Wapinzani waandaa hoja: Wamtaka Pinda kujiuzulu

Amejibu kwa HISIA kali kweli hadi kutoa machozi. Nadhani vyombo vyetu vya usalama havifanyi kazi yake vizuri. Vimejikita mno kwenye ulinzi na usalama wa viongozi wetu ambao sioni wanatishwa na yeyote.

sasa machozi yake yanahusiana nini na kiapo chake cha kulinda Katiba. Hakuapa kulinda hisia zetu, au kutufanya tumuonee huruma.
 
Nampongeza pinda kwa ubinaadamu wa hali ya juu alio uonyesha dhidi ya Albino, kwani albino sio watu? Niulize tu! Chadema na yumo ktk hizo harakati? Lakini ukweli ni kwamba hao watu wanao katisha huai wa wenzao wakikamatwa wakajua kuwa wanauwawa ni razima watataja watu waliowatuma mikono ya albino,sasabasi hao wanaompinga Pinda ni kwa maslahi ya nani? Kumlazimisha pinda ajiuzuru ndio hapo tumeonyesha busara na hekima pamoja na upeo wetu wa mwisho wakufikiri. Au sijui mm ndo sielewi au nipo shallow ktk kutambua lkn ingekuwa bomba kama chadema ingejitoa ktk hilo swala la Pinda, ni mtizamo tu! Binafsi nimeshangazwa na hiyo kambi kutaka wauaji albino wasiuliwe na wao. Nilitarajia kuwa wangeunga mkono hoja hiyo na kuongezea kipengere cha "walio watuma wauaji wa albino nao pia wauwawe" nilitarajia kitu kama hicho. Ok waafrika ndo tulivyo.

Mkuu ThinkPad, suala la mauaji ya Albino linatisha, linasikitisha na linaangamiza heshima na ustaarabu wa Kitaifa. Sio suala la kichama peke yake. Ni suala linalotakiwa kupingwa na kila mTanzania mwenye huruma na ustaarabu wa kujali maisha ya binadamu mwenzake. Ni kweli kwamba wote wanaohusika lazima wachukuliwe hatua kali iwezekanavyo. Ila hatua yoyote inayotakiwa kuchukuliwa, ni lazima izingatie sheria za nchi (ambazo tunazo).

Suala la kuua wauaji wa Albino halina mjadala. Lenye mjadala ni ruhusa ya mauaji bila kuzingatia sheria za nchi (Mob Justice). Hadi sasa wauaji wengi wanapopatikana na hatia, huhukumiwa adhabu za kifo (japokuwa wengi wao wameishia kukaa gerezani bila kutekelezwa kwa adhabu hizo). Wezi wa aina mbalimbali wamekuwa wakipata hukumu mitaani, na wengi wameuawa na wananchi wenye hasira kali. Hili la Albino lingeweza kufanywa hivyo hivyo na wananchi, bila kuhitaji kauli ya kiongozi mkubwa wa nchi anaetakiwa kusimamia utawala wa sheria.
 
Mwakyj, I disagree, kazi ya upinzani ni to keep the government on its toes and to hold it accountable at every possible turn. Unafikiri hii ingetokea Marekani, Obama akatamka kitu kama hiki Republicans wangesema eti amekosea let's forget about it? umesahau Clinton's Lewinsky case and his near impeachment?
Sorry, waziri mkuu Pinda amesema kitu ambacho ni unacceptable kutoka kiongozi wa nchi kwani he has flaunted the rule of law and has encouraged people to take justice into their own hands, also can be deemed as instigating murder, incitement etc. Ni maneno mazito sana aliyoyatamka and it is time we hold our leader's feet to the fire.

I doubt kama PM amekosea lets see an example in Kenya...what happened to Mungiki? and what happened to Robbers(majambazi) and thieves? Do you know what Hon. Michuki ordered the Police to do.... He said "Shoot to KILL" Mi nadhani PM alichokisema ni sahihi kwani this Albino killing has gone beyond hiyo mnayoita Katiba!!! Its all bullshit!!

Let the Albino killers die and they should die mercilessly!!!

I'm in support of Prime Ministers in this matter!!!

Lets face it life is not fair to our fellow human beings just because they are disabled!!.... FIGHT AGAINST ALBINO KILLINGS AT WHATEVER COST....
 
