Waraka: Alphonce Lusako alias Emekha Ikhe kwako prof. Rwekaza Mkandala

Aug 31, 2011
35
27
WARAKA WA ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE KWAKO PROF. RWEKAZA MKANDALA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

NI VEMA UNGENIPIGA RISASI NIKAFA NIKAPOTEA DUNIANI KWA UDHALIMU ULIOSHINIKIZWA KUFANYA JUU YANGU NA WANAFUNZI WENZANGU NDANI YA TAIFA LANGU.KULIKO KUKUPIGIA MAGOTI NA KUDHARAU UTU WANGU KWA KUKUOMBA MSAMAHA USIOTOKANA NA DHAMIRA YA MOYO WANGU. HOW LONG FOR THESE INJUSTICES IN MY COUNTRY - NOT LONG MR. PROFESSOR.

Pilato anamuhukumu yesu ingawa haoni kosa lake, anawaogopa wayaudi, anabembeleza urafiki wa kaysari. Ee Yesu usiye na kosa, hata mimi ningeweza kutenda mema mengi lakini naogopa macho ya wenzangu na maneno yao. Ee bwana uniimarishe utashi wangu nijitegemee katika kushika madaraka yangu.

"Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda".


Ni maneno yako Prof. Rwekaza Mkandala uliyoyatoa tarehe 14/12/2012, katika ofisi yako tukiwa na kikao baina ya sisi wanafunzi nane {8}tuliokwisha fukuzwa UDSM kwa maandamano niliyoyaongoza tarehe 11/11/2011, ya kudai haki za watoto wa wavuja jasho walionyimwa mikopo ndani ya vyuo vikuu vya umma nchini, akiwepo Prof. Makenya Maboko na Prof. Yunus Mgaya.".nilisikitishwa sana na kauli yako ambayo mpaka leo naikumbuka "chuo hiki kinawenyewe na wenyewe wako mjini".

Mimi binafsi nafahamu kwa dhati ya moyo wangu kuwa chuo hiki ni cha watanzania na si cha mtu binafsi au genge la wahuni Fulani ambao wako mjini kama ulivyosema ambao wanaamua kufanya lolote baya wanalolitaka kulifanya sababu ya madaraka waliyonayo. Tumewapeni madaraka na mamlaka ya kutuongoza kwa mujibu wa katiba ya nchi yangu na hatujawapa madaraka hayo kama nyundo ya kuwapigia wavujajasho ndani ya taifa langu.

Mh. Profesa, nimeona nikusalimu kwa kumbukumbu iliyopo hapo juu na niendelee na maada iliyonisibu, lakini pia usisahau kuwahabarisha usalama wa taifa unaofanya nao kazi, maprofesa wengine hata wanaotoka vyuo vingine ambao walishiriki kufanya maamuzi ya kidikteta ya kuwafukuza wazalendo wa taifa hili ambao naamini ni maraisi wajao, mawaziri wajao, wabunge wajao, wakuu wa mikoa na wilaya.nk.. ndani ya vyuo vyao kwa kushinikizwa na wanasiasa walioko mjini kama ulivyokuwa ukijitetea machoni petu kinyume na kweli uliyokuwa unaifahamu.

Lakini pia ni vyema ukawataarifu hao binadamu wa mjini waliokuwa wanakushinikiza kufanya maamuzi ambayo moyo wako haukuridhia, wataarifu kuwa kijana Yule Yule niliyemtimua UDSM amesema kuwa "madaraka mliyo nayo sio ndoa ya milele hivyo waitendee haki nchi yangu, Nguvu ya pesa walizonazo hazina nafasi milele ya kupoteza haki ya binadamu yoyote Yule kwa sababu Mungu ni taa ya kila mwanadamu.

Kwa kitendo ulichonifanyia na ulichowafanyia wanafunzi wenzangu ambao mpaka sasa wamepoteza ndoto zao kielimu ndani ya Taifa lao hakita potea hivi hivi kama unavyofikiri, kwa sababu ni kinyume na katiba ya nchi yetu ibara ya 11[2,3] inayotoa fursa kwa kila mtanzania kupata haki yake ya msingi kielimu ndani yataifa lake.

Mh. Profesa, nakumbuka taarifa za upotoshwaji ulizozitoa mbele ya vyombo vya habari juu yangu na juu ya wanafunzi wenzangu zenye lengo la makusudi la kuchafua taswira zetu kwa jamii. Ni ukweli kwamba unamamlaka, unanguvu ya Pesa na unashirikiana na mfumo wa usalama wa taifa na uongozi uliopo madarakani kuyafanya uliyoyafanya na unayoendelea kuyafanya. ndio maana uliweza kutumia vyombo vya habari vibaya lakini utambue kuwa haki ya mtu inacheleweshwa tu haipotei, hata ningepigwa risasi kwa wakati huo naamini wapo wazalendo wangesimama kutetea haki yangu nikiwa kaburini.

