Wanawake Ni Wasanii?

Je wanaJF, tudhibiti vipi hii hali ya kuonewa na hawa raia wa kike?
wewe unadhibitisha vipi?.
 
Wewe PakaJimmy ulifanya utafiti kabla ya kuandika hii thread? Au umecollect data kwa huyo aliekwambia nakuamua kupost huku kabla hujatafuta wanawake wengine na kuwauliza? Hivi nikuulize mfano labda mke wake ameambiwa na dr apumzike kipindi chote cha ujauzito asifanye kazi ngumu na ukiangalia kweli unaona kabisa hali yake haiko normal utasema ni usanii? Complication za mimba zinatofautiana kwa kila mwanamke waweza kuta mimi nikiwa kwenye hali hiyo siumwi na ninaendelea na kazi zangu mpaka naenda kujifungua je hujawahi sikia wengine wanaumwa mpaka anakua chini ya uangalizi wa dr sasa hapo utasema ni usanii? huyo aliekupa hayo maelezo yawezekana yeye huwa ana-act kuwa ni mgonjwa pindi awapo kwenye hiyo hali ili tu amsumbue mumewe.

Hajui kuwa in every generalization there is an irregularity.
 
Kila nikikumbuka usanii nilio kuwa nafanyiwa wa kulitouch nywele Tsh 70,000/= per week kweli wanawake nawakubali kwa usanii nawavulia kofia. Saizi sidanganyiki.
 
Kila nikikumbuka usanii nilio kuwa nafanyiwa wa kulitouch nywele Tsh 70,000/= per week kweli wanawake nawakubali kwa usanii nawavulia kofia. Saizi sidanganyiki.

wewe huo haukuwa usaniii ulikomolewa tu... hapa we are discussing something very senstive eti!
 
Kila nikikumbuka usanii nilio kuwa nafanyiwa wa kulitouch nywele Tsh 70,000/= per week kweli wanawake nawakubali kwa usanii nawavulia kofia. Saizi sidanganyiki.

teh teh, inabidi chama cha wanaume CCW, waweke tangazo la kupinga wanaume kuitwa ATM, kauli mbiu itakua SIDANGANYIKI!
 
Awali nilikuwa naambiwa, lakini baadaye nikaja kuhakikisha kwamba Wanawake pindi wawapo wajawazito huwa wasumbufu saana, na wanadeka ajabu!

Mwanamke mmoja akaja kunambia kwamba huwa wanafanya hayo mambo makusudi, maana ni nafasi yao ya pekee ya kutesa, kuomba kila watakacho, na kuwaonyesha mabwana zao kwamba ile shughuli ya kubeba mimba ni ya pekee, maana wanajua kwamba wanaume hawana uzoefu, na wala hawatakaa waijue!

Ni kweli mara chache huwa wanaumwaumwa, lakini asilimia kubwa huwa ni matatizo ya kupangwa na yanaandaliwa na kupikwa kitaalam!

Je wanaJF, tudhibiti vipi hii hali ya kuonewa na hawa raia wa kike?

WoS,Nyamayao,Penina na wengineo, kwanini mnakuwa wasanii kiasi hicho?

If you have nothing important to say it is better to keep quiet.

Have a great weekend
 
kuna wengine akisikia harufu ya ubwabwa anakasirika, akiona mtu ana pembua mchele anatishia kuumwaga. wapo wachache ila wengi huwa hali zao zinawafanya wanakuwa hivi

wenye ujauzito wa kwanza huwa wasumbufu sana
Paka jimmy kwa kweli wengi huwa na mataizo sio kudeka ila wengine wasio waadilifu wanaitumia hiyo nafasi kudeka zaid labda ni kwa sababu ya mitazamo tofauti na wenzi wao ,lakini shughuli ya kuleta mtu duniani ni ngumu kwa ujumla wake,hasa miezi mitatu ya mwanzo na miwili ya mwisho,mwanzoni ni kizunguzungu na kichefuchefu kisichoisha ,homa za asubuhi na jioni bila ya kuwa na malaria na kutokuwa na hamu ya kula,hasa huo wali uliotajwa mie huw naona una sukari ,pata picha ya sukari halafu uwe kwa nyama!
sikumoja nililetewa njegere zikiwa hazijamenywa na zilipigwa na jua zikawa na mvuke fulani hivi ,sikumwambia alieleta lakini ile harufu ilinitesa na nikazichukia njegere hata baada ya kujifungua ,huwezi amini lakini kitu ambacho wenzako wanaona cha kawaida wewe kinakutesa mpaka unajuuuuta!
ni hali ya kawaida kuwa na mabadiliko kwani mwili wenyewe umeshakuwa sio wamama pekeyake mwenzake alie tumboni kama hapendi kitu basi anamuambukiza mamake.
Ila kama mama mjamzito anapiga shule huwa anafaulu vizuri pengine kuliko kawaida sijui kuna uhusiano gani
 
