'Wapiganaji' walioko CCM wanapigania nini hasa?

Wanatakiwa kuleta msukumo wa Mabadiliko ndani ya Chama chao na kuushinda Ufisadi ndani ya Chama na kuwaondoa Mafisadi na makuwadi wao ndani ya chama kwanza, kabla hawaja kwenye Uwanja wa Taifa!

Mimi nasema to hell na lichama lao. Kama wanataka kuendelea kuwafuga hao mafisadi, let them go ahead.

It's us, the people, who can teach them muthafunkers a lesson by booting them out. But that would only happen if most folks thought like me. But I know better. It probably ain't gonna happen.
 
CCM imejaa kansa na dawa ya kansa ni kukata kiungo. Hawa wapiganaji inabidi waondoke ili kansa iweze kutibiwa.
 
Tukumbuke tu kwamba hata wakati wa kumwonda Hitler kulikuwepo na wapiganaji toka ndani ya utawala wake wakiitwa resistance group, hawa ndio waliofanya kazi kubwa ya kumwangusha Hitler ktk kila utawala alochukua iwe France, Urusi, na kwingineko.. Majeshi ya nchi za nje yalipokuwa yakiingia yalipata taarifa na sehemu na nyaraka za siri za Hitler hivyo kurahisisha mashambulizi.. kazi ambayo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sasa hivi nyumbani kiasi kwamba Mafisadi wanahaha!.

Jamani tuache kudanganyana hapa, waliojiita resistance group wakati wa Hitler walifanya vitendo vyao kwa kificho. Kujitokeza hadharani kulikuwa ni hatari na adhabu yake ilikuwa ni kifo kwani watu hao walitafutwa kwa udi na uvumba. Hawa wanaojiita wapiganaji kwa ulafi wao wanakubali kutumiwa na hao hao mafisadi kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Kamanda mkuu wa mafisadi ndiye huyo huyo kamanda mkuu wa hao wapiganaji na anawahitaji wote kwani wanatoa taswira ya vita vya ndani vya kisanii.

Mwisho wa siku wote wako pamoja katika kutetea sera, ilani na mfumo wa kiuongozi wa CCM unaohubiri mshikamano na kulindana. Adui anapotokea nje ya CCM wote wanakuwa pamoja na yeyote anayekuwa nje ya msitari, ananyoshwa kwenye vikao vyao vya kichama. Tumeshuhudia wanavyokuwa pamoja wakati wa kampeni za uchaguzi, wanavyokuwa pamoja kutetea katiba inayowapendelea, wanavyokuwa pamoja kuwashukia wapinzani, wanavyokuwa pamoja katika kuiba kura na wanavyokuwa pamoja kumsifia Kikwete kama mpiganaji dhidi ya ufisadi.

Hakuna adui wa demokrasia ya kweli nchini kuliko hawa waliovaa ngozi za kondoo kumbe ndio mbwa mwitu wa kutupwa. Hivi wana JF wenzetu kama wanazidiwa nguvu ndani ya CCM na wana hakika wananchi weng wako nyuma yao wanasubiri nini kukipa kisogo CCM ? Jibu ni rahisi - they want to eat their cake and have it. Hawana ubavu wa kutia mchanga kwenye kitumbua chao au kwa maana nyingine wanatanguliza matumbo yao, period. Mpiganaji wa kweli halali kitanda kimoja na adui halafu akiamka eti anamkana, no never - hawa ni wasanii tu.
 
Mmmmhhh too personal Mdau!
Siasa za Mbeya kwa kweli ni ngumu, unapoona mkuu wa nchi anatupiwa mawe ujue kuna tatizo......
Ukweli ni kua BAADA YA mWAKIPESILE KUDONDOKA KWENYE UCHAGUZI WA mBEYA.....Rais alifanya kosa sana kumfanya Mwaki kua mkuu wa mkoa ambao yeye anashiriki siasa, tangu ateuliwe amekua na tabia ya kuendesha siasa za hovyo-hovyo dhidi ya Mwakyembe. yeye Mwaki amekua Mbunge miaka kama kumi hana lolote alilofanya kweli, mimi nilifika hadi Kyela nikiwa katika mihangaiko yangu Nakuambia Mwakipesile hata akisimama na kijana aliemaliza kidato cha nne mwaka jana kweli atadondoka....amekua mwepesi mno kisiasa.
Sasa haya ya mwakyembe sijui kala michango ni porojo zinazotoka kwenye kambi ya Mwakipesile.....
Kweli mwaki amshukuru JK kwa kuendelea kumuweka katika ramani bila hivyo angekua anakula kitimoto pale banana.
 
unaweza kudhani hivyo wakati fulani kumbuka hii ni vita kamili, simpambano huu, kamati kuu imedhamilia kuwaondoa katika kinyang'anyiro cha uongozi 2010.....harakati za hawa watu zimesambaratisha serilkali, zimemkosanisha JK na Lowasa, zimewakosesha akina Dialo ulaji, zimemporomosha Zakhia hamdan Meghji katika siasa za nchi hii, wako wapi kina Mramba, Yona......hii ni vita kamili ndugu yangu.

Vita kamili ya maslahi yao na kuendelea kutetea uhalali wa mfumo fisadi ambao wao ni ama kwa miaka kadhaa wamekuwa makuwadi wake au wadau wakuu. Kinachoendela hapo ni spin ya kuwalaghai watanzania waliochoka kuwa KUNA MATUMAINI NDANI YA CCM kitu ambacho si kweli haswa ukichukulia MATUMAINI yenyewe yanajengwa kuwazunguka watu ambao hawana MORAL AUTHORITY ya kuupigia kelele ufisadi kwani nao ni sehemu yake....

Wengine ni kuwa wamekosa nafasi ya kufaidi zaidi na keki ya UFISADI wa enzi za UKWELI NA UWAZI na sasa ARI MPYA ambayo kina Lowassa na Rostam wamekuwa wakiendesha UKIRITIMBA wa mgawanyo.....

omarilyas
 
Na ndio maana sisi tunasema kuwa hakuna jipya hapa, wakati ni watu wale wale na mambo yale yale eti vita dhidi ya ufisadi.Kumbuka Butiamu na maazimo yao
 
tumeona watuhumiwa wa ufisadi waking'olewa/waking'oka kwenye
serikali lakini bado wamekumbatiwa na ccm. hii inatuma ujumbe mmoja tu
kwamba ccm kama chama hakioni ufisani ni noma.

waitwao wapambanaji ambao wamo ndani ya ccm watakuwa na wakati mgumu sana kubadili mfumo wa ccm ambao umejikita katika ufisadi. hata hivyo
kwa hali ilivyosasa makelele yao yanaweza sikika zaidi wakiwa ndani ya
mfumo wa ccm kuliko wakiwa nje ya ccm.

swali ni jee tunataka kusikia makelele bila vitendo dhidi ya ufisadi kutokea ndani ccm au tunaamini kuliko kelele zisizo vitendo heri hao wapambanaji ndani ya ccm wanyamaze tuu wakiachia ccm ikiendelea kujikita katika ufisadi?
 
