Wandwi amshushua Dk Slaa

Huyu Wandwi ana matatizo:

1. Je ni kweli kwamba uchaguzi ulikuwa wa haki? mbona waangalizi wote wa nje na ndani wameripoti kwamba haki ilifinywa?

2. Kama kweli hakukuwa na makaratasi ya kura bandia, wale wagombea wa CCM kama vile Mahanga walitoa wapi yale maboksi ya kura?

3. Kama ni kweli kwamba wananchi walikuwa wanafuata helikopta ya CHADEMA, mbona CCM walikuwa wanatumia helikopta tatu....na bado walihitaji kusomba wananchi kwa mabasi na malori pamoja na kuwapa posho ili kuhudhuria mikutano yao?

4. Kama ni kweli kwamba CUF wana mtandao mpana vijijini kuliko CHADEMA kwa kuwa walikuwa wakitumia magari kwenye kampeni kupita vijijini na kuwafikia wapiga kura wengi, mbona CHADEMA wamepata kura milioni mbili na zaidi pamoja na kuchakachuliwa...ambazo ni nyingi mno ukilinganisha na zile laki sita za CUF?....na mbona CHADEMA wamepata wabunge wengi katika kona mbalimbali za nchi wakati CUF wao wapo visiwani na Lindi tu?..Hapa ni chama gani kina mtandao mpana kati ya CHADEMA na CUF?

5. Ni kwa nini Wandwi aseme sasa? ...kwa sababu ameshindwa na CHADEMA ubunge musoma mjini?...ama CUF wapo karibu zaidi na CCM kimahusiano kuliko nyama vingine vya upinzani?.....

Mimi namuona huyu kama mfa maji na asiyevumilia maumivu ya kushindwa..tena kihalali.
 
Ubongo wa Wandwi haufanyi kazi tena ndio maana aliambulia kura chache uchaguzi 2010. kilichobaki kujipendekeza CCM tu
 
Hivi huyu wandwi si ni yule aliyekuwa akijipendekezaza kwa Lyatonga? si huyu huyu aliyetoka CCM akaenda NCCR-Mageuzi halafu TLP kabla ya kukimbilia CUF? mbona anakata tamaa ya kugombea ubunge mapema wakati hajamaliza vyama vyote? Hata kama anajiona hana nafasi ya kukubaliwa kugombea ubunge kupitia CHADEMA lakini anaweza angalau kukubaliwa kuwa mwanachama wa kawaida akitubu na kujirekebisha. Anaweza pia kujiunga na PPT Maendeleo, NRA, DP, CHAUSTA nk. Asianze kujidhalilisha kama bwana yake AL Mrema kwa kucheza ngoma za CCM akifikiri naye watamlinda. CCM hawatachukua mizoga kama yeye na wala hawatamsaidia kupata chochote maana Kondom haitumiwi mara mbili!!!!!!!!!!
 
ALIYEKUWA mgombea wa ubunge Jimbo la MusomaNMjini, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mustafa Wandwi, amemtaka aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa, kuacha kuzungumza mambo ya kuambiwa bali awe na ushahidi wa kutosha.

Pia amesifia uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu kwamba ulikuwa wa haki na huru zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki, alisema kuwa mgombea huyo wa Chadema amekuwa akizungumza mambo ambayo hakuyachambua kwa kina kama kweli yana ukweli wowote na yana madhara gani kwa jamii.

Alisema kitendo alichokionesha Dk. Slaa cha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, sio cha kiungwana kwa kiongozi mkubwa kama yeye ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kubwa ya
nchi.

"Dk. Slaa ana matatizo makubwa ambayo inabidi ajifunze na aache kutumia muda wake kusikiliza mambo ya kuambiwa na kuyaamini, kiongozi mkubwa kama yeye lazima awe na subira na kuyachambua kwa kina yale anayoambiwa kabla ya kuyasema," alisema na kuongeza:

"Mfano kipindi cha kampeni, wakati ule maboksi na karatasi za kupigia kura yakiletwa nchini, alisema kuwa kuna kontena limeingizwa mkoani Mbeya likitokea Afrika ya Kusini likiwa na kura za wizi.

“Serikali ilipofuatilia walikuta ni vipodozi, aache kudanganywa na watu wake wa karibu uongo ni adui mkubwa wa nchi yetu ".

Alisema kuwa kasoro ambazo Dk. Slaa amekuwa akizisema kwa baadhi ya majimbo kuwa maofisa wa usalama waliongia kwenye vituo vya kupigia kura, ni kasoro za kibinaadamu lakini hazikuwa na lengo ya kubadilisha matokeo kwa kuiba kura kama alivyosema mgombea huyo.