Waambie binamu
Ila matatizo ya kutafuta pesa na siyo ya kijinsia, tueleweke kwa hilo hasije akatokea MwanajamiiOne hapa akauliza matatizo gani, nimeshaweka clear Nyamayao maana na wewe huchelewi kuuliza dada

hizo mbona cku hizi tunazitafuta wote?
 
Mbu, huwa wanawapiga makwenzi au wanawafanyaje eti?

...makwenzi? si afadhali ya hayo... kashfa na matusi kem kem.. eti alipochuma mboga wao walimsaidia kuinama (?), ...wanateseka kweli da' zetu hawa!
 
teh teh, inabidi chama cha wanaume CCW, waweke tangazo la kupinga wanaume kuitwa ATM, kauli mbiu itakua SIDANGANYIKI!

Hahaha hili nalo neno mkuu jana nilimualika shori mmoja kwa dinner akaja na wapambe kama 2 na yeye wa 3 nikazungusha round duh wale wapambe walikuwa wanakunywa Miller mpambe Windhoek dah mazee niliaga pale pale fasta nikawaambia nina dharula.
 
sorry Paka umeoa?mana uckute tunamuelewesha mtu kama Fidel hapa hatutaelewana.

Nyamayao

Mimi ni mwanataasisi wa siku nyingi kidogo, kwahiyo naongea kitu kwa xperience! Kamwe sifananii na akina Fidel wanaohonga 70,000/= kwa wiki!

Sijui kama nimekupa jibu ulilotaka!
 
If you have nothing important to say it is better to keep quiet.

Have a great weekend

Tena ukiona watu wa hivi ndo ujue ameshikwa masikio saaana, hadi anaona discussion za hivi zinamng`ong`a yeye!

We are part of the society, where all these things happen, and so nothing will stop us! If anyone feels bad, he/she can go to other threads!

U r a free person Bubu!
 
...duuuh,....

kaka una bifu na pakajimmy nini? :D hata mimi nishadekewa kwa saana tu mbona... mwache jamaa ajinafsi bana.

Sina biff na mtu yeyote Mkuu Mbu, bali nasema kila ninachodhania kina stahili kusemwa.

Hebu soma hapa :confused: Mwanamke mmoja akaja kunambia kwamba huwa wanafanya hayo mambo makusudi

Kweli kauli ya mwanamke mmoja inaweza kutumika kama hitimisho la kwamba Wanawake ni Wasanii wanapokuwa wajawazito? :confused:

Soma hapa: lakini baadaye nikaja kuhakikisha kwamba Wanawake pindi wawapo wajawazito huwa wasumbufu saana, na wanadeka ajabu!

Mwandishi hatwambii alihakikisha vipi kwamba wanawake ni wasumbufu saana na wanadeka ajabu! Je, sample yake ilikuwa na ukubwa kiasi gani? na alifanya utafiti huo kwa miaka mingapi?

Mbu, Mimba nazijua nimeziona kupitia watu nilio nao karibu kabisa katika maisha yangu na wengine wengi wamepoteza maisha yao kutokana na ujauzito.

Jaribu kufunga dubwana tumboni ambalo ni sawa na ujauzito wa kati ya miezi sita na hadi tisa na utembee nalo hata kwa masaa machache tu na kulala nalo hata usiku kucha ili uone wanawake hata wale ambao mimba zao zinakuwa hazina matatizo wanavyopata shida kutokana na ujauzito.