Last edited:
Mkuu Pasco ukizungumzia Tanzania kufanya yale ya 1917 Urussi na 1886 Marekani kwa lugha nyingine unatamani Bongo tuchinjane? au? maana nisije nikawa nimekuelewa vibaya Mkuu.
Ndugu yangu Bishanga, mimi nazungumzia theory of change of system, mabadiliko toka mfumo mmoja hadi mwingine. Siyo lazima yawe ya umwagaji damu, cheche ya fikra inatosha kuanzia ila sio huu usanii wa kupigania nafsi wa makamanda kwa kutegemea nguvu za mshitiri na wengine msiwaone wanasema sana kwa jazba, hawana lolote, wanalishwa tuu maneno ili mshitiri afurahi na kuendeleza mgao wa milioni 100 kila jimbo la kamanda.
 
Pasipo kufahamu au kwa makusudi, kwa Kuogopa kuondolewa kwenye kura za Maoni 2010 na wakiwa wameshajijengea Maadui wengi ndani ya Chama wanachokishabikia, Wanejikuta wanapigania:

: Kurudisha imani ya Wananchi juu ya Chama hivyo kisianguke 2010

: Kwa Kufanya hivyo hao wanaopambana nao wanapata ahueni kwa sababu
Chama kutoanguka 2010 ni Ahueni kwao.

: Wanatafuta Sympath ya Wananchi
 
Naweka sehemu ya makala ya Muhingo Rweyemamu katika gazeti la RAI la 18.12.2008 yenye kichwa cha habari Unayo pumzi ya kugandamiza mpira?
http://www.newhabari.com/rai/habari.php?section=fikra&id=166

Tatizo la CCM si itikadi. Wote walio katika usukani wa chama, ni ma leftists. Jakaya Kikwete ni leftist anayeamini katika ujamaa. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni mjamaa, Pius Msekwa ni mjamaa, Kingunge Ngombale – Mwiru ni mjamaa pia. Tofauti kubwa inayotokea ndani ya CCM ni mgawanyiko wa ugomvi wa madaraka na kila mtu anataka kuwa juu ya mwenzake.

Mgawanyiko mkubwa uliotokea katika siku za hivi karibuni, ni kundi moja la wana CCM kuonekana kuwa katika vita ya ufisadi kuliko wanachama wenzao. Hawa ndio anawasema Rioba kwamba wameanza kujitokeza na wanakemea hali hii ya viongozi kujitakia manufaa binafisi. Mimi nasema sawa, lakini kama vyombo vya habari, tulitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo. Kwa kiasi fulani tunawafahamu wanasiasa wetu na hasa waliomo kwenye chama tawala na hasa hawa wanaoitwa mafisadi, na wale wanaowaita wenzao mafisadi.

Na tunafahamu kwamba kwa muda wa miaka zaidi ya 20 wengi wa hawa wanaoitana mafisadi walikuwa marafiki, tena marafiki wakubwa. Kundi lililoingia madarakani 2005 limeanza rasmi harakati hizo zaidi ya miaka 10 iliyopita. Mwaka 1995, ndiyo kundi lililochukizwa na hatua ya Mwalimu Nyerere kumbeba Benjamin Mkapa.

Wasio na kumbukumbu nzuri, wakasome magazeti jinsi kundi hili lilivyomchafua Nyerere. Mmoja ndiye alikuwa akitengeneza vichwa vya habari vya magazeti. Wengi, na hasa waandishi wa habari ni mashahidi. Mwanasiasa mmoja katika harakati hizi hajasahau kichwa cha habari alichokiasisi kilichosema: ‘Nyerere apaka chokaa makaburi'.

Hawa wanaoita na wanaoitwa mafisadi walikuwa pamoja, walipanga pamoja, walikusanya pamoja, walikula na kunywa pamoja, na lugha yao ilikuwa moja. Ilikuwa ndege wa mbawa zinazofanana wanaruka pamoja.

Kundi kubwa linalojulikana zaidi katika harakati hizi lilikuwa na watu wengi. Lakini vinara wake walikuwa Edward Lowassa, Samuel Sitta na Rostam Aziz.

Hili kundi liliendelea kuwa pamoja hadi uchaguzi wa 2005. Lilikuwa pamoja hadi kwenye kampeni ya Sitta kuwania ubunge.

Chai pamoja na maandazi ya wajumbe wa timu ya kampeni ya Sitta ilichemshwa/yalichomwa na mke wa Rostam Aziz nyumbani kwake hapa Dar es Salaam na Dodoma. Lowassa ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Sitta. Nusu ya hotuba ya Sitta ya kuomba kura iliandaliwa na Rostam. Sehemu ya utafiti kuhusu Bunge la Kenya ilifanywa na Rostam. Marehemu Juma Jamaldin Akukweti ndiye alikuwa kizingiti kwa Sitta kuwania ubunge, lakini ni marafiki zake hawa waliopewa jukumu kuachia nafasi hiyo. Hawa hivi sasa wamefarakana, lakini hawatuelezi wamefarakana lini na ni jambo gani limewafarakanisha baada ya kuwa marafiki. Je, ni fedha, ni vyeo au ni uzalendo? Kundi hili limetengana sasa. Wapo wazalendo na wapo mafisadi.


Nionyeshe rafiki zako nitakueleza wewe ni nani. Tungependa kujua, uzalendo wa wazalendo hawa ulianza lini na ufisadi wa mafisadi hawa ulianza lini.

Hawa waliogharimiana kila kitu, wamekorofishana lini na kwa sababu zipi? Waandishi wa habari tunatakiwa kuchunguza kwa kuwauliza maswali pande zote zinazohusika. Na tuache ushabiki kwa sababu ushabiki wetu kwa kiasi fulani umetuzuia kupata habari za pande mbili. Wapo watu hawataki kuwauliza wengine maswali eti wanasema hawa ni mafisadi. Huo si uandishi wa habari.

Na mwandishi anayejizuia kuandika habari za mtu, analo lake jambo. Inawezekana hataki habari za huyo zisikike kwa kuwa zikisikika zitaua ukweli alio nao. Lakini pia, inawezekana wapo watu, hawataki habari za huyo zisikike kwa sababu zikisikika zinaweza kuwa na mnyororo na habari zake yeye mwenyewe. Huyu atafanya kila mbinu habari za hawa wanaoitwa mafisadi zisisikike kabisa. Atahakikisha zimegandamizwa. Lakini tutagandamiza ukweli hadi lini?

Tuwape nafasi hawa ‘mafisadi' wa ndani ya CCM watueleze, walikosana lini na hawa ‘wazalendo'. Na tuwape nafasi hawa ‘wazalendo' watueleze walikosana lini na wenzao. Watueleze ufisadi huu umeanza lini? Ni hivi karibuni? Miaka 10 iliyopita au 20? Na hawa wazalendo watueleze wamejua lini kwamba hawa ni mafisadi? Tukiamua kuwauliza, tuwaulize swali la msingi kabisa. Kila mbunge wa CCM atueleze alikopata fedha zake za kampeni. Najua wapo watu wasiotaka kusikia swali hili likiulizwa. Lakini swali hili tu moja limebeba majibu ya maswali mengi.

Tusipokuwa waangalifu, tunaweza kukuta tunatumiwa na kundi la watu, lenye lengo la kutaka kunyamazisha habari kutoka upande wa pili wa marafiki zao waliokorofishana. Na uandishi wa habari, haujakamilika kama hatujapata taarifa kutoka pande mbili.

