kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,331
- 12,647
- Thread starter
- #21
Wacha ni kwambie ndugu yangu, pale Kenya wana katiba mpya ya kisasa kabisa, Wana mahakama yenye nguvu kabisa na Wana bunge imara, lakini hiyo haimaanishi kuwa Kenya wana hali nzuri kuliko sisi, pale Uganda na Rwanda Wana Rais huyohuyo miaka nenda Rudi lakini hiyo haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi tunaobadilisha Marais kila miaka 5. Uarabuni hakuna uchaguzi Kuna masulutani lakini haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi ambao tunachaguana kila miaka 5.Umeeleza vizuri shida zote zinazowakabili kiasi watanzania asilimia tisini 90% !
Ila umebananga uliposema eti Katiba mpya haihusiani na vyote ulivyovieleza 😅😅 !
Short and clear ni kwamba ili uweze kubadili hizo hali mbaya ulizozieleza inabidi upate pamoja na mambo mengine lakini pia upate Viongozi bora !!
Viongozi bora wa secta zote watapatikana endapo tu Katiba mpya bora itapatikana !! Na si vinginevyo !!
Shida yetu ni zaidi ya katiba mpya bro, think outside the box. Wanacholilia wapinzani ni wao pia wapate nafasi ya kula. Mfano, chadema walisusia uchaguzi na hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020, lakini Sasa hivi wanaona tabu akina Halima kuwa bungeni kwa kutumia janjajanja Yao. Wanataka akina Halima wafukuzwe ili wapeleke watu wao kwenye bunge ambalo hao wamelisusia.
Haohao wapinzani mnaweza kutumia nguvu zenu kubwa kuwachagua lakini wakaenda tena CCM kwenda kuunga juhudi. Watu walifanya hivyo tangu enzi zile za akina Lyatonga, mabere, lamwai, mkumbo, tumbili, selasini, sumaye, lowasa, mwita, nk. Ni mpumbavu TU ambae atapoteza nguvu na rasilimali yake kwa kumchagua mpinzani ambae hatabiriki na Wala Hana alama ya kuonyesha kweli ni mpinzani wa kwelikweli.