Wapinzani Tanzania ni Wanafiki - SAMWEL SITTA

Nilikuwa namuamini sana huyu mzee! Lakini baada ya kukaimishwa nafasi ya pinda pale mjengoni ndipo nimeamini maneno ya EL kuwa "TATIZO NI UWAZIRI MKUU! Tatizo la Sita lilikuwa ni hilo, hakuna cha vita ya ufisadi wala nini!

Tukumbuke Mh Sitta alijilimbikizia mali akiwa Spika wa bunge. Sema yote ila kwa swala la kupata faida ukiwa bungeni!! Mh Sitta ni mdhaifu. Hatufai kuwa kiongozi wa nchi hii.

• Wabunge CCM, wapinzani wazozana

na Tamali Vullu, Dodoma

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, jana alijikuta akizomewa na wabunge wa kambi ya upinzani huku wakimwita msaliti, kwa kuwa mmoja wa waasisi wa chama kilichonyimwa usajili cha CCJ.

Wabunge hao walifikia hatua hiyo baada ya Sitta mwenyewe kuanza kuwaambia wabunge wa kambi hiyo kwamba ni wanafiki kwa kukataa posho wakati baadhi yao wamekuwa wakipokea kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Majibu ya Sitta ambaye amekuwa kiongozi wa shughuli za Bunge akikaimu nafasi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, yalikuja wakati akitoa ufafanuzi wa kauli iliyoibua zogo ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR- Mageuzi), kwamba serikali ya Rais Jakaya Kikwete ni legelege kwa vile imeshindwa kukusanya kodi.

Hata alipotakiwa na kiti cha Spika kufuta kauli hiyo, Kafulila alikataa na kusisitiza kwamba yuko tayari kufa, ndipo Sitta alipoamua kusimama kutuliza mzozo huo.

Sitta ambaye wiki iliyopita alitumia nafasi hiyo kumshambulia Edward Lowassa, alisimama na kuwasihi wabunge wa CCM kuwa watulivu, kwani wapinzani kazi yao ni kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali.

"Wabunge wa upinzani kazi yao ni kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali, lakini sisi tutahukumiwa na wananchi. Siku zote wapinzani mambo yao ni ya unafikinafiki," alisema Sitta na kuibua zogo zaidi.

"Nitatoa mfano, baadhi yao wanadai posho za vikao ni kuwaibia wananchi, lakini wapo baadhi yao walichukua posho hizo miaka mitano iliyopita. Warejeshe posho hizo ndiyo wananchi watawaelewa… na wataendelea kuwa wapinzani," alisema.

Hata hivyo, maelezo ya Sitta hayakuweza kuzima mzozo uliokuwapo kwani wabunge wengi wa upinzani walisimama wakitaka mwongozo wa mwenyekiti, lakini aliahirisha Bunge kutokana na muda wa kikao kwisha.

Licha ya muda kwisha, baadhi ya wabunge wa upinzani waliwasha vipaza sauti na kuanza kumzomea kwa kumwita msaliti kwa vile alikuwa mmoja wa waasisi wa CCJ. Katika zomeazomea hiyo, wabunge hao walikuwa wakiimba CCJ, CCJ.

Kabla ya Sitta kuingia kwenye mzozo huo, kauli ya Kafulila kwamba serikali ya Kikwete ni legelege, ilionekana kuwakera sana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangwala, alisimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, akimtaka Kafulila kufuta kauli hiyo kwa kuwa ni ya kuudhi.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mbunge afute kauli kuwa serikali ya CCM ni legelege na haijashindwa kukusanya kodi. Kauli hii imeniudhi, serikali inakusanya kodi na imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka," alisema.

Baada ya maelezo hayo, Mwenyekiti Mhagama alimtaka Kafulila kufuta kauli hiyo, lakini alikataa kwa maelezo kuwa maneno hayo ni nukuu ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pia alisema mpaka sasa serikali haijafanikiwa kuongeza kiwango cha kodi kwani wakati ikikusanya kiwango hicho dola moja ilikuwa sh 1,000, lakini sasa dola imepanda na kufikia sh 1,600.

