Simba waliiogopa mno Yanga kabla ya mechi na wakati wa mechi.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,318
12,622
Hakukuwa na ulazima wa Simba kumfukuza kocha peke yake kwa kosa la kufungwa magoli 5 na Yanga. Kufungwa kwa Simba kulisababishwa na sababu na wadau wengi wakiwemo viongozi na wachezaji wenyewe.

Simba iliingia kwenye mechi ile wadau wote wa simba (kocha, wachezaji, uongozi na mashabiki) wakiwa na hofu kubwa sana ya kupoteza. Hofu yao ilitokana na ukweli ambao walikuwa wanaufahamu kuwa Yanga inacheza vizuri, ina wachezaji wazuri, ina kocha bora na uongozi mzuri kuliko Simba. Na kitendo cha kocha Gamondi kuhudhuria kwenye mechi za Simba kulizidisha hofu yao hii. Hofu hii ya wadau wote wa simba ilifanikiwa kujipenyeza kunye akili na miguu ya wachezaji wa Simba wakashindwa kucheza.

Hofu ya simba kabla na wakati wa mechi inathibitishwa na mambo yafuatayo:
1. Ahmed Ally, msemaji wao kabla ya mechi mbele ya kamera alisema kuwa Yanga ni timu imara na imekamilika kila idara, aliwatia hofu wadau wote wa simba.

2. Manula kudaka: Kitendo cha kumchezesha Manula kwenye mechi ile na kuwaacha makipa wote waliokuwa wakidaka kwa miezi karibu 7 ni dalili nyingine ya hofu kuu ya mechi, hofu hii ilikwenda mpaka kwa wachezaji na wadau wote.
3. Kuumia na kutolewa kwa Kibu Denis kuliongeza hofu kwa wachezaji. Simba amekuwa ikimuimba Kibu mbele ya wachezaji wenzake kuwa ndiye mchezaji bora na muhimu kwenye derby ya Simba na Yanga, hadi wakaampachika cheo cha kijinga cha mgeni rasmi wa mchezo; na baahati nzuri Kibu aliweza kusawazisha goli la Msonda ndaniya dk 6 tu. Kuumia na kuondolewa uwanjani "mgeni rasmi" aliyesawazisha goli kulizidisha hofu kwa simba na kusababisha kocha, wachezaji na wadau wengine kuwa na hofu kubwa.
4. Kutolewa kwa Chama. Chama anaamika kuwa mchezaji anaeweza kubadilisha matokeo yeye kama yeye ingawaje kocha hamtaki Chama kwenye mfumo wake wa uchezaji. Kutolewa nje kwa Chama kulizidisha hofu kwa wachezaji wengine kama Saido na wengine kwenye kikosi.
5. Kuingia kwa Onana: Wachezaji wote na mashabiki wote wa simba wanafahamu kuwa Onana ni unga, kuingia kwa Onana kulizidisha mashaka.
6. Kuundwa kwa kamati ya watu 21 muda mfupi kuelekea siku ya mechi ni ushahidi mwingine kuwa Simba ilikuwa na hofu (phobia) kuu.

Haikuwa sahihi kumuondoa KOcha peke yake, bali walitakiwa kutumia makosa ya mechi ile kujiimarisha zaidi. Vinginevyo, walipaswa kuondoka kocha, baadhi ya wachezaji na baadhi ya viongozi wakuu wa Simba.

Robertihno ana akili sana, aliweza kuwatumia wachezaji wabovu na wazee kupata matokeo, mtamkumbuka tu.
 
JamiiForums-312072181.jpg
 
Tatizo la simba ni kuanzia.
1. Muwekezaji.
2. Mwenyekiti mangungu.
3.Try again.
4. Body ya wakurugenzi
5. Management.
6.Benchi la ufundi lote.
7. Scout analyst,nk
8. wadau.
9. Washauri wa Bodi.
10 mashabiki mbumbumbu
Akitolewa chama wanalia na kuzomea pmf sana, wanamlilia miquisson kurejeshwa, Adebagor na manzoki
 
Hoja namba 3 kwa mtazamo wangu, naona ndiyo iliyolizamisha baharini jahazi la Simba. Ni sahihi kabisa kabla ya mchezo, mashabiki wengi wa Simba na hata baadhi ya hao viongozi wao walimkweza sana Kibu Dennis.

Na hata alipofunga goli la kusawazisha, alionesha alama ya kuwaziba mdomo mashabiki wa Yanga wakati anashangilia. Na kwa muda wote aliocheza kwenye ile mechi, mabeki wa Yanga walitumia nguvu kubwa sana kumkaba Kibu Dennis, ili tu kuepusha madhara yake, kiasi cha kuacha mianya kwa washambuliaji wengine wa simba mfano Baleke kukosa magoli ya wazi.