Wale viongozi wana CCM wanaowaita marafiki zao mafisadi, bila kutueleza urafiki wao umekoma lini, wana lao jambo. Kuna ukweli wanataka kuuficha. Wana kitu wanakijua, na wanatumia nguvu zao zote kuhakikisha hakitoki hadharani.
Kwa wasiomjua Muhingo Rweyemamu ndiye aliyekuwa mmoja wa vinara wa MTANDAO katika kazi ya kuhandisi habari kwa manufaa yao na kuwaangamiza washindani wao na hadi sasa ingawa amenyimwa ukuu wa wialaya aliotegemea/ahidiwa bado ni mlinzi imara wa MTANDAO. Sina hakika ni mtandao upi kati ya MTANDAO MATUMAINI ama MTANDAO MASLAHI ama MTANDAO WAPIGANAJI....

Nawasilisha...

omarilyas
 
Last edited:
- Kwani JF tunapigania nini hasa? Labda tuanze ku-establish hilo kwanza ndio tuhamie kwa wapiganaji si unajua ni kuwa viongozi ni reflection yetu wenyewe yaani wananchi, au?

FMEs!
 
- Kwani JF tunapigania nini hasa? Labda tuanze ku-establish hilo kwanza ndio tuhamie kwa wapiganaji si unajua ni kuwa viongozi ni reflection yetu wenyewe yaani wananchi, au?

FMEs!

JF ni forum, ina watu wa aina mbali mbali, so JF yote haiko katika direction moja, ndio maana kila mtu anasema anachotaka.

A. 1. Kuna wanaopinga ufisadi wa aina yeyote ile hapa Tanzania hawa wamegawanyika katika makundi 3.

1. Wale wa chama tawala CCM kama wewe
2. Wale wa vyama vingine vyoote vya upinzani
3. Wasio na vyama vyovyote wala itikadi yeyote wako kutaka Tz njema


2. Kuna wasiopinga ufisadi simply nao kwa sababu ni mafisadi, hawa kuagundua kazi sana, maana huwa wapowapo tu, lakini JF inawaruhusu wamo.

3. Kuna wasiotaka chochote hawa utawakuta kwenye thread nyingine za mapenzi,kuuza vitu, vichekesho n.k

B. 1. Katika wapinga ufisadi wa makundi 3 kuna makundi madogomadogo meengi sana.

1. Wapinga ufisadi ndani ya CCM( A.1.1)

Hawa ni waongeaji wazuri na ukweli wanapiga kelele kwa nia nzuri wakiwa na nia nzuri ila wamekosa

(a) Reality: kuwa katika historia ya Dunia hii hakuna walioshinda kwa kupinga watawala na mifumo ya kifisadi wakiwa ndani ya hicho chama hakuna, kwa hiyo hawa inawezekana

(i) wapiganaji vipofu wasio na techniques za kushinda
(ii) si wakweli wanapiga kelele kulinda vyeo vyao na maslahi yao
(iii) wanatumiwa na watawala hao mafisadi ili kuwagawa wananchi , na kukifanya chama tawala CCM kuendela kuongoza

(b) Unafiki: Pamoja na kelele zoote hizi, hawa watu wanaojifanya wapiganaji ni wanafiki, maana wanakula, wanakunywa na wanaongozwa na mafisadi(wenyeviti, marais, makatibu n.k) kwa hiyo hatima yake ni kucheza humo humo na kurudi kwenye point(a)

(c) Mbinu ya upiganaji:njaa

Wanajua ukweli, wanajua hawatashinda, wanajua hawataweza kuwaondoa JK na kundi lake wanajua kilakitu kwa uwazi, kabisa ila wafanyeje, maana

(i) Njaa na kazi ndio hiyo ndani ya serikali ya CCM, ila upepo wa revolution unawapuliza, wanajifanya kama malaika wa nuru, huku wakihubiri na kutaka tuwaamini kuwa ni wapiganaji ili hali hawana jinsi ya kujiondoa kwenye system hii ya kifisadi.(FMES wewe uko hapa)!(mawazo yangu tu mkuu, I may be wrong)!

(ii) Mbinu ya upiganaji, sijaona mpiganaji mpaka leo anayesema au aliyeshauri wananchi wahusishwe na washirikiane nao katika vitu kama maandamano, mijadala, debates, n.k HAKUNA YET NI WAPIGANAJI! thubutu! CCM mtawatenga!

(iii) If they are right; wabadili mbinu ya upiganaji! just imagine FMES hakuna aliyeenda jela wala kurudisha mali zetu yet wapiganaji, are they not evaluating themselves?

Wa vyama vingine( A.1.2)

Hili nalo nikijadili nitamaliza nafasi bure( ni khabari ndefu). nadhani unajua walichofanya CHADEMA juzi linakuwa kama tawi lenu, lakini anyway bado naamini wamejifunza. Ukiacha hawa; kuna wanafiki, waongo, wezi, mafisadi wa kambo, wenye ukabila, dini, waliokosa ajira n.k, wapo wenye nia nzuri bado wanapikwa na tutawaona tu hata kama si sasa the day will come when CCM will be a thing of the past! either wapiganaji waunde CCM B( inawezekana) , au tuone wajipange na JK mwakani ( this is valid and lively test)


Wasio na vyama vyovyote ( A.1.3)

Naamini JF wakati wa kujadili maada au maslahi ya kitaifa, tukiweka itikadi za vyama pembeni na kuweka reality mbele, then nadhani JF was meant for that.Woote regardless CCM au vyama vingine tunataka maisha bora! ikiwa hivyo basi hatutaweza kuwajua wenye itikadi kama wewe, kama na kama tu iwe forums ya kujadili na kuweka maslahi ya taifa mbele.

mathalani

1. MABADILIKO YA KATIBA
2. TUME ZA UCHAGUZI
3. Mfumo wa elimu
4. mAZINGIRA.
5
.

ONE TEST

1. JK hajafanya lolote lile in this past 4 yrs, tunataka kati ya hao unaowaita wapiganaji, wachukue form ya urais maana bila wao kuwa katika hiyo position , they will do nothing FMES hii haihitaji masters wala PhD kukubali , na nitakuonea huruma endapo utalala na kuamka ukidhani bila kati ya hao wapiganaji kushika ikulu wataweza never!

ulishawahi kupewa somo na haulewi mkuu!( angalia post number 30 ya Dr. Kitila Mkumbo)
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/36884-nini-iwe-hatma-ya-wapiganaji-warudishe-kadi-au-3.html

Ndiyo maana nimesema JF itakuwa nzuri sana kama tukisema tujadili mambo tu ya kitaifa na kupigana ni hili dudu fisadi pasi kujali vyama vyetu, truth prevails!

Ungekuwa umapata na kuilewa hiyo reality basi leo usingesema hivyo, kuendelea kusema kunatupa mawasli mengi kuhusu wewe
 
(i) Njaa na kazi ndio hiyo ndani ya serikali ya CCM, ila upepo wa revolution unawapuliza, wanajifanya kama malaika wa nuru, huku wakihubiri na kutaka tuwaamini kuwa ni wapiganaji ili hali hawana jinsi ya kujiondoa kwenye system hii ya kifisadi.(FMES wewe uko hapa)!

.

- Waberoya wewe ndiye namba one kwenye hili kundi maana ile nyumba ya wastaafu wa serikali umeinunuaje ndugu yangu kuwa mkweli basi japo kidogo?

