Wanawake: Mnapokosea kudhani mnawaelewa wanaume………!

Kwenye maisha si kila unachopenda unapata. Ukilijua hilo hutagombana na mwenza wako. Hakuna mwanaume au mwanamke ambaye ni perfect labda ujitengenezee mwenyewe. Wanaoishi kwa furaha na amani ni wale wenye uwezo wa kukubali tofauti zao na kuzichukulia kama spices kwenye mapenzi yao. Hayuko smart hakumbuki hata fungua za gari kaweka wapi mimi opposite naakikisha kila kitu nimempangia kesho asiangaike; then tumekamilisha couple. Naongea kwa sana yeye mkimya, kwa nini kutokee ugomvi uso na suluhu. Anamwaga maji hovyo mimi ku deki ni one of my hobbies. Need I say more.

Unakuta mtu anamwambia mke/mume wake umezidi kuongea sana; hivi ulivyomuoa hukujua kama anaongea. Wakati mwingine ku point mapungufu ya wenzetu ni cover up ya tatizo kubwa lililopo; ambalo ni kuchokana.
 
Duh.............sijui mchumba wangu amepita hapa...Somo zuri sana. Kuna wakati miaka kadhaa iliyopita nilifikiri mimi tu ndio sipendi kukaripiwa na mwanamke kumbe tupo wengi......Ukizungumza na mimi kwa upole na mapenzi nasahau makosa yako yote..kifupi umenimaliza.

Can charminglady came this way.............!
 
Last edited by a moderator:
couple_arguing.jpg

Picha haihusiani na habari hii..........

Kuna wakati mmeshawahi kusikia watu wakilalamika kwamba mume fulani amemuacha mkewe ambaye ana tabia nzuri, mcheshi, mvumilivu, mwaminifu na mweledi (anayeelewa mambo). Ukweli ni kwamba hizo ni tabia nzuri na zinachangia sana kwenye kuimarisha ndoa, lakini bado hazina maana sana kama mke hataweza kujua namna nzuri ya kuonyesha upendo wake kwa mume.

Kuna makosa ambayo hufanywa na wanawake katika juhudi yao ya kuonyesha upendo kwa waume zao bila wenyewe kujua kwamba wanafanya makosa. Ngoja niyadadavue makosa ambayo wanawake wengi huyafanya wakijua wanawaelewa waume zao:

1. Kwa mfano, mwanaume hajipendi, mwanamke anapojaribu kuikemea tabia hiyo anakuwa anajenga ukuta mkubwa sana kati yao bila yeye kujua. Inashauriwa, badala ya kumwambia moja kwa moja mumewe kwamba aache kutojipenda, inashauriwa ni vyema akamnunulia mumewe nguo na akizivaa amsifie sana kiasi kwamba mwanaume huyo atajiona kuwa kumbe akivaa nguo za kiwango au mtindo fulani anakuwa katika hali ya kuvutia kupita kiasi. Hapo mwanaume naye atajaribu kununua aina hiyo ya nguo. Kwa wanawake ambao waume zao wana tabia ya kutojipenda kimavazi wanaweza kujaribu hata leo ili wapime matokeo ya ujanja huu.

2. Wanawake wanafanya makosa pale wanaposhindwa kushukuru juu ya yale mazuri wanayotendewa na waume zao na badala yake kulalamika kwa yale ambayo hawakutendewa. Utakuta mwanaume anajaribu kufanya hiki na kile kwa sababu ya upendo alio nao kwa mkewe, lakini mwanamke huyo hata mara moja hashukuru au kuonyesha kwamba anathamini juhudi hizo za mumewe. Lakini pale mwanume anaposhindwa kumfanyia hiki au kile iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi mwanamke hukata kama wembe kwa kauli zake za kulaani na kulalamika. Ni lazima wanawake wafahamu kwamba kwa maumbile wanaume hupenda sana kuonekana kuwa wamefanya mazuri au ni mashujaa kwa wake zao.

3. Kuna wanawake hawajui ‘asante' kwa waume zao hawajui kuonyesha kwamba walichofanyiwa hata kama ni kidogo wamefurahi na kukikubali. Wanawake hawa kwa bahati mbaya wakati huo huo huwa hawajui kuacha kulaumu pale wanapoona hawakufanyiwa yale waliyotarajia kufanyiwa na waume zao. Mwanamke anapaswa ajifunze kusema ‘asante' na kuonyesha kwamba ameridhika na alichotendewa na mumewe. Ajifunze pia kuacha kulalamika sana pale ambapo hakutendewa alichopaswa kutendewa.

