Wanawake wengi wasomi au wenye kipato kizuri hawadumu kwenye mahusiano!

Hakuna ukweli hapo! Nijuavyo na kuamini mimi wanawake wasomi na wenye kipato huwa na mapenzi ya kweli na hujali sana ndoa zao, labda itokee mume awe bazazi, ndiyo sababu ya wadada hawa sababu wako independent huamua ku move on, Angalia Asha-Rose Migiro anatesa na ndoa yake, hajaota wala mapembe!

Mkuu Masanilo
Hapo kwenye wino hapo hapo hapo hapoooooo ndipo nina swali nako.

Ila mtu ukioa mwanamke msomi mwenye kazi ya maana kaza buti, maana uongo ndogo ndogo anaziwekea theory, ghafla bin vuu anakudaka tena kiurahisi. Maana anakuwa na matandao mkubwa wa habari na marafiki. Ila unaenjoy viburi vya kijinga hakuna
 
...kina Kaka walio nao katika mahusiano kuhakikisha mambo yanakwenda kama wengine tu.

NB:
Kumbuka kuwa simaanishi wasichana wote walio katika kundi hilo bali ni walio wengi wao.

...hakikisha unamuoa mwanamke angalau uliye na kiwango naye sawa cha elimu na kimapato. Ukimzidi kipato na elimu, raha na amani inazidi pia!
 
MwanajamiiOne mbona hautuelezi uzoefu wako binafsi instead unapoint a lady u know. Zile post zako ulizokuwa unatuma hapa kuomba ushauri zilikuwa umetunga tu kupiga watu fix?? kumbuka mada inasema hawadumu ama wanakuwa na migogoro mingi sana katika mahusiano na haimaanishi kuwa wao ndio chanzo cha matatizo hayo japokuwa inaweza ikawa ndio wao. Na pia ikumbukwe kuwa sio unaona mtu mmoja tu ama wewe mwenyewe unaishi vizuri ndio ukatoa conclusion kuwa hiyo kitu sio kweli.
Masanja kaelezea vizuri sana kwenye post yake, Tunahitaji mchango wako juu ya nini kifanyike katika kubadili huo mtazamo unaosema watu wanao juu wanawake wasomi.

Since umenipoint directly nitajitahidi kukujibu.

When I said a lady ... it could be me- Am the lady whom I know myself! but for this I would not refer to myself since I cant applause myself kuwa ni humble.

But the lady am takin about here I really know and she has been/ and continue to be a victim of this steriotype for a long time and only GOD knows when and how she is going to get out of it. Tatizo ni kuwa yeye anampenda sana mumewe but mume (though claiming kumpenda too) but has a very funny way of showing it.

Ukiachilia mbali threads ambazo nimecut and paste (ambazo nimeacknowledge) sijawahi kutunga. For this I cant say more but take it from me they are really realities of maisha ambayo watu wanayapitia chini ya jua hili, maisha ambayo wewe unawezausiimagine kuwa yanaweza kukutokea but they are HAPPENING.

Kama umenipata vema ni kuwa sijasema kuwa wanawake hao ndio huwa chanzo ni ila mara nyingi wengi wao wanafall under the victim-blaming situation. Kuwa hata kama mumewe ndo mwenye matatizo basi ataambiwa ni yeye na hii inategemea na mumewe anavyomchukulia. Sasa kama from the beggining mume alizoea kukuscon kuwa eh msomi , ukimjibu kidogo tu katika kueleweshana unaambiwa wewe msomi unategemea mkokorofishana katika point ya kuachana sababu itakuwa ipi? si wewe ni msomi? I remember one day zamani the lady I know alishawahi kuambiwa anaringa na videgree vyake wakati they are just piece of papers!! kisa the man alichelewa kurudi home na akarudi akiwa amelewa kupitiliza (then anadrive) The lady I know alipomwambia madhara ya kunywa na kuendesha jibu likatoka hilo!

Nini kifanyike?
You guys/ na wanawake we have to know na kukubali kuwa mapenzi na elimu havihusiani kabisa wala kipato as long as penzi ni la kweli. Unapomchumbia mke hakikisha kuwa husumbuliwi na usomi wake in the first place but ukishaanza kudoubt tu basi utamkaribisha shetani naye atakupokea
 
Hakuna ukweli hapo! Nijuavyo na kuamini mimi wanawake wasomi na wenye kipato huwa na mapenzi ya kweli na hujali sana ndoa zao, labda itokee mume awe bazazi, ndiyo sababu ya wadada hawa sababu wako independent huamua ku move on, Angalia Asha-Rose Migiro anatesa na ndoa yake, hajaota wala mapembe!