Wapinzani wamendaa hoja gani? Kichwa cha habari na uliyoandika haviendani kabisa...imekaaa kama habari ya udaku hivi. Mwanakijiji uandishi wa hisia wa namna hii hautakiwi na unapunguza credibility yako...au una usingizi?

Wewe lengo lako ni Pinda kujiuzuru?Kuna binadamu ambaye ni Mkamilifu? Kosa la Pinda siyo kubwa kiasi hicho mpaka ajiuzuru na kama wabunge wetu wakiwa na akili kama yako na kumtaka Pinda ajiuzuru nitawashangaa sana!

Wewe mbona kuna kipindi ulishawahi kutoa kauli flani hapa tata na ukaachwa na hatukukwambii ujiuzuru?

Andika Makala ya Pinda ajiuzuru huku ukijenga hoja nzito na siyo bla bla tu kwa kuwa unahisi anahitaji kujiuzuru.

Pinda 'Kill Killers' talk angers Opposition (The Citizen)
By Faraja Jube, Dodoma
The Opposition yesterday lashed out at Prime Minister Mizengo Pinda following his declaration that people caught killing albinos should also be killed.

The Leader of the Official Opposition in Parliament, Mr Hamad Rashid Mohammed, said there was no way the Opposition was going to let Mr Pinda go unpunished for the remarks, which, he added, were in total disregard of the rule of law.

He said the Opposition would agitate for the resignation or sacking of Mr Pinda, possibly by a tabling a private motion calling for a vote of no confidence in the Prime Minister.

Mr Mohammed, who is the CUF MP for Wawi, said the Opposition would also push for a parliamentary resolution for a major review of the constitution by tabling a private motion to that effect.

He said the remarks by Mr Pinda were contrary to the Constitution, and could have far-reaching ramifications.

"The Opposition will challenge the Prime Minister, who is a trained lawyer, during the current parliamentary session to clarify his remarks which are in direct contravention to the Constitution, which he has sworn to safeguard and uphold," Mr Mohammed said.

He said killing somebody who has been caught in the act of committing a criminal offence amounted to mob justice, adding that it was only the courts that were empowered to try and punish offenders in accordance with the law.

The Opposition has lent its voice to the chorus of condemnation that greeted remarks Mr Pinda made in Tabora last week.

With many Tanzanians convinced that the media had misquoted Mr Pinda, The Citizen on Monday sought clarification from the Prime Minister, who confirmed that he uttered the remarks, adding that he meant what he had said.

Mr Pinda told The Citizen on Monday that people who were condemning his remarks did not have an idea of the senseless brutality being wrought upon albinos by killers who were after their body parts.

He said his remarks were in line with the urgency and seriousness with which the Government treated the wave of albino killings in some parts of the country, and reflected its commitment to putting an end to the atrocities once and for all.

Mr Pinda added that his statement would not have shocked anybody who knew the extent of suffering the killings had caused.

"It may be an unusual statement by a prime minister, and I wish to confirm that I made the remarks to send a clear message to albino killers they should know that if they are caught, they will have to face the fate they had hoped their victims would suffer," he said in an exclusive interview with The Citizen.

Mr Pinda said he and the Government would no longer tolerate the senseless and brutal killings of human beings just because they happen to be of a different colour.

Speaking at yesterday's press conference in Dodoma, the deputy leader of the opposition in Parliament, Dr Wilibrod Slaa (Karatu-Chadema), said the Prime Minister's statement depicts failure by the Government to enforce the rule of law.

"Something somewhere within the Government machinery must be seriously wrong. This is an indication of a system that is about to collapsed," he said, noting that the Opposition would never allow this to happen as it could lad to anarchy.

The Opposition leaders also took issue with remarks made by President Jakaya Kikwete when he visited Pemba last week. The president said the Opposition should forget about wresting power from CCM in the isles.

On the Constitution, Mr Mohammed said the current statutes were outdated and in need of a major overhaul.

He added that the Opposition was planning to table a private motion seeking a parliamentary resolution for the review and amendment of the Constitution.

The opposition leader said the current Constitution gave the President vast powers, adding that this was not healthy for national development.