Ni ukweli kwamba Umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na familia zetu, ndugu na jamaa, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuudanganya umma, umefanikiwa pia kwa kiasi kikubwa, kutoa taarifa za uongo ndani ya mfumo na nje ya mfumo. lakini hujafanikiwa kitu kimoja cha msingi kunitenga mimi au sisi na Mwenyezi Mungu.

Mh. Profesa, nimeona umekuwa ni profesa mmoja hatari sana ndani ya nchi yangu uliyekubali kudharau utu na taaluma ya uprofesa ulionao, uliyekubali kuminya uwezo wako halisi wa kifikra kwa sababu ya shinikizo la wanasiasa unaodai wako mjini ambao kiuhalisia hawana hata uprofesa ulionao. Umekubali kuwaabudu mashetani wanaokushinikiza kufanya zambi za makusudi katika kupoteza ndoto za vijana watokao katika familia za wavujajasho. umekuwa ni pilato wa enzi za YESU.

Utambue kuwa Vilio vya vijana tuliofukuzwa vyuoni, vilio na manunguniko ya ndugu, jamaa na wazazi wetu, dua tulizoomba kwa Mwenyezi Mungu, hakika zimemfikia Mwenyezi Mungu na usubiri majibu yake wakati wowote tangia sasa. Ni heri vita inayotafuta haki kuliko kuendelea kuabudu shetani mwenye majina matatu "HOFU, WOGA NA SHAKA". Ni heri nipigwe risasi katika mapambano haya nikaweka historia ndani ya taifa langu kuliko nikaacha dhamira yako ya dhati ikanimaliza ndani ya taifa langu kimya kimya. Lakini pia NI BORA NIKAWA FORM SIX LEAVER MILELE, MWENYE FIKRA HURU KWA MASLAHI YA WATANZANIA KULIKO NIKAKUBALI KUUZA NA KUUDHARAU UTU WANGU KWA KUMUOMBA MSAMAHA PROFESA YOYOTE YULE ANAYEKANDAMIZA HAKI ZA WANYONGE NDANI YA NCHI YANGU.

Mh. Profesa, unalizika Taifa langu kwa kuzika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mwenendo hasi wa chuo kikuu chochote kile duniani ni muenendo hasi wa taifa husika. Umekuwa ni profesa kiongozi wa kulizika taifa langu na hii nikutokana na upeo wa mtazamo wangu. Umehusika kikamilifu katika harakati za kuzima fikra huru za wanafunzi ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam, unatumia madaraka yako vibaya kwa kuwafukuza wanafunzi waliojitambua, wenye uwezo wa kuhoji mambo, kukosoa mambo, na kushauri mambo kwa mustakabali mwema wa taifa lao.

Unamikakati ya makusudi ya kukiweka chuo kikuu cha Dar es Salaam kiwe genge la wahuni, genge la walanguzi na kisiwe kisima cha fikra huru "think tank of our nation" kama mwanzo kilivyokuwa, unamalengo ya dhati ya kutengeneza Taifa la Mambumbumbu ili watoto zenu na watoto wa viongozi wenzako walioko madarakani waendelee kulitawala taifa langu milele, unawafundisha wasomi nidhamu ya uoga, unashirikiana na usalama wa taifa kuwatisha wasomi wawe ni wasomi wa madesa na si kulisaidia taifa lao kwa kujadili mustakabali wa taifa lao.

Unaendelea kuwa chanzo cha kuzalisha viongozi mbumbumbu wataoligharimu taifa langu kama wengine walivyoligharimu taifa hili. Nikueleze ukweli kuwa Ukimya wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine nchini Unabomu zito litalolipuka mda wowote tangia sasa. Umewakandamiza kwa mda mrefu, wasomi wanamatatizo mengi ambayo yanahitaji kutatuliwa kidiplomasia, kwa sababu unatumia nguvu kubwa kuwanyamazisha hakika watatatua matatizo yao kwa nguvu. Huu ni unabii wangu ambao hakika siku za usoni utatimia. Umefika wakati wako wa kusoma alama za nyakati. Wasomi wamechoshwa kukandamizwa, wasomi wanataka walisaidie taifa lao ambalo kwa mda mrefu limekuwa shamba la bibi.

Wasomi wanataka kuwa na uhuru wa mawazo, uhuru wa kukusanyika na kujadili mabadiliko wayatakayo ndani ya taifa lao. Tusipopata mabadiliko kwa njia ya kidiplomasia tutayapata kwa njia ya nguvu.

