Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Nimekosea badala ya kuhusudu nimeandika kusujudia
Ukimuua albino, tutakuua tu. Na hili wala halikuhitaji Waziri Mkuu kulisemea ... Kwa mliotarajia "kula" kwa kuandika habari za mauaji ya albino, sasa subirini kuandika habari za kuuwawa kwa "wauaji wenyewe".
Hapo hakuna cha haki za binadamu wala nini. Ukiondoa uhai wa "albino", haki yako ya ubinadamu inaishia hapo hapo.
Acha Pinda ajiuzulu, lakini sisi tutawaua tu, kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa majambazi, n.k.
Ikionekana kuna wanaotetea wauaji wa albino, kama hao viongozi (wanasiasa) wa NCCR, nao tutawajumuisha kwenye list ya wauaji ... hii ni vita, si siasa!!!
Ole wenu!!
nadhani mheshimiwa PM alimahanisha kwamba mtu yeyote ikithibithishwa kuwa ameua ni kosa kisheria na pia adhabu yake ni kunyongwa sijui kama hii sheria ilitenguliwa maana kuna wakati wanaharakati wa haki za binadamu duniani walitaka ibatilishwe.
Napiga vita mauaji ya albino yanamayoendelea hapa nchi kwasasa.
Kesho kwenye kipindi cha maswali na majibu wabunge wanasubiri kwa hamu kusikia kama PInda atathubutu kutetea msimamo wake huo Bungeni au atakanusha.
Besides Pinda ameresonate na mawazo ya wananchi wengi wa kawaida(siku zote wamekua wakimalizana na vibaka mitaani), so kimtaani wananchi wengi wanaweza kumuunga mkono....wenye tatizo ni the so called wasomi, wadadisi wa mambo, na wauza magazeti.
Well... ndani ya mwaka mmoja tunaweza kuwa na Waziri Mkuu mwingine aliyejiuzulu? Well.. wapinzani inaonekana wanataka iwe hivyo. Wengi wamefikia hilo baada ya kusoma makala ya The Citizen la leo kuwa Pinda alimaanisha alichosema kuwa wananchi wawaue papo hapo wanaowatuhumu kuwa ni wauaji wa albino.
Kesho kwenye kipindi cha maswali na majibu wabunge wanasubiri kwa hamu kusikia kama PInda atathubutu kutetea msimamo wake huo Bungeni au atakanusha. Kuna kundi la wabunge wa CCM ambao nao wanasubiri kusikiliza kuwa alimaanisha nini hasa (sijui kama bado kuna utata hapo)
Hii habari ingekua strong zaidi kama tungesubiri kesho kwanza baada ya Pinda kuongea maana ni lazima kuwa na due process, gazeti limesema na especially haya magazeti yetu ya Bongo sasa ni zamu ya Pinda kujibu, ndio tuanzishe hukumu, au?
FMES!
Wapinzani wamendaa hoja gani? Kichwa cha habari na uliyoandika haviendani kabisa...imekaaa kama habari ya udaku hivi. Mwanakijiji uandishi wa hisia wa namna hii hautakiwi na unapunguza credibility yako...au una usingizi?
Wewe lengo lako ni Pinda kujiuzuru?Kuna binadamu ambaye ni Mkamilifu? Kosa la Pinda siyo kubwa kiasi hicho mpaka ajiuzuru na kama wabunge wetu wakiwa na akili kama yako na kumtaka Pinda ajiuzuru nitawashangaa sana!
Wewe mbona kuna kipindi ulishawahi kutoa kauli flani hapa tata na ukaachwa na hatukukwambii ujiuzuru?
Andika Makala ya Pinda ajiuzuru huku ukijenga hoja nzito na siyo bla bla tu kwa kuwa unahisi anahitaji kujiuzuru.
Pinda ameshaongea mara tatu. Hadharani, baadae akaenda kwenye gazeti, halafu akatuma mouth piece wake kurudia kile kile alichotamka. Mara tatu! Ungependa aongee mara ngapi?
Due Process tumpe Pinda? Pinda ndio ametuambia haamini katika Due Process. Mkimshika mhukumuni hapo hapo, mchinjeni. Hataki mambo ya Due Process!
Waziri Mkuu akihimiza wananchi wachukue sheria mikononi inabidi awajibike. Hakuna utata hapo.
Hauna sababu ya kudhania. Wengine tangu wiki iliyopita wamejaribu kutumia mstari huo wa "kumaanisha". Yeye kasema hakumaanisha watu wanavyofikiri alimaanisha, alimaanisha alichosema. Kwamba, wananchi wakimuona mtu wanayemshuku kuwa amehusika na mauaji ya albino (ati ana mkono, amelowa damu, na anakimbia akifukuzwa) basi wakimpata wasihangaike naye hadi Polisi, wamuue tu. Na huo ni msimamo wa serikali.
Adhabu ya kunyongwa bado ipo.
Ndio Mh. Pinda ameulizwa swali hilo na Kiongozi wa upinzani Mh. Hamad.
Wapinzani wamendaa hoja gani? Kichwa cha habari na uliyoandika haviendani kabisa...imekaaa kama habari ya udaku hivi. Mwanakijiji uandishi wa hisia wa namna hii hautakiwi na unapunguza credibility yako...au una usingizi?
Wewe lengo lako ni Pinda kujiuzuru?Kuna binadamu ambaye ni Mkamilifu? Kosa la Pinda siyo kubwa kiasi hicho mpaka ajiuzuru na kama wabunge wetu wakiwa na akili kama yako na kumtaka Pinda ajiuzuru nitawashangaa sana!
Wewe mbona kuna kipindi ulishawahi kutoa kauli flani hapa tata na ukaachwa na hatukukwambii ujiuzuru?
Andika Makala ya Pinda ajiuzuru huku ukijenga hoja nzito na siyo bla bla tu kwa kuwa unahisi anahitaji kujiuzuru.