Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Umeeleza vizuri shida zote zinazowakabili kiasi watanzania asilimia tisini 90% !

Ila umebananga uliposema eti Katiba mpya haihusiani na vyote ulivyovieleza 😅😅 !

Short and clear ni kwamba ili uweze kubadili hizo hali mbaya ulizozieleza inabidi upate pamoja na mambo mengine lakini pia upate Viongozi bora !!
Viongozi bora wa secta zote watapatikana endapo tu Katiba mpya bora itapatikana !! Na si vinginevyo !!
Wacha ni kwambie ndugu yangu, pale Kenya wana katiba mpya ya kisasa kabisa, Wana mahakama yenye nguvu kabisa na Wana bunge imara, lakini hiyo haimaanishi kuwa Kenya wana hali nzuri kuliko sisi, pale Uganda na Rwanda Wana Rais huyohuyo miaka nenda Rudi lakini hiyo haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi tunaobadilisha Marais kila miaka 5. Uarabuni hakuna uchaguzi Kuna masulutani lakini haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi ambao tunachaguana kila miaka 5.

Shida yetu ni zaidi ya katiba mpya bro, think outside the box. Wanacholilia wapinzani ni wao pia wapate nafasi ya kula. Mfano, chadema walisusia uchaguzi na hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020, lakini Sasa hivi wanaona tabu akina Halima kuwa bungeni kwa kutumia janjajanja Yao. Wanataka akina Halima wafukuzwe ili wapeleke watu wao kwenye bunge ambalo hao wamelisusia.

Haohao wapinzani mnaweza kutumia nguvu zenu kubwa kuwachagua lakini wakaenda tena CCM kwenda kuunga juhudi. Watu walifanya hivyo tangu enzi zile za akina Lyatonga, mabere, lamwai, mkumbo, tumbili, selasini, sumaye, lowasa, mwita, nk. Ni mpumbavu TU ambae atapoteza nguvu na rasilimali yake kwa kumchagua mpinzani ambae hatabiriki na Wala Hana alama ya kuonyesha kweli ni mpinzani wa kwelikweli.
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi vya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo.
#3 walizungumzie sana tena sana ,maana ccm imewasahau
 
Mfano, Kama wakiandaa mkutano na maandamano ya kupinga wizi na ufanisi mdogo kwenye bandari zetu hata Mimi nitahudhuria na kushiriki. Kama wataandamana kupinga kilimo kwa kutumia jembe la mkono nitawapongeza na kushiriki. Lakini kupinga juhudi za kutatua tatizo bandarini, hilo napinga, labda kama wangekuwa na mwekezaji Bora zaidi ya DP world lakini serikali ikamkataa na kumchagua do world.
 
Sawa sawa, tatizo hawaji na suluhisho ,mfn wakishinda watafanyaje khs vijana na ajira, khs bima za afya ,na mambo km hayo
 
Ulichoandika na hoja namba 6 Kuna tofauti Gani?
Kwani DP World ameiba nini so far? Hii ni dhana TU kwamba wataiba, wanauza. Mimi kavulata siamini kama Kuna mtu anaweza kuuza nchi yetu kwa wingi wetu huu. Pale Ufaransa Wana maguvu mengi lakini wanashindwa na vijana wadogo wanaoandamana kupinga kifo Cha mwenzao Nahel aliyeuwa na serikali. Mimi siamini kama watanzania wanaweza kushindwa kuja kumnyang'anya bandari zao DP world kama siku itagundulika kuwa hakuna faida tunayoipata kwa DP world kuwekeza kwenye bandari zetu.

Hizi ni porojo TU ndugu zangu za makuwadi wa umaskini wetu.
 
Mm na familia yangu na ukoo waooote ndio tunataka hoja hz za bandari. Pia tunataka bandari yetu tu
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi vya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo.
Kwa hiyo bandari siyo hoja nzito?
 
Wanasiasa wetu wa upinzani wanahangaika na matukio badala uhalisia wa mambo kwa ujumla wake.
Niambie siasa za wapi za sasa zinazoongelea mambo ya ujumla wake waliopo madarakani wanatetea kila uozo wao (kwa cost kubwa sababu tunawalipa) wapinzani wana-attack ili wao waingie kwenye ulaji (at least the latter hatuwalipi wala sio kazi yao kuweka mambo sawa kwa wakati husika)
Wanalalamika bila kutoa suluhu nini kifanyike.
Ni kazi yao kutoa Suluhu; na Suluhu ikitoka itafanyiwa kazi ? Na kama by design wapo pale ili waongoze unategemea watatoa suluhu ili hawa watekeleze hence wao wasiingie kwenye ulaji; Ndio maana nikasema mwisho wa siku ni wananchi wenyewe kwa umoja wao ndio wanaweza kujikomboa..., Ila kwa waliopo madarakani sio Hisani wala hizo mali sio zao ni za wananchi wote (Kwahio inabidi wanchofanya kwa niaba ya wananchi isiwe siri - we need transparency) sio kuja kuambiwa baada ya miaka kadhaa kwenye vitabu vyao kwamba waliteleza... De Ja Vu...
Walipaswa kuandamana baada ya ripoti ya CAG kuhusu umbadhilifu, walipaswa kuandamana kupinga ukosefu wa pembejeo kwa wakulima na wafugaji, walipaswa kuandamana kupinga ukosefu wa maji kwakuwa hitu vyote hivyo having uhusiano na katiba mpya.
Issue za Katiba Mpya ni debate nyingine siku ukianzisha niambie ili nije nijazilizie hapo; Issue za kuandamana walishaandamana mara ngapi na nini kilibadilika ? Sanasana inapigwa propaganda kwamba hawa watu ni wafanya fujo ? Na je ni jukumu la wapinzani kuandama kwa ajili yako au hao wakulima na wafugaji kwa ukosefu wao wa pembejeo wapige kelele wasikike - Kwahio wewe unaona waliofanya kosa ni wale ambao hawakuandamana mambo yalivyokwenda mrama na sio waliosababisha mambo hayo kwenda mrama ?
Maana katiba ya Sasa haizuii watu kupewa maji, chakula, elimu, mishahara mikubwa Wala ajira. Badala yake wanahangaika na Rais anaetaka kufanya mapinduzi kwenye bandari, maji, umeme, usafirishaji, michezo nk.
Kwahio hayo mapinduzi umeyaona wewe na wenyewe hawajayaona wala hawahitaji kuhoji ? Kwahio huyo huyo anayetaka kufanya mapinduzi hausiki na madudu ambayo umetaja hapo juu amabayo umeshauri wapinzani waandamane kwa kuyapinga ? Kwahio tumuamini vipi huyu aliyeshindwa kutatua hapo juu kwamba anachofanya sasa (bila kushirikisha wananchi wote) kwamba ni jambo jema; tunajuaje kama anayofanya sasa sio madudu kama yanayosemekana yalitaka kufanyika Bagamoyo ? Si ni watu walewale ambao hapo nyuma wametuingiza kwenye shida ? Iweje leo waaminike ? Kwanini kila kitu kisiwe wazi ili tuelewe huko anakotaka kutupeleka kama panafaa ?
Hakuna mwananchi mwenye akili atakaewaekewa. Hizi ni jitihada za wivu na kutaka kuingia Ikulu na wakishafika Ikulu wanakenua TU.
Unachanganya madesa even a Broken Clock is Right twice a Day..., hata kama wapinzani ni mashetaki mwenye busara anaangalia ni nini kinasemwa wakati huo na hata kama Watawala ni Malaika haimaanishi kila kinachowekwa mezani kimezwe tuanze kuchanganya issue utetezi wa kuongelea maisha magumu hakumzuii mtu kuongelea Bandari (in their defence na wao walivyoona ugumu huo wa maisha utazidi iwapo hata mandate ya hii commanding height yetu tutawapa watu na kutegemea hisani yao na goodwill kwamba hawatatuibia wakati tulishindwa kuwahimili wengine ambao kisheria tuliweza kuwakagua (hawa huenda hata kuingia ofisini kwao hautaweza)
Ruto alililia kwenda Ikulu na akafika Ikulu, je, wakenya wanapata ahueni gani chini ya Ruto? Ndugu zangu tatizo letu sio katiba Wala Chama tawala, bali tatizo letu ni zaidi ya katiba na Chama kilichoko madarakani,
Tatizo letu ni kubwa wala dawa yake sio moja; ila Chama Tawala ni moja ya Tatizo, hizi policy zote ni chama tawala; Chama Tawala kimeleta Tozo na kufanya watu wapunguze kutuma miamala; Chama Tawala kimepandisha Bundle kwa policy mbovu; Chama Tawala kinacheza siasa na wakulima leo msiuze nje kesho muuze; Serikali kwa matozo lukuki hadi mafuta ni bei juu; Sarakasi za waliopo sasa za kutafuta Crane n.k. Bwawa limechelewa kuisha; Unadhani nani ana mandate au kazi ya kuhakikisha maji, Umeme na Pembejeo zinafika panapofika ? Unadhani hata ukiagiza bidhaa kutoka China kwa Ndege ikafika hapa wakapiga Ushuru 60% hio ni sababu ya Bandari au kukamuana Kodi ambapo value for money haipo....
tusiwafanye watu kama vile hawana akili. Ukimuuliza mwananchi wa kule nanjilinji kuhusu bandari atakushangaa sana.
Kwamba hajui Bandari ndio inayosababisha kuleta mizigo au vitu vinavyoenda nje vinapatia pale au kwamba kukiwa hakuna security madudu yoyote yale yanaweza kupitishwa pale ? Hajui hayo yote ? Hata kama hajui mbunge wake inabidi ajue na afanye chini juu welfare yake huyu mwananchi na wajukuu wake iwe taken care of...
Wewe muulize habari za umeme, dawa, barabara, masoko, maji ya kufulia nk.
Na yote hayo haya connection na Chama Tawala wala matumizi bora ya Mali za Nchi kama vile Bandari ? Na kama hao wameshindwa kupeleka dawa, barabara masoko na hata kutoa maji sentimita mbili wataweza kumsimamia mtu ili asiibe au kufuja na kuiba katika utendaji wa bandari ?
 
