Anatafuta kaumaarufu kwamba alikuwepo au alitoa maoni..ni haki yake!
This is a quote from the man who held very sensitive positions in previous governments including the post of a Regional Police Commander! Sijui alikuwa anawaongoza vipi maaskari wake kwa jinsi alivyoonyesha poor reasoning hapa.ALIYEKUWA mgombea wa ubunge Jimbo la MusomaNMjini, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mustafa Wandwi, amemtaka aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa, kuacha kuzungumza mambo ya kuambiwa bali awe na ushahidi wa kutosha.
Pia amesifia uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu kwamba ulikuwa wa haki na huru zaidi.
Akizungumza na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki, alisema kuwa mgombea huyo wa Chadema amekuwa akizungumza mambo ambayo hakuyachambua kwa kina kama kweli yana ukweli wowote na yana madhara gani kwa jamii.
Alisema kitendo alichokionesha Dk. Slaa cha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, sio cha kiungwana kwa kiongozi mkubwa kama yeye ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kubwa ya
nchi.
"Dk. Slaa ana matatizo makubwa ambayo inabidi ajifunze na aache kutumia muda wake kusikiliza mambo ya kuambiwa na kuyaamini, kiongozi mkubwa kama yeye lazima awe na subira na kuyachambua kwa kina yale anayoambiwa kabla ya kuyasema," alisema na kuongeza:
"Mfano kipindi cha kampeni, wakati ule maboksi na karatasi za kupigia kura yakiletwa nchini, alisema kuwa kuna kontena limeingizwa mkoani Mbeya likitokea Afrika ya Kusini likiwa na kura za wizi.
Serikali ilipofuatilia walikuta ni vipodozi, aache kudanganywa na watu wake wa karibu uongo ni adui mkubwa wa nchi yetu ".
Alisema kuwa kasoro ambazo Dk. Slaa amekuwa akizisema kwa baadhi ya majimbo kuwa maofisa wa usalama waliongia kwenye vituo vya kupigia kura, ni kasoro za kibinaadamu lakini hazikuwa na lengo ya kubadilisha matokeo kwa kuiba kura kama alivyosema mgombea huyo.
"Kasoro ambazo anazisema Dk. Slaa ni za kawaida lakini kama ingekuwa suala hilo lingetokea nchi mzima basi tungesema CCM ameiba kura lakini kitu kingine ambacho Dk. Slaa anashindwa
kujua ni kuamini wakati wa kampeni zake, watu waliokuwa wanajaa kuwa ni kura halisi.
"Kuna wengine tangu wamezaliwa hawajawahi kuiona helkopta kwa kuwa kampeni za kutumia ndege ni chache katika nchi yetu na Bara letu la Afrika pia wengine walikuwa wanahudhuria lakini hawakujiandikisha kupiga kura kura,"alisema.
Alisema kuwa Dk. Slaa ameshindwa kujua kuwa kampeni zake zilijikita zaidi mjini ambapo wapiga kura ni asilimia 20 ikilinganishwa na asilimia 80 ya wapiga kura wengi ambao
wapo vijijini.
"Yeye amesafiri na kufanya kampeni kwa ndege, hakupita vijijini na kuona wapiga kura wake pia mtandao wa Chadema sio mkubwa nchini kama wa CCM na CUF ambao wagombea wao walitumia magari kuwafikia wananchi walio wengi vijijini, alisema.
Wandwi alikiri kuwa vijana wameamua kupiga kura na kuwachagua vijana wenzao kwa maana hiyo hana mpango tena kugombea nafasi hiyo mwaka 2015 kwa kuwa sasa wananchi wanahitaji viongozi vijana ambao wanaamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia.