Wakuu zangu,
Waacheni wapiganaji waifanye kazi yao..mimi sioni tatizo liko wapi..Yawezekana mimi nakosea lakini ndivyo vita inavyopigana..Mafisadi wanahitaji mashambulizi toka pande zote nje na ndani ndipo tunaweza kufanikiwa kwani hasira ya wananchi sio kwa chama CCM kama chama, isipokuwa viongozi wabovu waliomo ndani ya chama CCM...Chama ni watu.
Tukumbuke tu kwamba hata wakati wa kumwonda Hitler kulikuwepo na wapiganaji toka ndani ya utawala wake wakiitwa resistance group, hawa ndio waliofanya kazi kubwa ya kumwangusha Hitler ktk kila utawala alochukua iwe France, Urusi, na kwingineko.. Majeshi ya nchi za nje yalipokuwa yakiingia yalipata taarifa na sehemu na nyaraka za siri za Hitler hivyo kurahisisha mashambulizi.. kazi ambayo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sasa hivi nyumbani kiasi kwamba Mafisadi wanahaha!.
Binafsi Mwanakijiji kama mpiganaji akijiunga na CCM na kuahidi kuwaangusha Mafisadi nitamtazama sawa na mgombea mwingine maadam imani yangu ni huyu mwanakijiji na kile anachokisimamia. Chadema, TLP au CUF haina maana hakuna mafisadi ndani ya vyama hivyo, wapo wengi tu isipokuwa tunachoomba ni utawala mzima kutokuwa wa kifisadi hivyo agenda za watu binafsi zitakosa nafasi.
Tumeyaona nchi za jirani kama Zambia, Malawi na Kenya ambako mafisadi wametokea vyama ambavyo havikutegemewa kabisa kwani fisadi ni mtu sio chama. Kwa maana kubwa nasema hivi mchafu wa tabia ni binadamu sio dini yake. Mkandara hapa kam ni jambazi basi nafanya Ujambazi sii kwa sababu mimi ni mkristu au Muislaam ati nilibadili dini nitabadilika...hjapana kinachotakiwa ni mimi kuokoka na kazi kubwa ya jumuiya ni kumweka Lupango Mkandara iwe hata ndugu yangu akipiga simu Polisi nikakamatwa huo ndio uzalendo.
Mafisadi ni WATU, tafsiri nyingine nje ya imani hiyo mimi siikubali pamoja na kwamba naweza kuwa nimekosea sana. Sidhani kama CCM inawafundisha wanachama wake kuubeba Ufisadi ila kuna kundi la watu ndani ya CCM wanaoukumbatia.. na hakuina njia bora zaidi ya kuwakosesha nguvu hawa jamaa ila kuwaondoa ktk madaraka, kesho watajipanga upya wakifahamu sababu iliyowaangusha. Tumeyaona KANU, ZAPU, na vyama vinginevyo vilivyotangulia ktk nchi za jirani.
Nakubaliana na Mkuu Mkandala kuwa mafisadi ni watu na sio chama. Ukiangalia sera za chama cha mapinduzi ASILIA utaona kuwa kilikuwa kinajali sana watu na maendeleo yao na sio fedha kama ilivyo sasa; na kama mnakumbuka mpaka mwalimu alidiliki kusema FEDHA SIO MSINGI WA MAENDELEO. Hivyo kama ndivyo basi ni vizuri chama cha mapinduzi kikajisafisha kwa kuwaondoa mafisadi katika chama ili kiwezekuendeleza sera zake za kuwajali na kuwaletea maendeleo wanannchi. Tukirejea mfano aliotoa Mwanakijiji wa tenga la matunda, hilo tenga kama lina matunda mazima na yale mabovu, ukiwa kama mfanyabiashara utachukua hatua gani? Nadhani itakuwa sahihi kwa kuyaondoa matunda mabovu ili ubakie na matunda ambayo hayajaharibika ama sivyo yote yataharibika; kwahiyo basi kwa misingi hiyo hiyo ya tenga la matunda CCM ili ikiokoe chama haina budi kuwafukuza wanachama wote wanaohisiwa na pia kuthibitika kuwa mafisadi na kuwaacha wanachama safi kuendelea na chama chao na hii naona ndio sababu kubwa inayowafanya hawa wapambanaji wabakie humo walimo.!!