Wanaume wenye sura hii, wana misimamo ambayo hawako tayari kuivunja…!

leo ndio nimekuamini 100% juu ya sura za watu na tabia zao mkuu .mtambuzi ..maana huyo ni typical me na tabia zangu... Daah leo umeniweza aisee
 
Mwanaume asiyevunja msimamo wake... Ana tabia ya kutosamehe hata kwa watu wake wa karibu, kutotaka kuzungumzia yaliyopita hasa kama yalimkwaza, ana uwezo mkubwa wa kukuchanganya kwa kutojua wapi unasimama katika mawazo yake (anakupenda/kujali/kuchukia/m'boa/ n.k). Kiasi kwamba kama wewe ni mtu ambaye unataka sana kupewa sifa kila mara za "nakupenda/ you mean a lot to me" OR kupewa sifa zozote inakuwa imekula kwako.

Mtu ambaye ana msimamo hayuo tayari kuivunja ni mtu ambaye huwa unashindwa (mhusika) kutowa maamuzi kutokana na matendo yake sababu basics zitaenda kama awali kasoro tu msimamo wake juu yako. Pia ni wagumu, yaani ha melt, not matter umeonesha majuto kiasi gani. Na mara nyingi wao hawa bend.. Tutolee mfano; ni aina ya mtu ambaye hata akiwa na mpenzi atawajibika ipasavyo ni kwa kiwango kikubwa ni nadra kumchanganya mpenziwe, so kitendo cha kusema kafanyiwa kosa ambalo yeye mwenyewe (mwenye msimamo) hawezi kufanya kirahisi inamfanya kuwa mgumu sana kuvunja misimamo anayokuwa ametowa.

Bila kuwa flexible maisha mbona mtihani...
 
portrait-young-african-american-man-green-shirt-smiles-big-into-the-camera.jpg


Watu wenye sura hiyo hapo juu naamini kila mmoja wetu anaweza kabisa kuwa anamjua angalau mtu mmoja mwenye sura inayofanana na hiyo. Watu wenye sura hiyo ni watu ambao wana sifa ya uzungumzaji, usafi na wakati mwingine ukorofi na hasira zilizojificha.

Ni watu ambao huzungumza sana na hasa kama masuala husika wanayajua au kuyapenda. Kwa hiyo kama ni kwenye siasa, mpira, dini au kingine ambacho wanakifahamu kwa kiasi fulani, huwa ni wazungumzaji sana.

Watu wenye sura hiyo ambao ni wachafu sio wengi, kwani kwa sehemu kubwa huwa wanajipenda katika kuvaa na kuoga, yaani usafi wa miili yao. Siyo jambo la ajabu kukutana na mwanaume mwenye sura hiyo ambaye hana hata senti kumi, lakini akiwa amevaa vizuri na ni msafi sana.

Wanaume wenye sura hiyo kama wanakunywa pombe au kuvuta bangi, hawana amana kwani hutokea kuwa wakorofi. Kama wanapenda wanawake pia hutokea kunaswa kirahisi na kwenda hovyo. Lakini wana sifa moja, ambayo ni uangalifu. Hata kama watakuwa kwenye tabia fulani mbaya, hujificha sana na kuwafuma huchukua muda.

Kwa kawaida wanaume wenye sura kama hiyo siyo wazungumzaji sana. Ni wapole, hasa pale ambapo wanajua wakisema sana, kutazuka kelele au kusigishana na pengine huogopa kukosolewa. Lakini nje ya kuhofia kusigishana huwa wasemaji wazuri, wanaopenda kusikilizwa wao tu. Kwa hiyo, kwa asili ni wapole, lakini kwenye mazingira fulani, ni wazungumzaji sana.

Wanaume wenye sura hiyo wana hasira za chini chini au tuseme, hukasirika haraka lakini huficha kwanza. Kwa hiyo badala ya kusema hunyamaza, lakini huumia ndani kwa ndani. Hii mara nyingi sana huwaumiza kihisia na baadaye kimwili, ambapo hupata maradhi kama ya moyo, kisukari , shinikizo la damu na mengine.