Huku ni sawa na kuwatukana mama zetu, wake zetu na dada zetu. Kuna ubaya gani wa kumdekeza mkeo kwa miezi michache tu wakati mnategemea kiumbe ambaye mungu amewajaalia!? Je ukimdekeza kwa hiyo miezi michache utapungukiwa na nini maishani mwako?

Hata madaktari ambao huwaweka wajawazito kwenye bed rest, special diet na kutotakiwa kufanya kazi zozote ili kuhakikisha ujauzito wao unaendelea salama salimini mpaka watakapojifungua nao pia ni wasanii maana hakuna sababu zozote za kufanya hivyo kwa sababu wanawake ni wasanii wakubwa na wanadeka saana!

Nooo! Paka Jimmy!! I don't need that kind of freedom I know better than that

Duh! ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni
 
...inawezekana ukweli eeh?

...iweje mtu adai hindi la kuchoma tena saa sita za usiku? mbaya zaidi ukimshawishi asubiri mpaka majogoo anaangusha bonge la kilio!...
unashangaa hindi la kuchoma ,sasa chek na hii . Dada yuko kwao mumewe kasafiri yuko na mamake na wadogo zake kapika tambi ili wanywee chai asubuhi ,kaenda kuoga alipotoka akakuta katengewa chai na mdogo wake ,kumbe akili yake yeye ilikuwa kwenye ukoko wa tambi ambao wadogo zake walishakula wao wlijua dada ametamani tambi hivyo wakampakulia zakumtosha ,kwani alikula ni kilio na kusema nani kawaruhusu kupakuwa nilichopika .kwa hiyo ujue sio kudeka ili unajisikia hivyo involuntary hata kama mume hayupo.
 
...sawa kaka'ngu, nimekusoma... naona tumepishana lugha tu hapa. Mzee wangu aliniusia pakitokea hali hii ni bora kunywa mafunda mawili matatu ya maji kusaidia kushusha pumzi na munkari.

...Hakuna ubaya kumdekeza mkeo, awe mjamzito, mgonjwa au mzima bukheri wa afya,...

...pakajimmy nilivyomuelewa mimi anatanzika na madeko kupita kiasi ya mjamzito, kama kayaona kwa mkewe, allahu alam.. lakini binfsi naamini (kama) mwana umleavyo na akuavyo, hivyo hivyo kwa mkeo. Kama utamdekeza sana, hata kumsukuma huyo mtoto itakuwa shughuli...

Ni maoni yangu tu bro, calm down.
 
unashangaa hindi la kuchoma ,sasa chek na hii . Dada yuko kwao mumewe kasafiri yuko na mamake na wadogo zake kapika tambi ili wanywee chai asubuhi ,kaenda kuoga alipotoka akakuta katengewa chai na mdogo wake ,kumbe akili yake yeye ilikuwa kwenye ukoko wa tambi ambao wadogo zake walishakula wao wlijua dada ametamani tambi hivyo wakampakulia zakumtosha ,kwani alikula ni kilio na kusema nani kawaruhusu kupakuwa nilichopika .kwa hiyo ujue sio kudeka ili unajisikia hivyo involuntary hata kama mume hayupo.

...WWN, nakushukuru kwa kunitanabahisha hili,... dah, 'uncontrollable urge'...

...pakajimmy huenda nawe sasa umeelewa kwamba hawa la'aziz wetu hawayafanyi haya ati kwa usanii au madeko, 'hawajitambui' kwamba wanayafanya haya kwa makusudi bro, tuwasamehe tu.
 
Mwanamke mmoja akaja kunambia kwamba huwa wanafanya hayo mambo makusudi, maana ni nafasi yao ya pekee ya kutesa, kuomba kila watakacho, na kuwaonyesha mabwana zao kwamba ile shughuli ya kubeba mimba ni ya pekee, maana wanajua kwamba wanaume hawana uzoefu, na wala hawatakaa waijue!

Ndugu yangu huyo dada alikudanganya na inawezekana hata mimba hajawahi kushika,hivi mjamzito kutembea na kopo la kutemea mate kila aendako ni makusudi kweli? kula udongo, kuvimba miguu, na mengine mengi ambayo hawatuambi!!! ni makusudi!! sidhani.tuwape hongera kwa kazi nzito ya kutunza mimba.
 
Back
Top Bottom