- Mimi ni binadam huru ndio maana hata humu ninakataa kuburuzwa vipi na wewe ni huru kama mimi? Ninajifanyia kazi mwenyewe kwa kujiajiri binafsi na wala sifanyi kazi CCM, je na wewe ni hivyo hivyo ndugu yangu? Sasa nyumba ya serikali uliuziwaje na wewe sio mfanyakazi wa serikali ya CCM? mbona unajiumbua mwenyewe sasa?

- Kwa nini for once usije clean na unayoyajua kuhusu Meremeta? Yule mtoto wa masterminder wa Meremeta aliyekua akiishi kwako alikuwa akisoma na hela za nani mkuu kwa nini usiseme ukweli tu ukawa clean? Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!
 
Nimesoma maoni yote na nasikitika ni jinsi gani jamii yetu inavyozama na kuvutwa pande mbili na karibu kukatika katikati.

Mtazamo wangu kuhusiana na Makamanda wa Ufisadi (maana ya kumuita mtu Kamanda wa kitu ina maana yeye ni msimamizi mkuu wa kitu!) au Wapiganaji ni huu:

Watanzania tunadanganyana na kudanganywa na hivi vita vya nyati wawili ndani ya boma la CCM. Kinachoumia ni Nyasi ambao ni sisi Wananchi wa Tanzania bila kujali itikadi wala chama cha siasa tunachokishabikia.

Nimesema hapo awali kuwa Mzee Mwanakijiji, kawaonea haya na kuwauliza maswali mepesi, sitanii na napingana na Mzee Mwanakijiji kwa kuendelea kuwapa nafasi na hata tumaini hawa wanaojiita Wapiganaji wa Ufisadi kwa maana wanalofanya kwa kusema na matendo havisaidii nchi yetu ipate maendeleo.

Kifupi, Wapiganaji au ukipenda uwaite Makamanda wa Ufisadi, ni Wanafiki, Wajuvi, Wazandiki na Wabinafsi!

Hawana lengo la kuleta Maendeleo ya Kweli kwa Tanzania, bali wamechagua kibwagizo kinachonoga, kutetea Uhalali wa wao kuendelea kuaminiwa na kupewa dhamana ya kuwakilisha Watanzania wenzao na hata kuwaongoza.

Nasema ni Wazandiki maana wanachagua ni lipi lipendezalo na lililo tamu kusikika masikioni mwa watu na linalofurahisha na kuleta mvuto wa kupewa Ukurasa wa Mbele wa Gazeti na Maandamano Uchwara na hata Ushabiki wa kijinga ambao unaburutwa kisa ni kipenda roho(hula nyama mbichi)!.

Tanzania ina matatizo mengi sana ambayo yanahitaji Wabunge na Wapiganaji hodari ili kuleta Maendeleo na kutuondoa kwenye Umasikini na Unyonge, lakini husikii hata siku moja hawa wanaojiita Wapiganaji wakiongelea lolote la maana ambalo limekuwa machoni mwetu tangu tupate Uhuru ili kutupa Uhuru wa kweli wa kujitegemea.

Sijasikia wakipigia kelele hata kusitisha Bajeti ya Serikali, ili kumtetea Mfanyakazi wa Tanzania ambaye bado ananyonywa na Serikali yake kwa kupewa ujira hafifu ambao haukidhi na kukimu mahitaji yake.

Sijasikia wakipiga kelele kila siku, na hata kuiamrisha Serikali kutaka huduma bora za Afya na Elimu zidumishwe ili tuwe na Taifa lenye watu wenye nguvu na afya, walio na elimu na maarifa bora ili kuzidisha juhudi katika kazi na hivyo kuongeza si pato la Taifa pekee, bali kipato cha Mtanzania huyu katika safari yake ya kujitegemea.

Siwasomi wakimpigania kwa nguvu zao zote Mkulima, Mfugaji, Machinga, mchimba Madini, Mama Ntilie au Mtanzania yeyote ambaye anahitaji apewe kipaumbele ili aweze kuwa na nguvu za kujitegemea na Uimara wa kutosha aweze kujumuika kwa dhati katika ujenzi wa Taifa letu.

Hawajasimama kidete hata mara moja kutetea haki za Mtanzania wa Pemba, Waislamu wa Mwembechai, Mazeruzeru, Wanafunzi wa Vyuo, Waalimu, Wastaafu na wengine wengi ambao Dola imewadhulumu na kuwanyanyasa kama si kuwapuuza kwa kutumia mabavu na kuruhusu kikundi fulani kitumie Urafiki wao kwa Viongozi kujipatia wanachotaka. Nenda Loliondo, Simanjiro, Kilosa na hata sasa Kisarawe, Mtanzania ananyang'anywa haki yake na mali yake ya asili kwa kuzaliwa na kupewa mtu mwingine.

Siwasikii wakitoa hamasa na kuwa mfano wa kuigwa kiutendaji na kiuadilifu katika majimbo, mitaa na kata zao ambapo Wananchi waliowachagua wangeanza kupiga hatua za maendeleo kutokana na hamasa kutoka kwa kiongozi wao.

Hawajakaripia Serikali wala kupingana na Serikali kutokana n Serikali kushindwa kutimiza ahadi zake na wajibu wake kwa Mtanzania.

Sijasikia wakiikalia kooni Serikali na kuiwajibisha kwa matumizi mabaya ya fedha, kuongezeka kwa Umasikini, na ukosefu wa Ufanisi.

Siwasikii wakitoa hoja kufuta misamaha ya kodi kwa Wawekezaji ili kuongezea Taifa kipato, kufuta posho na malipo yasiyo ya lazima kwa Watu kufanya kazi zao?

Sijasikia hata siku moja, wakipinga na kupiga vita tabia ya Serikali kuomba misaada, kukopa na kutegemea kupewa fedha na wahisani, ili kujiendesha huku tuna Rasilimali za kutosha kujitegemea. Hawajaondoa kura, iwe ni Bungeni au kwenye vikao vya chama kupinga tabia chafu ya Utegemezi na Ombaomba inayofanywa na Serikali yetu na viongozi wake!

Sijawasikia wakiwafundisha Wananchi wao, mbinu bora za uzalishaji mali, elimu ya Uraia, Utu na Uhuru wa kujiamulia ili kujenga jami iliyo na Uhuru wa kweli na yenye kujitegemea?

Siwasikii wakiwaambia Wananchi wa majimbo yao kuwa wana haki kuwasikiliza na kuwakaribisha wapinzani wa kisiasa kujadili yale yaliyo ya msingi bila kuwafanya wao ni maadui au watu hatari kwa Taifa letu!

Wapiganaji hawa, ni maarufu kwa kulikariri na kulitamka Azimio la Arusha, Mwongozo wa Chama na kumuenzi Nyerere, lakini matendo yao hayaendani na kauli na hotuba wanazotoa.

Ni vipofu wa Makusudi kwa kujifanya hawaoni ubovu wa mfumo wa Utawala na Siasa Tanzania hasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambao unaua na kudumaza Demokrasia, Uhuru na Haki za Mtanzania.

Wao wamedhihirisha kuwa Wajibu wao ni kwa CCM na matakwa ya CCM. Lakini wanasahau kuwa matakwa wanayoyafanikisha sasa hivi si ya CCM bali ni ya wachache ndani ya CCM ambao wamekiteka nyara CCM na kukifanya mali yao na hivyo kila aliye ndani ya Chama amekuwa Mtwana!