Kaka Excellent
This is the truth
 
Masanja,
Umegusa penyewe haswaaa!!
Busara inabidi itumike kwa wote.Mwanamume akiwa mkorofi kupindukia basi ni mawili:
1.career ya mke itaharibika
2.Au ndoa ivunjike.
Wanawake hujikuta kwenye njia panda...inapofikia kuamua kati ya hayo mawili.Wanaoamua namba 1. Hujikuta wakifanya kazi ambazo hawazipendi ili tu kuwaridhisha waume zao.Kwa watu wasioelewa hudhani kuwa mwanamke huyo ni ama mvivu au hathubutu vyakutosha kuingia ushindani mkubwa.Kwa wenye kuchagua namba 2. ndio hujenga takwimu za KUTHIBITISHA kwamba wanawake wenye kazi nzuri na vipato hawadumishi ndoa zao.
Sijui ni jipi jema hapa.
jamani maisha ni kusaidiana,kushauriana kupeana moyo na kutiana nguvu ili kuboresha familia
mke au mume yeyote kati yao anaweza kukosea katika maamuzi mbalimbali ya kimaisha kinachohitajika ni kukosoana na kuelekezana kwa wema bila kubugudhiana wala kuweka mbele kuwa ni msomi hivyo hataki kuambiwa wala kushauriwa.
Tatizo mara nyingi ni wanaume kutegea majukumu yao ya kutunza familia kifedha ,hawatoi fedha mpaka ahakikishe mkewe kaishiwa kabisa na hata pa kukopa hana ukimwambia atadai anasimangwa kumbe ukifuatilia kwa makini utagundua ana matumizi yasiyo rasmi anayojua mwenyewe!
ukichelewa kurudi nyumbani kwa sababu za msingi kabisa za kikazi jamaa ananuna wiki nzima!
ukipata safari ya kikazi usiseme tena ,mara nyingine unaomba usipangwe safari ili uokoe ndoa lakini mwenzako haelewi na wala hajali
ukipandishwa cheo atasema bosi unauhusiano nae atashangaa baada ya kujua kuwa bosi ni mwanamke mwenzio ila uchapakazi wako ndio uliokupandisha
wanaume wawapende na kuheshimu michango ya wanawake ktk jamii kama mama zao,dada zao ,wake zao n.k
kwa baadhi ya wanaume wanawake wote ni wajinga na hawana mawazo mazuri isipokuwa mama zao.na wapuuzi zaidi ni wake zao.hawakumbuki kuwa huyo wa maana kwako pia ni mke wa mwingine (BABAKE) ambae pia humwona mpuuzi.
tuaminiane tujenge familia bora.
 
Kama umeolewa nadhani huna muda mrefu, ni dhahiri unachukia mumeo na ndoa yako! Binafsi napenda mwanamke msomi maana mtakuwa manapeana challenge nyumbani na kubishana kwa hoja!

Wewe unaonyesha uko kishari shari, hutaki kuulizwa kitu kwa maandishi yako unaamini kabisa wanaume wote duniani ni wabaya isipokuwa baba yako! Kitu cha muhimu nadhani wakati wa mahusiano ni kujuana kama mtaweza kuwa na LOVE na si LUST
 
Baba yangu mdogo baada ya kuishi sana ulaya akaja akakaoa kadada ka darasa la saba ,kisha anakaona kashamba ,kajinga hakajui kudifferenciate btn bad and good na fainaly akatafuta mamsapu msomi kama nyumba ndogo yake .
 
Ana akili sana huyo baba mdogo....anatafuta sehemu atakayokuwa anapata challenge, maana huyo wa darasa la saba kila kitu ni hewala mume wangu!
 
Hizi society zetu zinachangia pakubwa tu katika kum-stereotype mwanamke haswa aliyesoma, mwenye kazi na mapato mazuri.. mie i have been a victim of mama mkwe mtarajiwa kuuliza kama huyo mwenye PhD utamuweza???? sasa hata kama mie sina neno mambo yenyewe ndiyo hayo hata familia inakuwa macho wazi..u are constantly being watchd waone kama una zile 'tabia' za wanawake waliosoma!!! we need to change some of these mindsets!

ah! ningekuwa mwnamume i would love to have an independent intelligent woman as a partner and wife!!!!
 
....You guys/ na wanawake we have to know na kukubali kuwa mapenzi na elimu havihusiani kabisa wala kipato as long as penzi ni la kweli. Unapomchumbia mke hakikisha kuwa husumbuliwi na usomi wake in the first place but ukishaanza kudoubt tu basi utamkaribisha shetani naye atakupokea

...nakubaliana nawe mapenzi haihusiani na elimu wala kipato, lakini Ndoa inahusiana na hayo!

unless mmejiamulia kuoana wenyewe, lakini unapokwenda kuchumbia si ajabu mshenga kuulizwa;

-kabila lake

-ukoo wake

-elimu/kazi yake

-makaazi yake

-nk

sidhani kama posa itakubaliwa kirahisi iwapo mume atajulikana ni jobless fulani ambaye hakuona umuhimu wa madarasa ya msingi wala sekondari.
 