Mr Mohammed said their intention was to have a new Constitution in place before the 2010 General Election.

He said, for example, that it was time independent entity such as parliament vetted and endorsed key presidential appointments.

Mr Mohammed said another shortcoming was the executive's supremacy over Parliament in matters concerning the management of public resources.

"The current constitution, for example, does not empower Parliament to punish leaders who abuse public office-people such as those who enter into bad contracts on behalf of the Government.

"We would present the private motion and push for a parliamentary resolution on this. And if the ruling party uses its majority to block our motion, we will resort to people's power," he noted.

Swali:

Kosa langu miye hapa nini? NImeandika makala nyingine kusema kwanini ajiuzulu. Kwa kifupi ni kuwa kama ameshindwa kulinda, kutetea, na kuihifadhi Katiba yetu kwa sababu ya hisia zilizoumizwa akae pembeni, kumpa mtu mwingine kufanya hivyo kwa gharama yoyote ile. Uongozi si kwa wepesi wa moyo.
 
sasa machozi yake yanahusiana nini na kiapo chake cha kulinda Katiba. Hakuapa kulinda hisia zetu, au kutufanya tumuonee huruma.

Kuna mambo mengine yakifanyika na ukayashuhudia kama binadamu wa kawaida, unaweza kusahau kwa muda kwamba kuna KATIBA, MAHAKAMA,...
Amesema nia yake ilikuwa njema tu kuwaambia hawa wanaofanya mauaji haya ya kikatili kwamba "as a government they are fed up". Ameomba radhi kwa wale waliokwazika na kauli yake. Mzee, nadhani tujaribu kuelewa ukubwa wa tatizo hili na jinsi vyombo vyetu vya usalama vilivyoshindwa kulikabili.
 
Amejibu kwa HISIA kali kweli hadi kutoa machozi. Nadhani vyombo vyetu vya usalama havifanyi kazi yake vizuri. Vimejikita mno kwenye ulinzi na usalama wa viongozi wetu ambao sioni wanatishwa na yeyote.

Ni kweli Waziri Mkuu amelia. Lakini amelilia nini? Anajua madhara ya kuvunja Katiba na hivyo anapaswa ama kujiuzulu au kuvuliwa Uwaziri Mkuu. Alikuwa analilia Uwaziri Mkuu......... Hakuwa analilia Albino. Kama angekuwa analilia Albino, angelia huko ziarani na sio Bungeni alipoulizwa swali.

I like Pinda, but i can never ever entertain lawlessness. This is a constitutional Country, Pinda invites anarchy. We can not allow that. Next is a special motion to ask Pinda to restate what he said. What exactly did he say about those who killed Albinos.

Leo kashindwa kakiri kiaina. We want him to say in Parliament, to restate his stand so that a no confidence process initiated.

Tusithubutu kuruhusu viongozi kuropoka. We will be doing disservice to the country and invite killings, extra judicial killings. Viongozi wawajibike kwa maneno yao, kwa vitendo vyao na kutotenda kwao (words, actions and inactions)
 
Kuna mambo mengine yakifanyika na ukayashuhudia kama binadamu wa kawaida, unaweza kusahau kwa muda kwamba kuna KATIBA, MAHAKAMA,...

Hicho ndicho ninachokataa. Bush alireact hivyo hivyo baada ya Sept 11. Hata mimi siku ile naangalia matukio yale niliamini kama hawa jamaa wakipatikana wauawe hata mahakamani wasifikishwe. Ulikuwa ni mwitikio wa hisia. Baada ya kutulia nilirudi na kuamini kuwa sheria ndiyo maana zipo ili kuondoa maamuzi ya hisia.

Kwanini tunawapeleka wabakaji mahakamani, kwanini tunapeleka wauaji wengine mahakamani, kwanini tunapeka mafisadi mahakamani.. Kwanini leo wauaji wa maalbino tusema ni tofauti? Sheria inaposemwa kuwa ni msumeno maana yake ndiyo hiyo.. unakata ukienda mbele na ukienda nyuma.

Amesema nia yake ilikuwa njema tu kuwaambia hawa wanaofanya mauaji haya ya kikatili kwamba "as a government they are fed up". Ameomba radhi kwa wale waliokwazika na kauli yake. Mzee, nadhani tujaribu kuelewa ukubwa wa tatizo hili na jinsi vyombo vyetu vya usalama vilivyoshindwa kulikabili.

siyo kuomba radhi kwa wale waliokwazika, kwani sisi hamnazo. Maneno yake yangeandikwa na gazeti lolote au kama yangetolewa na kiongozi wa upinzani with such impunity ingekuwa kasheshe Tanzania. Hakusema kitu kinachokwaza, alisema kitu cha hatari! Grrrrrr..

well kama kaomba radhi I'll cut him some slack.

Gembe: Kwa mwaka mzima sijaandika kitu chochote kuhusu Pinda. Niliapa wakati ule anateuliwa kumpa nafasi ya kufanya kazi yake bila kuanza kukosolewa (nilisema miezi sita, lakini nikaamua kukaa mwaka mzima). NI hadi alipotoa kauli hii ndipo nimeandika. Wakati mwingine nafikiri umeanza kujua kinachonisukuma, mara zote ukireact you prove me wrong.

Hili la kutaka kuvunja sheria wazi, ndiyo limenishtua kuwa a popular leader is the most dangerous.
 
Ni kweli Waziri Mkuu amelia. Lakini amelilia nini? Anajua madhara ya kuvunja Katiba na hivyo anapaswa ama kujiuzulu au kuvuliwa Uwaziri Mkuu. Alikuwa analilia Uwaziri Mkuu......... Hakuwa analilia Albino. Kama angekuwa analilia Albino, angelia huko ziarani na sio Bungeni alipoulizwa swali.

I like Pinda, but i can never ever entertain lawlessness. This is a constitutional Country, Pinda invites anarchy. We can not allow that. Next is a special motion to ask Pinda to restate what he said. What exactly did he say about those who killed Albinos.

Leo kashindwa kakiri kiaina. We want him to say in Parliament, to restate his stand so that a no confidence process initiated.

Tusithubutu kuruhusu viongozi kuropoka. We will be doing disservice to the country and invite killings, extra judicial killings. Viongozi wawajibike kwa maneno yao, kwa vitendo vyao na kutotenda kwao (words, actions and inactions)

Pamoja na yote hayo nasema kuwa Pinda ni bonge la Waziri Mkuu na nimeshawahi kusema huko nyuma kuwa Pinda ni Muungwana mno kuliko watangulizi wake- anapokosea hukiri hadharani ambayo kwangu ni sifa ya ziada hasa kwa Watawala wetu.

Inawezekana anaulilia Uwaziri Mkuu kweli, kama Pinda atajiuzulu nadhubutu kusema Serikali hii itaanguka maana hakuna Waziri mwingine mnyoofu na mwelekevu kama Pinda (ukiongezea uzoefu kama waziri).

Kuna wakati ilipendekezwa kuwa Mawaziri wasiwe Wanasiasa (Wabunge) nadhani hilo lilikuwa wazo zuri sana, na Pinda ukimwangalia na kumsikiliza kwa makini utagundua kuwa yeyey si Mwanasiasa ila Mtendaji na yeye mwenyewe ameshawahi kukiri kuwa yeyey si MWanasiasa na yanayotokea (kauli yake dhidi ya wauaji wa Albino) inathibitiha hayo yote.
 
Kiongozi yeyote yule anapotoa kauli ya kutaka watu wavunje sheria kauli yake hiyo ni lazima imgharimu. Hakuna mapenzi kwa kiongozi yeyote ambayo yanaweza kutufanya tuache afanye apendavyo. Tukiruhusu hivyo tutakuwa tumeruhusu uimla.

Alichojaribu Pinda kilikuwa ni cha hatari sana.
 
Pamoja na yote hayo nasema kuwa Pinda ni bonge la Waziri Mkuu na nimeshawahi kusema huko nyuma kuwa Pinda ni Muungwana mno kuliko watangulizi wake- anapokosea hukiri hadharani ambayo kwangu ni sifa ya ziada hasa kwa Watawala wetu.

Inawezekana anaulilia Uwaziri Mkuu kweli, kama Pinda atajiuzulu nadhubutu kusema Serikali hii itaanguka maana hakuna Waziri mwingine mnyoofu na mwelekevu kama Pinda (ukiongezea uzoefu kama waziri).

Kuna wakati ilipendekezwa kuwa Mawaziri wasiwe Wanasiasa (Wabunge) nadhani hilo lilikuwa wazo zuri sana, na Pinda ukimwangalia na kumsikiliza kwa makini utagundua kuwa yeyey si Mwanasiasa ila Mtendaji na yeye mwenyewe ameshawahi kukiri kuwa yeyey si MWanasiasa na yanayotokea (kauli yake dhidi ya wauaji wa Albino) inathibitiha hayo yote.

Kiongozi anayetangaza hadharani kuwa sheria ivunjwe to the most extreme way, hana ubora wowote. Kiongozi wa namna hiyo ni wa hatari kwani anatawala kwa vitisho na siyo kwa ushawishi. Njia ya kwenda jehanamu imepambwa kwa nia nzuri msemo unasema.

Mauaji ya Albino hayawezi kukomeshwa kwa kupendekeza mauaji ya watu wengine! Period. Kiongozi anayeshindwa kuona hilo ni wa hatari kwani instincts zake ni kisasi. Kiongozi wetu tunataka instincts zake zielekee kwenye Katiba.
 
Zitto,
Wewe umejuaje kwamba alichokuwa analilia ni Uwaziri Mkuu? Yaleyale ya kuongozwa na HISIA! Angalau huyu anaonyesha hisia zake wazi. Ni suala la kurekebishana tu.
 
Zitto,
Wewe umejuaje kwamba alichokuwa analilia ni Uwaziri Mkuu? Yaleyale ya kuongozwa na HISIA! Angalau huyu anaonyesha hisia zake wazi. Ni suala la kurekebishana tu.

ameshakwambia amejuaje. Pinda hakulia alipoona albino waliokatwa viungo na alipopewa orodha ya maalbino waliouwawa kwenye ziara yake. Manake alipelekwa papo papo kwenye kijiji ambacho albino aliuwawa. Sasa kama hakulilia hao albino huko, kwanini alie bungeni kama sio kulilia uwaziri mkuu?

Lakini kama ni kuvunja katiba alianza kikwete aliyeacha utawala wa Sheria kwa kuwasamehe wezi wa EPA waliorudhisha fedha. Wakati mnataka Pinda aje aseme kauli yake kama ilivyo, tafadhali wakumbusheni IKULU pia watoe ile hotuba ya JK ili naye maneno yake yajadiliwa.

Tuna viongozi waropokaji ambao ipo siku watatoa kauli zitakazochochea maasi! Hawa hawafikiri kabla ya kusema.

Asha
 
Zitto,
Wewe umejuaje kwamba alichokuwa analilia ni Uwaziri Mkuu? Yaleyale ya kuongozwa na HISIA! Angalau huyu anaonyesha hisia zake wazi. Ni suala la kurekebishana tu.

Vyovyote unavyopenda kuita, unataka waziri mkuu wa kulia kulia anapoulizwa swali kuhusu kulinda na kuheshimu katiba ya nchi?

Alikuwa analilia uwaziri Mkuu, two wrongs never make it a right! unapohamasisha wanoua albino wauwawe hapohapo unahamasisha mauaji ya albino pia.
 
Last edited:
Leo kashindwa kakiri kiaina. We want him to say in Parliament, to restate his stand so that a no confidence process initiated.

Na hii kauli pia inahitaji ufafanuzi. Unataka aeleze msimamo wake tena ili iweje? Umesemaje hapo?

Unajua Wabongo hatujali, hatuzingatii, tunachokiongea. Tena kesi yenyewe inahusu watu kutokuwa makini na wanachokisema. Unasema ajieleze tena ili muanzishe utaratibu wa kutokuwa na imani nae! Aeleze nini sasa, si umeshasema hamna imani nae? Au wewe ndio ujieleze! Hebu jieleze vizuri.
 
Asha,
Hakuna anayetishia nafasi yake hiyo wala hakuna namna ya kumwondoa angalau kwa sasa. Ataililia kwa sababu gani? Uliza pia waliokuwa naye kwenye hii ziara wakwambie hisia na hasira zake zilikuwaje.
Wapinzani shughulikieni mambo muhimu yanayowanyima kura za wananchi. Hili la kumwondoa WM litawapa umaarufu wa muda tu.
 