Hata nikirudi katika nafasi zao za Ubunge na mengi ambayo yanafanyika Bungeni, wote hawa, Mwakyembe, Seleli, Kimaro, Sitta, Sendeka, Limbeli, Kilango walikuwa wapi kumtetea Mbunge na mpiganaji mwenzao Zitto alipoleta hija ya kuhoji mkataba wa Buzwagi kama si wao kujiunga pamoja kama Chama Tawala na kumdhalilisha na kumbeza Zitto na si kusimama kidete na kufuata mkondo wa halali na ulio sawa wa kuchangua hoja na kuifanyia uchunguzi?

Hivyo basi siridhiki na sifa tunazowamwagia hapa kuwa wao ni mashujaa, maana tunafurahia yale tunayoyataka kwa nafsi zetu kibinafsi na si kwa manufaa ya Taifa. Walichokifanya na kinachotulewesha ni kile walichokifanya Februari 2008 na kulazimisha Lowassa ajivue Uwaziri Mkuu. Lakini Mkataba wa Richmond bado haujatenguliwa, je mbona bado wako mguu pande huku tunaumia kwa bei kubwa za umeme na mbaya zaidi ukosefu wa umeme kutokana na uzembe uliozaa huo mkataba?

Vita ambavyo wanavifanya sasa hivi si kwa manufaa yako na mimi au na hata yule, bali ni kwa manufaa yao, ili waendelee kupaka siagi na jibini mkate wao.

Nimesema mara kadhaa, kuwa vita vya Ufisadi na Ufisadi, ni sehemu kiduchu tuu, katika kuangalia matatizo ya Tanzania na kupima Maendeleo ya Tanzania.

Kinachotokea CCM na hizi kambi mbili, ni ndugu kugombea tonge, sawa na Waprotestanti walivyoachana na Wakatoliki au jinsi Sunni walivyotengana na Sunni.

Ukiangalia, wote, Waprotestanti, Wakatoliki, Sunni na Shia, kila mmoja wao anatetea lile lililobora machoni pake na kujiita kuwa yeye ni bora na zaidi. Lakini wote hawa wanne, hawamjali yule ambaye si Mprotestanti, Mkatoliki, Msunni au Mshia.

Wapiganaji wa CCM, hawana nia ya kuleta Maendeleo Tanzania, kama ilivyotamkwa katika Azimio la Arusha au Mwongozo wa Chama wa mwaka 1981. Hata Ilani ya CCM ya 2005, hawaipitii na kuhoji utimilifu wake na nguvu za Wananchi na Serikali kwa umoja ili kutufikisha japo 75% ya malengo ya MKUKUTA, MKURUBITA na hata Milenia.

Hawamjali Mtanzania wa pale Kisiju ambaye leo hii, bado anatembea maili kadhaa, kwenda kuteka maji, kukata kuni, kupata tiba, huku akitumia jembe la mkono, akiishi kwenye nyumba ya tembe na watoto wake hawana mahali bora na vitendea kazi bora ili wajielimishe na kuelimika.

Ningewapa heshima, kama wangekuwa na msimamo thabiti hasa ndani ya Chama chao na ndani ya vikao vya Chama kwa kusimama kidete kumtetea Mkulima na Mfanyakazi kama katiba ya CCM inavyosema, jinsi Azimio la Arusha lilivyoagiza.

Ningeamini vita vyao, kama walipokaa Butiama, mwanzoni mwa mwaka 2009, wangesimama na kuwashurtisha watuhumiwa wote wa Ufisadi, wajieleze na wavuliwe Uanachama, la sivyo wao wangejivua Uanachama wa CCM na kueleza umma, ni jinsi gani Chama Tawala kilivyo haribiwa na Takrima na Rushwa na kukumbatia Mafisadi badala ya kuwaadhibu.

Haieleweki machoni mwangu kuwa leo hii, wale walio rudisha nyuma maendeleo ya Taifa letu kutokana na Uzembe, watu kama Lowassa, Chenge, Karamagi, Msabaha, Mramba, Yona, na wengine wengi hata ukiongeza Rostam, bado wana sauti zenye nguvu ndani ya vikao vya Chama na wana ushawishi wa hali ya juu, kiasi kwamba wamegeuza "Wapiganaji" kuwa kunguru mwoga.

MbonaWapiganaji hawakutoa tamko la kulaani kitendo cha Watendaji wa Chama na Serikali walioandaa maandamano kuwapokea Chenge na Lowassa watu waliokitia madoa CCM?

Je walipokuwa Dodoma mwezi wa August 2009, mbona hawakufurukuta ndani ya vikao vyao vya chama ili lijulikane moja kwa Taifa na ndani ya CCM kuwa wao ni "Wapiganaji" wa kweli na hawatayumbishwa au kuburuzwa na Uongozi usio makini? Kwa nini waliruhusu Sauti za Mafisadi kunguruma na kutawala vikao vya chama? Waliogopa nini kuropoka ovyo na kuvuliwa Uanachama kama NEC na CC ingeamua kuwatenda hilo?

Nikisoma kauli zao, nikipima matendo yao, bado siridhiki kuwa Wapiganaji, kweli wana nia ya kujitoa mhanga, kulifia na kulitetea Taifa lao.

Leo hii ninaposikia wakitoa vilio kuwa wanafanyia hujuma, lakini hakuna mmoja wao aliyekwenda mahakamani na kutoa ushahidi au kufungua kesi ya kuhujumia, je mnafikiri kuna ukweli kwa wanalosema?

Ikiwa wao kama Wabunge, rasilimali zote, nguvu zote na mamlaka waliyo nayo, wanaendelea kulialia na kulalamika kama mimi Mchungaji na wewe Mlalahoi mwenzangu na hawana hata Ubavu wa kusema sasa basi, ni vipi tuendelee kuamini kuwa wana nia nzuri na kilio chao na kampeni zao eti kupigana na Ufisadi ni kwa ajili ya manufaa ya Taifa?

Iweje leo waseme fulani na fulani wamefanya makosa na kutumia madaraka vibaya, lakini wao wenyewe wamefanya makosa kama hayo ili kujinufaisha na tunaambiwa walichofanya ni kwa ajili ya kumtetea mlalahoi?

Mimi nawauliza, si wanapigania nini, bali wanampigania vita hii nani? halafu ndipo wajibu wanapigani nini?

Ndio, Siasa ni mchezo mchafu, lakini iweje nao wafanane na wale wanaowatuhumu kuwa ni Mafisadi na wanacheza mchezo mchafu, ikiwa hawasimami kidete kuitetea Haki ya Mtanzania, kutumia Utu na Kweli?

Je ule mwiko na kiapo "Nitasema kweli daima, fitina kwangu Mwiko" ni maneno tuu ya kurudia kama wale wanaoimba Sala ya Bwana "Baba yetu uliye Mbinguni"?

Biblia inatufundisha, Imani bila Matendo ni Haba na Batili.

Wao Wapiganaji, wanatughairi kutuonyesha ni Waumini Safi, lakini matendo yao hayafanani kabisa na hata matokeo ya kazi zao, hazimsaidii Mtanzania, awe ni CUF, CHADEMA, TLP au CCM yenyewe, bali ni wao na vibiongo vyao vya kulemewa na mizigo ya tamaa ya Uongozi na kupenda Umaarufu.