4. Kuna wanawake ambao hupenda sana kuwaelekeza waume zao jinsi ya kufanya au hata kusema mambo fulani. Hebu fikiria juu ya mke ambaye anamuelekeza mumewe kwamba akioga bafuni asimwage maji hovyo kwa sababu kupiga deki ni taabu. Haya ni maelekezao ambayo humrudisha mume katika hali ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto mdogo ambaye anapaswa kurekebishwa na kuelekezwa kipi na kipi siyo cha kufanya. Mume hapa atajihisi kabisa kwamba hapendwi kwani haoni kama anathaminiwa, ni mtoto mdogo.

5. Wanawake huwa wanakosea sana pale wanapoeleza kukerwa hisia zao kwa kuuliza maswali ambayo hayana majibu, maswali ya kupita, ambayo siyo ya moja kwa moja kuhusiana na maudhi….. "unawezaje kufanya hivyo!" Ni vizuri mwanamke akaelezea kilichomkera moja kwa moja kuliko kutumia njia ya kuzunguka ya maswali yasiyo na majibu. "Sijui ndiyo nikueleweje?" Ni miongoni mwa maswali haya yasiyompendeza mwanaume.

Mtambuzi, asante kwa kitchen party nzuri haika umenifunza jambo ambalo Mungu akipenda nitaapply kwa mtarajiwa platozoom.....
Back to topic, hivi hayo ulosema yanapaswa kufanywa na mwanamke tu au me ndo cjaelewa?? Mf. No. 3 , je neno Asante anapaswa kusema mwanamke pekeyake? kwa maana kuna vitu vingi huwa tunawafanyia wenzi, kama kumfulia, kumpikia na vitu kama hivo je yeye mwanaume hapaswi kusema asante??
 
charminglady swali lako ni la msingi sana........
Ni kweli wote tunatakiwa kusema asante pale tunapokuwa tumeanyiwa jambo na wake zetu, hii inamuhusu kila mwanandoa ...............lakini iwapo mwanaume hana kawaida ya kuseme asante, basi hiyo isiwapasue kichwa unaweza ku-apply njia hii ya wewe kumwambia asante baada ya kuwa umemfanyia jambo zuri ambalo alitakiwa yeye ndiye aseme asante, naamini nafsi itamsuta na kama hatasema asante kwa wakati ule basi siku nyingine atakumbuka kusema asante .......... Inadaiwa kwamba maandiko matakatifu yanawaasa wanaume waishi na wake zao kwa akili, mimi nashauri wanawake waishi na waume zao kwa kutumia busara..............
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi asante sana kwa somo zuri ila liko kinadharia sana kimatendo mwanamke akitaka kumuweza mumewe hata kama ni mkorofi au sijui yukoje au ni mpole kanuni ambayo ni applicable na inafanya kazi ni hii hapa.

uwe na maneno yafuatayo, asante, nakupenda, karibu,pole na naomba. haya yanamfanya mume asifurukute na kama akifurukuta basi kanuni saidizi ni hii:-

ignore chochote akifanyacho usichokipenda, jipende san yaani muda wote uwe nadhifu na kisha timiza wajibu wako katika familia akiuliza kitu usimjibu kwa hasira kama unayo majibu unampa kama huna unamwambia sina majibu juu ya hili. unakaa kimya yaani usifurukute kwa lolote zaid ya kusali.

pia toka na friends kajiliwaze unapokereka wala usiseme na mtu ili kupunguza msongo wa mawazo.

Haya mengine yote mtambuzi tutaelezana hapa ila kwa wenye experience ya ndoa muda mrefu watajua hili nilisemalo na huku ndiko kumjua mumeo.

Mwiko na kamwe usitumie silaha zifutazo JEURI, KIBURI, WALA MASHINDANO. hiyo ndo weapon of marriage destruction.
 
Last edited by a moderator:
Duh.............sijui mchumba wangu amepita hapa...Somo zuri sana. Kuna wakati miaka kadhaa iliyopita nilifikiri mimi tu ndio sipendi kukaripiwa na mwanamke kumbe tupo wengi......Ukizungumza na mimi kwa upole na mapenzi nasahau makosa yako yote..kifupi umenimaliza.

