Wanawake wenye hadhi ya mama mdogo nawapata kirahisi, hii inaweza kuhusiana na mambo ya koroho?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853

Wanawake wenye jina la mama mdogo nawapata kirahisi, hii inaweza kuhusiana na mambo ya koroho?​


Ni jina la yule mama mdogo ambaye wamezoena zaidi na mama ukiachana na wadogo zake wengine wawili wa kike.

Nakumbuka sekondari form 3 hadi 4 kuna binti alikuwa na hilo jina aliniganda na tulipendana sana, alikuwa ananiletea biki, kwenye mpira ananishangilia, alikuwa anaacha daftari lake lenye mashairi ya mapenzi kwenye dawati langu, na mamboz mengine, alilia tulipomaliza form 4.

Niliwahi kwenda mkoa fulani kwajili ya likizo nilitokea kupendwa pia na mrembo wa mtaa wa pili, sikuwahi kufikiria hata kumtongoza japo nilimtamani lakini nilishajua hizi siyo levo zangu maana hata kiuchumi nilikuwa najikongoja.

Nakumbuka rafiki yangu wa hapo siku flani aliniletea salamu kwamba huyo manzi ananipa hi, wala sikuchukulia serious ila kuna siku tulikutana mtaani tukaongea mongezi automatically ndani ya muda mfupi tukawa kama marafiki, nilimuomba namba akanipa bila shida, ndani ya siku 2 tu tushazoeana sana, penzi nililifaidi na tuliachana kwa amani ilipobidi nirudi kwetu, mawasiliano yalipungua.

Huyu mwengine alikuwa kaajiriwa shirika flani yupo kwenye 27 hivi, status yake ilikuwa juu kuzidi yangu hasa kiuchumi maana hata gari yake tu inavyeka lita 3 kila siku. Niliwahi kwenda ofisini kwao kurekebisha meza na milango, wakati nipo bize naendelea na kazi zangu niliona anatoka na kurudi kila mara.

Nikamwambia kama kuna tatizo akajibu ni ishu za comouter hakuna mtandao, nikawa namshauri atulie tu mambo yatakuwa sawa. Tukaanza maongezi mengine ya kawaida tu chit chat huku naendelea na kazi yangu. Niligundua kanogewa sana na maongezi kwa hali yake ya kuwa na ushirikiano wa juu tunapozungumza.

Nilimaliza kazi katika ofisi yake kuhamia nyingine ila alikuwa anapita pita. Ninavyoondoka niliweza kupata chance ya kumuaga, baada ya siku 3 naona namba mpya, ni yeye kanicheki WhatsApp aliitoa namba kwenye daftari la wageni, wala haikunipa shida. Akawa anauliza ofisi yangu anataka aje anunue kibubu nikampa location.

Alikuwa anapenda kuja kuulizia bei za vitu ila aliwahi kuniungisha kibubu. Nikaongeza akili zangu nikaona huyu hafati kibubu wala bei za vitu, tuliweza kuwa couple tuliyodumu kwa miezi miwili na kiukweli binti nilifaidi penzi lake. Kiuchumi hakunipa stress kabisa alijihudumia ila kuna muda ilibidi nijtoe kidogo.
 
Tanzania ni nchi ya pili kwa kuamini uchaWi hahahahahaha sasa naona ile nafasi hatukustahili tulitakiwa kuwa wa kwanza
 
Back
Top Bottom