Na hii kauli pia inahitaji ufafanuzi. Unataka aeleze msimamo wake tena ili iweje? Unasemaje hapo?

Unajua Wabongo hatujali, hatuzingatii, tunachokiongea. Tena kesi yenyewe inahusu watu kutokuwa makini na wanachokisema. Unasema ajieleze tena ili muanzishe utaratibu wa kutokuwa na imani nae! Aeleze nini sasa, si umeshasema hamna imani nae? Au wewe ndio ujieleze! Hebu jieleze vizuri.

Hakusema nini alisema. Ninawaletea maneno yake verbatim (hansard) muone hasa kasema nini. Ninadhani kuna haja ya kumtaka aseme nini alisema (to restate what he said in Tabora). Unajua Bunge haliwezi kutumia kauli reported katika vyombo vya habari. Hivyo kuna haja ya kumtaka arudie alichosema Tabora ili hoja kutokuwa na imani ianze
 
Asha,
Hakuna anayetishia nafasi yake hiyo wala hakuna namna ya kumwondoa angalau kwa sasa. Ataililia kwa sababu gani? Uliza pia waliokuwa naye kwenye hii ziara wakwambie hisia na hasira zake zilikuwaje.
Wapinzani shughulikieni mambo muhimu yanayowanyima kura za wananchi. Hili la kumwondoa WM litawapa umaarufu wa muda tu.

Nilimwona kwenye TV waziri mkuu alipokuwa hiyo ziara, hakuwa mtu anayeelekea kutoa machozi. Kama waziri mkuu angetoa machozi kwa ajili ya maalbino huko kijijini hiyo ndio ingekuwa habari ya kurasa za mbele.

Yaani wewe suala la Waziri Mkuu kuvunja katiba na kukataa utawala wa sheria unaona ni suala dogo. Hili ni suala linalohusu umakini wa uongozi, uwajibikaji wa uongozi na maisha ya watuhumiwa ambao waziri mkuu ametangaza wauwawe kabla ya mahakama kuwakuta na hatia au la.

Siku katika kijiji chenu albino akiuwawa halafu wananchi wakamshuku babu au bibi yako kule wakamkata kwa mapanga kwa kumhisi tu ndio utajua kwamba hili ni suala kubwa.

BTW: Nimetaka la Pinda liende sambamba na la Kikwete kuvunja katiba na kudharau utawala wa sheria kwa kuwasamehe wezi walioghushi nyaraka kuiba fedha benki kuu na kurejesha. Zitto, ombeni na hotuba ya Rais iletwe bungeni ijadiliwe hata kama imepitwa na wakati kwa kuwa kuna kauli mbovu mbovu mule kuliko hata za Pinda.

Asha
 
Wapinzani wa Tanzania kiboko, inaonekana wanakaa wanasubiria nani achemshe wamlime(IMHO).
 
Hakusema nini alisema. Ninawaletea maneno yake verbatim (hansard) muone hasa kasema nini. Ninadhani kuna haja ya kumtaka aseme nini alisema (to restate what he said in Tabora). Unajua Bunge haliwezi kutumia kauli reported katika vyombo vya habari. Hivyo kuna haja ya kumtaka arudie alichosema Tabora ili hoja kutokuwa na imani ianze

Hamtegemei vyombo vya habari? Sasa umejuaje alichosema Tabora mpaka mnaanda hizo hoja za no confidence, ulikuwepo?

Akisema ambacho ni tofauti na ambacho umesikia alisema Tabora utatumia rekodi ya vyombo vya habari kumwambia "Mheshimiwa Pinda hicho sicho ulichosema"? Akiukuuliza umejuaje utamjibu "MwanaHALISI"?

Unataka yeye ndio akwambie alichosema, unaanda hoja dhidi ya ulichosikia sikia Waziri Mkuu amesema halafu huna rekodi, huna hakika, hujui, alichosema!

Unampeleka jirani yako kwa mjumbe kwamba amekwambia maneno machafu, unaulizwa kasema nini, unasema yeye ndio aseme alichosema. Sasa umekuja kushitaki nini, mjumbe atakufukuzilia mbali!
 
Back
Top Bottom