HOJA GANI YA MANUFAA ZAIDI YA KULINDA ARDHI YETU ISIUZWE NA WAKUJA?
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi vya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo.
Upinzani wangekaa kimya wangeambiwa wamepewa mgao wa fuba!! NB: Hata ww unaweza peleka kwa Wananchi hayo utakayo!!
 
Wacha ni kwambie ndugu yangu, pale Kenya wana katiba mpya ya kisasa kabisa, Wana mahakama yenye nguvu kabisa na Wana bunge imara, lakini hiyo haimaanishi kuwa Kenya wana hali nzuri kuliko sisi, pale Uganda na Rwanda Wana Rais huyohuyo miaka nenda Rudi lakini hiyo haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi tunaobadilisha Marais kila miaka 5. Uarabuni hakuna uchaguzi Kuna masulutani lakini haimaanishi kuwa wao Wana hali mbaya sana kuliko sisi ambao tunachaguana kila miaka 5.

Shida yetu ni zaidi ya katiba mpya bro, think outside the box. Wanacholilia wapinzani ni wao pia wapate nafasi ya kula. Mfano, chadema walisusia uchaguzi na hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020, lakini Sasa hivi wanaona tabu akina Halima kuwa bungeni kwa kutumia janjajanja Yao. Wanataka akina Halima wafukuzwe ili wapeleke watu wao kwenye bunge ambalo hao wamelisusia.

Haohao wapinzani mnaweza kutumia nguvu zenu kubwa kuwachagua lakini wakaenda tena CCM kwenda kuunga juhudi. Watu walifanya hivyo tangu enzi zile za akina Lyatonga, mabere, lamwai, mkumbo, tumbili, selasini, sumaye, lowasa, mwita, nk. Ni mpumbavu TU ambae atapoteza nguvu na rasilimali yake kwa kumchagua mpinzani ambae hatabiriki na Wala Hana alama ya kuonyesha kweli ni mpinzani wa kwelikweli.
Kenya wametuacha mbali katika nyanja zote !!
Kwamba wapinzani kelele zao zote ili na wao wapate ulaji kama vile waliopo miaka yote tangu Uhuru wanakula keki ya taifa ni sawa tu kwa sababu nao ni watanzania na ni haki yao kuchaguliwa !!
Je Mkuu wewe unaona ni sahihi wananchi waendelee kuwalaumu hao ambao wamekuwa wakipokezana madaraka wao kwa wao tu tangu tupate Uhuru mpaka sasa kwa yale matatizo uliyoyaainisha ??!

Hutaki na wengine nao waje walaumiwe kwa hayo uliyoyaainisha ??!!
 
Mikataba ya madini nchi kupewa 3% na Wazungu na Wazungu kusafirisha makinikia kwenda kwao wapinzani mlifanya nini? Nchi ilivuna nini kama matunda ya uwepo wenu? Mnachofanya nyinyi ni "nuisance" kwa watawala na serikali. Ni heri ya huu anaekodisha bandari angalau anatafuta utofauti katika kuleta ahueni kwa wananchi, Nia yake ni njema hata kama atakosea kidogo kuliko wizi na underperformance kwenye bandari.
Wapinzani ndio waliokuwa wanapiga kelele kuhusu wizi wa madini huko bungeni na nje, lakini waliokuwa na maamuzi ni ccm kutokana na wingi wao bungeni. Ama ulitaka wapinzani wakafunge migodi?
 
Sawa sawa, tatizo hawaji na suluhisho ,mfn wakishinda watafanyaje khs vijana na ajira, khs bima za afya ,na mambo km hayo
Hawasemi watafanya nn kwenye bandari ili isihamwe na wateja, watatoa wapi matrekta ya kuwapa wakulima walime saidi, watafanyaje kuwaondoa machinga barabarani. Wanalalamika tu
 
Umeeleza vizuri shida zote zinazowakabili kiasi watanzania asilimia tisini 90% !

Ila umebananga uliposema eti Katiba mpya haihusiani na vyote ulivyovieleza 😅😅 !

Short and clear ni kwamba ili uweze kubadili hizo hali mbaya ulizozieleza inabidi upate pamoja na mambo mengine lakini pia upate Viongozi bora !!
Viongozi bora wa secta zote watapatikana endapo tu Katiba mpya bora itapatikana !! Na si vinginevyo !!
Nitajie kipengele Cha katiba yetu kinachopinga kuwa na utawala Bora.
 
Vyama vyetu vya upinzani nchini ni reactive sio proactive. Watanzania wanazo shida zao zilizogandamana na ngozi ya miili yao utadhani wameumbwa na kuzaliwa nazo.

Mpaka leo watanzania Wana shida zifuatazo:.
1. Chakula: hadi Leo watu wetu wengi hawana chakula Cha kuwatosha kula Milo 3 kwa siku kwa mwaka mzima. 90% ya wakulima bado wanatumia jembe la mkono kulima, mbegu za hovyohovyo na kutegemea mvua.

2. Uchumi: Hakuna masoko na bei za uhakika ya kuuzia mazao, mifugo, na samaki wao. Watu wetu wengi ni maskini sana hata kama wanavuja jasho jingi sana.

3. Ajira: vijana wetu wengi hawana ajira na wenye ajira wanalipwa hela kidogo sana. Hii inasababisha rushwa na huduma mbovu.

4. Elimu: Elimu yetu ni duni sana kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa walimu vizuri na wakutosha, kununua vifaa vya kufundishia na kuwa na walimu wenye sifa na ujuzi.

5. Maji: mpaka Leo watu wetu hawana maji ya kunywa.

6. Wizi wa fedha na mali za wananchi unaofanywa na wenye mamlaka.

Mambo yote haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na katiba mpya, tume ya uchaguzi Wala ukodishaji wa bandari.

Jengeni hoja ni kwa vipi mtaondoa shida hizi za wananchi kwa njia nyepesi na rahisi sana kuliko wanavyofanya CCM kwa miaka 60 ya Uhuru.

Sisi watanzania tunawaona hata nyinyi mnababaisha TU kuwaona kama mko tayari kufa, kufungwa au kuitukana serikali kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna nchi duniani hazina uchaguzi lakini maisha ya wananchi wao yanakwenda vizuri.

Tuambieni namna mtakavyotafuta fedha za kuindesha nchi, namna mtavyokuwa na mahakama zinazomua kwa haki, mtavyobadilisha kilimo, mtakavyotafuta masoko ya mazao mifugo na samaki, mtakavyoleta ajira na mishahara mikubwa kwa watumishi na mtakavyokuza elimu.

Kule Kenya wapinzani wanahoja kwakuwa wanapinga ukubwa wa Baraza la mawaziri na matumizi vya hovyo, hawapingi uwekezaji wao ambao 95% ni wakoloni wanaomiliki uchumi wao.

Wapinzani wetu sisi wanapinga mambo ya kadhi, bandari kupewa mwarabu, katiba na tume ya uchaguzi mpya inayoweza kuwaingiza na wao madarakani ili wale.

Hatujaona nchi ya Afrika iliyopata nafuu za kiuchumi, kielimu, kihuduma baada ya wapinzani kuingia Ikulu, haipo.
Blah Blah za Bandari ndo mpango mzima.

Hoja zingine zisubiri kwanza maana hayo yote yametengenezwa na CCM ili yatumike kuombea kura
 
kumbe swala la bandari ni bla blaa 😂 ugua pole mtoa mada
 
Nitajie kipengele Cha katiba yetu kinachopinga kuwa na utawala Bora.
mwaka 2020 ni mfano tu !! Lakini pia hata Mwalimu alipata kuonya kuhusu Katiba kumpa madaraka makubwa sana Mkuu wa Nchi !!

Haya matukio mawili yanatosha kuona umuhimu wa Katiba mpya !
 
Back
Top Bottom