Wanawake Ni Wasanii?

wazungu wanatabia ya kwanza
sijawahi kuona/kusikia mzungu mwenye mimba anamchukia mumewe....
hii ni kwa wanawake wa ki TZ kumchukia mumewe na kumpenda mwanaume mwingine (utakuta alikuwa anampenda tokea zamani lakini halikua hana sababu ya kufanya hivyo)

...te he! hili darasa sasa linaanza kugeuka shubiri!

enhe? kumbe wanawake wa kitanzania ndivyo walivyo ee?
ndio hizo 'involuntary' behaviours au? habari kubwa hii!
 
Hata mie naona kamuona mkewe ana madeko ya kisanii, ndio anataka kusema hapa kila mwanamke ana madeko kipindi cha mimba. Nakumbuka kuna post yake hapa alisema mkewe mchafu, haoshi nywele zake, basi akaona wote wachafu. Kwanza sijui ulimuomba mkeo samahani kwa kumuanika mtandaoni kwamba mchafu.

Hivyo Pakajimmy sio wanawake wote ni wasanii, wengine inatokea tu involuntary action.

Pretty,
Ni kweli si wote, ndo maana nikasema asilimia fulani.
Lakini kuhusu mambo ya manywele...nilishamuomba msamaha yule mama, na bahati nzuri alinielewa, pia na yeye ni member MAARUFU wa JF.
Ila kuna ukweli fulani katika mada zangu hizi za Nywele na KUDEKA... au sio Pretty?
Enjoy yr weekend.
 
...baada ya 'kushughulishwa' kote huko kipindi cha kulea mimba, kwenye DNA unakuta kumbe hata toto lenyewe sio lako, weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh....!
 
Ingawa mimi siyo mwana saikolojia lakini siamini kama wanawake wengi hufanya hivyo[ kama wapo ni kidogo sana].
Kwa bahati mbaya sisi wanaume in vigumu sana kuelewa hisia za kina mama katika kipindi hicho.
Hebu fikiria hali ya kuwa na kiumbe ndani ya mwili wake ambacho kinapitia steji mbali mbali hadi inapofika kuzaliwa. ni dhahiri naye atakuwa anabadilika kimwili na kisaikolojia na katika hali hiyo.
Siyo wanawake wote wanakuwa na tabia ya aina moja na hata mwanamke mmoja anaweza kuwa na tabia tofauti katika ujauzito wa mtoto mwingine.
Kama wewe umeoa basi lazima utakuwa ume-observe mabiliko ya tabia.
Kuna mimba nyingine mke huwa anamchukia mume utadhani amepewa mimba hiyo na mtu mwingine, na vilevile anaweza kuwa na wivu au mapenzi kwa mume kupita kiasi .
Pengine wataalam watusaidie katika hili lakini suala la usanii sidhani kama lipo.
Niliwahi kumuuliza 'wife' kuhusu hili jibu lake ni kuwa 'kwa mwanamume kuelewa hali anayokuwa nayo mwanamke mjazito inabidi naye abebe mimba. na hali hii ingewezekana kina mama wangetukimbia katika kipindi hiki ili hadi baada ya kujifungua'
UPO HAPO??????
 
huyo aliyekuambia, ana lengo gani na wewe au mwenzio?
Asikuambie mtu, kubeba tumbo miezi 9, kutaabiika kipindi chote hicho, kukosa usingizi hadi asubuhi hasa miezi 3 ya mwisho, kusikia kichefuchefu miezi mitatu au minne ya mwanzo mfululizo, heartburn, pressure, kuvimba miguu na mengine mengi... Ambayo kila mama mjamzito anayapitia, ukiacha matatizo mengine makubwa.... Hapo bado hujafikia kilele yaani uchungu na kujifungua.sasa wewe pata picha, unapoumwa malaria siku mbili tatu tu unakuwa hoi..... Bado wanawake wanajifanya? Usanii??? Jibu unalo mwenyewe.


ni kweli kabisa usemayo maana sitaki kuongeza maana nitaharibu jibu analo mwenyewe
 
...baada ya 'kushughulishwa' kote huko kipindi cha kulea mimba, kwenye DNA unakuta kumbe hata toto lenyewe sio lako, weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh....!
Mbu! Astaghafirluh!
Yaani unamwita mtoto toto lenyewe! Mbona kila leo wanawake wanaletewa watoto ambao waume zao wamezaa nje na kutegemewa kuwalea kwa mapenzi tele?...whats good for the goose is good for...... malizia basi!
 
Mbu! Astaghafirluh!
Yaani unamwita mtoto toto lenyewe! Mbona kila leo wanawake wanaletewa watoto ambao waume zao wamezaa nje na kutegemewa kuwalea kwa mapenzi tele?...whats good for the goose is good for...... malizia basi!

....naaam, toto halisikii la muadhini wala mnadi swala, ...tundu, bishi, halafu halifanani nawe kwa ukucha, sura wala kichwa... lipo lipo tu, na mwanaume pamoja na doubts zote mke anang'ang'ania mtoto anafanana nawe, aarrrhhhh...

Heko kwa mvumbuzi wa DNA, lazima ni mtu wa peponi tu huyu!
 
Huyo aliyekuambia, ana lengo gani na wewe au mwenzio?
Asikuambie mtu, kubeba tumbo miezi 9, kutaabiika kipindi chote hicho, kukosa usingizi hadi asubuhi hasa miezi 3 ya mwisho, kusikia kichefuchefu miezi mitatu au minne ya mwanzo mfululizo, heartburn, pressure, kuvimba miguu na mengine mengi... ambayo kila mama mjamzito anayapitia, ukiacha matatizo mengine makubwa.... hapo bado hujafikia kilele yaani uchungu na kujifungua.Sasa wewe pata picha, unapoumwa malaria siku mbili tatu tu unakuwa hoi..... bado wanawake wanajifanya? USANII??? JIBU UNALO MWENYEWE.
Kwa kweli hamwafanyii haki wanawake, hiyo hali hata mungu kashasema mwanamke anapochua mimba anakua kwenye uangalizi mkubwa kwani ni hatua ngumu mnoo. Wala sikutegemea kama kuna mtu angeanzisha mjadala juu ya hilo. Kama wanafanya usanii hembu muulize mama yako akuthibitishie kuwa ni usaniii. Tuwaonee huruma wanawake jamani hata kama anafanya usanii kwa ajili ya ujauzito huoni tu kuwa huyo ni mgonjwa wa saikolojia iliyo sababishwa na mimba?
 
Back
Top Bottom