Can charminglady came this way.............!

Nimefika swthat,
ucjali.......
 
Mtambuzi asante sana kwa somo zuri ila liko kinadharia sana kimatendo mwanamke akitaka kumuweza mumewe hata kama ni mkorofi au sijui yukoje au ni mpole kanuni ambayo ni applicable na inafanya kazi ni hii hapa.

uwe na maneno yafuatayo, asante, nakupenda, karibu,pole na naomba. haya yanamfanya mume asifurukute na kama akifurukuta basi kanuni saidizi ni hii:-

ignore chochote akifanyacho usichokipenda, jipende san yaani muda wote uwe nadhifu na kisha timiza wajibu wako katika familia akiuliza kitu usimjibu kwa hasira kama unayo majibu unampa kama huna unamwambia sina majibu juu ya hili. unakaa kimya yaani usifurukute kwa lolote zaid ya kusali.

pia toka na friends kajiliwaze unapokereka wala usiseme na mtu ili kupunguza msongo wa mawazo.

Haya mengine yote mtambuzi tutaelezana hapa ila kwa wenye experience ya ndoa muda mrefu watajua hili nilisemalo na huku ndiko kumjua mumeo.

Mwiko na kamwe usitumie silaha zifutazo JEURI, KIBURI, WALA MASHINDANO. hiyo ndo weapon of marriage destruction.

nisemapo timiza wajibu wako atika familia namaanisha kumvalisha awe nadhifu, yeye pamoja wote walioko ndani mwako kuwalisha kuwahudumia as mama na siyo kama mwanamke tu. na hapo kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanamke na mama. inabidi ieleweke wazi.
mama anaweza kuwa mwanamke yeyote lakin siyo kila mwanamke anaweza kuwa mama. Mama ninyemaanisha hapa hapa ni yule ambaye moyo wake umejaa qualities za umama, anaupendo, mkarimu,siyo mchonganishi siyo mtu wa kupendelea au mbaguzi, awe mwenye kupenda kuona watu wa nyumbani mwake muda wote wanaraha ajue kuwakumbatia watu wa nyumbani kwake. anajua kuitafuta amani na furaha naupendo wa nyumbani mwake kwa gharama ya busara na hekima yake. asiwe mtu wa kufuja mali kwa mambo yasiyofaa awe mtu ajuaye kutunza mali zake kwa umakini na aonyeshe kuumia zinapoharibika kwa makusudi tena awe msafi si tu wa mwili bali wa mazingira pia.
 
afu ndo ukurupuke kumwambia mtu 'hujanifikisha'
nyie acheni kutudanganya eti 'muwe mnasema'

kama tu kuvaa ukikosolewa napo ishu?

hivi kumbe inakuwaga ni ishu eee, bac huyu wangu nadhani kashazoea hiyo, acponifikisha yeye nani anifikishe? lazima nimwambie aisee, na kama anajua hana nguvu za kumtosha cku hiyo bora aache tu ajipange...sasa mkiogopa/mkihofu kuwaambia kitu kama hicho mnagumgumia nacho tu hamuoni kama mtajiumiza/jihudhunisha wenyewe?...
 
Mambo ya ndoa jamani magumu sana kumesa kila mtu anakuja na tathimini yake mavitabu na mavitabu uchambuzi na uchambuzi
 
.....hivi, unajihangaisha nini kutaka kumjua mtu ambaye mwenyewe hajijui? Hebu acheni bana....kama unataka u perfect ishi mwenyewe....
 
Kwenye maisha si kila unachopenda unapata. Ukilijua hilo hutagombana na mwenza wako. Hakuna mwanaume au mwanamke ambaye ni perfect labda ujitengenezee mwenyewe. Wanaoishi kwa furaha na amani ni wale wenye uwezo wa kukubali tofauti zao na kuzichukulia kama spices kwenye mapenzi yao. Hayuko smart hakumbuki hata fungua za gari kaweka wapi mimi opposite naakikisha kila kitu nimempangia kesho asiangaike; then tumekamilisha couple. Naongea kwa sana yeye mkimya, kwa nini kutokee ugomvi uso na suluhu. Anamwaga maji hovyo mimi ku deki ni one of my hobbies. Need I say more.