"Kasoro ambazo anazisema Dk. Slaa ni za kawaida lakini kama ingekuwa suala hilo lingetokea nchi mzima basi tungesema CCM ameiba kura lakini kitu kingine ambacho Dk. Slaa anashindwa
kujua ni kuamini wakati wa kampeni zake, watu waliokuwa wanajaa kuwa ni kura halisi.

"Kuna wengine tangu wamezaliwa hawajawahi kuiona helkopta kwa kuwa kampeni za kutumia ndege ni chache katika nchi yetu na Bara letu la Afrika pia wengine walikuwa wanahudhuria lakini hawakujiandikisha kupiga kura kura,"alisema.

Alisema kuwa Dk. Slaa ameshindwa kujua kuwa kampeni zake zilijikita zaidi mjini ambapo wapiga kura ni asilimia 20 ikilinganishwa na asilimia 80 ya wapiga kura wengi ambao
wapo vijijini.

"Yeye amesafiri na kufanya kampeni kwa ndege, hakupita vijijini na kuona wapiga kura wake pia mtandao wa Chadema sio mkubwa nchini kama wa CCM na CUF ambao wagombea wao walitumia magari kuwafikia wananchi walio wengi vijijini, “ alisema.

Wandwi alikiri kuwa vijana wameamua kupiga kura na kuwachagua vijana wenzao kwa maana hiyo hana mpango tena kugombea nafasi hiyo mwaka 2015 kwa kuwa sasa wananchi wanahitaji viongozi vijana ambao wanaamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia.

Huyu Wandwi ni majeruhi wa Chadema. Amekosa Ubunge wa MSM TWN sasa anatafuta huruma za CCM. Apuuzwe huyo Wandwi
 
Ni vizuri Mzee wandwi akajua kwamba NOTHING IS PERMANENT EXCEPT CHANGE na mabadiliko siku zote yanahitaji uthubutu, mambo haya yanahitaji siku zote nguvu mpya toka nje ya CCM otherwise CCM inaogopa kuleta mabadilko kwa sababu ya hofu juu ya future yao
 
Sasa nimeamini kuwa CUF ni tawi la CCM.
Pia sitoshangaa nikisikia Wandwi amehamia CCM.
 
Wandwi amesema kweli kabisa na kweli kama tuijuavyo inauma ,labda Mheshimiwa Wandwi aliwapiga dongo ,hivi miaka iliyopita ni akina nani waliyakubali matokeo na akina nani waliyapinga ? Kama sikosei Chadema walikuwa wa mwanzo kujipendekeza kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki ,sasa mkuki kwa ngedele. Chadema mnayo kazi ,afu mnaposema mnaweka vijana kugombea basi wekeni vijana na sio vizere ,watu ambao hata akili zinakuwa zinaanza kunoki na inabidi zisikumwe ili ziwe na kasi,hivi yale makontena si aliokota hapa JF akaenda kusema kwenje viwanja ,kumbe ni uvumi tu,ndio akili za kizee hizo hazina mshiko.
 
wote hawa ndo walewale wanaokunywa na kula baa nyumbni watoto wanalala na njaa yaani CCM
 
TANU na ASP vilizaa CCM, naomba jibu la CCM na CUF kutazaliwa chama gani safari hii....je katiba itabadilika kufuata maamuzi mapya au itabaki hii ya Ccm?
 
Wandwi ni mmoja wa wanasiasa wa zamani aliekosa mvuta kabisa pale Musoma; hapo alipo anajisemea kujitafutia sifa tu


Kuhusu vipodozi, je yeye huyo Wandwi kweli aliviona na kuthibitisha kuwa vilikuwa ni vipodozi na wala hakukuwa na masanduku ya kura? je yale msanaduku ya kura walishokwa nayo watu wa CCM yalitoka wapi?, mbona na yeyeye mwenyewe anafuata aliyoambiwa tu. Tuliambiwa kuwa lori lilikuwa na vipodizi lakini wala hatukuonyeshwa picha ya vitu vilivyokuwa kwenye lori hilo. Lilishikiliwa kwa siku mja na mara baada ya amri kutoka kwa bosi likaachiwa na ndipo tukapangiwa hadithi za vipodozi.
 
Hivi kwani yeye anaongea kama nani? kwa nini asianze kukaa kimya yeye? watu wengine bwana, kama kweli ana nanihii angetumia msemo huu ambao wengi ndo tunautumia" Never argue with a fool, wise men may not see the difference" mpelekeeni hii meseji
 
Hivi kwani yeye anaongea kama nani? kwa nini asianze kukaa kimya yeye? watu wengine bwana, kama kweli ana nanihii angetumia msemo huu ambao wengi ndo tunautumia" Never argue with a fool, wise men may not see the difference" mpelekeeni hii meseji

wengine wanatafuta umaarufu kupiti kwa Dr Slaa na hawatapata hasa kwa kuwa Slaa si size yaoo
kwani wandwi kuna tofauti gani kina khdija kopa?
 
Back
Top Bottom