Mh. Profesa, Napenda ufahamu kuwa duniani hakuna jipya, mtesa na mteswa wote hatima yao kifo yaani binadamu huishi mara moja tu na hufa. Hakuna mtu kutokana na madaraka yake, vyeo vyake, umaarufu wake, hadhi yake ya elimu atakufa atazikwa hewani. Sisi sote tutarudi vumbini. Jaribu kuitendea haki taaluma ya uprofesa kwa kulisaidia Taifa hili, kinyume na hilo utabakia na uprofesa wa jina usio na faida ndani ya taifa langu.

Nimefikia sehemu ninahoji uhalali wa uprofesa wako kwa sababu, mambo unayoyafanya ndani ya Taifa langu yananipa wasiwasi kwani hayaendani na taaluma uliyonayo. Mh.Profesa naomba litendee haki taifa langu, wewe ni mzee kwa umri sasa tuachie vijana tutaoishi na taifa hili kwa mda mrefu. Kiache chuo kikuu cha Dar es salaam kiwe huru. Usiendeleza udhalimu uliokwisha tufanyia sisi, kinyume na hayo dhambi hii itakutafuna leo na mpaka kaburini kwako.

Namalizia kwa kumnukuu Hayati Mwalim. J.K. Nyerere aliyesema kuwa kazi kubwa ya vyuo vikuu ni kutafuta ukweli, kusema ukweli na kuuishi ukweli huo kwa gharama yoyote ile bila kujali madhara yatakayokutokea kutokana na kweli uliyoisimamia. Nitasema ukweli daima fitina kwangu mwiko. Kwa wale wote walioandika barua za msamaha kwenu hawakujua walitendalo,walivamiwa na shetani mwenye majina matatu "HOFU, SHAKA NA WOGA".

Kwa sasa wanajuta, wamekubali kushusha utu wao kwa sababu ya ukatili wenu. Niliwahi jiuliza swali moja kwa nini waasi wanatokea katika mataifa mengine, nimepata jibu kutokana na mazingira niliyopo tusifikie huko lakini najua unakifahamu ulichokifanya, najua unafahamu upotoshwaji ulioufanya ndani ya mfumo wa uongozi wa nchi hii na nje ya mfumo, najua unafahamu umepoteza nafsi ngapi za vijana kwa kupoteza ndoto zao kielimu. Yote haya uyapime katika mizani ya haki na ujiulize kutokana na uliyo yafanya unastahili nini hapa duniani.

Mh. Profesa. Nakutakia tafakari njema. Muombe Mungu Hekima na Busara zenye utashi wa kujitegemea katika madaraka yako. Kinyume na hapo unarithi ya pilato, sauti za walala hoi, wavujajasho wa taifa hili zitakulilia hata kaburini kwako.

ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA

TRUTH IS POWER, CHANGES IS MY MISSION AND GOD IS MY LEADER.
 
Solidarity forever but not for everything.Uliowapigania haki zao hawawezi kukuchangia hata ada ya ku-reseat,Kwa sasa,Yesu mwenyewe aliomwomba mungu amuondolee kikombe cha mateso,ingawa alitumwa kuwakomboa wana wa israeli.Kwa taarifa yako usalama wa taifa wamo miongoni mwa uliokuwa unapigania haki zao,
 
Mkuu ALPHONCE LUSAKO, pole sana kwa changamoto ulizokutana nazo hapo chuoni, lakini nimefarijika sana baada ya kung'amua ya kuwa wewe ni miongoni mwa vijana wachache wanao jitambua. Tafadhali zingatia yafuatayo;

  • [*=left]Haijawahi na haitatokea nguvu ya dhuruma ikaishinda nguvu ya haki.
    [*=left]Haijawahi na haitatokea uongo ukaishinda ukweli.
    [*=left]Haijawahi na haitatokea giza likaishinda nuru.
    [*=left]Haijawahi na haitatokea Shetani akamshinda Mungu.
Hivyo basi usikate tamaa wala kuteteleka katika misimamo yako unayosimamia, "it is just a matter of time".
Ujumbe kwa Mh. Professor Mkandala " Malipo ni hapa hapa Duniani"​
 
Honest nimefadhaisha na ili tuko pamoja hakika Mungu yupo ndio mpiganaji wetu ukwel utashinda msife moyo tanzania ni yetu tutaikomboa very soon.
 
