKO HAYATAISHA MAJUKWAANI.NI BORA UJIFANYE MJINGA ILI UPATE UNACHOKITAKA.FIKIRIA WALE ULIOKUWA UKIWAPIGINIA HIYO HAKI WAKIO WAPI?JE HATA SIKU MOJA WAMEAHI KUKUMBUKA?YOU STAND ALONE

maisha bila elimu ya chuo kikuu inawezekana. hao unaosema kuwa wanaweza kuendeleza mapambano baada ya kupata elimu hawawezi daima watageuka kuwa vibarakwa wa watawala

 
Prof. Mkandara Mungu wetu yupo, Jack Zoka Mungu wetu yupo watawala wenye nia mbaya na Tz Mungu yupo hakika Mungu wangu yuko hai ukweli utashinda kwa kishindo machozi yanatoka lakin ipo siku yatakwisha naamini hvyo nitaendelea kuomba kwa Mungu wangu.

aminaaa brozer
 
mkandala kawa feki anaabudu form 4 anasahau uprof.wake kawa mtumwa wa ccm nadhan angekuwa na power hata kitila angemfanyia hila ka alvyomfanyia baregu...
 
how long for these injustices? not long. we must fight them side by side, inch by inch and cm by cm until we win the batle. join me in this struggle coz together we shall overcome...
 
acha kumhadaa huyo kijana,fursa yake ya kupata elimu ya juu ni sasa na siyo 2016,mambo uwenda yakibadilika,kufukuzwa chuo siyo mwisho wa yeye kupata elimu kwa sasa,kuna mambo mengi ya kumsaidia pasipo kuingiza siasa,tuanzie hapo sasa.

Sema sasa wewe mambo gani ya kumsaidi.
 
yap, baadhi nawafahamu, pia nafahamu kuwa siwezi sameheka from these injustice people. nimetembea sana ndani na nje ya mfumo wa nchi yangu kuueleza ukweli halisi kinyume na taarifa walizozitoa wao. nafahamu jinsi gani watawala wa chuo changu walivyoulisha sumu mfumo mzima. nafahamu ni nini wamekipanga juu yetu. lazima niseme kuwa nahitaji mimi kuwasamehe wao kwa ukatiki walio nitendea na walicholitendea taifa. lazima niliambie taifa langu kweli kuwa kunawatu ambao ni hatari kwa maisha ya taifa langu kabla ya kifo changu. na niwaambie wavujajasho wa taifa hili kuwa watoto zenu wamefukuzwa kwa sababu ya uzalendo wa taifa lao hivyo wawaunge mkono kwa namna moja au nyingine katika mapambano ya kulikomboa taifa langu... wasikate tamaa kwani hakuna marefu yasiyo na ncha. patient, percstance and percivialence toward justice ndicho kinahitajika.
 
GOD is Marching, Mungu wangu anapigana sasa, hakika amesikia sauti za wanyonge.. na hakika yeye ndiye mwenye suluhu ya wenzangu wote waliofukuzwa vyuo kwa sababu ya kutetea haki zao za msingi na haki za taifa hili. Lakini lazima niseme kweli ya moyo wangu. leo mafisadi papa wanapunga mikono majukwaani lakini watetezi wa wanyonge tulitupwa segerea, keko, leo twiga, tembo na wanyama wengine wanasafirishwa kwa manufaa ya wachache, walioshiriki wapo na wanapunga hewa safi nje ya magereza, nchi yetu imebakia mashimo tu madini hayapo na yamenufaisha wachache walio husika wapo tu na wana amani. leo walio saini mikataba iliyoligharimu taifa wapo na wanapata hewa safi nje ya magereza, waliotuingiza katika giza la elimu wapo na hawawazi hata kung'atuka, leo nchi yangu imekuwa shamba la bibi na waliosababisha haya wapo. mimi ninaye simama kuhoji, kukosoa, na kutoa ushauri juu ya kuenenda vyema nafutwa kwenye mfumo wa elimu ndani ya taifa langu. Mwenyezi Mungu hajalala. na Mungu asipoulinda mji, binadamu anajisumbua bure. timua timua vyuoni ni janga la kitaifa ndani ya vyuo vyetu. limeligharimu taifa, limeumiza taifa, limeumiza familia nyingi za walala hoi. lazima yote haya yapimwe kwenye mizani ya haki. kisha yaamuliwe kwa haki. hakuna jambo jema hapa duniani zaidi ya kuwatendea haki binadamu wasiojiweza, kutumia madaraka kama nyundo ya kuwapigia walalahoi ni kumchokoza mungu, hakika Mungu hawezi kuacha ukatili uendelee milele. hivyo Mh. Profesa afahamu. atende haki ndio ulinzi.
 
Aisee pole sana hebu mtafute Dr Kitime wa SAUT Mwanza najua atakusaidia kuipata elimu ya Chuo Kikuu kwenye vyuo vyake aisee, japo nasikia mkataba wake ndio unaisha!!
 
Ipo siku jua litakuwa giza kuu kwa walio tutenda mabaya kwa wanyonge wa taifa hili, maiti zao zitakuwa jehanamu kwao kabla hawajafa.,,,
 
Du bwana mkubwa pole sana ila haki hushinda dhuluma. Usiogope, wala usihuzunike kwani ktk harakati hizi hutakiwi kurudi nyuma, utakuwa jiwe la chumvi.

We are going to have freedom soon.
If you want to walk a long distance and faster than any one then walk alone. Si lazima usome UDSM.
 
Prof. Mkundala is also a professor in this type of game. Be on his way, he will show you fully his capacity. He is excellent in Academic FITINA. Katengeneza mazingara na kuwatenda wahaya wenzie itakuwa wewe mtu wa mataifa. Ni yeye aliyemwondoa Prof. Baregu Mlimani. Na ni yeye aliyakataa kumwongezea mkataba Dr. Azaveli Lwaitama. Ni yeye "amecontrol" situation mlimani hakuna wasomi kuikolomea kolomea serikali sikivu ya CCM. Yeye anadeal na watu individually. Si unaona siku hizi panel discussion zilivyopungua chuo? na hata zikitokea zinakuwa za ushabiki fulani hivi kama za kumwita Membe afunge mjadala. Critical thinking hiyo haimhusu. Chezea Mkandala wewee anatisha
 
Sasa nimeelewa kwanini Mnyika JJ alisema atamalizia masomo yake mpaka CDM ichukue iingie madarakani.Naye angekosea timing angedisco
 
mkuu pole sana,wewe ni kizazi cha akina Nyerere,Isiaka Steven,Mandela,Gamal Abel Nasser,Lumumba nk, ambao walijitolea kwa dhati dhidi ya africa lkn leo historia imewatupa,usiofu tupo pamoja songa mbele
 
Back
Top Bottom