Kama kweli Wapiganaji wangetaka niwaheshimu, wangesimama kidete kutaka Muafaka wa Suala la Muungano, Wangeilazimisha Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya dhuluma dhidi ya kila Mtanzania, iwe ni Waislamu wa Mwembechai, Wapemba wa Unguja, Mazeruzeru au ndugu zetu wanaonyang'anywa mali na ardhi ili kumnufaisha Mwekezaji na Bepari.

Wangekuwa ni Wapiganaji kweli, wasingeweka matumbo yao mbele na kujiongezea vipato na kupewa posho, huku kima cha Chini hakijaongezea, Bei za Mazao zinadidimia, Wastaafu wananyimwa mafao yao, Wanafunzi wananyimwa ada na mikopo, Wauguzi na Waalimu wanadanganywa kuhusu mishahara yao, Polisi na Wanajeshi wetu wanaishi maisha duni yanayosababisha wajiingize katika vitendo vya utovu wa nidhamu na kuvunja sheria.

Wapiganaji hawa, hawana Sera, Msimamo, Itikadi au mwelekeo.

Bali ninavyowapima, vita vyao ni kugombea Madaraka na mianya ya kujiongezea kipato binafsi na umaarufu, dhidi ya lile kundi la Kifisadi ambalo limedhamiria kumnyonya Mtanzania abakie mifupa mitupu.

Vita vyao, vingeleta maana kama vingekuwa ni vishirikishi vya Watanzania wote kwa kudai Uwajibikaji kutoka Serikali na Chama chao, ili kutimiza ahadi za Uchaguzi, kuibana Serikali kutokana na ukosefu wa nidhamu katika matumizi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuishurtisha Serikali ijenge upya mchakato wa Demokrasia ya kweli (Katiba Mpya kwa manufaa ya Watanzania si CCM pekee) ulio huru na shirikishi ili haki na utu wa Mtanzania uimarike naye aweze kushiriki kikamilifu kulijenga upya Taifa lake.

Sikatai, vita dhidi ya Ufisadi ni muhimu, lakini kitendo cha wao kuamka miaka mitatu baadaye tangu vita vilipoanza ni kuonyesha wazi kuwa hawana nia kupiga vita ufisadi.

Kilichotokea Bungeni Februari 2008, ni wazi ndio kichocheo cha mfarakano ulioko ndani ya CCM, na si ukweli kuwa wanachokifanya ni utashi wa kulinda maslahi ya Mtanzania na hazina ya Taifa letu.

Kama kweli hiyo ni nia yao, mbona hawakusikiliza, kutafakari na kufanyia kazi kelele, mayowe na vilio vyetu kila siku tulipong'amua kuwa tunahujumiwa? Hata la EPA, RICHMOND na mengine, kama si sisi kulizungumza na kuhoji tunachokisoma magazetini na kutoka kwenye mikutano yao, wasingejipukutisha na kukifanyia kazi. Kama Slaa asingeileta ile listi ya Mafisadi, ambayo iliorodhesha "Wabaya" wao, wasingeamka na kumlazimisha Rais aunde tume kuichunguza BOT!

Buhemba wanaathirika na Sumu, lakini hamjaitaka Serikali isitishe mkataba wa Barrick. Buzwagi ilifanyika kiharamia, aibu yenu ya kumtukana Zitto, imewafanya mfumbie macho makosa ya Mkataba na hivyo Taifa kuendelea na mkataba ambao ni wazi kuwa ni batili!

Labda niwaulizeni, je katika majimbo yenu, ambako mnadai wanaandaliwa makuwadi wa Mafisadi kuwanyang'anya tonge, mmefanya nini la maendeleo kuwa Wananchi wa Majimbo yenu hata hizo rushwa za Mafisadi hazitawababaisha nao watawachagua nyinyi tena?

Tukitaka kupima mafanikio na maendeleo tangu muwe wawakilishi na Wabunge wa wilaya zenu, tunaweza kuona Ufanisi katika Uzalishaji mali, Uadilifu katika Uongozi, na mipango bora inayotokana na Siasa safi?

La mwisho ambalo limenifanya niongee kwa ukali kuliko Mzee mwenzangu Mwanakijiji, ni kitendo chenu cha kuhalalisha Takrima na Rushwa.

Leo hii mmeshindwa kuwafundisha Wananchi wa Tanzania na hasa majimbo yetu, utu, uwajibikaji na uadilifu kwa kuhimiza wapokee hongo zitokazo kwa Mafisadi na hao mnaowaita Mafisadi kwa kisingio kuwa hizo pesa ni haki yao, ni marejesho ya walichodhulumiwa.

Spika Sitta na Mwakyembe wamelisema hilo wazi katika mikutano ya kunadi dhamira ya Wapiganaji.

Mnachofanya ni kuruhusu Mtanzania aendelee kushangilia Takrima na kunogewa na kipato cha ziada kitokanacho na Rushwa.

Ningekuwa mimi nyie, ningewaambia na kuwakumbusha Watanzania wote, kuwa Rushwa ni Adui wa Haki na watakapomuona yeyote anayeleta hongo, wasipokee, bali wawakamate watu hawa na kuwapeleka Polisi na Serikali iwe ya Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa au Taifa hata TAKUKURU ili sheria ifuate mkondo wake kupiga vita Ufisadi.

Mlichofanya ni kuwaambia Wananchi kuwa ni Ruksa kupewa hongo, na waitumikie vizuri, kama aliyewapa ni mzungumzaji mzuri kama nyie mnavyojifanya kuwa ni Wapiganaji.

Kwa hilo la kuhalalisha haramu ya Rushwa, Takrima, Kidogodogo na Hongo, mmelitia aibu Taifa letu, mmekiuka kiapo chenu kupita Katiba zote, anzia Katiba ya Jamhuri na hata Katib yenu ya CCM.

Je tuwaamini vipi basi kuwa nyinyi mna lengo la kuleta mabadiliko Tanzania yatakayoamsha Uwajibikaji, Ufanisi, Ushindani, Haki, Utu, Juhudi na Maarifa ili kujenga Taifa linalojitegemea na linaloshinda (si kupiga vita kwa maneno na maandishi tuu) Umasikini Ujinga na Maradhi, ikiwa mnachokipiga vita sasa hivi Ufisadi ambacho ndio msingi mkuu wa Rushwa, mnauhalalisha kwa kuwataka Watanzania wapokee hongo kutoka kwa "Mafisadi" na kuwapigia kura nyinyi?

Kama kilio chenu ni cha kweli na mnaamini Uongozi Mkuu wa Chama chenu CCM na Serikali yake haufai, mbona hamuutii Uongozi huu matumbo joto kama Mafisadi wanavyowafanyia nini?

Ni nani kati yenu yuko tayari kuwa Kondoo wa Zaka na kumwambia Mwenyekiti wenu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa ameshindwa kazi, hawezi na kuongoza Tanzania katika kuleta maendeleo na hana nia ya kupiga vita Umasikini, Ujinga, Maradhi na Ufisadi?

Msimtegemee Slaa, Mrema, Lipumba, Mtikila au Zitto kuwatatulia tazizo mlilo nalo ndani ya Chama chenu ambacho ndicho mnalialia na kunung'unika.

