Wanawake na msamiati mpya dhidi ya wanaume………!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
wedd9.jpg

Saloon hizi zina mambo............................!

Jana nilikwenda kunyoa hizi mvi zangu, nilikuta kuna wateja wananyolewa katika saloon hiyo, hivyo ilibidi nikae nje kusubiri huku nikisoma gazeti langu. Pembeni ya hiyo saloon kulikuwa na saloon nyingine ya kike na hapo nje walikaa kina dada wakisukana. Mara akapita kijana mmoja wa pale mtaani ambaye ninafahamiana naye, tulisalimiana kisha akapita na hamsini zake wale kina dada walianza kumjadili……………

"Shoga unamuona yule kaka alivyo mzuri, yaani ana sura nzuri utadhani mwanamke." Alisema dada mmoja kati ya wale kina dada.

"Mwenzangu hayo macho je? Mwanaume ana macho mazuri kama nini, na kifua chake mmekiona? Na huo ndio ugonjwa wangu….." Alidakia mwenzake.

Mwenzao mmoja ambaye alikaa kimya akiwasikiliza alidakia...... "Ni mzuri ndio, lakini kizuri hakikikosi kasoro?"

Wale wenzie wakamuuliza ana kasoro gani?

"Hana kazi mwenzangu..........Yuko mtaani tu na anashinda vijiweni na jioni utamkuta uwanjani anajifanya kocha anafundisha mpira timu ya watoto wa hapa mtaani........... " Alijibu yule dada.

"sasa hiyo ndio kasoro?" Mwenzake mmoja alidadisi........

"Hee, mwanaume asiye na kazi atamtaka nani? Nani atamtaka mwanaume suruale........" Yule dada alijibu kisha wote wakacheka kwa pamoja kwa kebehi................

Duh, mazungumzo yale yalinifanya nitafakari.... Hivi siku hizi mwanaume asiye na kazi huchukuliwa kwamba ana kasoro!

Nilibaki mdomo wazi.
 
Saloon hizi zina mambo............................

“Shoga unamuona yule kaka alivyo mzuri, yaani ana sura nzuri utadhani mwanamke.” Alisema cacico -Hapa alimsema X HB wake

“Mwenzangu hayo macho je? Mwanaume ana macho mazuri kama nini, na kifua chake mmekiona? Na huo ndio ugonjwa wangu…..” Alidakia BADILI TABIA

@Remmy alidakia...... “Ni mzuri ndio, lakini kizuri hakikikosi kasoro?” Hapa wanamsema Bishanga )

Wale wenzie wakamuuliza ana kasoro gani?

“Hana kazi mwenzangu..........Yuko mtaani tu na anashinda vijiweni na jioni utamkuta uwanjani anajifanya kocha anafundisha mpira timu ya watoto wa hapa mtaani........... “ Alijibu yule dada.

“sasa hiyo ndio kasoro?” Yummy alidadisi........

“Hee, mwanaume asiye na kazi atamtaka nani? Nani atamtaka mwanaume suruale........” sweetlady alijibu kisha wote wakacheka kwa pamoja kwa kebehi................

Duh, mazungumzo yale yalinifanya nitafakari.... Hivi siku hizi mwanaume asiye na kazi huchukuliwa kwamba ana kasoro!

Nilibaki mdomo wazi.[/QUOTE]
Lol mi sina neno
Nimeamini wanamke Umbea
 
Saloon hizi zina mambo............................

"Shoga unamuona yule kaka alivyo mzuri, yaani ana sura nzuri utadhani mwanamke." Alisema cacico -Hapa alimsema X HB wake

"Mwenzangu hayo macho je? Mwanaume ana macho mazuri kama nini, na kifua chake mmekiona? Na huo ndio ugonjwa wangu….." Alidakia BADILI TABIA

@Remmy alidakia...... "Ni mzuri ndio, lakini kizuri hakikikosi kasoro?" Hapa wanamsema Bishanga )

Wale wenzie wakamuuliza ana kasoro gani?

"Hana kazi mwenzangu..........Yuko mtaani tu na anashinda vijiweni na jioni utamkuta uwanjani anajifanya kocha anafundisha mpira timu ya watoto wa hapa mtaani........... " Alijibu yule dada.

"sasa hiyo ndio kasoro?" Yummy alidadisi........

"Hee, mwanaume asiye na kazi atamtaka nani? Nani atamtaka mwanaume suruale........" sweetlady alijibu kisha wote wakacheka kwa pamoja kwa kebehi................

Duh, mazungumzo yale yalinifanya nitafakari.... Hivi siku hizi mwanaume asiye na kazi huchukuliwa kwamba ana kasoro!

Nilibaki mdomo wazi.

Mkuu kama ulikuwepo, maana hiyo timu uliyoishirikisha katika huu mjadala, kama kweli vileeee......................LOL
 
Mkuu kama ulikuwepo, maana hiyo timu uliyoishirikisha katika huu mjadala, kama kweli vileeee......................LOL
Hahahaaa hiyo timu iko nusu lol
Ungemkuta Zinduna hapo na Erotica ndio ungeshangaa maaana wangeanza hadi kuchambua wanavyokuwa chumbani na haoo wenye vifua lol
 
Last edited by a moderator:
Kama huna kazi mkuu, basi wewe una kasoro..................!
Hahahaaaa na wanajua kuchambua aisee lol
Kumbe ukiwa na kazi unawadaka kirahisi lol
Sasa Bishanga muuzandizi inakuwaje?
Ile sio kazi au?
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaa hiyo timu iko nusu lol
Ungemkuta Zinduna hapo na Erotica ndio ungeshangaa maaana wangeanza hadi kuchambua wanavyokuwa chumbani na haoo wenye vifua lol

Ukitaka kujua vifua vya wanawake basi jibanze kwenye Saloon.
Nasikia walituma maombi ya kutaka kuwekewa jukwaa lao la Urembo, Mods wakashitukia litakuwa ni la kuchapa umbea wakawatolea nje......... walikasirikaje!
 
Last edited by a moderator:
Hebu ngoja niende kwenye lile jukwaa la matangazo ya kazi niangelie ni wanaume wangapi wanaotafuta kazi kisha niunganishe dot (Wana kasoro)
 
Hebu ngoja niende kwenye lile jukwaa la matangazo ya kazi niangelie ni wanaume wangapi wanaotafuta kazi kisha niunganishe dot (Wana kasoro)
Teh hivi lile jukwaa huwa lina Mod?
Lol kama yuo muulize yeye atakusaidia kukupa list haraka
 
Teh hivi lile jukwaa huwa lina Mod?
Lol kama yuo muulize yeye atakusaidia kukupa list haraka
Nikiwajua nitawaanika hapa kwamba wana kasoro...................................

Kwa mujibu wa dada zetu
 
Back
Top Bottom