Sashel
JF-Expert Member
- Mar 6, 2012
- 212
- 84
SI wajibu kwa kuwa hata mimi ananifanyia yale ambayo yeye ni the best at. Tuna complement each other. Mfano hubby ananinyoshea nguo, kitu ambacho mwingine anaweza akashangaa kwa kuwa amekariri kuwa ni wajibu wa mke kunyoosha nguo. He is good at that, why not? Unachoweza kufanya vizuri fanya na usichoweza basi mwenzio afanye.
Yaani 'things we do for LOVE' sio kufanya kwa shurti bali hiyari na upendo. Watu wengine huwa hawaelewi kuwa upendo ni kitu cha pekee sana na ukimpanda mke/mme wala haitakusumbua kumfanyia mambo ambayo wengine wanaona si majukumu yako. Mimi ni mkristo na ktk Bible imeandikwa 'nikitoa mali zangu zote kuwalisha masikini..nikitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo hainifaidii kitu' kupenda ni kutenda kwa kujali na hiyari hata yale yasiyo 'majukumu' yako. Ndio maana hata Mungu hamlazimishi mtu kutenda mema maana hiyo itakuwa ni kutenda pasipo kupenda ni sawa na utumwa tu. Ila unapotenda ktk upendo haijalishi jukumu ni la nani.