Kutokana na maelezo hayo, Mhagama alisema kuwa hoja ya Kafulila ina mantiki, lakini haiendani na maelezo aliyokuwa akitoa, kwani ameitumia vibaya nukuu hiyo na kusisitiza Kafulila kufuta kauli hiyo.

Wakati Mhagama akieleza hayo, baadhi ya wabunge walikuwa wamewasha vipaza sauti vyao na kusikika wakipinga suala hilo huku wale wa CCM wakibeza hoja hiyo.

Pamoja na hayo, Kafulila alieleza kushangazwa na hali hiyo na kusema huo ndio ukweli na kwamba yupo tayari kwa lolote.

"Nashangaa tunachukua muda mrefu kujadili suala hili. Huu ni ukweli mchungu na nipo tayari kuufia," alisema Kafulila.

Awali akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Kafulila alisema inasikitisha kuona kuwa wakati nchi inaelekea kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, bado bajeti ya sekta ya afya ni tegemezi.

Alisema hali hiyo inatokana na tatizo la kimtazamo katika serikali na kumtaka waziri asikubali bajeti ndogo na hata ikiwezekana ajiuzulu.

"Leo dunia nzima sisi ndio tuna uwiano mbovu kati ya daktari na wagonjwa. Ni aibu bajeti ya sekta ya afya kuwa tegemezi kwa asilimia 97. Haiwekezani.

"Serikali haitozi kodi. Serikali imeshindwa kukusanya pesa, inasikitisha kwa sababu sekta ya afya inahusu maisha ya Watanzania," alisema.

Kafulila alisema hazungumzii suala hilo kama mpinzani, bali ni ukweli na kuongeza kuwa serikali hata inashindwa kuwekeza katika masuala mengine ya afya kutokana na utegemezi.

"Kuna matatizo mengi zaidi ya ukimwi, lakini kutokana na kuwa tegemezi tunashindwa kuwekeza katika masuala mengine ya kiafya," alisema.

Mbunge huyo alieleza kuwa watoto wa wabunge na mawaziri wanatibiwa katika hospitali bora ndani na nje ya nchi, lakini watoto wa wanyonge wanatibiwa katika hospitali ambazo hazina hata dawa.

Kutokana na kauli hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti na kumtaka mbunge huyo kutotoa kauli za jumla jumla.

Kauli hiyo ya Maige, iliibua minong'ono miongoni mwa wabunge wa upinzani na mwenyekiti kusimama na kuwataka wabunge kuheshimu nidhamu ya Bunge.

Baada ya maelezo ya mwenyekiti, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, alisimama na kuwataka wabunge kuzungumza kwa nidhamu.

"Mtoto wangu ni daktari Muhimbili na wanangu wanatibiwa katika hospitali za kawaida. Baba yangu anatibiwa

Hospitali ya Katesh na mimi natibiwa huko, naomba Kafulila ukubali taarifa hii," alisema Nagu.

Hata hivyo, Kafulila alikataa taarifa hiyo na kuongeza kuwa familia ya mbunge na waziri zinatibiwa bure.

"Hii ndiyo sababu inayofanya msiwekeze kwenye sekta ya afya… waziri wakati mwingine usikubali bajeti ndogo namna hii, hapa tutakuchanachana shati," alisema.

Kafulila alisema inawezekana serikali kuwekeza katika sekta ya afya vijijini, kwani nchi hii ni tajiri.

"Tanzania ni nchi tajiri, lakini ni taifa la saba kwa kupatiwa misaada duniani, tunaongozana na nchi zenye machafuko. Haiwekezani," alisema huku akionyesha jarida la Ecomomist.

Akizungumzia bima ya afya, Kafulila alisema kitendo cha kutopatikana dawa ni utapeli kwa wananchi.

mimi nawashauri wabunge wa upinzani waungane na wapeleke malalamiko kwenye kamati ya kudumu ya uongozi ya bunge, si mnakumbuka hata bi kiroboto alikuwa hivyo hivyo, lakini baada ya kupeleka mbele, angalu.

Naungana na Kafulila "Huu ni ukweli mchungu na nipo tayari kuufia," yaani serikali ya Kikwete ni legelege!!!! period!

Mwanasiasa msiamamo bana.kama kweli unatumikia wananchi na una moyo wa kizalendo,basi issue ya posho lazima ikuguse.Siyo kwamba wasilipwe mishahara inayostahili.Isipokuwa kutokuwaonea huruma wananchi kwa kufanya matumizi makubwa hata uongee lugha gani ni unafiki tu.Ubinafsi na uongozi wapi na wapi.Matumizi makubwa ya viongozi kwenye nchi yenye watu masikini kama TZ ni dhambi kwa Mungu.

Naungana na Kafulila "Huu ni ukweli mchungu na nipo tayari kuufia," yaani serikali ya Kikwete ni legelege!!!! period!
ukitaka kujua tofauti ya kiongozi bora na bora kiongozi mwambie ukweli umguse uone majibu yake, BIG UP SANA KAFULILA

Sitta asubiri next game plan ya RA: si anajifanya mshindi na kundi lake la CCJ uamusho.

Nilifurahi sana alipokataa kufuta. Huo ndio ukweli na huyu 6 aache kujichanganya juzi tu kasema hatuwezi kutoa maamuzi mazito kwa kuwa watendaji si waadilifu= legelege

Wakatae wakasirike hawakusanyi kodi wanakura 10% na kutoa misamaha ya kodi kiholela

Swali langu kwa Mh. Sitta: anaamini CCM ni chama safi na chenye/dhamira ya kweli ya kuwakomboa Watanzania? Kama jibu ndio, ni kwa nini aliasisi chama kingine (CCJ)? Na kama jibu ni hapana, kwanini bado yuko CCM?

Kwasababu ya U-N-A-F-I-K-I

Nilimsikia 6 akisema yale aliyoyasema jana,sawa lakini hatakwepa hukumu yetu muda si mrefu

Kusema kweli nashindwa kuelewa serikali na Wabunge wa CCM. Nashindwa kwa sababu wanakitayarishiria CCM safari ya kwenda kuzimu kama ilivyo kwa KANU na Vyama vingine vinavyojiita vyama Ukombozi . Sijui ni ukombozi gain waliofanya hasa CCM. Maisha ni magumu, heri enzi ya Mkoloni kwani hao wazee waliopambana na ukoloni wametuhadaa sana. Wao walikuwa wanasomeshwa Bure na wakoloni, wanapata matibabu Bure tena kwa kulazimishwa na hao wakoloni.
Anayewalaani wakoloni ni ADUI YANGU NAMBA 1 Kama CCM ilivyokuwa ADUI yangu No 1 !
Jana nilikuwa naangalia Bunge Hongera Kafulila Pia Hongereni Wabunge wote wa Upinzani kwa kumpa moyo mwenzenu wa Upinzani ila nina wasiwasi na wabunge wa CUF.
Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni yaani Samweli Sitta amethibitisha unafiki wake kwa vitendo:-