Fanyeni kweli na aliye mwanaume na mpiganaji wa kweli kati yenu, akaze kende na atikise Kiberiti na kuutaka Urais wa Tanzania kupitia CCM kupingana na Kikwete , ili vita vyenu vilete maana na tuone kama mkipata hayo mamlaka, kama mtaleta maendeleo kwa Taifa letu na kuushinda Ufisadi!
 
Rev. Kishoka..
Mkuu mimi sikubaliani na usemi wako na nitanukuu tena maneno ya Field Marshall Es.. Wanachokifanya makamanda hao ni sawa kabisa na sisi hapa JF..mapungufu unayoyaona kwao ni sawa na yetu sisi isipokuwa wao wako chama CCM, wewe na mimi tupo TZ na ndio tuliowachagua na tutaendelea kuwachagua Mafisadi. wanachokifanya na kukitangaza ndio waraka wa kweli, waraka unaokubalika na watu wote, leo ukiwaponda hawa sijui kesho Kardinali Pengo utamtazama vipi!

Sasa tujiulize mwenye kosa tangulizi nani kati yetu kama sio sisi wananchi tuliwapa kura zetu hao Mafisadi..Leo hii hawana hata wizara, hawana wadhifa, Uheshimiwa umebakia wa tuzo..Wamebakia ktk chama kutokana na sheria ambayo hawa Wapiganaji hawawezi kuivunja kwani sisi wananchi ndio tuliowachagua.

Mafisadi ni wabunge wetu. Lowassa, Chenge, Karamagi, Rostam na wengine wote ni chaguo la wananchi. na kibaya zaidi tuliaswa mapema kuhusu watu hawa lakini sisi wenyewe tulimwona Nyerere kichaa Mjamaa mwenye roho mbaya!.

Hivyo waacheni jamaa waifanye kazi yao kama Mwanakijiji anavyokuja hapa kijiwezi na kumwaga manyanga yake.. Mwanakijiji ni Mpiganaji kwa njia yake lakini ukitaka ku question Upiganaji wake unaweza kuzua maswali mengi tu..Na hakika hadi tunavyozungumza hivi sasa Mwanakijiji anaweza kuwa mwanachama wa chama CCM!..
 
Rev. Kishoka..
Mkuu mimi sikubaliani na usemi wako na nitanukuu tena maneno ya Field Marshall Es.. Wanachokifanya makamanda hao ni sawa kabisa na sisi hapa JF..mapungufu unayoyaona kwao ni sawa na yetu sisi isipokuwa wao wako chama CCM, wewe na mimi tupo TZ na ndio tuliowachagua na tutaendelea kuwachagua Mafisadi. wanachokifanya na kukitangaza ndio waraka wa kweli, waraka unaokubalika na watu wote, leo ukiwaponda hawa sijui kesho Kardinali Pengo utamtazama vipi!

Sasa tujiulize mwenye kosa tangulizi nani kati yetu kama sio sisi wananchi tuliwapa kura zetu hao Mafisadi..Leo hii hawana hata wizara, hawana wadhifa, Uheshimiwa umebakia wa tuzo..Wamebakia ktk chama kutokana na sheria ambayo hawa Wapiganaji hawawezi kuivunja kwani sisi wananchi ndio tuliowachagua.

Mafisadi ni wabunge wetu. Lowassa, Chenge, Karamagi, Rostam na wengine wote ni chaguo la wananchi. na kibaya zaidi tuliaswa mapema kuhusu watu hawa lakini sisi wenyewe tulimwona Nyerere kichaa Mjamaa mwenye roho mbaya!.

Hivyo waacheni jamaa waifanye kazi yao kama Mwanakijiji anavyokuja hapa kijiwezi na kumwaga manyanga yake.. Mwanakijiji ni Mpiganaji kwa njia yake lakini ukitaka ku question Upiganaji wake unaweza kuzua maswali mengi tu..Na hakika hadi tunavyozungumza hivi sasa Mwanakijiji anaweza kuwa mwanachama wa chama CCM!..

Mkandara,

Una haki kutokukubaliana nami. Nami nitaendelea kuuliza, je hao tunaowatetea kuwa ni Wapiganaji, malengo yao ni yapi? Je wakishaushinda Ufisadi (kama wataushinda) ndipo Tanzania itapata maendeleo?

Ukirudi kusoma tathmini ya Mwanakijiji kuhusu Ufisadi (Ufisadi 101), utagundua kuwa ni sehemu moja katika matatizo ya Mtanzania!

Tunang'ang'ania vita vya Ufisadi, vita ambavyo tumezidiwa mbinu za medani na kuachilia mbali kuweka kipaumbele kwenye mambo mengine ya msingi?

Nilichowauliza Wapiganaji ni cha msingi,
  • Kwa nini hawajaongeza kima cha chini cha mshahara wa Mtanzania? Kwa nini wanaruhusu Bajeti kuendelea kufujwa?
  • Kwa nini wanaruhusu Deni la Taifa kuongezeka bila kuidhibiti Serikali na matumizi yake ambayo huifanya iendelee kukopa na kuchapa pesa na hivyo kuangusha thamani ya shilingi yetu?
  • Kwa nini wanaendekeza Serikali kujiamulia kutoa Rasilimali zetu na kutoa upendeleo wa misamaha ya kodi na ushuru kwa Wawekezaji kwa kisingizio cha kivutio cha uwekezaji?
  • Kwa nini hawato masharti ya kubana fedha kwa Wizara, Taasisi na ofisi za Serikali ambazo zimefuja pesa na hazina mahesabu mazuri na kila mwaka wanapokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa mahesabu?
  • Kwa nini wanaendelea kuegemea kwa kufanya inachokitaka Chama na kwa Manufaa ya Chama na si kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na manufaa ya Tanzania?
Kwa nini mimi na wewe tuendelee kuwakumbusha na kung'ang'ania wafanye kazi zao kwa umakini na si kwa utashi wao binafsi?

Nchi haina Umeme, Barabara, Reli, Bandari madhubuti, hakuna maji, Shule hazina Waalimu, Vitabu au madawati, Hospitali hazina Madaktari, Wauguzi wala Dawa, hayo hayapewi kipaumbele na kuimbiwa Pambio kama si Kaswida na Wapiganaji, lakini hili la wao kugombea mlo kwa kudai fulani Fisadi, ndio wanaloona ni bora?

Je wao wako upande gani kuleta mabadiliko ya kweli ya Demokrasia Tanzania? Sijasikia wakileta mswaada wa kubadilisha Katiba ya Tanzania, kushinikiza kuwepo kwa tume huru ya Uchaguzi, kote Serikali ya Muungano na Zanzibar, sijasikia wakikemea tabia chafu ya kugeuza Bunge kuwa chombo cha Chama cha kisiasa au Mahakama kunyimwa na kuminywa nguvu zake!

Kama mnataka Wapiganaji, basi wajue kupigana vita, wajue ni kwa nini wanapigana, wabainishe wanapigana vita kwa niaba ya nani na wawe na malengo ya maana na si malengo ya kupamba magazeti na kusifiwa.