Ila baada ya kutolewa nje kwa huyo Kibu Dennis kutokana na majeraha aliyoyapata, ndipo kwa bahati mbaya sana vijana wa Mangungu waliingia kwenye mfumo wa Yanga. Na kilichotokea baada ya hapo, ni maumivu tu.
 
Tatizo la simba ni kuanzia.
1. Muwekezaji.
2. Mwenyekiti mangungu.
3.Try again.
4. Body ya wakurugenzi
5. Management.
6.Benchi la ufundi lote.
7. Scout analyst,nk
8. wadau.
9. Washauri wa Bodi.
10 mashabiki mbumbumbu
Akitolewa chama wanalia na kuzomea pmf sana, wanamlilia miquisson kurejeshwa, Adebagor na manzoki



Management inasajili wachezaji wastaafu.

Saido mstafu.
Chama mstafu.
Ngoma mstafu.
Boko mstaafu.
Miquisson mstaafu.
Kapombe.
Shabalala mstafu
Phili mstaafu.
 
Robertihno aliweje kuwatumia wachezaji hawa kupata matokeo? ni falsafa yake ya objective football?

wachezaji wengi sana waliteseka sana Kumudu aina ya falsafa ya Robertinho.

Wachezaji walio enjoy ule mchezo wa kukabia juu na kushambulia kwa nguvu ni..
Kibu.
Mzamiru na
Saido tu
Wengine waliteseka mno.
 
wachezaji wengi sana waliteseka sana Kumudu aina ya falsafa ya Robertinho.

Wachezaji walio enjoy ule mchezo wa kukabia juu na kushambulia kwa nguvu ni..
Kibu.
Mzamiru na
Saido tu
Wengine waliteseka mno.
aombe kurudi Vipers. Uzembe wa Robertihno ni kuwasifu wachezaji kupitiliza wakati wa pre-season kama vile alishikiwa mtutu wa bunduki asifu kitu kibovu na asichokiamini. Papatupapatu zilikuwa nyingi sana kupata matokeo.
 
Mkuu kavulata Nawashauri kwa maana nzuri tu, ACHENI KUTAFUTA SABABU. Ili kuisaidia timu na maumivu yenu ya baadae, mnatakiwa kuwa na kauli moja tu! YANGA NI WAZURI SANA WAMETUFUNGA SABABU SIMBA IMEZIDIWA NA YANGA. Baada ya kuwa na hii concept mtajifunza na probably mtajifunza kutoka Yanga
 
Mkuu kavulata Nawashauri kwa maana nzuri tu, ACHENI KUTAFUTA SABABU. Ili kuisaidia timu na maumivu yenu ya baadae, mnatakiwa kuwa na kauli moja tu! YANGA NI WAZURI SANA WAMETUFUNGA SABABU SIMBA IMEZIDIWA NA YANGA. Baada ya kuwa na hii concept mtajifunza na probably mtajifunza kutoka Yanga
Simba kuna watu wengi sana wa kufukuza. hata hivyo haikutakuwa iwe ni robertihno. Kocha alikuwa akitumia mbinu zake mwenyewe kupata matokeo kwa kutumia wachezaji wabovu na wazee. Tanga wanamsajili kutoka vipers walikuwa wanajua robertihno anatumia mfumo gani uwanjani, na hata alivyofika tu kuna wachezaji kama Chama na wengine kama Phili aliwakataa kwakuwa hawaendani na mfumo wake. Alipojaribu kumtoa Chama nje wadau wote walimjia juu kocha hadi ikambidi amtumie Chama hivyohivyo kishingo upande.
 
Tatizo la simba ni kuanzia.
1. Muwekezaji.
2. Mwenyekiti mangungu.
3.Try again.
4. Body ya wakurugenzi
5. Management.
6.Benchi la ufundi lote.
7. Scout analyst,nk
8. wadau.
9. Washauri wa Bodi.
10 mashabiki mbumbumbu
Akitolewa chama wanalia na kuzomea pmf sana, wanamlilia miquisson kurejeshwa, Adebagor na manzoki
Wapigaji ni wengi sana, wote hawa ni wapigaji, wanaitafuna club. Mo anaidhulumu timu, na wengine wanamdhukumu mo, wanadhulumiana.

Unamtuhumu mchezaji kisha unampanga kwenye mechi. Simba 0 - 1 Namungo
 
Back
Top Bottom