Hakuna ukweli hapo! Nijuavyo na kuamini mimi wanawake wasomi na wenye kipato huwa na mapenzi ya kweli na hujali sana ndoa zao, labda itokee mume awe bazazi, ndiyo sababu ya wadada hawa sababu wako independent huamua ku move on, Angalia Asha-Rose Migiro anatesa na ndoa yake, hajaota wala mapembe!
Masanilo, kwa lugha nyingine unakubaliana kwamba dada hawa wasomi na wenye kipato kikubwa wako tayari kuwaacha waume zao walio mabazazi kwa sababu wako independent kwa sababu wana elimu na kipato kizuri cha maisha. Hawawezi kuvumilia tabia mbaya au chafu katika mahusiano kwani wanajiweeza. Kama ni vivyo basi ni kweli kwamba ndoa zao nyingi hazidumu kwa vile hawako tayari kuvumilia ujinga. Kumbe kudumu kwao katika ndoa ni conditional.
Hii inawatofautisha na wale wenye elimu ndogo na kipato kidogo ambao lazima wavumilie hata kama mume ni bazazi kwani hawana jinsi. Je, nimekupata vizuri?
 
Masanilo, kwa lugha nyingine unakubaliana kwamba dada hawa wasomi na wenye kipato kikubwa wako tayari kuwaacha waume zao walio mabazazi kwa sababu wako independent kwa sababu wana elimu na kipato kizuri cha maisha. Hawawezi kuvumilia tabia mbaya au chafu katika mahusiano kwani wanajiweeza. Kama ni vivyo basi ni kweli kwamba ndoa zao nyingi hazidumu kwa vile hawako tayari kuvumilia ujinga. Kumbe kudumu kwao katika ndoa ni conditional. Hii inawatofautisha na wale wenye elimu ndogo na kipato kidogo ambao lazima wavumilie hata kama mume ni bazazi kwani hawana jinsi. Je, nimekupata vizuri?

Oooh yeah umenisoma kabisa mazee, ongezea na lichoandika ShiShi hapo Juu....
 
Hapa kuna matatizo kwa pande zote mbili mwanaume awe msomi au siyo msomi na upande wa pili mwanamke msomi

Kwa upande wa mwanaume ni kukosa kujiamini kuwa huyu mwanamke atamuheshimu au la. Na je akiwa na kazi ambayo itakuwa na pesa sana itakuwaje

Kwa upande wa mwanamke ni kuwa kuna tatizo la kimalezi ambalo kwa mila za Kiafrika tunaamini kuwa mwanaume siku zote yupo juu na ni kichwa cha familia, sasa huyu mwanamke anavyokuwa na elimu ya juu anakuwa aidha kazi yake inamlazimu kuchelewa kurudi nyumbani au kusafiri sana lakini wengi wao hushindwa kuwaweka chi waume zao na kuwafafnulia kwa kina kuhusiana na kazi zao. Kwahiyo mume hujiona kutengwa sana na kuanza kusononeka na hatimaye magomvi yasiyokwisha.

Nini kifanyike
Ni kupendana kwa dhati tu
 
...ah! ningekuwa mwnamume i would love to have an independent intelligent woman as a partner and wife!!!!

...Shishi, ungekuwa mwanaume wala usingefikiria hivyo, au ndio mambo ya 'if i was a boy' by sasha fierce? :)

Hapa kuna matatizo kwa pande zote mbili mwanaume awe msomi au siyo msomi na upande wa pili mwanamke msomi

Kwa upande wa mwanaume ni kukosa kujiamini kuwa huyu mwanamke atamuheshimu au la. Na je akiwa na kazi ambayo itakuwa na pesa sana itakuwaje

Kwa upande wa mwanamke ni kuwa kuna tatizo la kimalezi ambalo kwa mila za Kiafrika tunaamini kuwa mwanaume siku zote yupo juu na ni kichwa cha familia,...

Nini kifanyike
Ni kupendana kwa dhati tu

...ambalo ni jambo lisilowezekana!
 
Hawawezi kuvumilia tabia mbaya au chafu katika mahusiano kwani wanajiweeza. Kama ni vivyo basi ni kweli kwamba ndoa zao nyingi hazidumu kwa vile hawako tayari kuvumilia ujinga.QUOTE]

Eheeeee kumbe unajua kuwa wanaume uwa mna ujinga mwingi saa zingine... sasa basi habari ndo hii hapa..if a woman knows her rights and can stand up to claim them....tayari anakuwa branded mjeuri kwa sababu kasoma na ana hela zake... in short she can take care of you and your entire clan!!!!! alot of times mbona nyie wanaume ndio wenye hizo complexes!!!

we are learned, independent, loaded and sexy!!! take it or leave it!
 
Ila wanawake mkiwa na pesa mnakuwa na nyodo za kishamba kishamba sijui kwa nini.
 
Back
Top Bottom