Nitarudi kwenye swala moja tu, Richmond. Kwa nini mpaka leo hii, zaidi ya Lowassa kujivua Uwaziri Mkuu, hakuna lililofanyika kuvunja mkataba wa Richmond, kufanikish mapendekezo ya kamati au kuhakikisha kuwa Tanesco na Serikali zinahakikisha tuna mfumo mzuri wa kutuletea Umeme?

Kam wao walileta mapendekezo, na Serikali mpaka leo inajivutavuta kufanya kazi, wanashindwa nini kutumia nguvu yao waliyopewa na Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kutaka uwajibikaji kutoka Serikalini?

Kama Serikali inajivutavuta kufanya kazi na kuleta ufumbuzi wa jambo la Richmond, sawa na lile la EPA na Meremeta, kwa nini hawaleti mswaada wa kutokuwa na Imani na Serikali Bungeni na hivyo kumng'oa Waziri Mkuu au hata Rais kwa kushindwa kutekeleza majukumu?

Kwa nini hawafuati alichofanya Augustino Lyatonga Mrema aliyesema na kuamua kuachana na kudanganyana?
 
- Waberoya wewe ndiye namba one kwenye hili kundi maana ile nyumba ya wastaafu wa serikali umeinunuaje ndugu yangu kuwa mkweli basi japo kidogo?

- Mimi ni binadam huru ndio maana hata humu ninakataa kuburuzwa vipi na wewe ni huru kama mimi? Ninajifanyia kazi mwenyewe kwa kujiajiri binafsi na wala sifanyi kazi CCM, je na wewe ni hivyo hivyo ndugu yangu? Sasa nyumba ya serikali uliuziwaje na wewe sio mfanyakazi wa serikali ya CCM? mbona unajiumbua mwenyewe sasa?

- Kwa nini for once usije clean na unayoyajua kuhusu Meremeta? Yule mtoto wa masterminder wa Meremeta aliyekua akiishi kwako alikuwa akisoma na hela za nani mkuu kwa nini usiseme ukweli tu ukawa clean? Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!

Tunguaneni tu wanaccm ikifika january wote tumewajua na hamtaweza kutuzuga kama hao wanaojiita makamanda wa ufisadi kumbe ni wapaliliaji wa ufisadi.
 
- Waberoya wewe ndiye namba one kwenye hili kundi maana ile nyumba ya wastaafu wa serikali umeinunuaje ndugu yangu kuwa mkweli basi japo kidogo?

- Mimi ni binadam huru ndio maana hata humu ninakataa kuburuzwa vipi na wewe ni huru kama mimi? Ninajifanyia kazi mwenyewe kwa kujiajiri binafsi na wala sifanyi kazi CCM, je na wewe ni hivyo hivyo ndugu yangu? Sasa nyumba ya serikali uliuziwaje na wewe sio mfanyakazi wa serikali ya CCM? mbona unajiumbua mwenyewe sasa?

- Kwa nini for once usije clean na unayoyajua kuhusu Meremeta? Yule mtoto wa masterminder wa Meremeta aliyekua akiishi kwako alikuwa akisoma na hela za nani mkuu kwa nini usiseme ukweli tu ukawa clean? Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!

Kaka kumbe humu ndani mnajuana, na pengine huwa mnaoneana aibu hata kuelezana ukweli.

Mkuu mimi ni junior staff chuo kimoja kikuu, sina nyumba nina kiwanja mbagala, niko masomoni nje, sina na sijawahi kuota kununua hizo nyumba, hata kama pesa ningekuwa nayo.

Umenishtua kuzungumza kwa ujasiri kiasi hicho mkuu! sijakuelewa na ninazidi kushtuka badala ya kujiibu HOJA unarusha tuhuma tena za uwongo. Humu ndani watu tunatumia majina ya yasiyo yetu, UMENIJUAJE?

Hivi mkuu una umri gani? maana ni vizuri nitamshauri invisible watu wawe wanadisplay umri wao hata kama watadanganya, ni vizuri tuwajue wenye frustration za kunyimwa migao na mafisadi!

Anyway, tufanye uliyosema ni kweli; KWA HIYO NA WEWE FISADI KWA SABABU MIMI FISADI??? NDIYO MAANA MNAONGOZANA NA FISADI Mkuu?? unaona ulivyoingia kwenye mtego? kwa hiyo kumbe kweli siku zoote hizo unajifanya malaika wa nuru?? unajifanya kukusanya mawazo ya wana JF uwapelekee wapiganaji, eti wapiganaji woote wanamsikiliza FMES, na hawafanyi lolote mpaka FMES ASEME KITU!!!! mkuu unaseduce mawazo ya wanaokufuata!

Hiyo Meremeta nilivyo shallow, at least free copy za MKJJ zilinitoa tongotongo!!!

FMES narudia teena hapa sio wewe, sijaamini mkuu, for future the best way ya kuona huwezi kujibu tuhuma ni kukaa kimya! this is great weapon, na sio kujibu ulivyosema

OK, waambie wana JF mimi ni nani na toa details zote, thibitisha hizo tuhuma.INA , NYUMBA GANI MEREMETA GANI LOL!, TOA DATA ZANGU ZOTE NA ZANGU SITATOA MIMI;MODS watatoa kwa niaba yangu maana wana record ya malipo yangu ya mwezi mmoja!!!!!mkuu huna pa kukimbilia

Ukishindwa kuthibitisha tukuiteje???? utakubali kubatizwa majina yooote nitakayo mimi?

Nacheka nakuwa kama nakuona vile umebanwa, this is JF bwana ukiona nyingine copy, unapewa vidonge vyako na nenda kaseme uko kwa wakubwa wako!

Hili jiwe unalo mkuu, tafuta kubadilika na kuwa honesty na siyo kuzushia watu tuhuma as if you know everbody, wazee bwana!

Mkuu wewe ukipingwa tu kwa hoja unazushia watu uongo? ili wakimbie JF na kuwaharibia status zao? kwa faida ya nani? sijashtuka sana anyway, inadhihirisha ulivyo CCM damu! LOL

Hii sijawahi kutegemea kutoka kwako!!!!!!!!He!!

waambie tena sentensi hii fupi, kuwa hakuna msafi CCM!

ukome kusema wapo na ukome kujiita mpiganaji ndani ya mafisadi, wachawi mko humuhumu, MIMI nimekujua kwa post zako tu mkuu, sina namna ya kukujua zaidi ya hapo, maana hutanisaidia kitu!

Ndiyo mnamualika rais azindue zahanati! mafisadi nyie!

He!!! YA LEO KALI!!!

ASSIGNMENT!

1. JIBU HOJA
2.THIBITISHA TUHUMA, maana si vizuri ukawa unaishi ukiwajua mafisadi, wewe ndiyo unakuwa fisadi mkubwa! hili nalo linakuweka pabaya sana, nimesema jina langu halisi watatoa MODS na si mie!
 
Kifupi, Wapiganaji au ukipenda uwaite Makamanda wa Ufisadi, ni Wanafiki, Wajuvi, Wazandiki na Wabinafsi!

i!

Glory to God, I am not alone! thanks sir! hizo comments zikitoka kwa wazee kama nyie mnaifanya JF kuinuliwa kuwa sehemu salama! na kuwavuta weengi tuwasikie wanasemaje , jamani nchi yetu, hata safari yetu ikiisha kukamilika tutakuwa na raha, kuwa wajukuu zetu wanaishi nchi salama ya mababu zao!
 
Back
Top Bottom