Wapendwa mnisaidie how to move on,nataka kumdelete mme wangu parmanently

Pole dada kama ni ndoa ya kanisani haina jinsi vumilia tu,ninyi ni waislamu unaweza ongelea issue ya talaka lakini kama ni mkristo na ndoa imefungwa kanisani mama hapo pana kazi maana yeyote atakayeachana na mwenzake na kwenda kuolewa ili hali mwenzake wa ndoa bado yu hai AZINI.,hakikisha hakuna kuchoka mahusiano yale yale yaliyokuwepo kabla ya kuzaa yanaendelea kama mume wako ni wa goli tano mpaka asubuhi jitahidi angalau ukiishia nne sio mbaya lakini kama kabla ya kuzaa mlikuwa mnafunga tano umezaa zimepungua mpaka moja au sifuri asikudanganye mtu lazima mwenzako atatoka tu..Ushauri wa bure huo.

Manyusi umenifanya nicheke haa haaaa haaaaa hope na Amelie amecheka pia ujumbe mzuri na mzito kazi kwako mama
 
Pole sana Dada, Jaribu kufikiri sana nini kinamfanya mumeo atoke nje au ulishawahi kumuliza kosa lako liko wapi mpaka anakutendea vituko kama hivyo?...

Yaani hapo mie ndipo ninapopakataa (nashukuru The Boss kwenye Uzi wake alisema wazi kuwa wanaume wengi wancheat si kwasababu mke ana matatizo.), hakuna sababu yoyote inayompa mwenzi legitimacy ya kucheat; poor us most of the time sio tu tunalaumiwa, but worse enough twajilaumu wenyewe kwa makosa ya waume zetu!

Huyo mumewe kama walivyowengi he is just arrogant son of his father! Na anafanya hivyo just because he CAN; si ndio wanaume husema kuwa naturally ni poligamist!

Sasa bidada, you can either live with it and wait for divine intervention or do something (quit that ndoa)!
 
Manyusi, assume mumewe Amelia yumo humu ndani, hebu mshauri tisikie ushauri wako! Coz wanaume design hiyo wapo wengi humu, u could be one of them!
 
Mimi ni mke wa mme mmoja,tuna watoto wawili 2yrs na 10moths.Nilishamfumania live kwa small house tena chumbani nikasamehe,alishawahi tengeneza number ya kufanana na yangu akampa small hs nikasamehe.ana small hous 3 ninazozifahamu.alisafiri kwenda mkoani akasema siku zimeongenzwa.nikaingia kwenye mail yake nikakuta alitakiwa kurudi Dar jana,nipo nje ya Dar nikamtuma mdogo wangu aende air port jamaa aliingia DaR JANA.WHy ALINIDANGANYA?B'COZ ALIPAKA KUSTAY KWA ONE OF SMALL HOUses.NIMECHOKA I NEED TO MOVE ON,PLS help.AMELIE

Mara nyingi katika mambo makini kama haya huwa natoa ushauri wangu kwa wino mwekundu. Nashauri kama ifuatavyo
  1. Ulizaliwa peke yako, tunashirikiana hapa duniani, ila kila mtu atakufa kivyake
  2. Hapo kwenye nyekundu, nahisi ulimaanisha wewe ni mwaminifu
  3. Je, wewe hujawahi kumtenda mmeo kwa namna yoyote ile?
  4. Ukiamua kuachana naye, nina uhakika baada ya muda utapata mwanaume mwingine aka hawala na si mume, kwa sababu wewe si malaika. Mwili wako utadai mahitaji yake, naye atakutimizia. Si mimi si wewe hakuna anayejua litakalotokea baada ya kuwa na huyo mwanaume.
  5. Kuachana naye ili upate amani ya moyo, sawa, ila kupata mwanaume mwingine mwaminifu si guarantee.
  6. Mpe probation period kwa kutengana naye kwa muda kama wa miaka miwili hivi. Hapo utajua kama amebadilika na wewe kujihakikishia kama unaweza kuishi bila yeye kwa maisha yako yote.
 
kwan ndoa ni kitu gani we mtu...ni muhimu zaidi ya uhai na maisha yako? Mmekutana watu wawili ambao hamjuani wala hamfanani wala sio ndugu...mkakubaliana kuanzisha familia ili muje kuwa na mji wenu hapo mbeleni...leo makubaliano yenu mmoja anayatia doa kwa makusudi kabisa huku akijua hali ya sasa ya maradhi akijua kabisa makubaliano yenu yameleta matunda ambayo ni watoto na jukumu lililo mbele ni kuwatunza yeye fedha anaenda kutumia na malaya wachafu wachafu wanaotembea na mtu kwa sababu ya fedha anauuza utu wako bila hidhini wala kibali chako kuna haja gan ya kuendelea kuvumilia na kuendekeza upumba.vu...kama wewe ni mdhaifu usiwe unachangia mada kama hizi

Uko desperate!! no wonder!
 
POle sana Amelie na wote mlioguswa hisia zenu za ndani ila wale walioguswa zaidi inabidi mpoe kidogo maana tukileta maneno ya kumsimanga huyo kaka inazidi kumuumiza Amelie na kumuona mumewe hafai...binafsi naamini huo ni upepo tu na uchungu wa mke kwani wanajuana wanapendana wakiwa wenyewe hatujui wanachofanya na akirudi tu akimuona moyo wake unapoa ila sasa ni upweke na hasira ya kudanganywa ambako hatuna hakika km jamaa karudi au vip.Wengi wamemuombea hope nayy kajiombea ...Amelie is going to be well and fine ila piga goti lazima kieleweke Mungu wako yu hai umebakiza sehemu kidogo sana uuguse moyo wake.
 
Kama mmefunga ndoa kanisani pengine ungefafanua kanisa gani. Kama in RC basi ushauri wangu ni usali sana kumuombea mume wako, mwenye pepo wa ngono, rozari takatifu na kujitahidi kumuwekea misa ikiwezekana kila siku. Maana hakuna kinachoshindikana kwa Mungu.Sali kwa novena pamoja na watoto maana sala zao zinapenya mawingu.
 
pole sana dada vp ndo yenu ni takatifu? namaanisha mmefunga ndoa if yes naomba nenda kwa viongozi wa dini wajaribu kumkanya na kama wazazi wapo nao washirikishe ili uokoe ndoa yako usimdelete fasta hivyo watoto wanaitaji malezi yenu wawili ukiokoa ndoa utawsaidia sana watoto




fuata huo ushaurio utakusadia
 
Dada yangu jambo la muhimu ni kutulia kwanza kuna wimbo mmoja wa zamani unasema usimpe talaka subiri japo kwa mwaka kwani talaka ya hasira ni mbaya sana .Hivyo dada yangu kuwa na subira mambo mazuri hayataki haraka vumilia japo kidogo ili uwatunze watoto wako kwani utajisikiaje pale watoto wako watakapokuwa wanalelewa na mama wa kambo na wanateseka itakutesa sana kuliko unavyoona jipange kwanza subira huvuta heri
 
Back
Top Bottom