1. Kwa kipindi hiki anapokaimu uwaziri mkuu ameonyesha jinsi gani alivyo mtu wa Visasi,
2. Hana tofauti na Muimba Mipasho
3. Uadilifu anaomshupalia lowasa ni upi ? wakati jana Mchango wa Kafulila ulikuwa na asilimia 100 za ukweli kuhusu Uadilifu wa Serikali ambapo serikali hii ya CCM haina. Na sita alivyomjibu lowasa kuhusu maamuzi magumu alisema yawe adilifu.
4. Bunge si Jukwaa la Mkutano wa Hadhara! Sita unaposema kuwa wabunge wengine walikuwapo kipindi cha nyuma warudishe posho za kipindi hicho ndio wasimamie mgomo wa posho si kitendo cha kizalendo. Upambanaji wako dhidi ya Ufisadi uko wapi! Bwana Sita. Hivi Posho sio sehemu ya Ufisadi! Huo unafiki wa wapinzani ni upi?
5. Hao wananchi watakaopembua ukweli na uongo unaowasemea ni wa nchi gani? Kama ni ya Tanzania wanataka ukweli gani mwingine zaidi ya kusema CCM imechoka na ipumzishwe sasa,
6. Nafikiri tusubiri uchaguzi mdogo wowote utakaofanyika hapa nchini ndio utaujua vizuri ukweli unaoutaka .
7. Ndio Maana hata kesi za kupinga matokeo ya Uchaguzi zinacheleweshwa kwa makusudi kwa sababu mnajua hamkushinda kihalali na uchaguzi ukirudiwa mtalia. Mwaka 2005 katika kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi zilikuwa zinaamuliwa mapema kwa sababu mtanashati wenu(kikwete) watu walikuwa na Imani naye.
8. WATANZANIA WANAJUA KUWA ULIAHIDIWA UWAZIRI MKUU 2005 WENZAKO WAKAKUZUNGUKA NDO MAANA UNAONGEA TU BAAAA BAAA BAAAA KAMA BATA! HUNA HOJA,HUNA UZALENDO WOWOTE, WEWE NI MNAFIKI !
Hapo jirani kwa RA kutatosha kuwa pimajoto

Kusema kweli nashindwa kuelewa serikali na Wabunge wa CCM. Nashindwa kwa sababu wanakitayarishiria CCM safari ya kwenda kuzimu kama ilivyo kwa KANU na Vyama vingine vinavyojiita vyama Ukombozi . Sijui ni ukombozi gain waliofanya hasa CCM. Maisha ni magumu, heri enzi ya Mkoloni kwani hao wazee waliopambana na ukoloni wametuhadaa sana. Wao walikuwa wanasomeshwa Bure na wakoloni, wanapata matibabu Bure tena kwa kulazimishwa na hao wakoloni.

Anayewalaani wakoloni ni ADUI YANGU NAMBA 1 Kama CCM ilivyokuwa ADUI yangu No 1 !

Jana nilikuwa naangalia Bunge Hongera Kafulila Pia Hongereni Wabunge wote wa Upinzani kwa kumpa moyo mwenzenu wa Upinzani ila nina wasiwasi na wabunge wa CUF.

Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni yaani Samweli Sitta amethibitisha unafiki wake kwa vitendo:-

Kwa kipindi hiki anapokaimu uwaziri mkuu ameonyesha jinsi gani alivyo mtu wa Visasi,

Hana tofauti na Muimba Mipasho

Uadilifu anaomshupalia lowasa ni upi ? wakati jana Mchango wa Kafulila ulikuwa na asilimia 100 za ukweli kuhusu Uadilifu wa Serikali ambapo serikali hii ya CCM haina. Na sita alivyomjibu lowasa kuhusu maamuzi magumu alisema yawe adilifu.

Bunge si Jukwaa la Mkutano wa Hadhara! Sita unaposema kuwa wabunge wengine walikuwapo kipindi cha nyuma warudishe posho za kipindi hicho ndio wasimamie mgomo wa posho si kitendo cha kizalendo. Upambanaji wako dhidi ya Ufisadi uko wapi! Bwana Sita. Hivi Posho sio sehemu ya Ufisadi! Huo unafiki wa wapinzani ni upi?

Hao wananchi watakaopembua ukweli na uongo unaowasemea ni wa nchi gani? Kama ni ya Tanzania wanataka ukweli gani mwingine zaidi ya kusema CCM imechoka na ipumzishwe sasa,

Nafikiri tusubiri uchaguzi mdogo wowote utakaofanyika hapa nchini ndio utaujua vizuri ukweli unaoutaka .

Ndio Maana hata kesi za kupinga matokeo ya Uchaguzi zinacheleweshwa kwa makusudi kwa sababu mnajua hamkushinda kihalali na uchaguzi ukirudiwa mtalia. Mwaka 2005 katika kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi zilikuwa zinaamuliwa mapema kwa sababu mtanashati wenu(kikwete) watu walikuwa na Imani naye.