Prof. Mkandara Mungu wetu yupo, Jack Zoka Mungu wetu yupo watawala wenye nia mbaya na Tz Mungu yupo hakika Mungu wangu yuko hai ukweli utashinda kwa kishindo machozi yanatoka lakin ipo siku yatakwisha naamini hvyo nitaendelea kuomba kwa Mungu wangu.
 
chochote kilichowapata nyie vijana ingawa siwezi jua ni nini
ila nasema hata kama ikatokea hatuamini kila kitu kina mwanzo na mwiho na pia kuna nguvu inayotuongoza wanadamu
huyu prof na mahalamia wanasiasa na majangili wafanyabiashara wanaokesha usiku kucha kuangamiza na kudidimiza elimu ya watoto wa kitanzani,siku zinahesabika hata kama sio kizazi chetu ila kuna vizazi vijavyo tu kutoka kwetu.hii mchi haina usalama wa taifa period!!

kitaeleweka siku

huwezi kuwadanganya wau wote siku zote

poleni sana vijana ili ndilo ninaloweza sema sasa
 
Dah! kweli maisha ni safari ndefu sana,hakuna anaeweza kuzuia/kuchua haki ya mtu vyoote hivi kwa pamoja huwa vinacheleshwa tu wakati ukifika kila kitu kinakuwa wazi.Poleni kwa waliokata tamaa,mimi nnawatia moyo pengine Prf kakufungia dirisha na Mungu atakufungulia geti kubwa la maisha bora kwako.
 
Alphonce Lusako,
Unajua wenzako walioomba msamaha wamesema nini katika barua zao za kuomba msamaha? watafute na utajua kwa nini huwezi sameheka hata ukiomba msamaha mara sabini.
 
Unajua wenzako walioomba msamaha wamesema nini katika barua zao za kuomba msamaha? watafute na utajua kwa nini huwezi sameheka hata ukiomba msamaha mara sabini.

Mhimili wa uovu!
Hata kama haumo ktk mhimili huo lkn u mtetezi wa Mhimili huo mwovu. Anyway, matunda ya hao unaowatetea tumeanza kuyaonja; kwenye matokeo ya kidato cha nne na mauaji yanayohusishwa na dini.
 
Mkuu pole sana,njoo huku M4C tuongeze nguvu. Daima tutashinda hawa maprofesa uchwara taab sana, WASOMI WENGI NI WATUMWA WA WANASIASA
 
Kijana usihofu yana mwisho haya,na mwisho wenyewe hauko mbali sana. Weka nia yako ya kusoma tuu na NAKUHAKIKISHIA jiandae 2016 utaendelea na masomo hapo hapo UDSM. Kipindi hiki tumika na makamanda wengine kuhakikisha hilo linawezakana.
 
Pole,nadhani waliosoma wapo pia waliokutendea maovu watajitafakari na kuona wamekosea watajirudi.
Ndio tatizo la kila kiongozi mkuu wa idara kuteuliwa na Rais matokeo yake anafuata aliyemteua bila kufikiria matokeo yake,au kumshauri tu kwa hoja zinazoeleweka.
 
Du bwana mkubwa pole sana ila haki hushinda dhuluma. Usiogope, wala usihuzunike kwani ktk harakati hizi hutakiwi kurudi nyuma, utakuwa jiwe la chumvi.

We are going to have freedom soon.
 
Mkuu pole sana,njoo huku M4C tuongeze nguvu. Daima tutashinda hawa maprofesa uchwara taab sana, WASOMI WENGI NI WATUMWA WA WANASIASA

Kwahiyo kujiunga M4C kuna maana zaidi kuliko kumsaidia huyu mwanafunzi arudi shule,acheni kuingiza siasa katika mambo mazito ya kitaaluma.
 
Kijana usihofu yana mwisho haya,na mwisho wenyewe hauko mbali sana. Weka nia yako ya kusoma tuu na NAKUHAKIKISHIA jiandae 2016 utaendelea na masomo hapo hapo UDSM. Kipindi hiki tumika na makamanda wengine kuhakikisha hilo linawezakana.

acha kumhadaa huyo kijana,fursa yake ya kupata elimu ya juu ni sasa na siyo 2016,mambo uwenda yakibadilika,kufukuzwa chuo siyo mwisho wa yeye kupata elimu kwa sasa,kuna mambo mengi ya kumsaidia pasipo kuingiza siasa,tuanzie hapo sasa.
 
Du bwana mkubwa pole sana ila haki hushinda dhuluma. Usiogope, wala usihuzunike kwani ktk harakati hizi hutakiwi kurudi nyuma, utakuwa jiwe la chumvi.

We are going to have freedom soon.

Kwahiyo huyu kijana anasaidiwaje ili aweze kuendelea na masomo,hata kama ni chuo kingine
 
Back
Top Bottom