Wanaume wenye sura hiyo hufuata sana kanuni na taratibu zilizowekwa na jamii na hutokea kuwa waaminifu kwa kazi au mali za watu. Kuna idadi kubwa ya wanaume wenye sura kama hiyo ambao ni waaminifu sana. Hufanya kazi kama yao wanapoaminiwa na kupewa uhuru wa kufanya. Wanapenda kulinda majina na heshima zao hata kama kwa kufanya hivyo hawapewi shukurani.

Kwa upande wa ndoa au mahusiano hawana matatizo sana na kinachowasaidia ni misimamo yao. Wanaume wenye sura hiyo wana misimamo ambayo hawako tayari kuivunja, iwe ya kazini kwao au kwenye ndoa zao. Lakini pia mara nyingi ni watu wanaopenda kubaki na wake zao wa awali, hata kama wanatokea kuoa tena. Lakini hata hivyo,tabia ya kuwa na wake zaidi ya mmoja au nyumba ndogo, haiwakumbi sana wanaume wenye sura kama hiyo.

Kwa kawaida hupata bahati ya kuoa wanawake ambao ni wachapa kazi, wakomavu na wenye juhudi. Lakini wake zao wanapobadilika kitabia huwa wasumbufu sana. Hata hivyo hawatoi nafasi kwa wake zao kubadilika kutokana na misimamo yao.

Kwa kawaida wanaume wenye sura hiyo ni watu wa kipato cha kati, elimu ya kati na umaarufu wa kati. Hawapandi juu sana na wala hawashuki sana. Pamoja na hayo yote, hujitahidi kufahamu vitu vingi au kupenda kujifunza kupitia kwa wengine.

Umenigusa.
I am more or less like that ( I mean, "kitabia".. mie sina sura kama hiyo).
Kuwa na msimamo thabit?.. Yes. Sipendi zig-zag. Lakini msimamo wangu zaidi unatokana na maamuzi ya wengine. Mtambuzi , kama tupo kikundi kimoja, leo akisema tufanye hiki kitatuletea maendeleo... watu tunajipanga, kisha anakuja kubadilisha sera, hatutaelewana kabisaa. Mimi nitakuacha na sera zako mpya, nitaendelea na zile za zamani.

Kuburuza mtu? Kwa kuwa mimi sipendi kuburuzwa, vilevile sipendi kuburuza. Isipokuwa ukianza kuniburuza, utanikoma!!
 
Sura hiyo sio ya msimamo
Bali ni ya kupatwa na jazba na kulia lia ovyo
Sura za msimamo zasomeka kutoka side angle! I mean mashavu na misuli yake
 
Hakunaga kitu kama icho binadamu anabadilika muda wowote .sio kwamba et sura flan ndio wanatabia fulan no

Sent from my BlackBerry 9105 using JamiiForums
 
hahahaha! Wewe mwanaume wewe! Lol.

Nyie ndiyo wale ambao Mtambuzi angesema kuwa hata akukosee namna gani akikusemesha tu ama ukimuona wajikuta tu umemsamehe na pengine kujilaumu wewe na hali makosa ni yake! Lol

Tupo pamoja ODM... Always.
Amina shemeji, Amina.

Sasa waweza niruhusu ODM wako niondoke kwa amani? Kwa maana macho yangu yameliona tabasamu lako. Na tabasamu lako wajua ni nini kwangu ODM? Usimwambie mtu shem............ mitanzania mingine ina wivu wa kike..... Source: Pius Msekwa.... (Hili la wivu wa kike nitakuomba shem tukae kitako siku moja unielimishe, hivi huo wivu ukoje?)
 



Watu wenye sura hiyo ambao ni wachafu sio wengi, kwani kwa sehemu kubwa huwa wanajipenda katika kuvaa na kuoga, yaani usafi wa miili yao. Siyo jambo la ajabu kukutana na mwanaume mwenye sura hiyo ambaye hana hata senti kumi, lakini akiwa amevaa vizuri na ni msafi sana.


heheheheheee.........kama wakongomani......hahahahaaa Vin Diesel njoo unisaidie huku..............
 
Last edited by a moderator:
msimamo kwangu, naona uweze kuendana na muda na mazingira ya jambo husika na sio Kuwa king'ang'anizi kwa mambo mengine Yakawaidea mno ...
 
Back
Top Bottom