WATANZANIA WANAJUA KUWA ULIAHIDIWA UWAZIRI MKUU 2005 WENZAKO WAKAKUZUNGUKA NDO MAANA UNAONGEA TU BAAAA BAAA BAAAA KAMA BATA! HUNA HOJA,HUNA UZALENDO WOWOTE, WEWE NI MNAFIKI !

Hapo jirani kwa RA kutatosha kuwa pimajoto

Huyu mzee jana alichokifanya ni kujitwisha fedhaha, umri wake na alichokiongea kwa kweli havishabihiani. Kama ndo tunaongozwa na watu wenye mtazamo finyu kwama huyu mzee kweli tumejichanganya.

Nlipata hasira sana aliposema wananchi watapima...... huyu anamaanisha anadhani sisi wananchi hatuna uwezo wakubaini utumbo na vitu sensible. Kimsing katutukana jamani.

Anaongea upupu kwa kuwa dhamira inamsuta kutokana na sualiti wake wa kuasisi uanzishwaji wa CCJ. Sikujua kuwa mvi ni rangi tu hata wasio na busara wanazo. Kama kiongozi kaonyesha busara gani kwa kuropoka maneno yale??nadhani hajui kuwa haongei yeye kama Sitta bali ni kiongozi wa shughuli za bunge. Ombi langu Mzee Pinda rudi uchukue kiti chako huyu bwana inawezekana anafanya Sabottage, mana anasifa ya USALITI

CCM imekwisha kabisa mnafikiri kuna watu humo wote ni walewale, wote wameoza na wako kimaslahi ya chama zaidi. yahani sasa hivi tuangalie nchi yetu itaongozwa vipi na si muda wa kuijadili ccm tena hawawezi kuleta mabadiliko. hvyo tusitarajie lolote na kama tutaendelea kuwabeba basi wimbo huu unajirudia palepale kama kolasi

Waungwana, it is a pity that kwa mtu aliyetumainiwa kama Samwel Sitta kutoa kauli kama zile dhidi ya upinzani. Pamoja na kuwa yupo CCM , lakini alionekana kusema ukweli hata kama utawaudhi wenzake wa CCM. jana sikuamini kauli zake alizozitoa bungeni. Mheshimiwa Sitta, umetuvunja moyo. Ilikuwa inatia moyo kuwa pamoja na kuwa uko CCM, pale penye ukweli ulikuwa unautetea hata kama unatoka kwa wapinzani. Labda kukaimu nafasi ya Waziri mkuu bungeni kumetengua msimamo wako wa kutetea haki, wanyonge etc. TUMEKWISHA, KAMA NI NDIVYO ULIVYO, BASI EL ATAUKWAA URAIS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Maana bila wewe hakuna tena CCM wa kutetea wanyonge. I stand to be corrected.

Nilifurahi sana alipokataa kufuta. Huo ndio ukweli na huyu 6 aache kujichanganya juzi tu kasema hatuwezi kutoa maamuzi mazito kwa kuwa watendaji si waadilifu= legelege

Wakatae wakasirike hawakusanyi kodi wanakura 10% na kutoa misamaha ya kodi kiholela

Ni kweli kabisa NATA. Yaani haaw jamaa hawana aibu kabisa kusema uongo. We angalia hata mawaziri wanapojibu maswali. Wanaonekana kabisa wanasema uongo.

Msisahau kipindi alipokuwa spika ndipo hizi posho zizizo na tija zilipigiwa pande,zikaboreshwa

Kwa maneno ya jana amejikaanga kwa mafuta yake mwenyewe

6 ndio legelege,

Legelege ni, mkuu wa kaya, ndo maana mpaka sasa umeme hauwaki lkn yeye yuko anachekacheka tu kwenye kila anakokwend, bila kuchukua hatua madhubuti.
Kila m2 anakubali kuwa viongozi walioko madarakani ni legelege

Back
Top Bottom