Unakuta mtu anamwambia mke/mume wake umezidi kuongea sana; hivi ulivyomuoa hukujua kama anaongea. Wakati mwingine ku point mapungufu ya wenzetu ni cover up ya tatizo kubwa lililopo; ambalo ni kuchokana.

Kumbe unayaweza majukumu yako! Ha ha! Hadi funguo za gari unampangia, asihangaike! Ila kule kwingine umebiiisha dah! Wakati mwingine wanawake huwa mnajua bongo zenu zilivyo.
 
afu ndo ukurupuke kumwambia mtu 'hujanifikisha'
nyie acheni kutudanganya eti 'muwe mnasema'

kama tu kuvaa ukikosolewa napo ishu?

Umeona eeh..yaani ni kichekesho..useme huku kifua cha kubebea hawana.
 
life is so simple tetea hadi dk ya mwisho kuish kwa amani na mwenzi wako but if it is not happening just quit. ili uwe na amani. huwez kuish maisha yote kila siku unawaza ndoa ndoa tu. hakuna jingine la kufanya?

Define your rules, regulations and terms before anything between you in such a way that one understands his/her limitations. thats all.
 
mambo mengine ni kuendekezana yani uoge bafuni pawe kama bwawa halafu mtu akuchekee akwambie darling unajua............ ni ngumu sana kwangu mtu kama amekerwa ni mara mia atoe lililo moyoni mwake kuliko kupretend kuna wanaume wengine vichwa maji usipoonyesaha umekasirika ukimwambia kwa utaratibu haelewi,mwanaume anavaa nguo anairudia na wakati umepasi nguo nyingine umemwandalia si makusudi hayo.waelimishe wanaume wenzako kwanza ndipo uangalie wengineo its not fair.:coffee::coffee:
 
Asnam bado kitambo kidogo binti utaolewa na utayaona hayo.............Kumbuka utakuwa humkomoi mumeo bali unajikomoa na ndio maana nikasema kwamba kama hamuwezi kuwa-handle wanaume wa aina hii basi nibora msiolewe mzae tu na maisha yasonge mbele kwani kanuni ya maumbile haijui kuolewa wala kuoa bali inajua kuzaa na ndio maana Mungu aliseme na muende mkazaane muijaze dunia na sio kuoana..........
 
Last edited by a moderator:
mi sio binti,ingekuwa ni hivyo basi hakuna umuhimu wa ndoa kwani hakuna mtu anaependa kuishi kwenye kero zisizo za lazima wengi wangezaa tu na kulea watoto ya nini kushurutishwa,hata leo fanya utafiti kwa hao wanaolea watoto peke yao kama walipenda au ilikuwa option yao ya kwanza utakuta ni asilimia chache sana ndio waliopenda wengi wao ni matatizo ndo yamepelekea.
 
Bondspot usipindishe nilichosema. Nafanya hayo si kama ni wajibu wangu kuweka funguo mahala pake ila ni hiari kwa kuwa nampenda na sitaki ahangaike; si wajibu kwa kuwa hawezi nigombeza kama hatauona funguo wake.
SI wajibu kwa kuwa hata mimi ananifanyia yale ambayo yeye ni the best at. Tuna complement each other. Mfano hubby ananinyoshea nguo, kitu ambacho mwingine anaweza akashangaa kwa kuwa amekariri kuwa ni wajibu wa mke kunyoosha nguo. He is good at that, why not? Unachoweza kufanya vizuri fanya na usichoweza basi mwenzio afanye.

Kumbe unayaweza majukumu yako! Ha ha! Hadi funguo za gari unampangia, asihangaike! Ila kule kwingine umebiiisha dah! Wakati mwingine wanawake huwa mnajua bongo zenu zilivyo.
 
hivi kumbe inakuwaga ni ishu eee, bac huyu wangu nadhani kashazoea hiyo, acponifikisha yeye nani anifikishe? lazima nimwambie aisee, na kama anajua hana nguvu za kumtosha cku hiyo bora aache tu ajipange...sasa mkiogopa/mkihofu kuwaambia kitu kama hicho mnagumgumia nacho tu hamuoni kama mtajiumiza/jihudhunisha wenyewe?...

Duh...hii nimeipenda.
 
Back
Top Bottom