Wao wakishinda magoli ya offside na nyie shindeni pia ya hivyo hivyo. Mambo ya kulalamika wakati wewe umeshindwa kutumia nafasi hayana maana

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
618
1,569
Kitendo cha mashabiki wa Yanga kuanza kulalamikia bao la John Boko kuwa alikuwa offside naona ni kupotezeana muda tu, Boko kafanya home work yake iliyomfanya awe uwanjani na kaikamilisha na refa karuhusu kuwa ni goli halali makekele ya nini?

Ukiona mwenzako anatumia mbinu za kimafia kushinda mechi utakiwi kupiga mayowe mtandaoni unatakiwa na wewe kuaply mbinu Ile Ile Tena kimya kimya mwisho wa siku atakaemzidi ujanja mwenzake ndio championi!

Yanga wamefanya kosa kule mbeya ya kuruhusu kufungwa kwa uzembe wao ivyo wasitake na wenzao wafanye kosa kama wao, watulize akili wafocus kwenye mechi zinazofata na wasirudie kosa kama lile, ninavyawajua Yanga mechi ya mbalali imewapa funzo na inaweza kuwa ndio starting point yao ya kuanza kuusaka ubingwa kwa gia kubwa atakaewabeza kwa matokeo ya mbalali basi atakuwa anapotea njia na ajui mpira!

Yanga anacho kikosi bora kinachoweza kufanya lolote na kwa muda wowote, hivyo habari za malalamiko mara waamuzi waliwabeba ihefu, mara hivo mara vile ni ujinga wa wapumbavu wachache, akuna goli lililofungwa na yanga mbalali likakataliwa sasa unapataje hoja ya kusema ayo yote?

Mashabiki na wanachama wa Yanga acheni upuuzi wenu pambanieni timu yenu ndani ya uwanja na nje ya uwanja na sio ukizidiwa ujanja unaleta hoja zisizokuwa na kichwa wala miguu, Mumlaumu kocha wenu kwa kuanza na wakaa benchi mbeya na sio vinginevyo!
 
Back
Top Bottom